Mwanamuziki Mkongwe wa muziki wa Soukous aliyetamba sana katika nchi za Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla Mzee Makassy amesema kwamba ameamua kuachana na muziki kwa kuwa Mungu amemuita amtumikie ili afike kwake mbinguni,Katika mahojiano yake na Nifahamishe Mzee Makassy pia ameponda muziki wa sasa kuwa hauna ladha kutokana na wanamuziki wengi kulewa sifa.

Kwa habari kamili link ni hii

http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.
aspx?NewsID=1796898&&Cat=8

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Hi! Mzee Makassy namukubali mkongwe ni adhina katika burudani,mziki wetu wa vijana wa kisasa kweli umekwisha nguvu,kama analonga Gwiji Makassy,vijana wa kisasa wanalewa sifa,
    Mzee ni wakongwe wachache sana waliobakia barani Afrika,kwani mzee alikuwa mpiga gita katika bendi ya marehemu Bokelo Isenge,miaka hiyo wengine tupo wadogo au atujazaliwa.
    Mzee kama kahamua kumtumikia Mungu
    tunampa saluti!Lakini basi ombi letu kwa nini? asiwe anatoa ushahuri kwa wanamziki wachanga?MAANA YEYE NI MTALAAM SIYO WA VYOMBO NA MDUNDO TU BALI PIA UTAWALA KATIKA BIASHARA YA MZIKI

    ReplyDelete
  2. Much as I can recall it is not the first time God has beckoned Mzee Makassy. He responded to the call but I think Satan made another call a few years later after making a vital call to Cosmas Chidumule. Is it not time we stopped giving our phone numbers to the devil? A piece of advice: If you are call Satan at any time, just withhold your number. The good thing is that God has access to all phone directories...

    ReplyDelete
  3. Huyu ameshaona hela ipo wapi. Miziki ya Dini inalipa sasa hivi. Watu wengi wamekosa matumaini kwa sababu ya umaskini sasa wanakimbilia kwa Mungu kama tegemeo pekee. Angalia umati wa DECI watu walivyoumia na kujeruhiwa kwa sababu ya kujiandisha kurudishiwa hela zao. Yaani ni rahisi kuwadanganya watu siku hizi kwa sababu wanaangalia tegemeo ni wapi na huko ndio wanambilia hata kama haileti maana. Mzee Makasi ameona Chidumule, Remmy wana make money saa hivi anaona bora aanze huko.

    ReplyDelete
  4. we ano 1:19AM please usikurupuke kutoa maoni kama kitu huna uhakika nacho mzee makasi hajaokoka leo sema tu ni vile wewe uneipata habari leo mzee makasi aliokoka kitambo zaidi ya miaka 5 iliyopita na hadi vyombo vyake vya music akavitoa kanisani tusipende kuhukumu suala na mtu kumgeukia MUNGU ni suala binafsi baada ya kujiona ameishi maisha yasiyompendeza MUNGU kwa muda mrefu sio kuwaza tu pesa kama wewe

    ReplyDelete
  5. Anomy wa April 23, 2009 1:19 AM pole sana. Si kweli kuwa wote wanomkimbilia Yesu wamekimbilia hela, WAMETAMBUA NI WENYE DHAMBI NA KWAMBA YESU KRISTO ALIKUFA KWA AJILI YAO PALE MSALABANI, MIMI BINAFSI NIMEGUNDUA SIRI HIYO NA KUMKIMBILIA YESU, HAKIKA NI MZURI SANA, AMENITENDEA MENGI mf. NINA MAISHA YA USHINDI JUU YA DHAMBI, NINA TUMAINI LA UZIMA WA MILELE, AMENIBARIKI MNO KIUCHUMI n.k n.k

    NAKUSHAURI NAWE UIONJE NJIA YA YESU UONE KAMA ATAKUANGUSHA, HIZO PESA UNAZOSEMA ATAKUPA NJIA YA KUPATA IWAPO TU UTAKUBALI KUSIMAMA KTK NENO LAKE.

    HIVI KAMA WATU WAMEONA YESU ALIVYO NA BARAKA NYINGI + UZIMA TELE WAKAMKIMBILIA SHIDA IKO WAPI. ULITAKA WAENDELEE KUMTUMIKIA SHETANI? KARIBU UPANDE WA YESU NI KWEMA SANA. MAY GOD BLESS U

    GAP

    ReplyDelete
  6. Wenzio wanachuma kwenye ujana wewe unachuma uzeeni? saa za magharibi?

    Hata huyu Mungu hatakuona!!!!!

    ReplyDelete
  7. Ni kweli kabisa, nijuavyo mimi Mzee Makasi aliokoka siku nyingi sana. Tena nadhani yeye ni miongoni mwa washawishi wakuu wa Dr Remmy kuokoka. Sijui kwanini hii posti imekuja leo, inawezekana mtoa mada amechemsha namna ya kuiwasilisha. Nakumbuka kama miaka mitatu nyuma tulimualika mzee Makasi kwenye harusi ya mdogo wangu iliyofanyika pale Lamada Ilala, alikuja na kikundi chake wakatutandika na nyimbo za Injili safi kabisa zilizoenda shule mpaka kila mmoja alitamani aokoke siku hiyo. Wadau hapo juu isijekuwa mnamchanganya na Makassy Joniur (yule aliyeimba Baba Paroko)ambaye bado anaimba nyimbo ya kidunia.Mzee aliamua kumalizia siku zake duniani kwa kumtumikia Mola wake, hilo ni jambo jema lafaa kuigwa.

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  8. Mdau 1:19 AMApril 23, 2009

    Jamani mnaosema kuwa mzee Makasi ameokoka miaka mitano iliyopita, point bado ipo pale pale kuwa ameona wapi panalipa na amekimbilia huko. Kama Mdau
    Tarehe April 23, 2009 3:31 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

    Alivyodhibitisha "Ni kweli kabisa, nijuavyo mimi Nakumbuka kama miaka mitatu nyuma tulimualika mzee Makasi kwenye harusi ya mdogo wangu iliyofanyika pale Lamada Ilala, alikuja na kikundi chake wakatutandika na nyimbo za Injili safi kabisa zilizoenda shule mpaka kila mmoja alitamani aokoke siku hiyo.
    Mdau
    Cardiff"
    Kwa hiyo anaitwa kwenye sherehe analipwa kuimba, huko ndio ulaji upo. Piga ua wala msibishe.

    ReplyDelete
  9. Sasa wewe ulitaka afe kwa njaa. Hata mashehe na makasisi wanakula kutokana na Sadaka zitolewazo madhabahuni. kwanini yeye asipatiwe chakula kwa njia hiyo. Hilo la muziki wa dini kulipa mnajua nyie lakini yeye alichofuta ni kumtumikia Mungu kwa kutumia kipaji chake. Hayo mengine ni yaziada, kama Yesu alivyosema "Tafuteni kwanza ufalme wa mbingu na hayo mengine yote mtapewa kwa ziada". Kama suala ni kulipa basi wote akina MR II, yule mseminali aliyeshindwa (Dudu zuri) na wengineo ambao wanaanza kuzimika katika anga la muziki nao wangehamia kuimba kwa Yesu.
    Jamani karibuni kwa yesu kuna raha.

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  10. Mdau 1:19 AMApril 24, 2009

    Mdau Cardiff, naona Point imefika nyumbani, sasa unaanza kutapata ohh makasisi na masheikh..ukweli unaelewe haipingiki umaskini unachangia watu kupoteza matumaini na wanakimbia kwenye neno lolote wanaloona lina matumaini. Na hao masheikh na makasisi wana take advantage..Sio umeona DECI? Ilikuwa na Maaskofu..yaani WIZI Mtupu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...