
Jacob Zuma wa ANC akiwa na Mzee Nelson Mandela

Zellen Zille wa DA

MH. Lekoata wa COPE
Kaka Michuzi,
Kama wengi mjuavyo masaa machache yajayo Afrika Kusini wataingia kupiga kura kumtafuta Rais wa tatu wa Afrika kusini huru baada ya kuondolewa kwa utawala wa kikaburu mnamo 1994.
Swali tunalojiuliza ni nani atakuwa Rais mpya wa nchi hii? Kutokana na kura za maoni zilizokusanywa nchi nzima zinaonyesha kuwa mchuano mkali utakuwa kati ya Mr Jacobo Zuma(ANC), Mwanamama Mahiri Zellen Zille (DA) na Mr Lekoata wa (COPE).
COPE ni chama kipya kilichojiengua kutoka ANC mwishoni mwa mwaka jana. Juzi jumapili katika kuhitimisha kampeni zao chama cha ANC kilifanya "Suprise" kwa kumbeba Mzee Nelson Holithatha Mandela uwanjani bila watu kutarajia kuwa angekuwepo.
Nitaendelea kuwaletea matokeo zaidi.
Na Mdau James Sabuni wa Cape Town


Kuna kila dalili kuwa wasauzi watampa kura zao zuma. kinachonisikitisha sana ni kuwa wasauzi mbali ya kuwa wana asilimia kubwa sana ya wagonjwa wa ukimwi na wanahitaji mtu mwenye kuelewa tatizo lao hili kuwaongoza katika kupiga vita wanamnachagua mtu mwenye mawazo finyu juu ya jinsi ya mtu anavyoweza kupata ukimwi. itakuwaje unamchagua mtu kuwa kiongozi wa nchi yeye gonjwa sugu kama hili ambae amekiri kufanya mapenzi na mtu mwenye ukimwi na excuse yake ni "lakini nilikoga baada ya tendo" hi si sawa kabisa na ile excuse ya "i smoke but i did not inhale"
ReplyDeleteMr Lekoata wa (COPE) hangombei urais..kulikoni mleta news au ndio upo nje ya ulingo wa news?
ReplyDeleteAnony wa kwanza, samahani hao wasauzi wanajua wanachokifanya, sio wababaishaji hao, wanamjua Zuma. tena ni bora Zuma aliyekiri kwamba alifanya hiyo kitu na kuoga, kwani hata wataalam huwa wanasema hivyo kama umefanya bila "kifanyio" basi maji ni moja ya njia za kuweza kukuepusha na maambukizi. Zuma ni mtu wa watu na ni mpiganaji tangu zamani sana, usije mfananisha Zuma na wauza sura wa mataifa mengine ambao uhuru waliupigania wenzao na wao kuja kuanza kuhujumu tu.
ReplyDeletetaifa la wabakaji,,,
ReplyDeleteanyway kila kipindi kina maana yake na mtu wake
Zuma ni kituko yan ata ukimwangalia tu yan bazaz mtupu hahahaaaaa
mzee wa totoz,ikulu yao ntaenda na jinsi nlivyo?lazima asalende apa!
IVI JAMANI MZEE MANDELA NDO ADI ASHIKILIWE HAWEZI KABISA SIKU IZI KUTEMBEA??
ReplyDeleteSI WANGEMBEBA KTK WHEELCHAIR SIO VIZURI WAMTESA IVI SHUJAA WA AFRIKA
Mungu amjalie afya na siku tele
Hivi huyu anayemsaidia Mzee wetu kuinuka ni Ma Winnie?
ReplyDeleteweka basi habari za uchaguzi bondeni!
ReplyDeletekwanini njia wanaotumia wao na sisi tusiitumie. kwani ni nzuri.
tunatakiwa kujua idadi ya viti vya bunge na idadi ya wapiga kura halafu tunagawanya kujua kila kiti cha bunge ni kura/kula ngapi.
halafu watu wanakwenda kupiga kura..
/kula!
hakuna kampeni za wagombea viti vya ubunge ni uraisi na chama tuuuuuuu
hapo imekaaje??
nadhani tutaondokana na majimbo yale ya zenj yenye wapiga kura 10,000 wakati kule njombe kuna jimbo la zaidi ya 100,000
..kwa namana hiyo utaona mbunge mmoja wa bara ni sawa na wabunge zaidi ya 5 wa zenji...
wadau mnasemaje???
heri mimi sijasema!
http://www.sowetan.co.za/News/Article.aspx?id=987257
South Africans are a joke and Zuma is a clown. Hii design si ndio iliyoifikisha Zimbabwe ilipo? Ingalikuwa ni mimi ningempa kura Mama ajaribu kuliko huyu mpuuzi Zuma.
ReplyDeleteMdau, Boston, US