msanii akitoa burudani kwa wimbo maarufu wa
 injili wa 'nibebe' wakati wa uchaguzi mkuu wa CUF katika 
ukumbi wa diamond jubilee hall jijini dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Nyimbo za Injili na Uchaguzi mkuu wa CUF wapi na wapi? Nyimbo hizi sasa ni biashara tu hakuna lolote. Tena nyingine ukiangalia wanakata viuno mpaka mtu unashangaa. Ni kweli wengine wameweza kutajirika na hizi nyimbo na inavyoonekana hili ndilo lengo la wengi la waimbaji hawa ndiyo maana wanakumbwa na kashfa za mara kwa mara - za kingono, kifedha n.k. Biblia ilishaonya - kila mtu ashike sana alichonacho. Wengi wa waimbaji hawa wanaushushia hadhi ukristo!

    ReplyDelete
  2. Tembelea

    Nyimbozadini.blogspot.com

    au

    Youtube.com

    Utaona collection ya gospel singers mbalimbali na wengine unatazama mpaka unashangaa kama kweli wanamwimbia Mungu ama devil. Uwanja huu wa Gospel songs umevamiwa na ni lazima kuwa macho. Kama huyu why sing gospel at CUF general election? Waache Uislamu na kuwa saved au? God help us!

    ReplyDelete
  3. JINA LA BWANA LIHIDIMIWE,HALELUUYAAA!! its better kuliko ingewekwa taarabu chuki,majungu n.k

    ReplyDelete
  4. Hii Safi sana,Kila mwenye pumzi na amsifu Mungu.

    Mdau Trondheim

    ReplyDelete
  5. better gospel than bongo flava,taarabu nk nk

    ila waimbaji wa gospel ata kama ndipo mnapopatia fweza nanyi muishi!!ILA ANGALIZO MSIKWAZE WATU NA KUMSHUSHIA KRISTO HESHIMA YAKE,USHABIKI HAUTAKIWI,LENGO LIWE KUCHAPA INJILI TU.
    ni kweli kuna watu ata hatuelewi wana mana gani yan wanakata MAUNO adi khaaaa,style za mapanga shwaa,ngwasuma nk nk.WANAKERA SANA.

    ni ayo tu

    ReplyDelete
  6. This is THE BEST video clip I have seen for ages! BWANA YESU ASIFIWE SANA!
    Mdau München

    ReplyDelete
  7. ingekuwa ndio wenzetu nyinyi waislamu sipati picha hayo makofi ambayo mngechapana hapo!wakristo tunaamini kila mtu hatima yake itajulikana siku yake ya kufa na kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe.

    ReplyDelete
  8. Yakaisari mpe kaisari, na usimpe kaisari ya mungu au usimpe mungu ya kaisari??? mh! haya!

    Ushauri wangu kwa hao wanaojiita wasanii, na ushauri wangu kwa hao wenye mikutano na mahafla nyimbo ziendane na matukio yenyewe hapo nibebenibebe inahusu nini hapo? Hebu tungeni nyimbo zinazohusiana na maukio na kuleta hamasa, wahusika unaona gharama gani kumlipa msanii akakutungia nyimbo hata kama atabadilisha maneno sauti ibaki ileile? Hapo pangekua hapatoshi kwa hamkani endapo nyimbo ingehusu na mambo ya kafu, nachelea kusema mashekhe wengi hapo imebidi wabaki vitini kuhofia huo wimbo kama hamuamini wekeni ambao unahusu shughuli yenyewe mf.eee chama chama chama chama cha wananchi cufu uone mtibwiriko hapo hapatotosha. Acheni hizo nyimbo za taarabu na za injili au kaswida, leteni nyimbo za hamasa za uzalendo mutumie vipaji vyenu vya ubunifu kibiashara na kiburudani na kiheshima,sio mchanganye mchanganye kwenye mikutano ya siasa.

    ReplyDelete
  9. Nibebe kwenye mkutano wa CUF! Potelea mbali hata ingekuwa TLP au CCM!

    ReplyDelete
  10. im happy that wamesema YESU nibebe,
    yaani pole pole neno litamuingia kila mtu!!
    bado kitambo kidogo "kila mtu atakiri"
    BE GLORIFIED JESUS!!

    ReplyDelete
  11. walisema Kila mwenye pumzi atakiri jina la YESU,ata shetani anajua YESU ni nani Jina la YESU libarikiwe

    ReplyDelete
  12. ITS ALL ABOUT COMPAIN..
    TOKA LINI WAJAHIDIANA WAKACHEZA NYIMBO ZA MAKAFIRI? HAMPATI KURA NG'OOOO

    ReplyDelete
  13. Wanaopinga hii wana mawazo finyu! Vyama ni kwa watu na nyimbo ni kwa ajili ya watu. Mradi wimbo ulifikisha ujumbe na watu wakaburudika vile vile lipi baya? Je mungependa kusikia mipasho ya matusi? hata wasiomwamini yesu umeona wamechangamkia tenda. KRISTU TUMAINI LETU NA ASIFIWE NA KILA KIUMBE KIPUMUACHO!!!

    ReplyDelete
  14. Hi! Balozi wa nani?ninii??
    Hongera sana kwa kugawa usawa,sasa wale wanaodai oh mkuu wa Tageta ni CCM mtandao u!unawasuta kwa kugawa usawa! hii blog ya jamii

    ReplyDelete
  15. MAANA YA KAFIR???UNAIJUA WEE MTU??

    oooh usitake watu tutelemshe mada apa pachimbike!!

    kafir

    ReplyDelete
  16. Kweli CUF ni chama cha wananchi wa dini zote.

    ReplyDelete
  17. Ama kweli leo nimeona na nimejifunza ya kuwa amwaminiye Mungu si mtovu na pia kucha Mungu si kilemba cheupe (The fear of God is not wearing a white turban http://www.mwambao.com/methali.htm)
    Hii inaonyesha tayari watu wameng'amua ya kuwa kumcha Mungu ni chanzo cha Hekima(Mithali 9:10a - Proverbs 9:10a). Basi mbegu imepandwa (Matayo 13:3-8) na wenye masikio ya kusikia na wasikie

    (angalia hapa hadithi ya mpanzi http://bibleresources.bible.com/passagesearchresults.php?passage1=Matthew+13&version=45)

    Binafsi nimeshindwa kushangaa maana nilidhani ni maluweluwe au ni mbwembwe za kuunganisha stori na picha za watu ambazo hufanywa sana katika nchi zilizoendelea! Lakini kusema ukweli huu wimbo una ukweli ndani yake na ndio maana umekubalika na wengi.

    Jina la Bwana na lihimidiwe

    Mmbarikiwe.

    BELEN

    ReplyDelete
  18. Jina la bwana lihimidiwe..........

    lakini kama quran ingesomwa tungekuja juu kusema hiki ni chama cha waislamu tu....lets not be bias

    ReplyDelete
  19. MIMI NIMKULIA KWENYE CCM, NIKO NJE YA NCHI KWA MIAKA 10 BADO NAFUATILIA HABARI ZA HOME CUF NIMEWAPENDA NAMENIFURAHISHA KWA HILI SIKUTEGEMEA KUONA MITANDIO IKIMBA NA KUMTAJA YESU SIUNAJUA UISLAM NI MGUMU NA NIWAGUMU KWA SABABU WENGI NI KWENYE CUF NIWA.........MALIZIA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...