Muhidin,
Naomba uwape pongezi Clouds kwa mjengo wao mpya. katika masijala ya kumbukumbu zangu kuna hili tangazo la Clouds Discotheque enzi hizo.
Wape jamaa pongezi nyingi sana.
PS/ Tafadhali bin tafadhali naomba jina langu uweke kapuni.
Weekend njema.
Mzee mwenziyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Michuzi achana na yaliyopita tugangie ya muhimu yajayo. Hebu fanya kazi eti tunasikia Ncho YETU IMESHAANZA KUUZWA huko vipande vipande ni kweli haya ya KIGAMBONI ? Wenye viwanja huko tunaambiwa tutapata fidia ya kwamba KIGAMBONI ameusiwa MMAREKANi aje kuweka JEshi ? TUnaomba ufanye uchunguzi utuletee habari kam ni KWELI haya........ Na kama ni kweli mimi binafsi narudisha Kadi yangu ya Uanachama wa CCM , mana hii sasa itakuwa IMEPITA BEYOND UFISADI.

    ReplyDelete
  2. haya Pongez na hongera zenu! wazee wa Cloud FM,kumbu kumbu hiyo inaonyesha mabali mlikotoka na sisi wadau wenu,tangu enzi zile za suali aina ya Pekosi bin bwagaloo nchi upana nch 28 na kiati raizon bora shoe ngazi 3,si mnakumbuka wazee na viwalo hivi bado mnavyo kabatini kama kumbu kumbu ya agano la kale la ujana au? ngoja niwapishe waosha vinywa saa hizi washarudi kubeba BOX

    ReplyDelete
  3. Duh!kumbe cloud inabidi mshukuru mungu sana kwa kufika mlipo na mbali mlikotoka! naona picha Papa Joe Kusaga na tangazao la nguvu!
    bango hili kwa wakati ule lazima lilichorwa na Manju David rajab? kama sisi yeye basi labda Ibra Washikera akisaidina na Maalim Ebony !bongo yetu inasonga mbele,lakini ni muhimu kukumbusha tulikotoka au vipi?
    we acha wenye kujua kusukutua midomo wameshachoka na kubeba MABOX waje kuliona hilo bango na hasira zao

    ReplyDelete
  4. Yani hapo kama namuona Tungi, Titi Morris ,Mdopes ,Melisa Khan , Kibibi Mishy Kombo na Lulu Mwakyusa kwenye dancin flour , nimekumbushwa mbali sana wow!

    ReplyDelete
  5. wow! that is some flashback right there!.....

    but that was far ahead.who remembers where it all started? it was with Biribi Discotheque, na kaka yake Justin aliyekuja na vyombo vya music toka majuu enzi hizo!

    ReplyDelete
  6. jamani kweli hata mimi imenikumbusha kweli kweli enzi za maclouds, ilikuwa never miss every week-end. Na hawa kina Mdopes, Chuwas,Mserikalis na tungi wako wapi? Yaani those days were the days!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...