simba na yanga wakiingia uwanjani leo katika mchezo wao wa marudiano wa ligi kuu ya vodacom. matokeo yalikuwa ni 2-2. nimeona si vibaya mdau angalau ukapiga chabo japo kiduchu mambo yalivyokuwa kabla ya gemu.
hii ni katika kuendeleza libeneke kwa njia ya video ambapo kama nilivyowahi kuahidi huko nyuma, nitajitahidi kuwaletea taswira zinazotembea kwa kadri ya uwezo wangu. si kazi ndogo ukizingatia spidi ya mtandao wetu hapa bongo, lakini kwa kuwa mie kutoa visababu huwa sipendagi, piga ua lazima wadau mpate video mbalimbali kila siku kwa kwenda mbele!
ANGALIZO: Ukiangalia chini kulia utakuta zile tarakimu za idadi ya watembeleaji wa globu ya jamii zikionesha kwamba mdau wa milioni 6 atapatikana muda si mrefu ujao. hivyo si vibaya kukaa mkao wa kula kwani kuna ishara kwamba mfadhili atayetoa zawadi kwa huyo mdau wa milioni 6 atapatikana pia. siwezi kutaja aina ya zawadi kwa sasa ila ninatafuta maradufu ya dola 500 za kawaida. ikishindikana basi itabidi nijipinde mie mwenyewe niibanje hiyo zawadi...


WE MICHUZI YANGA NINI! MBONA UMEBANA LINE UP YA SIMBA! ONGEZA KIPANDE HICHO.
ReplyDeleteIT IS WHAT IT IS.
Naona Umeniwahi nilitaka kusema hivyo ila Michuzi, ingawa Net ni Slow, Tunashukuru kwa Mchango wako kwa kutuwekea Video, najua sio jambo rahisi kuvumilia kusubri Ku-upload Video hizo. Thanks Mdau wa Newala
ReplyDeleteMICHUZI HUNA CLIP YA MAGOLI?
ReplyDeleteMambo vipi kaka michuzi!
ReplyDeleteMi ni mdau mkubwa wa blog hii nipo Gold Coast-Australia. Nikiamka lazima nichungulie yaliyojiri kwenye blog hii na silali bila kuiona.
ebu nieleweshe kuhusu hili shindano maana naona tu tarakimu hapo chini lakini sijui namna ya kushiriki wala mshindi napatikanaje.
Mwisho, hongera sana kwa kutuhabarisha na kudhibiti nidhamu ya lugha ndani ya blog yetu
Mdau
Big up kaka michuzi, nashukuru sana kwa kazi yako nzuri ya kutuletea mapicha kibao toka sehemu mbali mbali. Nimefurahi kuwaona ndugu zangu katika picha inayoonyesha mashabiki wa Yanga, Namuona pale Bw. Arsen and Wife, Bibie Sara, Lily na wengineo. Salaam saana wapendwa.
ReplyDeleteMdau Beijing.
kaka michuzi unastahili nishani kwa kazi nzuri unayofanya kila la kheri mdau west london
ReplyDelete