kariakoo, mtaa wa msimbazi
kariakoo, mtaa wa lumumba
gerezani, mtaa wa sikukuu

vikwangua anga vipya jijini dar siku hizi vimenakshiwa vioo kama inavyoonekana pichani. uzuri kila mtu anauona ila labda wadau wataalamu watuambie faida ya vioo hivyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Vioo vinasaidia jengo kua na park za kutosha.

    ReplyDelete
  2. sababu kubwa ni urembo. Ila inaweza kusaidia kuakisi miale ya jua pia!

    ReplyDelete
  3. !nadhani kwa vile umeme Tanzania ni wa mgao wadau wa ujenzi wameamua kuvisha ghorofa solar panel ili kujiwekea akiba dowans/tanesco ikishindwa kutoa umeme wa kutosha watumie umeme JUA!

    ReplyDelete
  4. HAHAHAHAH
    BONGO TAMBARAREE....... SIO!
    HIZO NI MALI ZA NDUGU ZETU WAHINDI NA WAARABU WAZAWA TUNANI??

    ReplyDelete
  5. Yes mbali ya kupendezesha pia nadhani inapunguza zile gharama za ku-repaint kila baada ya misimu ya mvua kupita!

    ReplyDelete
  6. mifwedhwa ya EPA!

    ReplyDelete
  7. Hao waliosimama hapo karikao mtaa wa malumba wanaoneka kama vile wana subiri under grownd Train sasa kweli Bongo ni ulaya asante Rais wetu Mr J ,kikwete kwa kuleta maendeleo mungu akuzidishie nguvu siku moja wazungu wafike hapa kuja kuomba badala ya sisi kwenda kwao haipo mbali hiyo siku mzee wangu

    ReplyDelete
  8. Anony hapo juu unaonekana hujaja bongo siku nyingi sana. Kuna mtu kakusaidia hapo juu kwamba hayo magorofa ni ya wahindi na waarabu wewe unazungumzia maendeleo sijuwi underground train??!. Thubutu yako underground train kabla ya barabara???/

    Michuzi wapigie yale mahandaki ya city centre kama haidary plaza uwawekee hawa jamaa naona taswira waliyonayo ya bongo ni tofauti. Kwa taarifa yenu huku life kila siku ni heri ya jana.

    ReplyDelete
  9. enzi za mwalimu wamiliki wote wa haya makwangua anga wangekuwa selo...

    wizi mtupu angewaambia..
    mmezipata wapi hizo pesa..kama si za kagoda,epa,richmond,meta meta,meremeta,dowans n.k

    ona enzi zile jinsi mambo yalivyokuwa
    http://www.theeastafrican.co.ke/magazine/-/434746/479582/-/item/1/-/tcy0r2/-/index.html

    ReplyDelete
  10. Sasa nyie mnaona raha kwa kua na magorofa ya vioo yasiyo na uhakika wa kuwa na basic necessities 24/7? Au ndio maana ya utambarare wenyewe wa kibongo?

    Hayo magorofa yamejengwa kwa kutumia teknolojia na michoro ya ki mwaka 47.. Halafu pembeni tu mwa hayo majengo ni vumbi na tope mtindo mmoja..

    Ushauri wa bure: Wajenzi wanapaswa ku-plan ahead vitu kama miundombinu surrounding their buildings na vitu vingine kama bustani na kadhalika. Hivi hamshangai why mkienda ubalozi wa US hapo bongo mandhari ilivyokuwa planned accordingly.. hivi hamjisikii vichefuchefu kweli? Hakuna haja ya kutuma wajenzi kwenda lets say China, Jo'burg ama Dubai kufanya study tour ya jinsi wajenzi wenzao wanavyo-plan ahead vitu vingine vinavyoambatana na majengo. Wanaweza tu tembelea ubalozi wa marekani hapa Dar na kufumbuka macho.

    Ni aibu kwamba design ya High Schools za nchi nyingine ni bomba kuliko ofisi za wizara ya utumishi. Ebu michuzi wamwagie hawa jamaa mapicha ya kueleweka.

    ReplyDelete
  11. Je vioo hivyo vimefuata viwango vya TBS ktk suala la milipuko ya bomu, tetemeko la ardhi au moto.

    Maana sije ikatokea majanga niliyo yataja ktk 'para' hapo juu, na kipande kizima cha kioo kikachinja vichwa vya waokozi kama wazima moto na raia.

    ReplyDelete
  12. Leo nilienda kwenye gorofa la picha ya chini na nikakutana na "kikopo" chooni. Kesho nakwenda tena, nitachukua na digital camera yangu niwamwagie mavituzz

    ReplyDelete
  13. sasa kusafisha hayo madirisha niaje? huku waspanish ndio kazi zao na wana vifaa vyote lakini wanaanguka na kufa kishenzi. sasa huko bongo hizo kazi za kuosha zitakua machinjioni

    ReplyDelete
  14. Lazima vioo vyote viwe rangi moja?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...