
WaPi...Tamasha la sanaa la kila mwezi. TUTAKUWEPO BRITISH COUNCIL kama kawaida mtaa wa Ohio/Samora kati kati ya jiji DAR.
Tunawatakeni radhi kwa usumbufu wote uliojitokeza mwezi uliopita, kwa kutokuwepo na Tamasha la WaPi. Tumerejea na muundo mpya na sasa tutakuwa na tamasha letu kila miezi mitatu.
Kutakuwepo na WaPi ndogo kabla ya hapo kwenye mashule na vyuo. Tutajadili fursa na nguvu ya redio kwa jamii yetu na mabavyo tunaweza kuitumia ili kuleta mabadiliko endelevu kwenye mada yetu Nguvu ya Redio kwa jamii...
kwenye KIJIWE MAARIFA tutakuwa na Ozzey atakayetoa warsha ya Nadharia ya mziki. Zavara kwenye taaluma ya "KUEMSII" ..hii inaendelea na tunaingia kasi mpya sasa. itakuwa ijumaa saa 12 jioni pale British Council.
Yawaletea
Nyota kali, Ozzey,Twetu lobo, Jipe Moyo na wengineo
Mitindo na Kemi Kalikawe,
Wasanii wa sauti ya handaki(undeground), Katika harakati.
Madijei, ma emsii, machata, mabreka ,michoro mbali mbali, ushairi,ngoma, maigizo na usanifu mitindo.
Mahali:British Council Dar Es Salaam
(maelekezo: mtaa wa Ohio/Samora, kati kati ya jiji Dar)
Jumamosi, 25-04- 2009
mida; saa 9 - alasiri-hadi 2 usiku
Mada ya mwezi:Nguvu ya Redio kwa jamii
Hivi hiyo miaka 75 inajumlisha na kile kipindi cha ukoloni walipokuwa wakitunyonya na kututawala kimabavu?
ReplyDeletebritish council watuandalie onyesho la kitamaduni???utamaduni wa kibantu au???
ReplyDeletejamani!!!
ivi makumbusho yetu ya taifa na kituo cha utamaduni tanzania kazi yao nini??
"mashule" kisw cha wapi
aya tunashukuru