HABARI TOKA VISIWANI ASUBUHI HII ZIMETHIBITISHA KWAMBA MELI IITAYO MV FATHI IMEZAMA KATIKA BANDARI YA ZENJI NA JUHUDI ZINAENDELEA KUOPOA MAITI TOKA KATIKA MELI HIYO AMBAYO ILIKUWA INAJIANDAA NA SAFARI YA KUELEKEA DAR IKIWA NA SHEHENA YA MIZIGO MBALIMBALI NA ABIRIA.
HABARI ZINASEMA HADI SASA MAITI WATATU (MWANAUME MMOJA NA MWANAMKE NA KIJANA WA KIUME WA UMRI WA MIAKA KATI YA 14-17) WAMEOPOLEWA HADI SASA, ILA MAJINA YAO BADO KUPATIKANA.
SABABU YA KUZAMA KWA MELI HIYO BADO HAIJAJULIKANA NA IDADI KAMILI YA ABIRIA WALIOKUWAMO NA WALIOPOTEZA MAISHA AMA KUOKOKA PIA BADO KUJULIKANA KWANI KAZI YA KUOPOA MAITI BADO ZINAENDELEA. INASADIKIWA KUNA WATU ZAIDI MAJINI.
HABARI ZAIDI NA PICHA TUTAPATA BAADAYE WAKATI GLOBU YA JAMII IKIENDELEA KUFUATILIA KWA UKARIBU AJALI HII

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 30, 2009

    ooh noo, am tired and sick na hizi ajali za bongo kila kukicha, hebu tupatie majina aisee kwani wengine ndugu zetu ni wafanyabiashara dar to zenji, it is so sad jamani.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 30, 2009

    jamani nisaidieni hivi maiti zinaokolewaje? naona hapa kazi yakuokoa maiti, any way si mjuzi sana wa kiswahili anyway

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 30, 2009

    akitena mkuuu wa nanihii hii blackberry iweke kando kwanza hadi uweze kuimudu maana tangu uipate unachapia sana, sasa mweli ndo nini na je kuokoa maiti unaokoaje?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 30, 2009

    gudi, naona umerektifai makosa, hapo lazima umetumia laptop

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 30, 2009

    Tunashukuru sana kwa taarifa

    Mdau kutoka USA

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 30, 2009

    Tunasikitika kuwatangazia ajali mbaya ya meli ya mizigo (Mv. Fathi ya kampuni ya Seagul mali ya Bwana Said Mbuzi) ambayo ilikuwa ikitokea Zanzibar kuja Dar. Inasemekana kuna idadi kubwa ya watu waliopoteza maisha

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 30, 2009

    nyie mlio mkosowa michuzi soma tena alivyo andika kabla ya kukosoa , ameandika kuopoa sio kuokoa tofautisha kuokoa na kuopoa

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 30, 2009

    why why why?jamani kila siku sasa haya mambo ndio yanatufanya watu tulioko ughaibuni tushindwe kufanya maamuzi kwamba turudi ama tupige box na hizi phd zetu,sasa boti litazamaje kabla ya kuanza safari,kikosi cha uokoaji hakuna?

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 30, 2009

    Kaka michuzi hebu fatilia habari vizuri,sisi huku zenj tunajua kua meli ilitoka dar na abiria na mizigo na sio kua ilikua inataka kuondoka ikazama hapahapa. Maelezo yako yananitia mashaka kidogo na habari nilizozipata. Kwa ufupi meli ipo upside-down kwamba mtu anaweza pita juu yake. Askari wa kuzuia magendo (KMKM)na majeshi wanasemekana kuokoa maiti. Asubuhi watu walikua wakizuiliwa wasiingie bandarini ila wakasubiri maiti zao Hospitali ya Mnazi mmoja.
    Mwisho wa yote Captain lazima awajibishwe,kwanza amepakia mzigo mwingi na watu umoumo. Aliona mapema kuwa meli imezidiwa na mizigo akaiondoa ivoivo. Aliomba kufunga gati Forodhani (mchangani) wakuu wa bandari wakamkatalia,sasa yeye ndo anojua hali halisi ya meli,akalizimisha kufunga gati bandari kuu kufuata matakwa ya mabosi,huku akijua kwa yakini meli iko hatarini. Alitakiwa afunge ukouko mchangani watu wangeweza kuokolewa wazima na meli isingezama,isingeweza kua upside-down. Ni mzembe awajibishwe.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 30, 2009

    Jamani mimi naona wengine ndio mmesahau hata kusoma Kiswahili! Imeandikwa kazi ya kuopoa Maiti na sio KUOKOA maiti! Nafikiri nivizuri kusoma mara kadhaa kabla ya kurusha dongo! Kuopoa ni kutoa kitu chochote kilicho zama majini! Kumbe maiti iliyozama majini inaopolewa!
    Michuzi asante kwa taarifa, tunasikitika kwa wenzetu waliopata ajali hiyo mbaya.
    Mungu awalaze pema peponi. Amina.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 30, 2009

    Enyi wajuzi
    Misupu asema kazi ya kuokoa maiti inaendelea hiyo ni lugha sah
    Kuokoa ina maana pia ya kitendo cha ku-recover,kuondoa.ku-recoup
    Sahau atamaduni wa lugha, sisi tuna ndugu. jamaa na marafiki huko visiwani,tupe habari zaidi utuondolee hofu
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 30, 2009

    Siajaona sehemu iliyoandikwa MWELI;
    Na kilichoandikwa ni kuopoa na si kuokoa. Please try to serious!!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 30, 2009

    Inamaana ilikuwa haijaanza safari? Imezama ikiwa kwenye gati? Tueleweshe tafadhali

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 30, 2009

    poleni
    nikwanini hizi ajali za vyombo vya usafiri ziwe kwetu kila siku? wakaguzi hakuna?

    mbomu umelipuka tena mbagala na wanajeshi 7 hoi! taitizo ni ukaguzi...

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 30, 2009

    Hivi jamani kwanini mnaonekana kushangaa sana ajali zinapotokea? To be honest mm sishangai wala sishtuki ajali zinapotokea kwani ninaona namna tunavyoendesha mambo yetu kama maigizo vile hatuko seriuos hata kidogo.No one cares kutoka kwa wandesha baiskeli; magari;meli;ndege na wengine so kutokutarajia ajali ni sawa kukumbatia maji kwenye kiganja kama jiwe;

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 30, 2009

    Ina lillahi wa ina ilaihi rajiun .

    kaka michuzi kwanza hongera kwa kazi nzuri unayoifanya .

    habari imetushtuwa sana lakini tumekuelewa 100% hapa kuna wachache inaonekana inaonekana hawajanufaika na muungano mpaka kesho ! kwani moja katika faida za muungano ni kujua kiswahili.

    kaka michuzi kazi nzuri sana keep it up !

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 30, 2009

    Ajali ya kusikitisha na imetokea bandarini!!!! Kwanini abiria hawajaokolewa kabla? Watu wanazama wakiwa bado wako bandarini... haileweki kabisa! Mwenye boti na wafanya kazi walikuwa wapi? Serikali ilikuwa wapi? Ni kosa la nani hili?

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 30, 2009

    Wewe anony wa 9:39 lazima usome hayo maandishi kwa umakini kabla ya kuropoka! Michuzi amesema Kuopoa maiti, ambalo ni neno sahili! Wewe ndio unamakengeza katika kusoma.

    Michuzi ukipata majina tafadhali yaweke kwenye blog.

    Tunashukuru kwa juhudi zako za kutuhabarisha.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 30, 2009

    Inna lillah wa Inna ilaihi rajiun...Tunakuomba Mkuu wa wilaya ya nanihi utuletee khabari hizi kwani siye huku sweden tuntaabika hatujajua kama jamaa zetu wamo au hawamo...Halafu hapo wadau juu Nanihi ameandika KUOPOA SIO KUOKOA SOMENI VYEMA K-U-O-P-O-A

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 30, 2009

    Msishindane kuhusu matumizi ya maneno. Tuna ajali hapa na kuna watu wamefariki. Tujadiliane kuhusu vipi tunaweza kusaidia ili ajali namna hii isitokee tena. Ni ajali mbayo ingeweza kuepukwa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...