mabaki ya mabomu ya mbagala
Kesho kuanzia saa tisa alasiri Jeshi la Wananchi litalipua masalia ya mabomu yaliyobaki katika ghala la jeshi hilo katika kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), 671 Mbagala kuepusha uwezekano wa mabaki hayo kuleta madhara zaidi.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi amesema leo kwamba kazi hiyo itafanywa na wataalamu wa Jeshi na hakutakuwa na madhara yeyote kwa watu kwani yatalipuliwa kiufundi.
Lakini alisema watu itabidi kuanzia muda huo wakae mita 500 kutoka eneo la Kambi hiyo.
Kiasi cha watu 25 wamepoteza maisha yao katika mlipuko huo wa mabomu uliotokea wiki iliyopita, na mamia walijeruhiwa. Takriban watoto 200 walipotezana na familia zao, ingawa hivi sasa karibu wote wamerudi makwao.
Mh. Mwinyi amesema wananchi wasiwe na wasiwasi kwani zoezi hilo litafanyika kwa umakini. Amesema kwanza kabisa kutakuwa na milipuko miwili midogo kwa ajili ya kutoa tahadhari. Baada ya hapo amesema itafuatia milipuko mingine ya mfululizo ya nguvu kiasi hadi saa 11 jion.
Mh. Waziri wamewaomba wananchi waondokea maeneo hayo na kuwa umbali wa mita 500 kutoka kambi ya Mbagala na kusisitiza kwamba wananchi wasiwe na hofu kwani zoezi litaendeshwa kwa utaalamu. Silaha zitakazoharibiwa ni pamoja na masalia ya risasi, baruti, viwashio na mabomu ambayo hayakuweza kulipuka siku ilipotokea ajali.
Mh. Mwinyi amesema mabomu 75 ya kutupa kwa mkono aina ya Stick hand grenades na dazeni kadhaa za viwashio pamoja na fyuzi zake zitateketezwa. Alisema mabomu hayo inabidi yaharibiwe eneo hilo kwa sababu yanaweza kulipuka wakati wa kuyahamisha na kuleta madhara kwa watu watakao yahamisha.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, John Lukuvi alisema wananchi waendelee na kazi zao kama kawaida kwani zoezi hilo halitaweza kuingilia kazi za watu.
Lukuvi alisema hata wanafunzi waendelee kwenda shule kama kawaida na kusitokee kisingizio chochote cha wanafunzi au watu kushindwa kwenda kwenye shughuli zao au shuleni.
Naye Mkuu wa Usalama wa JWTZ, Brigedia Generali Paul Mella alisema kambi ya Mbagala ina wanajeshi 200 ambao watasaidia kuwaelekeza wananchi kabla ya ulipuaji wa mabomu kuanza.
kama ni utaalam kwa nini wasi-dismantle tuu na kutumia baruti katka shughuli nyengine?
ReplyDeleteNatumai wamewatangazia wananchi kwenye vyombo vya habari,Tunamuomba Mwenyenzi Mungu awasaidie waliokumbwa na hili janga.
ReplyDeleteMh Luku, haya madude yalipolupuka ulisema ni tukio la lwaida, sasa leo wataalamu wanasema watu wake mita 500 badala ya kusisitiza hilo unasema waendelee na shughuli? Kwa hiyo maa ntilie wa kambini aendelee na biashara tu. Haya mambo ya kiutaalamu na politiki mbalimbali jamani, angalia usijeukakuta unayameza maneno yako mwenyewe!Tueleze mmejipangaje, unakumbuka juzi watu wengine walikuwa wanakimbilia kuona yanavyolipuka?
ReplyDeletehapo watu wametaadhalishwa lkn wengine watataka washuhudie kimtindo na hivyo kujificha maeneo ya karibu ili kuona kinachoendelea.
ReplyDeletenaomba kusitokee na makosa yeyote na kufanya mwelekeo wa utokomezaji wa hayo masalia kuleta kimbembe kingine.
afadhali wameamua kuyaangamiza maana ni ya zamani mno na yashachoka sana kwa jua kali la bongo.next time watafute njia ya kuhifadhi "kiutaalamu" ardhini.
Utawala wa Obama una mambo mengi ya kujifunza toka Tanzania.
ReplyDeleteinamaana hamna namna nyingine ya kuya disarm mpaka kulipua???
ReplyDeleteBREKING! AU BREAKING MZEE MITHUPU????
ReplyDeletePamoja na kuyalipua, nafikiri cha msingi wafikirie zaidi juu ya uhifadhi wa hayo makombora. Mambo ya kuendelea kuyahifadhi kwenye maghala ya bati, siamini kama ni sahihi. Security is always expensive, waanze kuyahifadhi kwa njia za kisasa zaidi, surely ACs should be involved...
ReplyDeleteMKUU WA MKOA NI WILLIAM LUKUVI NA SI JOHN LUKUVI MISUPU UWE UNA EDIT COMMENTS YA WADAU
ReplyDeletemkuu wa mkoa Dsm ni William Lukuvi na sio John Lukuvi
ReplyDeleteHabari mhemishiwa Michuzi,
ReplyDeleteMimi nilikuwa na ushauri wa bure kwa huyu muheshimiwa waziri aliyetoa hii taarifa. Hii issue iko very sensitive na watu bado wana hangover na wasiwasi mkubwa ya yale malipuko ya awali. Mh. waziri alitakiwa kuhoji alipoombwa na vyombo vya usalama kwenda kutoa hii taarifa kwa vyombo vya habari kwamba kwa nini iwe ni masaa kadhaa kabla ya tukio...hapa namaanisha taairfa ilitolewa jana mchana tukio linafanyika baada ya masaa kama 14 hivi. Ukiangalia huu muda hautoshi na tayari wameshasababisha kizaaza kwa wakazi wote wa Mbagala na maeneo ya jirani. Imagine milipuko ya kwaza ilikuwa ya mabomu madogo kutokana na kauli za vyombo vya usalama na sasa hivi wanataka kulipua mabomu yaliobakia zaidi ya sabini ambayo mengine ni makubwa sana.....tayari wananchi ambao hawana hata sehemu za kukaa mpaka leo hii watakuwa wameshathiriwa kisaikolojia ...
Tujifunze basi wakati mwengine kutoa taarifa za mambo nyeti na ya hatari kama haya mapema at least siku tatu kabla ili kwa wale wanaoumwa magonjwa kama presha waweze kuondoka kabisa maeneo haya kwa kipindi hicho...
Watanzania lini tutubabalika?
Nawasilisha,
KK
SWALI
ReplyDeletemtikisiko hautakuwa mkubwa ikibidi watu wakae nje ya majengo marefu??
nilisikia sababu ya ku-disharm izo roketi nzito za kivita VIMEPATA MTIKISIKO/DISTURBANCE (yan yamechanganyikiwa ivi) KUTOKANA NA KULIPUKA YALE MABOMU,SO HAYAKO SALAMA HERI WAYALIPUE.
nawaheshimu wajeshi,,
mh!!!!!