HABARI KUTOKA ZANZIBAR ZINASEMA KUNA MELI YA ABIRIA IITWAYO NA MIZIGO INAYOSEMEKANA INAITWA MV SPICE IMEZAMA MAJIRA YA SAA TANO USIKU HUU WAKATI IKIANZA SAFARI TOKA VISIWANI KUELEKEA DA NA INASADIKIWA KUNA MAAFA.
JUHUDI ZA GLOBU YA JAMII KUPATA HABARI ZA UHAKIKA ZINAENDELA NA TUTAJULISHANA MARA MOJA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 30, 2009

    Pilato wa Buguruni jana aliisambaratisha ndoa ya Deo na Joyce Msilanga,baada ya kuridhika kwamba kitendo cha Joyce kumng'ata ulimi mwanaume mwingine wakiwa kwenye penzi ni cha aibu.

    Hivi karibuni, kituo kimoja cha televisheni kiliripoti kwamba mwanaume mmoja (jina kapuni) wa Jiji la Tanga aling'atwa ulimi na mwanamke baada ya kunogewa na utamu wa penzi.

    Kamanda wa Polisi mkoani Tanga alidai mwanamke huyo alimng'ata mwanaume ambaye siye wake akiwa kwenye nyumba ya kulala wageni .

    Kufuatia tukio hilo, mumewe Joyce ,aliamua kwenda mahakamani kufungua kesi ya kuomba kuvunjwa kwa ndoa yao kwa kuwa mkewe amemdhalilisha kwa ndugu, jamaa na marafiki zake.

    Ombi hilo alilifikisha Mei 13 mbele ya Hakimu, Jamila Massengi kutokana na tukio hilo la aibu ambalo alidai hawezi kulivumilia kwa hali yoyote.

    Mkewe alipoitwa kwa pilato na kuulizwa kama aliridhika na maamuzi ya mumewe, alikubaliana na maamuzi hayo na kutaka wagawanyishwe mali walizopata wakati wa ndoa yao iliyofungwa Kikristo mwaka 2003 na kujaliwa kupata mtoto mmoja.

    Ndipo mahakama ilipoanza kusikiliza maelezo ya kila moja hadi kufikia uamuzi wa kuvunjwa kwa ndao yao na iliamua wagawane mali ambazo walipata wakiwa ndani ya ndoa na kuamua mtoto abaki kwa Sangu kwa kuwa mwanamke huyo hana kazi.

    Awali, mumewe huyo alidai mbele ya pilato kuwa aliamua kumpeleka mkewe mkoani Tanga kwa ajili ya masomo ya uteacher,lakini badala ya kusoma aliendekeza zinaa na hivyo kushindwa kumaliza masomo.

    NDO MAANA MUNGU ANATULAANI

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 30, 2009

    poleni sana.tuombe salama kwa abiria au wafanyakazi wa meli.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 30, 2009

    Inna lillahy wa inna ilayhir rajiun ..

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 30, 2009

    Asante kutuhabarisha habari hii mbaya.Mungu asaidie, maana kama ni usiku huenda jitihada za kuwaokoa zikashindikana. Ni meli gani na inabeba abiria wangapi?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 30, 2009

    Mwanakijiji alisha zungunzia sana maswala haya, Bahada ya milipuko ya mabomu Mbagala.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 30, 2009

    Tunasikitika kuwatangazia ajali mbaya ya meli ya mizigo (Spice) ambayo ilikuwa ikitokea Zanzibar kuja Dar. Inasemekana kuna idadi kubwa ya watu waliopoteza maisha

    ReplyDelete
  7. mdau, umanganiMay 30, 2009

    ni mv spice ya mizigo, ila wanasema ilikuwa na abiria lukuki. Mola saidia

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...