hali ilivyokuwa katikati ya jiji la dar maeneo ya posta mpya leo mchana. ni hali ya kukatisha tamaa hasa kwa wenye magari, na hata waenda kwa miguu kwani barabara ni finyu na daladala ni nyingi kiasi hata hamna raha. nini kifanyike kupunguza kama si kuondoa msongamano huu?
Home
Unlabelled
Dar leo mchana
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


hio ndio raha ya public kukontrol public transport ndio maana madalala yote au usafiri hauna time maalum kila daladala linataka abiri,sasa ni nani wa kumlaum
ReplyDeleteMichuzi wenye MJi hawakuwepo nini au unajuwana nao Mitaani? hahaha naona unajifanya kuoneshea ROLEX au Jolex hiyo za TAIWANI, MICHUZI unavunja sheria za njia njia ya mapambo ya Miti wewe unapita kwa miguu tutakupiga Fine Wadau. Pazi.
ReplyDeleteMichuzi umelipia Kodi yakutembea hapo?
Mtaa wa Azikiwe Posta Mpya uwe 'exclusive' kwa daladala kati ya saa moja asubuhi mpaka saa moja jioni kuanzia jumatatu mpaka ijumaa (yaani siku za kazi).
ReplyDeleteMagari ya familia yatumie barabara za Ohio, Bibi Titi, Ghana, Samora siku hizo wakiwa na shughuli maeneo hayo ktk siku hizo Jumatatu mpaka ijumaa saa moja asubuhi mpaka saa moja jioni.
Usafiri wa jumuia/umma uboreshwe na kupewa kipau-mbele ktk misongamano ya vyombo vya moto.
Nini kifanyike wakati bado tunataka kujenga chuo cha utalii katikati ya mji? Hii ndiyo ingewapa wapangaji wa miji, wizara ya Ardhi changamoto ya kupanua mawazo na kuusambaza mji..sio lazima kila mtu aende kazini downtown maeneo kibao yako wazi na yanafaa kwa ujenzi wa maofisi na idara za serikali...
ReplyDeleteMkuu wa wilaya, una bima ndugu yangu...maana naona unakatisha tu barabara iliyofunga magari...anyway, heko kwa kutupatia hii wadau tujionee. Kwa kifupi, hali hii si njema hata kidogo. Kero hii haijaanza leo, nafikiri siku zinavyozidi kwenda inazidi kuwa kubwa! Tatizo lipo kwa mipango miji, sidhani kama bongo hakuna hela ya kuboresha barabara, at least hata kuwa na Bus Lane. Mabasi yakitengewa njia zao, itasaidia kuondoa foleni zisizo na maana. Ila swali linabaki pale pale, wahusika hawaoni?
ReplyDeleteJamani yan notn looks familiar yani TZ imebadilika sana.I cannot imagine hiyo traffic watu wanashije...sasa hivi are people mindful of time kweli?? Cause kama traffic yenyewe ndio hiyo there is no way you can predict how long will it take you to get somewhere.
ReplyDeleteMabasi makubwa tu yanayobeba abiria kuanzia 45 ndio yaruhusiwe kuingia katikati ya mji.
ReplyDeleteTatizo hili linachangiwa kwa kiasi kikubwa sana na huu mtindo mpya wa madaladala kusimama katikati ya barabara kwa ajili ya kupakia na kupakua abiria
ReplyDeleteSijui wenyewe wanautaje huu mtindo, lakini mimi ningependa niubatize jina la "FISADI STYLE"
Utakuta kuna kituo kizuri kabisa kimejengwa kwa ajili ya mabasi, lakini badala ya daladala kuingia kwenye hilo egesho mahususi, huamua kusimama katikati ya barabara. Na kama njia ni double way, utakuta anakuja mwenzake naye anapaki sambasamba na huyo wa kwanza, Matokeo ndiyo hayo - wanablock njia. Ukiangalia kituo - kiko empty kabisa!
City Council, traffic police, Je tunahitaji World Bank ituambie kuwa hii hali ni ya kupigwa vita?
TATIZO SI BARABARA BALI NI MATUMIZI MABOVU YA BARABARA HUKU TRAFIKI WAKIANGALIA BILA KUWAFUNDISHA MADEREVA MATUMIZI SAHIHI YA NJIA NNE. TULIDHANI BARABARA YA KILWA IKIISHA MSONGAMANO NAO UTAISHA, LAKINI WAPI MSONGAMANO UKO PALEPALE NA WAKATI MWINGINE MAGARI HUTUMIA NJIA ZA UPANDE USIORUHUSIWA, HATA MANGINE HUPITA JUU YA TUTA LINALOTENGANISHA NJIA NNE! HUU NDIO UDEREVA WA TANZANIA HAUNA NIDHAMU.
ReplyDeletetaasisi inayoshughulika na usalama barabarani haiko makini.
ReplyDeleteMbona taasisi ya usalama wa anga wanafanya kazi zao vizuri?
mamlaka husika ifanye kazi na serikali iipe support
kulitakiwa kuwe na bus lane au daladala lane
ReplyDeleteJaman hivi ndio tulivyo wakazi wa Dar;matumizi mabovu ya barabara ndio msingi mzima wa kero hii ya msongamano. Ebu fikiria tunapakia/kushuka daladala popote tunapojisikia,tunakatiza barabara popote pale,tunatupa taka kwa mitaro ya barabarani.Kama abiria hatukai kituoni tunataka daladala ikapakie nini hapo kituoni? Madereva wazembe na wabinafsi wasiotii sheria za barabarani,traffiki polisi wasiozingatia maadili ya kazi na misafara ya viongozi lukuki wenye safari sizizo na mbele wala nyuma na mengineyo mengi yanafanya Dar kuwa jiji lisilo na mpangilio kabisa.
ReplyDeleteWa kulaumiwa ni sisi wakazi wa Dar na vyombo husika katika usimamiaji wa uendeshaji wa jiji letu.
Kama hatuwezi badilika hakika kero hii haiwezikwisha kamwe bali itazidi ongezeka.
.....balabala. kazi kweli ipo. kiswahili kinaharibiwa na mswahili mwenyewe.hasa waandishi.
ReplyDelete