










Timu ya soka ya Watanzania kutoka mjini Houston, Marekani, jana Jumamosi ilifanikiwa kuibana timu ya Watanzania wa mjini Washington DC na kutoka naye sare ya magoli 2-2.
Ilikuwa ni Washington DC iliyoanza kupata bao kunako dakika ya 5 kupitia kwa mshambuliaji wake Geus Tall. Kwenye dakika ya 35, Houston walisawazisha bao hilo baada ya Mudrika Majaliwa kupiga mpira wa adhabu ndogo.
Kipindi cha pili kilianza kwa Washington DC kushambulia kwa nguvu huku Houston wakihofia kukandamizwa na refa ambaye ni mkazi wa Washington DC. Hatimaye kwenye dakika ya 25, Elvis Mnyamuru alitingisha nyavu za wageni.
Haikuchukua muda, mshambuliaji Majawali alisawazisha tena kwenye dakika ya 30. Itabidi Washington wajilaumu kupita kiasi kwani mshambuliaji Majawali alikuwa mchezaji wao kutoka mjini Seattle ambaye walimtema wakati wa kupanga listi nusu saa kabla ya mechi.
Hii ilikuwa mechi ya marudiano baada ya ile ya mjini Houston, Novemba mwaka jana ambapo timu zilitoka sare ya magoli 3-3. Mchezo mwingine wa marudiano inatazamiwa kuchezwa Novemba 2009.
Aidha, Houston walilalamikia uwanja kuwa katikati ulikuwa na mgongo kama wa nyangumi na magoli kama midomo ya papa. Timu ya Houston hata hivyo imepiga hatua kubwa baada ya kuchapwa mabao 8-2 kama vidagaa katika mchezo wa kwanza uliofanyika mwaka juzi.
Baada ya mechi baadhi ya wakazi wa Washington DC walimlalamikia refa wao kwamba hakufanya jitihada za kuhakikisha timu yake inashinda nyumbani. Baada ya mchezo ilifuatia sherehe ya nyama za kuchoma ambayo ilisindikizwa na disko la nguvu katikati ya Jiji ilipofika usiku.
Mgeni wa adabu katika shughuli zote zilizofurika watu alikuwa nanihii.
Nikiripoti kutoka uwanja wa Greencasttle, ni mwandishi wako wa blogu ya jamii.
huyo aliyeweka filimbi mdomoni mbona anafanana na Jay-Z. Jay-Z ndo alikuwa refa??
ReplyDeleteHuyo mrefu kuliko wote hapo picha ya kwanza si mngemuweka pembeni kabla ya kuchukua picha jamani?? manake kawafanya wenzake woote waonekane mbilikimo wakati washkaji na wenyewe warefu!!! huyo hashimu thabit nini!!
ReplyDeletejamani ndugu zangu wa dc tusikimbilie mambo ya aggregate sasa baada ya kutoa droo ya 2-2 mnakimbilia aggregrate?? ningependa kujua ni nani aliyepost hii message kwa michuzi!! manake si mshindani wa kweli bali anataka kufurahisha umati wa watu na wanablog wakati reality ni kwamba mechi imeisha 2-2 na kwa kweli DC wametuaibisha kwa kutupeleka kwenye uwanja mbovu usio na hadhi ya kuwa kwenye jiji kubwa kama lile!!
ReplyDeleteD.C mnahaibisha. Hayo magoli kama yale tuliyokuwa tunachezea shule za msingi bongo !!
ReplyDeletehee hao walikuwa wanacheza rede?? japokuwa sports is not rechable ila hayo mabao ya tobo hayo.
ReplyDeletewewe chururu vipi mbona comments nyingine hutoi wewe vipi wewe,
ReplyDeleteDuuh yote 9 mimi hayo magoli ndio yameniacha hoi kama ya ragbi hata hapa kwetu kisiju tuna magoli mazuri.
ReplyDeletemdau
kisiju pwani
Yaani mlikosa kabisa uwanja hadi mkatumia uwanja wa Rugby?
ReplyDeleteHaki ya nani, wewe anony wa kwanza umechukua comment yangu. Maana refa Jay zee mtupu, kah? Duniani kweli wanne wanne....
ReplyDeleteHapo ndio globu ya jamii inapoleta raha. Habari kama hizi huwezi kuzipata kwenye Uhuru na Mzalendo.
ReplyDeletemleta habari inabidi aende TSJ kusomea uandishi wa khabari!
ReplyDeletekwani haina vionjo vya mwandishi mahiri
Yaani Richard Mawenya (refa) ndo amekuwa JayZ these days? people please, he ain't close to Jay Z. huyo aliyeweka hizo comments lazima is one of his baby mamas
ReplyDeleteWhere the haters at all the hatin cats
ReplyDeleteYeah Look in the mirror nigga hate on dat...HAHAHAHAH!
WABONGO BWANA, KAZI YENU KUSENGENYA 2 ....Yeah let em c me
Hi hater
Pull of easy. Bye Hater
U dont like me? Why hater
Won't U tell em how mad I make ya
I ain't caught up in all da hot talk.....
KAKA MICHU NAOMBA UMPE Hİ NDUGUYANGU AMRANI HAPO MWAMBIE KIPARANG'ANDA ANKUPA Hİ FROM turkey
ReplyDeletekwi kwi kwi
ReplyDeleterefa bila jezi,mmechacha sana
iyo migoli
aya wabeba box
timu ilovaa jezi ya njano namjuwa dedi ruba peke yake wa madison ya zenji.
ReplyDeletePeter Bategeki kikapu vipi? Mbona tunakuona kwenye soka tu.
ReplyDeleteWABONGO WA DC MMECHOKA NA MEMORIAL WEEKEND ILIKUWA MBOVU SANA..MMETANGAZA HUMU FOR A LONG TYME WATU TUMESAFIRI HADI HUKO NYAMA ZENYEWE KAGRILL KADOGO WATU 100....HEBU MJE MASS MUONE TUNAVYOFANYA SHUGHULI ZETU..
ReplyDelete