wa picha zaidi
Rais Kikwete ana kwa ana
na Rais Barak Obama wa Marekani
. Awa kiongozi wa kwanza wa Afrika kukutana na Rais huyo wa Marekani
. Rais Obama asema kuwa inatokana na uongozi ulitukuka wa kiongozi wa Tanzania
. Rais Obama ahaahidi kuendelea kusaidia jitihada za Serikali ya Rais Kikwete kuleta maisha bora kwa Watanzania
. Ataka kuja kutembelea Tanzania wakati wowote Rais Kiketwe akiwa tayari kumwalika
. Awa kiongozi wa kwanza wa Afrika kukutana na Rais huyo wa Marekani
. Rais Obama asema kuwa inatokana na uongozi ulitukuka wa kiongozi wa Tanzania
. Rais Obama ahaahidi kuendelea kusaidia jitihada za Serikali ya Rais Kikwete kuleta maisha bora kwa Watanzania
. Ataka kuja kutembelea Tanzania wakati wowote Rais Kiketwe akiwa tayari kumwalika
Na Mwandishi Maalum, Washington D.C., Marekani
Rais Barack Obama wa Marekani amemhakikishia Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa ataendelea kuunga juhudi za Serikali yake katika kupambana na umasikini na kuwaletea Watanzania maisha bora.
Ili kuhakikisha kuwa ahadi hiyo inatekelezwa ipasavyo, Rais Obama amemwelekeza Waziri wa Mambo ya Nje wake, Mama Hillary Clinton na wasaidizi wake katika Ikulu yake ya Washington kufutilia kwa karibu na kwa makini ahadi hiyo.
Rais Obama ametoa ahadi hiyo leo, Alhamisi, Mei 21, 2009, wakati alipomkaribisha Rais Kikwete katika Ikulu ya Marekani kwa mazungumzo, akiwa kiongozi wa kwanza wa Afrika kukutana na Rais Obama tokea achukue madaraka ya kuongoza Marekani Januari 20, mwaka huu.
Mama Clinton alikuwa mmoja wa maofisa sita waandamizi wa Serikali ya Obama waliohudhuria mazungumzo hayo katika Ofisi ya Rais wa Marekani ya Oval Office.
Wengine waliokuwapo ni pamoja na Mshauri wa Rais Obama wa uchumi, Larry Summers ambaye amepata kuwa Waziri wa Fedha wa Marekani, Mshauri wa Masuala ya Usalama Jenerali James Jones, Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia Afrika, Balozi A.S. Carson, ambaye alipata kuwa mwalimu wa kujitolea katika shule ya Malangali ya Iringa wakati wa ujana wake.
Rais Obama amemwambia Rais Kikwete kuwa uamuzi wake wa kumkaribisha na kumfanya kiongozi wa kwanza wa Afrika kukutana naye tokea kuapishwa kuwa Rais wa Marekani, kunatokana na sera za mafanikio na uongozi ulitukuka wa Rais Kikwete.
“Napenda kukupongeza kwa uongozi wako mzuri wa Tanzania na pia kwa uongozi wa Umoja wa Afrika (AU), hata kama umemaliza muda wa uongozi wako wa umoja huo,” Rais Obama amemwambia Rais Kikwete na kuongeza:
“ Nataka ufanikiwe katika uongozi wako. Niambie unataka tukuunge mkono vipi ili uendeleza mafanikio ambayo Serikali yako imeyapata…Unakuwa kiongozi wa kwanza kukutana nami tokea niingie madarakani. Hii ni ishara ya imani yangu na ya Serikali yangu katika uongozi wako. Ninafurahishwa na uongozi wako.”
Bila kusita Rais Obama amemwambia Rais Kikwete: “Nataka kuja kutembelea Tanzania. Mara ya mwisho niiona Tanzania kutokea upande wa pili wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.”
Ameongeza Rais Kikwete katika mkutano huo: “ Serikali yangu nzima inavutiwa na uongozi wako. Tunapenda kuunga mkono uongozi wako na kufanya kila linalowezekana kufanikisha hilo ili uendelee kuwatumikia wananchi wa Tanzania.”
Rais Obama pia amemsifu Rais Kikwete kwa uongozi wake katika kuboresha elimu nchini, na kumhakikishia kuwa misaada yote ya ujenzi wa miundombinu itakayotolewa chini ya akaunti ya Millennium Challenge Account (MCC) itaharakishwa, ili ujenzi wa miradi hiyo uanze. “Msimamo wako wa kuweka mkazo katika elimu ni mfano usiokuwa na kifani wa uongozi. Hii miradi ya MCC… tutaangalia nini kifanyike ili ianze kutelekezwa haraka iwezekanavyo, na kama lazima tuiongeze.”
Utawala wa Serikali ya Rais George W Bush uliondoka madarakani baada ya kuwa umeidhinisha msaada wa kiasi cha dola milioni 700 kwa ujenzi wa miundombinu katika Tanzania chini ya MCC.
Obama hakusema kuwa ataongeza kiasi gani katika raundi ijayo ya misaada ya MCC kwa Tanzania ama kama anakusudia kukipiku kiasi hicho kilichotolewa na Rais Bush.
Rais Kikwete amempongeza Rais Obama kwa kuendelea kuiunga mkono Tanzania na Afrika, lakini akataka Marekani kuunga zaidi juhudi za Tanzania katika jitihada za kufuta umasikini, kuhakikisha kuwa kuna chakula cha kutosha katika Afrika kwa kuunga mkono jitihada za kuboresha kilimo, kuendelea kuunga mkono jitihada za kuboresha elimu na hasa ile ya sayansi, na kuendeleza mapambano dhidi ya magonjwa ya malaria, ukimwi na kifua kikuu.
Rais Kikwete pia ameutaka uongozi wa Rais Obama kuendeleza na juhudi za kupunguza vifo vya akinamama wakati wa uzazi na kuisadia Tanzania na Bara la Afrika kukabiliana na athari za kuvurugika kwa uchumi duniani.
Viongozi hao pia wamejadili baadhi ya migogoro mikubwa katika Afrika ukiwemo ule wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Darfur katika Sudan, Somalia na hali ya kisiasa ilivyo katika Kenya.
Rais Kikwete pia amemweleza Rais Obama kuhusu jitihada zinazofanywa na Serikali yake kuleta suluhu ya kisiasa katika Zanzibar.
Rais Obama amemwomba Rais Kikwete kuendelea kuwasilisha na Serikali ya Marekani kwa namna ya kushauri kuhusu jinsi gani Serikali hiyo inavyoweza kuchangia katika kutafuta utatuzi wa migogoro inayolikabili Bara la Afrika hasa ile ya DRC na Darfur.
Mapema kabla ya kukutana na Rais Obama, Rais Kikwete leo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mama Hillary Clinton kwenye Wizara ya Mmbo ya Nje ya Marekani mjini Washington.
Mama Clinton alitaka kujua jinsi gani Marekani inaweza kulisaidia Bara la Afrika kuondokana na matatizo yake, na Rais Kikwete ametoa maelezo ya kina kuhusu jinsi gani jambo hilo linaweza kufanikishwa.
Viongozi hao pia wamejadili Kenya na hali ya kisiasa katika Zanzibar na kuhusu migogoro mingine inayolibaliki Bara la Afrika.
Rais Kikwete leo anaendelea na ziara yake katika Marekani kwa kukutana na viongozi wa vyombo vya kimataifa vya fedha duniani.
Ends
aah wewe!!nimeipenda hiyo
ReplyDeleteIts Neyma
obama ana mvi??JK anaweka piko au
ReplyDeleteok ni vema tu tuzidi "kuwasihi donors tu"
asanteni
jamani tuwekeege zile tenzi za nyimbo za "MJOMBA"jina lake sifaham
ReplyDeletekaka analonga yule yan km viongozi wenye akili wanasikiliza na kutafakari na kutendea kazi!!basi inchi itasongoza walao
nisaidien jinsi ya kupata CDs zake
MJOMBA UMEIMBWA NA MRISHO MPOTO; TURUDI KWENYE AJENDA YETU, MJOMBA RUDI NYUMBANI SIKU ULIZOKAA HUKO ZINATOSHA KWANI HATA UKIKAA MWAKA HAZITATULETEA MABADILIKO KATIKA UCHUMI WA NCHI NA MAISHA YA MTANZANIA. KUWA WA KWANZA KUMUONA OBAMA NDANI YA OVAL NI USHINDI USIO NA TIJA KWANI SHNDANO HILO TUMELITUNGA SISI BILA KUWASHIRIKISHA MARAISI WENGINE. JE, MJOMBA UTAKAPORUDI SISI TUTABADILIKA KATIKA MAISHA YETU YA UMASIKINI ULIOKITHIRI?
ReplyDeleteTWO GREAT LEADERS MEETING!! ONLY GOOD CAN COME OUT OF SUCH MEETING. MR PRESIDENT (JK) YOU HAVE MADE US PROUD AS ALWAYS!!! MAY GOD BLESS YOU IN YOUR EFFORTS. WENYE KUSEMA WASEME WEWE TENDA TU!!! WAHENGA HUSEMA SI YULE MWENYE KUKOSOA NDIYE BORA BALI YULE MWENYE KUTENDA AKAKOSOLEWA!! HONGERA MHESHIMIWA RAIS.
ReplyDeleteIMETULIA MKUU. THIS IS 100% PERFECT. Huwa napingana na baadhi ya 'masafari' ya J.K ila kwa hii ni funika bovu.
ReplyDeleteKwa tathmini yangu, na maoni pia, safari za JK kukutana na viongozi wakubwa zina manufaa makubwa sana kwake kama kiongozi na HASA KWA TAIFA LETU ambalo piga ua, kwa WAKATI HUU WA SASA lazima tuegemee misaada ya kifedha na kiufundi ili tusonge mbele.
Tukumbuke pia kabla ya kuosha vinywa mjomba Obama a.k.a shemeji a.k.a jirani lazima atataka 'wake' waige mfano kwetu. So, we must really appreciate this initiative.
JK kaza buti kupigana na ufisadi. Pia nakushauri, ili kujenga siasa ilyo bora, na uongozi wako uwe chachu ya mabadiliko, tafadhali, next uchaguzi usiwapigie sana debe mafisadi ili warudi madarakani. Wapinzani watakusaidia sana wewe na chama.
Enyi wana wa Busanda, msimwangushe JK kwa kumchagulia CCM, bali mpeni mpini wa CHADEMA ili bunge liamke.
Watanzania wenzangu, chonde chonde uchaguzi ujao msimwangushe JK. Mpeni kura za kishindo. Ili kumsaidia zaidi, tafadhali mpeni mipini ya upinzani. Tuongeze idadi ya wapinzani bungeni.
Hongera sana JK. Sasa fanya mpango wa kumkaribisha OBAMA. Nchi itapaa kinoma kimataifa.
Ndugu zangu wake kwa waume... tukazane kwa kutumia rasilimali za ndani kwa maendeleo, ili za nje ziwe ziada ama nyongeza ya kufukia pengo. Uwezo tunao. Tukiondoa mambo ya ubinafsi kwenye mikataba na tukadhibiti madini, utalii, tukawa safi kwenye NISHATI (hapa hata kifikra hatujafunguka), tukaongeza juhudi kwenye kilimo, na mkazo wa pekee kwenye elimu ya juu (maana tuko nyuma, tunakuwa maPS kwa wageni) na SOTE KUPIGA VITA VVU/UKIMWI kwa nguvu zetu zote, tutapaa tu.
Ni hayo kwa sasa mjomba. Sitanii
kaka michuzi sisi wamatumbi umetufanyia kitu bomba sana ahasnte kwa niaba make uwezo wa kusoma unao lakini kutafuta dictionary na kuanza tafsri ya neno moja moja kazi kweli kweli kwa sasa hata mtu akiuliza juu ya msafara wa jk nitamjibu kwa ufasaha nimehelewa vizuri zaidi ubalikiwe kaka
ReplyDeleteJamani kiswahili kumbe kigumu hivi? Rais Barak Obama wa Marekani
ReplyDeletehivi kuna Rais Barak Obama wa nchi nyengine :)
Mdau hapo juu yule aliyeimba MJOMBA anaitwa Mpoto.
ReplyDeleteNimekaa Marekani miaka zaidi ya 10 ukweli ni kwamba America doesn't care about anybody ila wanaofungamana nao....
GoodLuck na misaada, serikali ya marekani ndio ya mwisho kutoa misaada sababu katiba ya marekani hairuhusu ugawaji wa fedha.... Full Stop
Thank God
Mchumi wa Dtown
Why CNN, BBC na zinginezo hazikucover this historical event ya Rais kwanza mweusi wa Marekani kukutana na Rais wa kwanza wa Kiafrika tangu alipoingia madarakani?
ReplyDeleteWHAT A VISIT! I AM PROUD OF MY PRESIDENT KIKWETE. YOU ARE A GREAT LEADER. TUKO NA WEWE MZEE NA TUNARIDHIKA SANA NA UONGOZI WAKO. MAY GOD BLESS YOU SIR.
ReplyDeleteEcho November
.....
THE WHITE HOUSE
Office of the Press Secretary
_________________________________________________________________
FOR IMMEDIATE RELEASE May 21, 2009
Readout on President Obama’s Meeting with President Kikwete of Tanzania
The President and President Kikwete met this afternoon and had a valuable discussion on a range of issues. President Obama expressed his appreciation for the close bilateral relationship the United States shares with Tanzania. President Kikwete and the President exchanged views on approaches to enhancing the U.S.–Tanzanian partnership, improving development policy in the fields of health, education, and agriculture, and working with other partners in the region to solve some of the most pressing conflicts on the African continent. President Obama and President Kikwete expressed a desire to work together to solve common problems in the future. This was the first African Head of State to visit President Obama at the White House.
To view a high resolution photo of the President’s meeting with President Kikwete of Tanzania, click HERE.
mi ninavyojua marekani wamemwaga hela nyingi sana hapa tanzania kwenye afya hususani HIV/AIDS, education ni kidogo angezungumzia hilo kwa sababu ukimwi tanzania unaharibu ingawa kuna dawa za kupunguza makali lakini bado! Nafikiri angelisemea hilo pia.
ReplyDeleteHongera zake kwa kuwa wa kwanza kukutana na Obama!
HONGERA KK NAONA UKO MATAWI YA JUU.
ReplyDeleteILA KK MAMBO YA BULLET PROOF VEST YA NINI UMEJAJAAA ...UKO WHITE HOUSE ULINZI NI FULL KUJIACHIA...WASHAURI WAKO HAWAKO MAKINI...
JK ungesafisha serikali yako kabla mshikaji hajaja ingekuwa bomba kweli, maana du kwa sasa hivi kwa kweli ni aibu kweli kweli.
ReplyDeletehello... hapi blogging... have a nice day! just visiting here....
ReplyDeleteWatani wa Jadi naona watajinyonga kwa wivu!
ReplyDeleteYANI MAREKANI WAAKIKISHE NCHI YETU INA CHAKULA CHA KUTOSHA? AU NIMESOMA VIBAYA KAULI YA JK?
ReplyDeleteMhhhh mwandishi bwana, enheee
ReplyDelete"Ataka kuja kutembelea Tanzania wakati wowote Rais Kiketwe akiwa tayari kumwalika"..
Huyo KJ si angemuambia ht tuongozane wote home saiv kwa jinsi misifa ilvyomjaa...
HAYA JK PIGAKILUNGU CHA MAANA NAAMINI ALIVYOKUONA TUU ALIMKUMBUKA MAREHEM BABA YAKE.SASA KUWA MATONYA WETU ILI ZITUSAIDIE UKO KWETU
ReplyDeleteKILA LA KHERI JAKAYA NRISHO CHIKWETE
MUNGU NISAIDIE NISIJESHAWISHIKA KUWA MWANASIASA-AMIN Mdau Majuto-Uswidi.
ReplyDelete"Nchi masikini haiwezi kuendelea kwa kutegemea misaada kutoka nchi za nje" haya sio maneno yangu.
ReplyDeletesijui sisi watanzania ulemavu wetu upo wapi. nikisema kwenye miguu watu watasema we mwongo mbona mabarabarani wanaotembea kwa whealchair, magongo,crow, n.k. ni wachache sana. wasio na mikono watasema mmh! mbona nao ni wa kuokoteza. macho! hapa watanishushua mbona idadi ya wanao piga CHABO ni kubwa mara mia zaidi kuliko wateule.
Sasa wadau hebu tudiscuss ulemavu wa UBONGO labda hili ni tatizo (msimind cos sina uhakika na mental capability yetu)tukiachana na wale wanaotembea uchi barabarani...
haiingii akilini hata kidogo kila uchwao kiongozi wa kitaifa akitoka tu nje ya nchi anashika KARADASI/DAFTARI, PICHA NA KALAMU.
Lumbo
Arusha
dah.....politiki bwana!!!!..eti kiongozi wa kwanza kukutana na Obama..so what?
ReplyDeletehahahaha ukiangalia hiyo picha kwa makini unamuona Kikwete anasalimia kwa uoga hapo, hajiamini anapokutana na wenye dunia.Angekuwa mdau Nyerere hapo, unegona confo alilonalo Nyerere yeye haangalii kama ni rais wa wapi, anajiamini kwa kuwa ni the best.
ReplyDeleteSasa mdau michuzi unaposema Kikwete amekua rais wa kwanza afrika kuonana na Obama SO WHAT???Mbona Ghana hawajatamba kwa Obama kufanya ziara huko July
Tangu uwe Raisi angalau dunia inajua Tanzania iko wapi kama wakati wa JKN. Viva president JK na Mungu akulinde siku zote.2010 uendelee kuongoza TZ. Amen
ReplyDeleteMdau
London
mungu akubariki Rais wetu jk pamoja na rais obama!!!
ReplyDeleteMungu ibariki Tanzania!
Mungu ibariki Africa!
Mungu ibariki America na dunia!!
Mdau canada.
mdau wa 3:33, nani kakwambia Ghana hawajatamba kuwa anakwenda kwao???umeshaingia kwenye mitandao yao wanavyojidai kuhusu Obama kwenda kwao!!JK usijali bwana nchi yetu unaiweka juu na watu kwa sasa wanakukubali...wanaobwabwaja ni wachache kama ulivyosema ...kelele za wapangaji hazimzuii mwenye nyumba kupata usingizi mnonno.Keep it up Our Hon...presidaaa... u rock man.
ReplyDeletemdau Oxford,UK.
Hii kitu ilafanya wakenya waanze kulalamika kuwa tunataka kuanzisha propaganda za kuwa baba yake Obama alitoka "Tanzania" na siyo Kenya. Yaani JK kawapiku wakenya kuwa wa kwanza kushikana mkono na Rais Obama?, watasema mboa alipokuwa senator hatukujishughulisha naye.
ReplyDeleteIla mimi kinachonishangaza hapa ni kwa nini hii statement ya "JK kawa kiongozi wa kwanza toka Africa kukutana na Obama" imewekewa msisitizo sana? why? why?
Ukisoma kwa makini hizi comments inaonyesha wazi kuna watu ambao wako nje ya Tanzania roho zinawauma kwanini nchi amabayo wameikimbia inaanza kunyanyuka na watu wakepamoja na raisi wao wako bomba na hawana mzaha katika kutafuta maendeleo na maisha,hivyo basi wanaogopa watashindwa kutafuta sababu kwanini wamekimbia nchi na kuenda kuishi kwenye nyumba ya chumba kimoja ulaya au kwanini wameenda kuoa vibibi vizee umri sawa na mama zao.Ukweli ndugu zangu mtake msitake Tanzania inabadilika sasa hivi kama unashule yako na uko makini maisha ni bomba sana na huhitaji kuja huko tutakuwa tunakuja kuwatembelea tu lakini mambo yote nyumbani ni nyumbani na sio mahali ambapo ni second class citizen.Hiyo elimu tutakuja kusoma huko huko lakini tutarudi home kuendelea na maisha bomba na yenye heshima.Kwa hiyo hata mkisema vipi ukweli ni huo mtake msitake nyumbani ni kutamu jamani.Mwacheni JK awakilishe!
ReplyDeleteheeeee
ReplyDelete"balozi A.S CARSON ambaye alipata kuwa mwl wa kujitolea..shule ya malangali-Iringa wakati wa ujana wake"
aisee shule nilojitolea pia mie duh!mwaka gani alijitolea uyu mzungu?ngoja niaze kutafuta zile contacts za volunteerz nilokuwa nao uko nyuma
who knows??
asante
ndio maana yake annon
ReplyDelete"kuhakikisha kuna chakula cha kutosha ktk afrika"
"ameiona tanzania katika pande ile ya serengeti"
ReplyDeletejamani??wakenya ni wakenya tuuu
sasa ndo nini maasai mara au the great serengeti??
ovyo kabisa,ata asipokuja aende uko kwanza yeye pia ni moja ya watani wet
kaka michuzi habari za saa hizi.
ReplyDeleteme ni mdau wa blog hii tokea ikiwa na miezi miwili. naishi moshi na ningependa kukupa matokeo yanayojiri mjini hapa.. hivyo ombi langu ni kuwa ripota wa mji huu.
maadili kuzingatiwa(sio msaada tutani)E-mail kilinjaro@yahoo.com
JK ACHA MASKHARA IMEKUWA WIMBO WAKO UKIENDA NJE ZANZIBAR ZNZBAR MBONA HATUONI ULICHOTATUA?
ReplyDeletesorry kaka u may put kili.njaro@yahoo.com
ReplyDeleteSwali langu ni kuwa!! Kwanini huyu jamaa anajiona kama Mungu? Eti nimeamua kukufanya kuwa aisi wa kwanza kukutana nami baada ya kuaishwa kwangu... for how long are we going to worship these people!!?
ReplyDeleteI am sick and tired of this really!!
Kama raisi Kikwete alikuwa anapanda mlima mrefu,sasa amefika "kileleni" kilichobakia kuutundika mwenge na bendera ya taifa letu kabla hajashuka mlimani.
ReplyDeleteHeshima ya kuwa kiongozi wa kwanza bara la Africa kukaribishwa na raisi Obama inatokana na uongozi wake wa amani na msimamo mzuri wa kazi za wizara ya mambo ya nje.
mickey@mail-online.dk
Denmark
Hakuna lolote....hapo ni mwendo wa kutembeza bakuli tu!
ReplyDeleteMimi nina swali,kwani walikuwa wanaongea nini?kuna mtu anajua ama anayo transcript yaliyo ongelewa na rais Obama? naomba utuanikie na sisi tupate kuisoma.
ReplyDeleteAu picha zilizo kuwa posted hapa zinatosha kueleza kila kitu
it wasnt official people,thats why it didnt have any media coverage watsoever. mzee waku force king,shikamooo
ReplyDeleteKuwa kiongozi wa Kwanza kukutana na rais Obama itaisaidiaje Tanzania.
ReplyDeletePia anataka USA isaidie Tanzania katika vita vya kuondoa umasikini wakati vita hivyo hata yeye Obama anapigana navyo nchini kwake.Vita vya umasikini ni vyetu wenyewe watanzania na tusiwape mzigo watu wengine kabla ya kuhakikisha tunapambana na mafisadi vita ambavyo vinawezekana lakini inaonekana CCM na Serikali yake wanaficha na wemeshindwa vita hivyo sasa mtu kutoka Usa atatusaidiaje.....Hahahahaha Tanzania nchi yangu na mawazo mafupi ya viongozi wetu
mkullu bwana alijua jamaa democratic atavaa tai ya blue na akajiwahi,kwikwikwi
ReplyDeleteNakufagilia JK BIG UP,KIdumu CCM
ReplyDeleteMdau wa May 22, 2009 8:19 AM ningependa umtafute Mpoto mwenyewe umpe contact zako ili akufikishie mzigo wako,vinginevyo hela yako itaishia kwa pirates tu na jamaa atachelewa kupata nauli!
ReplyDeleteNi tukio muhimu sio siri lakini hawa jamaa zetu hawatuthamini kiivyo, kwani ilitakiwa kwanza Rais ampokee rais mwenzie pindi anapozuru nchi husika kwa safari ya kiserikali(nakaribisha changamoto)
Ila ka mtazamo wangu nadhani hakuna kikubwa sana cha kujivunia hapo maana tuna uwezo wa kujitegemea tukitaka. Kwanza tuwadhibiti wezi na mafisadi ambao tunawajua ila serikali haijawafahamu bado tukiweza hilo basi tujitokeze vifua mbele tukilinga,ila kama tukishindwa hilo tusitokee kabisa mbele maana hatuna cha kuonesha. Sio kuishia kufunga mahakimu wadogowadogo tu,tuwashughulikie hawa jamaa na hutumia maliasili zetu sio kuwapa wawekezaji wa kigeni kwa mikataba mibovu huku viongozi wetu wakiambulia tuhela twa vocha tu. Tutaweza kujivunia siku tutakapofahamu kwamba utumishi wa umma si njia panda ya utajiri bali ni utumishi wa umma
Bro, Michuzi nakupongeza sana kwa kutuletea habari na picha nzuri kama hizi. Na kuomba Mungu blog yako ikue mpaka watu wote hadi kina kikwete waweze kusoma yale yote watanzania wanayolia nayo. Kiukweli kweli ni poa kuona Kikwete ndani ya nyumba kama rais wa kwanza wa afrika kukutana na Obama. Mambo yaliyozungumziwa ni ya maana lakini tukumbuke maendeleo ya mtanzania hayaji kwa msaada peke yake. Misaada mingi inayokuja bongo haitumiki ipasavyo, story ni nyingi sana kila msaada unapotua bongo. Sisi bado tupo nyuma masikini na sijui lini tutasonga. Hebu angalia, toka mbagala imepata matatizo, mpaka leo hakuna kinachoendelea watoto wamekaa chini wanafanya mtihani , Raisi yuko marekani ziarani. Naungana na mchangiaji wa 4, endapo Rais atarudi bongo na watanzania wabadilike kimaisha poa, otherwise sioni sifa yoyote kwa Kikwete kuwa wa kwanza in the white house
ReplyDeletemadau aliyesema hajaona cnn wakitangaza kuhusu Kikwete kuja kuonana na Obama. yaani wewe unataka cnn na bbc watangaze umatonya wa Kikwete au? mi nafikiri tungesubiri, Obama aje bongo kwanza ili aendelee kuitangaza bongo...
ReplyDeleteTarehe May 22, 2009 5:48 PM, Mtoa Maoni: Anonymous inaelekea tofauti kati yako na wadau unaowataja wa ughaibuni ni kwamba pengine wewe unajiangalia hali yako binafsi ilhali walioko ughaibuni wanaangalia hali ya nchi nzima.
ReplyDeleteUnasema nchi imeanza kunyanyuka lakini hili sio geni. Ilianza kunyanyuka toka ilipopata uhuru, ndio sababu kuna kipindi ilikuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza duniani kwa kufuta ujinga. Karibu kila Mtanzania alikuwa anajua kusoma na kuandika. Angalia sasa hivi. Tunatamba kwamba tuna madarasa zaidi lakini vile vile tuna Watanzania wengi zaidi ambao hawajui kusoma wala kuandika. Mbagala mpaka leo hii Watanzania wenzetu wanaishi maisha ya kubahatisha baada ya kupoteza vitu vya thamani kwao. Wakazi wa Kipawa wamelazimika kumng'ang'ania mkuu wa wilaya aone maisha yao yalivyobadilika na kuwa ya kubahatisha kwa ahadi zisizotekelezwa. Hata suala la kujilisha Rais wetu imebidi akammatonye Obby kujaribu kujiokoa nalo. Ya mikoani hata kuyajua inakuwa vigumu. Nikimnukuu mmoja wa viongozi wa chama fulani aliyekuwa akipiga kampeni Busanda, habari za vyombo vya habari binafsi zenye kutoa sifa mbaya kwa chama chake haziwafikii wananchi wa Busanda kwa kuwa hawana umeme.
Hayati Osagefyo Kwame Nkrumah alisema pasipo Afrika yote kuwa huru hakuna nchi ya kiafrika inayoweza kusema kwamba iko huru. Kwa mtizamo unaofanana na huo, kama umezungukwa na umaskini si halali kusema kwamba umejitoa kwenye umaskini. Kurekebisha maisha binafsi kwa kutegemea hela za madona kunasumbua dhamira za wengine ndio wanaona bora wapige boksi.
Huyu Kikwete nae kazidi. Kila leo yuko White house. Na huyo anayesema kuwa marekani imetoa misaada mingi sana kwa TZ hasa kwenye secta ya afya, did u get to know the conditions behind those misaada au unasema tu? Ni heri mara 100 kutotupa misaada kuliko kutupa misaada yenye masharti yanayoizidi hata hiyo misaada yenyewe. Nchi yenyewe bado masikini, halafu hawa wamarekani wanaleta zao eti oo misaada lazima kwanza watu wapunguzwe makazini. Now do u call this msaada au biashara?
ReplyDeleteA.S carson.,alikuwa mwalimu malangali,haha safi sana,shule yangu hiyo bwna nilipiga advanced pale.mdau UK
ReplyDeletemichuzi unajirusha sana bwana,kama utaki urudishie pesa zetu.
ReplyDeleteMichuzi unalala sana bwana aaa.Tusha zoea 1*3 kila siku.
ReplyDeleteUkitaka utaratibu wa itifaki za White House kong'oli hapo chini:
ReplyDeletehttp://www.state.gov/s/cpr/what/c18027.htm
Ukishasoma yaliyomo kwenye hiyo linki ndiyo utajaza kama ziara hii ilikuwa really au bosheni.
Michuzi, umebania au JK hakupigiwa mizinga 21? Hawakuimbiwa Mungu Ibariki ya Kibongo wala ya Kinyamwezi? Hakuandaliwa dhifa ya kiserikali (State banquet)? Vipi hakutembezwa wala kufanya joint press conference kwenye Rose Garden?
Mwanawane Michuzi, weka mipicha ya mizinga 21, dhifa ya kiserikali tuwaone kina JK, Membe and the delegation wakiwa wametinga kwenye maboo tai na toksido suti huku wameshikilia viglasi wakijichanganya na vigogo wa White House. Halafu kukata mzizi wa fitina tuletee picha ya JK na BO kama ile ya Mwalimu na Kennedy wakiwa kwenye Rose Garden. Mwanawane, hapo waosha vinywa utakuwa umewafunga magoli 100 kwa bila.
Hongereni sana, raisi wetu ndio raisi wa kwanza wa kiafrica kukaribishwa White House na Obama...... pia raisi wa kwanza wa kiafrica kuikaribisha Real Madrid...... Raisi wetu handsome bwana, raisi wetu anajua kusmile bwana, raisi wetu anajua kuvaa bwana........
ReplyDeleteKwanza kasaini kitabu cha wageni...pengine asubuhi kabla ya kuonana na Obama.
ReplyDeleteWakati huo kavalia tai tofauti na hiyo aliyovaa wakati anakutana na Obama!
La sivyo, huo muda wa kufika na kuzungumza...Rais wetu hawezi kupata nafasi ya kubadili shati na tai...pengine shauri ya jasho!
Hivi Mama salma naye alikuwepo kwenye hayo mazungumzo? Maana naona kuna kitenge mkono wa kushoto hapo chini.