Kikundi cha kwaya  kutoka kanisa la Azania Front la hapo Dar  kipo hapa katika jiji letu la Dallas. Kwa kweli kikundi hiki kimetoa burudani ya hali ya juu katika kanisa letu la  Umoja pamoja na kanisa la wamerikani ambao walikuwa wanashangilia kama wabongo. 

Kikundi hiki kimeweza kutangaza nchi yetu vema katika jiji la Dallas pamoja na jiji la Oklahoma ambako nako wamefanya vitu vya nguvu. Leo jioni kutakuwa na dhifa maalumu ya kuagana nao katika jiji letu tayari kurudi katika jiji la Oklahoma ambako watafanya maonyesho kadhaa kabla ya kuingia ndani ya pipa tarehe 8 na kurejea nyumbani.

Mwisho kanisa la Umoja linapenda kuishukuru  jumuia ya watanzania hapa dallas chini ya mwenyekiti wetu Saimon Nkanda kwa msaada wote waliotoa kuhakikisha kila jambo linakwenda vizuri.

 Siku zote Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
 Pastor Abisalom Nasuwa
 Umoja International Outreach Church
 12727 Hillcrest Rd,Dallas Texas 75230
 Email:umojachurch@yahoo.com
 Tell:214 554 7381

Kwaya ya Azania Front ikiwajibika kiutamaduni
Nyuso zinaonesha furaha
wanakwaya wa Azania front wakiimba Dallas
wametia fora kwa unadhifu na uzuri wa nyimbo zao
tamaduni zote za tanzania zilioneshwa
wanakwaya na wenyeji wao
wanakwaya kinadada walipendeza sana
wahudhuriaji wakiburudika
vifijo kwa kila onesho

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Wabongo wanafiki sana. wakiwa home wanaona kuvaa kama hivi ni dhambi/ushamba na upuuzi.Mkija majuu mnataka kufagilia mavazi ya watu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 05, 2009

    Mwaka huu wameleta wamama wote hakuna atakaye baki

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 05, 2009

    Mdau wa Dallas Pastor Abisalom Nasuwa fanya uturushie video clips za hiyo show kwa Youtube.com

    Omba msaada kwa wanaojua endapo hufahamu Youtube.com ni kitu gani.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 05, 2009

    kwa nini mnakuwa wanafiki watumishi wa Mungu? mbona huku hamvai hivyo?
    mulienda kutangaza utamaduni wa kitanzania au kumtumikia Mungu? sasa
    kwa nini mnafika huko mnavaa vibwaya kama wacheza ngoma wakati huku hamsubutu kufanya hivyo.

    unafiki ni mbaya sana mbele za Mungu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 05, 2009

    Mbona mahudhurio yenu hafifu?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 05, 2009

    ni annon mahudhurio,ila fahamu watu wengi majuu awaindi kusali wala nini!!ndo mana apo wazee watupu,labda ao watoto wa kibongo

    mungu atusaidie!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 05, 2009

    Aliyosema Anonymous 5.53 hapo juu ni kweli kabisa, sielewi sijui ni ushamba au kuwavutia wazungu! Je kweli hao walienda kulitangaza neno la Mungu au kuonyesha mavazi na ngoma za kitamaduni? Neno la Mungu ni lile lile Tanzania au Ulaya, Iweje nyie wabongo muwe hivyo? Acheni unafiki jamani!!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 05, 2009

    mmependeza lakini mgependeza zaid kama mgevaa mavazi yenye asili za kwenu tanzania instead hoyo mavazi na mishono yenu yenye asili ya kihindi wenyewe wanaita sari.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 05, 2009

    Good job guys, you all look cute!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 06, 2009

    Ndugu zangu Watanzania wenzangu, hawa wenzenu wamefanya kazi nzuri sana na wanastahili kupongezwa, nyimbo zao na utamaduni waliouonyesha siyo unafiki mbele za Mungu, Hakika mpinga Kristo siku zote huponda kazi ya Mungu. Big Up Azania Front Choir

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 06, 2009

    Hongereni sana Azania Front, nyimbo zenu zimeonya na kuponya, Mungu apewe sifa, Karibuni sana tena sanaaaa Dalas kwa mara nyingine watoto wa Mungu.

    ReplyDelete
  12. safi sana mzee rumisha elri masa, masawe

    ReplyDelete
  13. safi sana mzee rumisha elri masa, masawe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...