
Kwa mara nyingine tena uongozi wa continental kwa heshima nataadhima unapenda kuwakaribisha watanzania wote wanaoishi maeneoya Tokyo, Kanagawa, Chiba na maeneo jirani katika onyesho no.2 la Band ya TANZANITE inayoongozwa na Wanamuziki mashuhuri Mr. Fresh Jumbe, Mr. Abuu Gitaa na Mr. Lister Elia.
Onyesho litafanyika:
Siku :Jumamosi Tarehe:23 May 2009
Mahali: Club Continental (SOBUDAIMAE)
Kiingilio : 1500Yen
Onyesho litaanza saa tatu usiku mpaka majogoo.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na,
MR. Abuu Gitaa : 080-5648-6575
Club Continental :
080-3532 -4043
KARIBUNI TUBURUDIKE PAMOJA.
Jamani mwenzenu ubahili umenizidi, hivi yen moja ni sawa na shilingi ngapi za madafu?? Sijui kwanini nilizaliwa na wapare!! mweh!!!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteKaka Fresh Jumbe kazi nzuri endeleeni kupeperusha tu sasa ni wakati wa mziki wa Bongo.
ReplyDeleteKaka Fresh Jumbe pole kwa kazi.....samahani kaka namtafuta rafiki yangu wa siku nyingi anaitywa Rashid Njenga....Naamini kaka yake huyo Rashidi mtakuwa mnapiga naye bendi (Mr. Abuu kama sikosei).....naomba anisaidie Email address ys Rashid.
ReplyDeleteThanx.
Bwana Freshi, na wenzio (Majina hatuyajui sawasawa) Kazi zenu ni nzuri sana. Tumekuwa tukiwaona sana kwenye TV hapa nyumbani na hata kwenye YOUTUBE.
ReplyDeleteIla kitu kimoja inabidi mkiangalie. Hizi video zenu mtu anaye-EDIT anaacha vivuli kwenye sura zenu, hata hamuonekani vizuri.
Mara nyingi tunaona sura ya Fresh tu ndiyo inaonekana vizuri na kwa muda mrefu. Jaribu kuonyesha wapigaji wote, kama bendi zingine zinavyofanya. It looks like a "ONE MAN BAND" Mnakuwa kama wakongo wa enzi zile. Nyinyi ni vijana bado.
Nadhani hii ni kazi ya kikundi na siyo kazi ya mtu mmoja. Msifiche sura zenu. Itapendeza zaidi kama wote wataonekana, kama ilivyo kwenye picha hii hapa juu. Huko Japan ndiyo kwenye teknolojia ya hali ya juu sana. Kwa nini mnashindwa kuonyesha sura za WAPIGAJI WOTE???? tafadhali rekebisheni hili.
Muziki wenu ni mzuri mashallah, na video zenu tunaziona na kuzifurahia. Tunashangaa kuona Wajapani wakichangamkia nyimbo za kiswahili, na kucheza kwa nguvu zote. Hongereni kwa kuutangaza mziki wetu.
Tafadhali Fanyeni Hayo Marekebisho,
tunataka kuona wapigaji wote kwenye video zenu.
MDAU - Mpenzi wa muziki wa ki-bongo,
Mikocheni, Dar
kaka fresh hongera kwa kazi nzuri,ila mimi nina wasi wasi na hilo jina la tanzanite kwani tanzanite ninayoijua sio hii,tanzanite ya mwanzo kabisa ni ya kina john muhina,abaraham kapinga na wengine ambao mika ya 80 na 90 mwalikuwa wanapiga bahari beach then kilimanjaro hotela halafu baada ya hapo wakaenda arabuni kwa muda mrefu sana na nasikia bado ipo sasa hito tanzanite yako mzee jumbe ni moja na ninayoijua mimi au umeiba jina????
ReplyDeleteMtoa maoni Tar 21, May 7:30am. Nadhani ungetoa jina au e-mail yako ingesadia zaidi.
ReplyDeletemtoto wa tanzanite ya mwanzo umeongea ukweli hata mimi tanzanite ninayoijua sio hii kwenye picha sasa fresh jumbe sijui hilo analitambua au laa,kama unasoma maoni haya fresh tafadhali tudadavulie.
ReplyDeleteAnd this is what put us down! usiku wa mwafrika yaani unatenga siku moja tu unaiita usiku wa mwafrika izo usiku nyingine ni usiku wa nani? if this not makes yourselves victims of "whatever" what is it? I just do not get it. In amerika they have Balcks month, I am like what about all those other months? did you leave them to other races? come on.
ReplyDeleteJUMBE SISI WA MANGESANI TUTAKUJA USIWE NA WASIWASI
ReplyDeleteKaka Fresh Jumbe, pole kwa shughuli.....Mimi namtafuta Rashid Njenga...namba yangu ya simu (Tz-mobile) ni 0714-199452......Asante sana
ReplyDeleteMimi ni mtu wa karibu sana na Jumbe. Alipoanzisha hii bendi yake mimi pia nilimuuliza kuhusu hili jina na majibu yake yaliniridhisha. Alivyosema yeye ni kuwa hii bendi yake haiitwi TANZANITE kama watu wengi wanavyokosea. Nafikiri hata hilo tangazo hapo juu ya picha yao ninauakika hao wenye baa ndio walioliandika na wamekosea. Hii bendi ninavyoijuwa mimi inaitwa THE TANZANITES na si TANZANITE angalieni vizuri (angalia hata kwenye website yake fresh Jumbe mwenyewe alivyoandika). Ni bora tusikurupuke tu na kuanza kuropoka. Halafu hawa wote ni watanzania sasa kuna ubaya gani hata kama majina yakifanana. Tena hawa kina Jumbe wako nje ya nchi kuna ubaya gani kuitangaza nchi yao. Halafu kama hamna habari hata bendi za KILIMANJARO ziko mbili na watu hawapigi kele. Kuna KILIMANJARO WANA NJENJE na KILIMANJARO CONNECTION ya Kanku Kelly na wote wako Bongo. Msitake kuhukumu mambo bila ya kufanya utafiti...kudadadeki.
ReplyDeleteSISI TUAMBIE HABARI ZA BOX HAPO TOKYO KAMA ZINALIPA ILI TUZUKE. HABARI ZA UBISHOO WAKO HATUTAKI NA HATUFAGILII.
ReplyDeleteSISI TUAMBIE HABARI ZA BOX HAPO TOKYO KAMA ZINALIPA ILI TUZUKE. HABARI ZA UBISHOO WAKO HATUTAKI NA HATUFAGILII.
ReplyDeleteLister, kazi nzuri naiona; kila la kheri nakutakia kila la kheri huko ughaibuni. Nawapongeza sana pia Fresh Jumbe na mwenzako mwingine Abuu Gitaa. Endelezeni libeneke la muziki wa kibongo mpaka (zamani tunasema)lyamba!! - Ndaga B.
ReplyDelete