MLANGO MPYA WA ELIMU NYUMBANI
Semina za Freddy Macha :
Mwanamuziki na Mwandishi mkazi wa London
Kuanzia Alhamisi Mei hadi mwisho wa mwezi, mwandishi na mwanamuziki, Freddy Macha, ataendesha semina zenye mada mbalimbali mjini Dar es Salaam na sehemu nyingine mikoani.

Semina zimegawanywa katika mada nne : maisha ya ughaibuni, uandishi, muziki, mazoezi na afya. Lengo lake ni kufungua dira mpya ya wataalamu wetu nje na ndani ya nchi kujitosa kusaidia kuendeleza elimu nchini.
Kwa kuanzia sitakuwa bure lakini ukitaka vitabu, maandishi au bidhaa nyingine husika zitauzwa kwa bei nafuu.

Semina za mwanzo zitafanywa bure katika ukumbi wa utamaduni wa TAYOA (Nyumba ya Sanaa, Upanga) British Council na SOMA cafe, Mtaa wa Regent.
Kama utapenda kuhudhuria au kupata habari zaidi piga simu namba :
0784 687644
AU
0784-272993.

Ratiba kamili ni:
1-Alhamisi Mei 21- Saa 11 jioni hadi saa 2 usiku. British Council.
2-Ijumaa Mei 22 - Saa 11 jioni hadi saa mbili usiku. Soma Cafe, Regent Estate, Simu : 22-222772759.
3-Wikiendi Mei 23-24 : Saa 8 mchana hadi saa kumi na moja jioni. Ukumbi wa TAYOA (Nyumba ya Sanaa).
4-Jumatatu Mei 25: Saa 11 hadi saa mbili usiku jioni. Ukumbi wa TAYOA (Nyumba ya Sanaa).

Kuna baadhi ya wananchi wanaotaka semina hizi zifanywe miji mingine ya Tanzania. Kama wewe unaishi nje ya Dar es Salaam na uko tayari kutayarisha siku moja au mbili za semina za mtaalamu huyu usisite kuwasiliana nasi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Safi sana Anko Macha, tupo pamoja.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 21, 2009

    Hii taarifa mimi wala sijaelewa, ina maana hizo semina zitakuwa bure au kuna kiingilio?

    ReplyDelete
  3. Goddam! Lakini watu wengine wana wivu za ajabu. Hata wanaume wanaweza kutaja majina ya wanawake wengine wakati wa mapenzi!

    Rest in Peace!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...