Katika kuhakikisha burudani, ubunifu  , sanaa na utamaduni kitanzania unawakilishwa ipasavyo katika shindano la urembo,; Miss Tanzania EU 2009 litakalo fanyika mjini Essen Germany, wasanii mbali mbali kutoka bongo wamealikwa...

Akielezea Blog ya jamii  kwa njia ya simu mratibu wa mashindano hayo Nashe Mvungi amesema  wasanii wa muziki wa kizazi kipya MB Dogg  na Bushoke watapanda jukwaani kutumbuiza, mbali na hao kutakua na makundi mengine ya burudani kutoka sehemu mbalimbali za Ulaya.

Katika kinyangányiro hicho mgeni wa heshima ni Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mheshimiwa A.Ngemera.

Akizungumzia washiriki wa mashindano hayo Nashe alisema nafasi bado ziko wazi kwa watakaotaka kushiriki, form za kushiriki  zipatikana katika:
www.misstanzania.eu 
 au
 email info@misstanzania.eu

Vile vile mratibu huyo alisisitiza kuwa washindi wa 3 wa mwanzo  watapata nafasi ya kwenda United Kingdom kwenye mpambano wa Miss Tanzania mjini London.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...