HIVI karibuni uongozi wa timu ya soka ya Moro United ulitoa taarifajuu ya kiungo wake wa kimataifa, Nizar Khalfan kutakiwa England kwamajaribio ya kucheza soka ya kulipwa katika timu ya Ligi Kuu ya huko,Tottenham Hotspur `Spurs’.
Baada ya Bodi ya Wakurugenzi kujadili ombi hilo na baadayekumshirikisha mchezaji husika, ilionekana kuwa ni heshima ya pekee,lakini kutokana na mazingira ya soka yetu, mchezaji huyo anahitajimaandalizi ya dhati kuweza kuingia katika ushindani wa kuwania nafasikatika klabu kubwa kama Spurs.
Hili lilikwenda sambamba na ujio wa mwaliko mwingine kutoka klabu yaVANCOUVER WHITECAPS FOOTBALL CLUB ya Canada iliyozuru nchini mapemamwaka huu na kuvutiwa na uwezo wa Nizar baada ya kumuona akiichezeatimu ya taifa `Taifa Stars’.
Kwa kuona Vancouver inaweza kuwa mahali pazuri pa kuanzia kucheza sokaya kisasa, Nizar ameridhia kwenda Canada kwa majaribio ya wiki mbilikuanzia Juni 8, mwaka huu. Vancouver itabeba gharama zote za Nizarwakati wa majaribio ngazi.
Mkurugenzi Mkuu, Azim Dewji ameuzungumzia uamuzi huo kwa kusema: “Kwakuangalia hali halisi, Nizar anaweza kupata nafasi kwa urahisiVancouver kuliko Tottenham, hivyo tumekubaliana akaanzie Canada ambakoatapata mwanga zaidi wa soka.
“Na kwa kuwa umri wake bado ni mdogo (miaka 21), bado atakuwa nanafasi ya kujaribiwa katika klabu nyingine kubwa za Ulaya, lakinibaada ya kuwa ameshaivishwa Vancouver. Bado tuna mawasiliano na Spursna Moro United itaendelea kushirikiana nao.
“Kwa kuwa hii ni changamoto kwetu, tunarudia kusema sasa ni wakati waMoro United kuzama katika soka ya vijana. Mtazamo wetu utaanzia katikakikosi cha msimu ujao wa Ligi Kuu.”
Naye Nizar, alikiri kuwapo kwa makubaliano hayo, huku akisisitizakuwa, anaamini njia itakuwa nyeupe kwake kama ataanzia Vancouverkuliko Spurs.
“Hata mimi mwenyewe nadhani Vancouver nitafanikiwa. Waliniona hapanami nimeona uwezo wao, napata faraja kwamba inawezekana. Lakiniieleweke nako nitapita, kiu yangu ni kufika mbali kisoka, hasa kuchezakatika moja ya ligi kubwa za Ulaya.”
Nizar anatarajiwa kuondoka wakati wowote wiki hii, baada ya kupataviza ya kuingia Canada tayari kwa majaribio kuanzia Juni 8.
Uongozi wa Moro United unamtakia kila la kheri Nizar, kwani mafanikiohayatakuwa ya klabu pekee, bali hata kwa Taifa Stars.



Hongera kwa uongozi wa Moro United na pia kwa Nizar kwa kufanya upembuzi yakinifu wa ukweli na uwazi.
ReplyDeleteMaana timu zinazocheza Premier league ya Uingereza hata ikiwa Tottenham Hotspurs kuna ushindani mkubwa kuweza kukubaliwa kupata nafasi premier league ya Uingereza.
Pia natoa hongera kwa Maximo kumwona Nizar alivyoiva Moro na ukampatia nafasi Taifa Stars ambako pia amejifunza mengi yatakayomsaidia ktk ulimwengu wa soka.
Mdau Kisiju vipi tena Kaseja kutupiwa virago Yanga?:
ReplyDeleteMABINGWA wa soka Tanzania Bara, Yanga wamewatupia virago wachezaji wake watatu nyota, akiwamo kipa Juma Kaseja.
Wengine ni Maurice Sunguti na Gaudence Mwaikimba ambaye alikwaruzana na uongozi karibu na mwisho wa msimu.
Pia, klabu hiyo imewauza beki Nadir Haroub "Cannavaro" anayetarajiwa kwenda Canada kuichezea Vancouver WhiteCaps iliyozuru Tanzania mwaka huu.
source:www.mwananchi.co.tz
Canada hamna kitu! Soccer huko ni sawa na Marekani. Jamaa na soccer ni mbali mbali. Atenda kuua kipaji!
ReplyDeleteHamna cha kuua kipaji wala nini. kuna mawili ya muhimu hapo, kwanza jamaa wako mbali kiutaalam na hatujawafikia hata sumni, pili kule ni njia rahisi zaidi ya kuingia ulaya kuliko kusema eti nacheza moro united, timu ambayo hata champion league haichezi.
ReplyDeleteKila la heri Nizar, katafute maisha dogo
We Nizar, ukishindwa majaribio kumbuka una VISA ya Canada na ni rahisi sana kwako kuingia US. Njoo huku US tubebe box. Mimi nitakupokea hakuna noma wala nini.
ReplyDeleteMdau May 31, 2009 7:56 PM, fananisha soka la bongo na Canada. Merekani imeingia vipi hapo?
ReplyDeleteni kweli premier ligi ni kiwango lakini isiwe kigezo kwamba watu waogope kwenda kujaribu.
ReplyDeleteHONGERA SANA KWA MORO UTD PAMOJA NA NIZAR MWENYEWE, MECHI ZA KIMATAIFA ZA STARS NI MUHIMU SANA KUONEKANA NA MAAGENT PAMOJA NA MAKOCHA WA NJE, HIO TUNAWAOMBEA WACHEZAJI WA STARS MCHEZO MZURI WIKI IJAYO AMBAPO PIA TUNAAMINI BAADHI YA WACHEZAJI WA STARS WATAPATA KUCHUKULIWA ABROAD KAMA WATAONYESHA KIWANGO KIZURI CHA SOKA,HICHO NI KIPIMO KIZURI KWA WACHEZAJI WETU KUTOKA KTK UMASIKINI NA KUANZA KUOTA NDOTO ZA UTAJIRI,PAMOJA NA KULISAIDIA TAIFA BAADAE,
ReplyDeleteMdau wa May 31, 7:56PM kwa nini unafikiri Nizar akienda Canada ataua kipaji? Ukilinganisha na soka ya bongo au Arabuni, Canada kunaweza kumsaidia sana huyu dogo kwa kuwa wenzetu wapo juu kisoka. Hata hiyo marekani iko mbali kisoka kuliko nchi nyingi tu. Tumpe moyo badala ya kumkatisha tamaa
ReplyDeleteduh! hii kali sana, mchezaji wa kiwango cha kimataifa halafu hawezi kuja cheza spurs? come on! kwa nini mnawapachika viwango wasivyokuwa navyo? eti "mchezaji wa kimataifa" hivi mnajuwa mnachosema hapa? international footballer halafu hata hajulikani nje na hana hata kiwango cha kuchezea timu ya spurs ilhali kila mtu anajuwa spurs ni timu ovyo kabisa katika PL hapa UK
ReplyDeletehebu nisaidieni hapa mchezaji wa kimataifa si kwa kiingilishi ni international footballer? sasa huyu jamaa amepata wapi title ya international footballer lakini hapo hapo anashindwa kwenda kucheza uk katika timu ambayo ni ya kati tu katika ligi ya uingereza?
ReplyDeleteWizi mtupu, hawa jamaa hawakuwa na deal yoyote na Spurs.
ReplyDeleteKama walikuwa na deal na Spurs, kwanini asijaribiwe kwanza Spurs halafu ikishindikana ndiyo aende Canada?
Hata kama atakuwa hapati number kuwa tu ligi ya UK ni nafasi tosha kuingia ligi zingine za chini UK.
Hawa hawakuwa na mpango wowote na Spurs.
Kama kweli Spurs nao wanamtaka kwa majaribio yeye anawatosa ili aende canada, basi hajatulia.
Bahati haiji mara mbili
Naupongeza uongozi wa Moro Utd kwa kuhakikisha mchezaji anafika mbali hata hivyo uamuzi wakuja Canada ili kuonwa na kuweza kucheza ligi kama UK hautamsaidia sana afadhari angeenda nchi za Europe kama France, Italy, Holland nk ambako hata wachezaji wenye umri mdogo hapa Canada wanaenda huko (Europe)kwani huku soka la wanaume hakuna labda wanawake au Hockey!
ReplyDeleteSikukatishi tamaa, angalia mbali zaidi!
Mdau 2nyi
Ontario Canada
Nizar kafanya jambo jema kuanzia Canada huko kuna GYM atajenga mwili na vitu kadhaa wa kadhaa.
ReplyDeletespurs wako juu sana.namba yake kuna JENAS na pia bob zakora ambaye hana namba ya uhahika.
spurs ni wakali kuliko westham.
hata kina DROGBA walikataliwa na ARSENAL huko nyuma kabla ya kupitia ufaransa na kujiweka sawa.
pia kuwa international footballer ni sawa kwani NADIR HAROUB CANAVARRO alimzuia Etoo wa barcelona mara mbili. lakini EVRA wa manchester kashindwa kufanya hivyo.
hivyo basi canavalo wa Yanga anaweza kuwa bora kuliko VIDIC NA EVRA.
nataka Nizar aende canada ili akapate mafunzo sahihi kukaa kwake maximo FC (TAIFA STARS)hataongeza kitu.
kutokana na maximo uwezo wa ufahamu wake kufikia kikomo NA HANA JIPYA.
tizama makocha kama Hiddink wa chelsea wanajua wanafanya nini au kocha wa barcelona kaona hana beki kampa jukumu YAHYA TOURE na kuwa beki wakati ni midfielder.na kazi ikaonekana ingekuwa maximo angekuja na kilio ooh beki yetu ilikuwa na kadi nyekundu ndio maana tukafungwa, international footballing hakuna visingizio.
nizar nakutakia mafanikio mema, mafanikio haya hayajaletwa na maximo ni kudra tu ya Mwenyezi Mungu
kwani hivi sasa hakuna kocha stars ila tuna mtu wa majungu.
Kaseja yanga wameshindwa kumlipa hawana pesa za kumlipa.kama ambavyo Man united wameshindwa kumlipa TEVEZ pounds milioni 25 na mwarabu wa man city anamchukua.
ni mimi mdau Kisiju mkereketwa wa timu yetu ya taifa.
Kisiju.
Mwenyekiti,nimefuatilia taarifa hii kwa Karibu sana, Whitecaps hawana taarifa zozote, nimeongea na kev amesema yeye ajui hilo, anachojua kuwa kuna mpango wa kumleta Cannvarro. Basi kama atakuwa anakuja itakuwa changamoto nzuri sana. Wanaobeza soka ya Canada na USA ni wale wale watu wa tamaa. Mchezaji wa Whitecaps anapokea dollas 2000 kwa mwezi ni zaidi ya Million mbili na nusu za bongo sasa ni ndogo hizo? kuna wachezaji wanachukua hadi dollas 5000 kwa mwezi, kumbe bora aje huko kuliko kungojea get collections za bongo.
ReplyDeleteMdau
Vancouver
Kaseja ni bomu la kutupwa na mikono. Makocha waote wa nje hawamtaki. Hata akienda kufanya majaribio Malawi atashindwa.
ReplyDeleteNizar mfuatilie wakala wa Uswizi aliyekutaka 2007 hivi sasa ungekuwa mbali sana.anza France,Uswizi,Norway na sweden. then UK inakutafuta yenyewe.
ReplyDeleteMaximo ana vyeti gani?alipatikana vipi?alifanyiwa interview? amewahi kuchukua kikombe au kufundisha timu gani ya maana?nadhani kocha wa simba phiri ana uwezo zaidi ya Maximo.
ReplyDeleteWe mdau wa 11.40pm acha ushamba! Mchezaji wa kimataifa haimaanishi kuwa anacheza kwenye timu za ulaya au za nje, maana yake ni kuwa anachezea timu yake ya taifa! Kama hujui kaa kimya, alaaa! Nizar ni mchezaji wa kimataifa!
ReplyDeleteSohar naona wewe ndio hapa ukae kimya nawe ndio unaeleta ushamba kabisa hapa. rudi shule ukasome kwanza halafu ndio ulete vikomnti vyako hapa
ReplyDeleteHii stori ya moro imekaa kiujanja ujanja sana.
ReplyDeletekama Tottenham walimtaka kwanini wao waogope?mwacheni aende nyie sio makocha wala watalaam wa benchi la totenham.
mlijuaje kama atakuwa na kiwango kidogo?hapa Totenham hawakumtaka ilikuwa ni story tu ya kutunga na kujipa ujiko.
hawa walisema anatakiwa june moja awe tottenham wakati TRIALS ZA totenham zinafanyika july.
tuache kujikweza ndugu zanguni.
Hii habari imenitatanisha kabisa. Kwa nini Moro United na Nizar wamekosa kujiamini kiasi cha kuogopa hata kufanya majaribio na Tottenham? Nizar, kama unasoma hii habari hapa, nenda kafanye majaribio na Tottenham. Waachie wao ndio waseme kwamba kiwango chako hakiendani na mahitaji yao, sio kunywea kabla hata hujawaonyesha uwezo wako. Ukipata nafasi Spurs, kitendo cha kufanya mazoezi mwaka mzima na kina Didier Zokora na Jermain Jenas kinatosha kukuinua kiwango. Isitoshe Vancouver haichezi kwenye ligi kuu ya Canada, wanacheza ligi daraja la kwanza. Ukifanikiwa kuingia Spurs, hata kama wakiona wanashindwa kukutumia wanaweza kukutoa kwa mkopo kwenye timu ya ligi daraja la kwanza Uingereza, ambako boli liko juu kuliko Canada. Na la mwisho ni kuwa safari ya kutoka Canada kuja kuchezea Taifa Stars ni ndefu sana kuliko ya kutoka Uingereza kwenda Tz. Maximo akiondoka Stars na kwa pesa za TFF za nauli, unaweza kusahaulika Stars.
ReplyDeleteTuambizane ukweli lakini...hili ni changa la macho nini? Huu ulikuwa mpango feki au namna gani? Wakala gani aliyeusuka?
hahhahh..nizar ana miaka 21...hahahh...mama aliwahi kuniambia mtu hayeyushwi anajiyeyusha...na mie nasema mtu hadanganyi ana jidanganya...mpira kucheza spurs sio jambo dogo....acheze kwanza lipuli....tuache kuota ndoto za mchana...nataka nione wabongo wanacheza ulaya lkn tujiandae kwanza jamaa...mpira ni km kipaji na maandalizi ya toka mapema...lkn kwa wachezaji wetu hao sijui...tuwe wakweli kwa wenyewe kwanza ndio tutapata tunachohitaji...sasa ukijidanganya mwenyewe nn unategemea...wangu mtazamo tu
ReplyDelete