wadau wa chuo kikuu cha Kerala university kusini mwa india wakila pozi kwa raha zao baada ya kula nondozzz zao katika computer Electrical & Electronics Engineering, civil, computer science& engineering na Electronics & communication.
-------------------------------------------------------------
kaka michuzi habari yako.
kwanza kabisa pole na kazi na veksheni ya huko unyamwezini(marekeani) mm ni mdau kutoka hapa uturuki ningependa kuwapongeza wabaongo wenzetu ambao wamekula nondoooooz hapo KERALA UNIVERSITY.
Bila ya kuwasahau washikaji zangu wa karibu sana waliopo katika picha hiyo ya pamoja.waliosimama kutoka kushoto wa kwanza kabisa SHABANI AHMADI aka shebby na watatu kutoka kushoto waliosimam apia SALAVATORY AMOS aka roberto karlos.
hahahaha ebwana hongereni sana
John

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2009

    Jamani hicho chuo ni cha weusi tu??

    ReplyDelete
  2. Hongera sana wadau kwa kula Nondoz. Nawatakia kila la heri na Mungu awabariki.
    Mdau, Mysore http://www.washindi.blogspot.com/

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 20, 2009

    Hivi kwa nini serikali isipeleke watu UK au US maana indina yeneyewe inapeleka UK na US. Wanajuwa vyuo vyao bado.

    Serikali ya bongo inabidi ibadili mitazamo. Nchi zoote zenye kasi ya maedndeleo zimesomesha watu wao US, UK, Canada, Fr, kama vile china, japan, nk.

    ReplyDelete
  4. Mwema JrMay 20, 2009

    hongereni wabongo, wana nondozzzzzzz. mpo juu, juu sana....

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 21, 2009

    Huwa ninafurahi sana ninaposoma maoni ya baadhi ya watanzania humu ndani. Kuna watanzania wengi mawazo yao ni HASI. Kwa uchunguzi mdogo niliofanya, nimegundua wengi wanaokosoa hata vitu vizuri ni watanzania wachache wanaoishi nje tena kinyume na sheria na shule pia hawajaenda. Upeo wao wa kuchambua mambo ni mdogo sana. Wewe anon wa may 20, 2009 9.38. Unajua kuna wataalamu kiasi gani marekani wanaofanya kazi na walisoma India. Unajua gharama ya kumsomesha mtu ulaya na marekani? Mbona hujiulizi mbona wewe umeshindwa umeishia kufanya kazi za ajabu. Si kila kitu kinachofanywa bongo ni cha kukosolewa. Sikatii yapo mambo mengine. Ili ni tatizo la kutokujua dunia inakwenda vipi. box masaa 16 ukirudi umelala. muda gani utasoma kujua dunia inakwendaje.

    ReplyDelete
  6. Al MusomaMay 21, 2009

    Are you sure chuo hicho kiko India na siyo Iringa? Isijekuwa ni spelling error hapa imetokea...

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 21, 2009

    khaaaa
    wanawake kulikoni mboni hampo?kozi za wanaume au

    ila jamani india?

    hongereni graduates

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 21, 2009

    anon wa May 20, 2009 9:38 PM wewe ni mwehu...
    usikurukupe..! wewe hujui nchi inakwenda vipi, JK ameongelea mara ngapi kuhusu sera mpya ya kusomesha watu nje? (tafuta).
    naaliye kwambia hao wanasomeshwa na serikali india ni nani?

    unapoongelea swala la science & technology india achana nao, jamaa wapo juu mbaya.....

    tafuta mwenyewe kwenye export business ya india IT products inacontribute kiasi gani kwenyepato lao la mwaka
    honereni wadau...!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 21, 2009

    why no one with nondozzz in mathematics? this is the field i like.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 21, 2009

    Hata hivyo tukubali tusikubali vyuo vingi India ni fake! Watanzania wengi wanakwenda kule kwa kuwa ada na maisha kwa ujumla ni nafuu! Kwa hiyo ni lazima kuwa makini unapokwenda kusoma vyuo vya India! Wahindi kama kawaida yao ni matapeli mpaka kwenye elimu! Ingawa sikatai kuna vyuo vizuri ila ni vichache!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 21, 2009

    Mimi napenda nikupongeze anon wa May 21, 2009 12:57 AM, umenena.
    Wabongo wengi tuna tatizo la kupayuka payuka. Huyo anon wa May 20, 2009 9:38 PM haitaji shule bali kuelimika, make nimekutana na wabongo waliosoma ila bado akifungua mdomo unatamani kukimbia.
    The point is, tunatakiwa kufikiria kabla ya kuongea. Vitu vingine ni complex kuliko mabox tunayobeba au kufagia nursing home.
    We just like to criticize for the sake of it, instead of critically analysing issues.
    Wake up people.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 21, 2009

    w anon wa may21 6:24pm,koma tafadhali watu wanaweza wakawa wanafanya kazi nursing kwa malengo kijana.na ana vitu vya maana TZ.plz zingatia hilo WE NDO NAONA UNALOPOKA.

    ReplyDelete
  13. Ni bei nafuu, angalia bei zao hapo chini, ila degree ni degree iwe India au Somalia. Ni mambo ya kizamani yakusema hii ni kali zaidi ya hii. Jwa walio na hiyo elimu wanashukuru sana, maana huenda wangebaki TZ wasingeweza hata kukubaliwa kuingia Dar-es-salaam Tech Institute, na sio kwa ajili ya yoyote ile bali nafasi kuwa zimejaa UDSM hadi DAr institute.
    Hongera ndugu zangu. Njooni UK sasa muongeze Masters zenu na mkimaliza hapa Masters UK , nendeni huko majuu zaidi yaani US , mkachukue PHD zenu.
    Bei za hicho chuo ni kma ifuatvyo kwa semester, bei nafuu, bwerereere!!

    RATE OF TUITION FEE
    Subject / Course
    Under Graduate Programme (Per semester)
    Post Graduate Programme (Per Semester)
    M.Phil. Programme (Per Semester)
    Ph.D. Programme (Per annum)
    Humanities / Social Sciences /Commerce
    US $ 200
    US $ 300
    US $ 450
    US $ 1200
    Science Subjects
    US $ 350
    US $ 500
    US $ 650
    US $ 1600
    Professional Courses
    US $ 600
    US $ 750
    US $ 900
    US $ 2000

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 22, 2009

    haya bana tutafika

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 22, 2009

    Wahindi hawaruhusiwi kufanya kazi US kama hawajachukua digrii yoyote ya US. Ndo maana wengi husoma bachela india na kumalizia mastaz US, UK, au Canada ambapo hutafuta kazi na kupata.

    Wengi mnaosema india wako bomba pimeni uhalisia sio kujisikia vibaya tuu kwa kuwa criticized kusomea kwenu india.

    Nakubali kuna vyuo vichache saana india ambvyo vina viwango vya kimataifa kuzidi hata vya tz.

    Swali, je tunaenda kwenye vyuo hivyo vikali au tunavyovipata?

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 22, 2009

    mtowa maoni wa tatu kutoka juu umenichekesha sana kiasi kwamba ilinibidi kupata maji kabla ya kukujibu. pole sana kwa kiwango chako kifupi cha kuelewa mambo.

    kwanza kabisa nitakufahamisha kuwa sio watanzania wote wanaokwenda nje kusoma wanapelekwa na serikali.

    pili kwa baadhi wa wananchi wa nchi moja kwenda kusoma nchi nyengine haimaanishi kuwa kiwango cha elimu nchi mwao ni kidogo. Mimi nimesoma UK na katika hostel yetu kulikuwepo na wanafunzi kutoka Canada, denmark, greece, turkey, israel, france, malaysia, pakistan, japan na china. Nchi zote nilizozitaja huwezi kusema kuwa viwango vya elimu ni vidogo na ndio wakaamua kuja UK.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 22, 2009

    We anon wa May 22, 2009 11:35 AM, hizo nchi zoote ulizotaja zina viwango vidogo vya elimu, ukilinganisha na UK, ukiacha france, labda kidogo na Israel. Pia umesahau kuorodhesha Tz.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 22, 2009

    Jamani angalieni sana watu mnaosoma vyuo India! Vyuo vingi ni fake na wahindi walivyo matapeli! Kwa upande wangu ni bora hata mtu akaenda Africa Kusini kuliko India!

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 23, 2009

    mimi ninavyojua kwanza KERALA ni jina la stete ambayo inaongoza kwa kiwango cha elimu india nzima na ipo kusini mwa india, halafu kama hawa jamaa watakuwa wamemaliza katika chuo kikuu chenye jina la state basi lazima kitakuwa cha serikali na hawa watu watakuwa siyo wabahatishaji kama mnavyofikiri, hawa watu wapo juu sana, hongerani aisee, huyo anayesema hapo ni iringa anatia huruma sana maana hajui chochote.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 24, 2009

    Watanzania wanaenda popote kutafuta elimu kwa kuwa wengi hatuna uwezo wa kulipa ada. India hutoa scholarship kila mwaka ili Watanzania waweze kusoma huko. Watanzania wenye uwezo pia unaweza kulipa ada India ndogo kuliko Ulaya au Marekani.

    Kama duniani kote, kuna vyuo feki pia. Mimi nimesoma Marekani. Kuna vyuo katika kila kona ya nchi. Sio vyuo vyote Marekani vinaheshimika au kujulikana kwa jina. Msomi aliyomaliza Kentucky State University au Springfield College hana hadhi zaidi ya msomi wa Harvard University, Yale au Princeton. Chuo kilicho na jina unalipa ada zaidi na ni vigumu kuingia. Tunaongelea dola 40,000 kwa mwaka. Hao Wamarekani wenyewe aidha wamepata scholarship au wamekopa serikali kusoma hata katika vyuo vya kawaida visivyo na jina kubwa. Vyuo vingi vinategemea wageni kwa kuwa tunalipa cash.

    Kwa nchi za kitajiri, kusoma nje peke yake pia ni elimu. Unaenda kujifundisha lugha ya nchi nyingine na utamaduni wao. Unafungua macho yako. Nilipokuwa chuo kikuu, tunaweza kwenda kusoma nje an kurudi kumaliza digrii yetu chuoni. Pia, kama unasoma lugha kama Kifaransa au Kiyahudi, ni vizuri utumie mwaka mmoja kwenda nchi zao kujifunza vizuri. Kuna wanafunzi wengi UDSM kutoka nchi tajiri kwa kuwa chuo kinajulikana kwa elimu inayoitoa ya Kiswahili. Pia, kuna wale wanaosoma magonjwa ya nchi za kimasikini ili wawe mabingwa wa udaktari wa "tropical diseases".

    Wahindi sio peke yao wanaosoma kwao na kujiendeleza Marekani au Ulaya. Nimekutana na wasomi wa Bongo waliomaliza UDSM na Mzumbe na wanasoma Master's au MBA. Nilichokiona ni kwamba wahindi ni hodari katika elimu. Fungua website yoyote ya chuo muhimu chochote duniani, hauwezi kukosa profesa angalau mmoja wa Kihindi. Wahindi wanaoishi Marekani asilia kubwa yao ni wasomi na ni matajiri sana zaidi ya Wamarekani wenyewe kwa kuwa wana umoja na wanapenda kufanya biashara zao wenyewe kuliko kuomba kazi ofisini.

    Ni muhimu kujua shule kabla hujachukua digrii yao, lakini hawa wasomi katika picha hawajachuzwa. kama mdau alivyosema hapo juu, kerala inajulikana sana kwa elimu yao. Tatizo ni kwamba kuna wadau wengi hapa hawaelewi mambo lakini wanapenda kuropoka ropoka wakiwa na muda katika internet ya Mhindi. Inatia huruma kweli kwa kuwa elimu ipo katika internet hio hio anayeitumia kuropoka. Aki google hiko chuo, atapata majibu yote kabla ya kufungua mdomo.

    Mdau anaedai kuwa Wahindi lazima wawe na digrii ya Marekani kufanya kazi, sio kweli. Kampuni inaweza kumleta toka India na akaruhusiwa kufanya kazi kama walivyoruhusiwa kufanya kazi za Internet miaka ya 90 huko California. Wanakuja kusoma Master's kwa kuwa India ni rahisi kwao kusoma Bachelor na kama watapata credit ya digrii yao ni rahisi kuliko kupoteza pesa kusoma digrii ya kwanza Marekani. Kusoma marekani sio mchezo, miaka ya 90, wazazi wangu walilipa dola 1000 kwa kila darasa. Kama sijasahau, digrii ya kwanza inahitaji usome madarasa 40. Hapo sijalipa hosteli wala nauli bado.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 26, 2009

    Dah wenzetu mnaraha mko wengi sana sie hapa ubatani unajikuta chuo kimoja ngozi mmoja tu chuo kizima.hata wa kumuomba maji hayupo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...