Mwenyekiti Dk. Kamuzora akihutubia wanachama wa CCM tawi la Urusi
mmoja wa wanachama wapya wa CCM tawi la Urusi akimwaga wino baadaya kupewa ganda lake
Mwenyekiti wa CCM tawi la Urusi akigawa kadi kwa mmoja wa wanachama wapya
Sehemu ya waliohudhuria hafla hiyo

Dr. kamuzora:  “Hili ni tawi la CCM-MOSCOW , Si Vinginevyo.”! 

Mwenyekiti wa tawi la CCM nchini urusi , Dr.Alfred Kamuzora, jana ameweka bayana tafsiri harisi ya tawi la CCM-URUSI , na kusema kwamba  tawi linalotegemewa kufunguliwa rasmi hivi karibuni nchini Urusi ni tawi la CCM-MOSCOW , likijumuisha wanachama wa CCM wanaishi nchini Urusi.. “ndugu wanachama naomba ieleweke kuwa hili ni tawi la CCM-MOSCOW na si Vinginevyo” 

Akihutubia katika sherehe za Kugawa kadi kwa wanachama wa CCM, wanaishi mjini Moscow-Russia tarehe 3/5/09, Mwenyekiti wa tawi alifafanua kuwa mwamko wa kufungua tawi la CCM, ni kutokana na idadi ya wakerereketwa wa CCM, kuongezeka nchini hapa, ambapo mchakato huu ulianza tangu Jan 2007  kwa Vikao vya kamati ya Muda ya uanzilishi, hadi tarehe 31/8/08 , Azimio na tamko rasmi la Ufunguzi wa tawi nchini urusi ulipotangazwa. 

Katika sherehe hizo jumla kadi 92 za wanachama wapya wa CCM waishio Mjini Moscow –Russia , ziligawiwa, huku zikiambatana na shamrashara mbalimbali toka kwa wanachama kwa kuchangia maoni , kwa maslahi ya Kujenga Azma za kuliendeleza tawi.

Akiendelea kuhutubia,na akinikuu maneno ya Hayati baba wa taifa, Mw/kiti alisema  “ Nia, sababu na Uwezo wa kuanzisha Tawi hili Tunazo, naamini Tutashinda vikwazo vyote, na kujenga muhimili imara wa Chama cha mapinduzi”  

Alisema “tawi imara ni lile lenye wanachama wanaozingatia kanuni,itikadi na sera za chama ,hutaweza kutangaza kauli mbiu ya chama,kama wewe haujakamilika: maana yake:-chama kama hakina mikutano,wanachama,michango ya uanachama,na sera basi SI chama.Sisi tunaamini kwamba tuna sera, tuna Mikutano ya kujenga na tuna wanachama hai, hivyo tutafanikiwa katika lengo la ufunguzi rasmi na tunategemea kupata wageni toka Tanzania” 

Kwa upande wake, katibu Mwenezi ,sera na itikadi wa tawi Ndg Mfungahema salimu aliwakaribisha wanachama wapya wa CCM tawi  na kujiunga na chama ili kulinda Misingi ya Utawala bora  kwa lengo la kupata viongozi bora  , Katibu  mwenezi  alisema “ CCM ni chama Bora na Chama chenye Nguvu, ni chama chenye Uelekeo mzuri na sera safi zinazozingatia utawala bora, ni chama chenye viongozi bora na ni chama tawala cha serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,

Akifafanua Jumuia ndani ya tawi , alisema UVCCM , ni Jumuiya  makini, yenye nguvu na historia ya kutoa viongozi bora, hatuna budi kuipa nguvu jumuia hii na kuithamini, napenda kuchukua fursa hii kumpa moyo Mw/kiti wa UVCCM-URUSI katika tawi letu  Ndg Bakunda Chrispin  aendelee na jukumu hili makini kwa chama cha mapinduzi la kuandaa makada wa chama , na Viongozi wa baadae wa Serikali,” 

Katibu mwenezi alizungumzia kwa kirefu mafanikio ya CCM, chini ya Raisi Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, alisema mafanikio mengi katika nyanja za Elimu-mfano , elimu ya juu -ongezako la vyuo vya serikali , elimu ya shule za msingi –kuimarisha na kuboresha  mpango wa shule za msing MEM na upande wa Sekondari –SEDEP.  

Naye Mw/kiti wa UVCCM  tawi la Moscow –Urusi Ndg Bakunda Chrispin , akiwasilisha Ujumbe wa UVCCM –URUSI  alianza kwa kusema Dhima ya chama chochote cha Siasa  “Umoja wa Vijana tawi la Moscow unatambua  kuwa :- Kazi ya chama cha siasa imara ni kuwa kama daraja la kuwaunganisha watu na serikali waliyoichagua na kulinganisha serikali na watu inayotaka kuwahudumia. Mbali na jukumu hilo, ni wajibu wa chama kusaidia watu kuelewa serikali yao inafanya nini na kwa nini. Ni wajibu wake kusaidia watu kushirikiana na serikali yao kwa juhudi ya pamoja ili kuwaondolea umasikini, ambao umewaelemea” 

Akiendelea , Bwana Bakunda  alisema kuwa “Chama pia kinawajibu kuhakikisha kwamba serikali inaendelea kuyajua maoni, shida na matakwa ya watu na inawajibika kuwakemea watu wanaokwenda kinyume na matakwa ya watu wengi. Hata hivyo, chama nacho kinawajibu wa kuwaelimisha watu na wanachama ili kusaidia kuona shughuli za serikali, zinawaletea maendeleo yao na zina maana kwa usalama wao wenyewe wa siku zijazo na fursa zao pia katika siku zijazo.” 

                 Kwa kuzingatia dhima hizo , aliongeza kwa  kusema “Umoja wa Vijana hasa wa CCM ni chemchemi ya viongozi wa kesho wa taifa hivyo hawana budi kuhakikisha kuwa wanatimiza wajibu kwa kuzingatia dhima za chama chochote cha siasa alizozitaja hapo awali.”

         

                  Akizungumzia chaguzi ndani ya jumuia za ccm, alisema chaguzi hizo zinalengo la kuweka wigo mpana wa Demokrasia ndani ya chama na kukuza Misingi ya Utawala bora. Chaguzi ndani ya jumuia hizo ni  tegemeo kwa maendeleo ya kisiasa, kijamii na kiuchumi kwa siku zijazo, wanachama hawana budi kuwajibika  kikamilifu  ili kupata viongozi bora na si bora viongozi.  

    Akizungumzia swala zima la Kuwa  mwanachama wa CCM ukiwa kijana , bwana bakunda alisema ,Mkutano huu , unakwenda sambamba na sherehe za ugawaji wa kadi za wanachama wapya wa CCM. Zoezi hili ni moja ya Mafanikio ya Uongozi wa Tawi, japokuwa kuna matukio makubwa zaidi ya leo, yanategemewa katika siku  zijazo.

 Kupokea kadi ya CCM leo ukiwa kijana ni ishara tosha ya kuingia katika safari ndefu ya mabadiliko ndani ya chama na serikali kwa Pamoja “ TOGETHER WE CAN”  kwa maana hiyo Uongozi wa Vijana-tawi Una imani kuwa :- wanachama wote wa CCM tawi la Urusi watakua na staha, Uadilifu,busara na Nidhamu kwa viongozi wa Chama na watendaji wa serikali katika eneo lao la Uwakilishi, ili kufikia malengo ya kila mmoja wetu katika kutatua matatizo ya kijamiii hapa Urusi ,bila kusahau dhima ya kupata viongozi bora na si bora viongozi, pindi unaporudi Tanzania. 

                 Mwisho Mwenyekiti huyo wa UVCCM –URUSI, anawataka vijana wote  kuvunja makundi yoyote , na   kufanya kazi kwa kushirikiana  na kuenzi misingi tuliachiwa na waasisi wa Taifa na Chama. “Makundi yoyote ni dalili za uvunjifu wa maadili na nidhamu ya chama na haviwezi kufumbiwa macho…….”  “Nawataka wanachama wa CCM katika tawi letu kuvunja  ishara zozote za makundi na kufanya kazi kwa upendo na mshikamano ili kuimarisha chama. na ninawasihi kuenzi misingi tulioachiwa na waasisi wetu wa taifa la Tanzania na Chama cha mapinduzi., hayati Mwl JK Nyerere na Karume -Raisi wa kwanza wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.. 

Sherehe hizo , zilihudhuriwa na watanzania mabalimbali wanaoishi Moscow , huku wawakilishi toka katika vyuo wakiwakilishwa na wenyeviti wao.

Sherehe hizo zilifanyika katika jumba la Ukumbi wa Mikutano wa Block 6, YUGO ZAPADNAYA, hapa katika JIJI LA MOSCOW- RUSSIA. 
 

Kwa maelezo zaidi ,

Wasiliana na Ofisi za Tawi ,kwa Anuani, 

Moscow 119526, Russia 146, Leninsky prospect.,                                                                    

Fax : +74954386744

Tel: +79150901289

       +79264766204

Email : ccmmoscow @gmail.com

Website: ccmmoscow.blogspot.com  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 42 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2009

    Tuna mambo ya ajabu sana, CCM tawi la Urusi! Juzi nilikuwa na jamaa wa Ghana kwenye kijiwe fulani wakatushangaa sana, yaani haijawahi kutokea Baada ya uhuru, bado kuwa na matawi ya vyama vya siasa,badala yake wenzetu wana taasisi za kiuchumi na kusaidia maendeleo ya kwao bila itikadi. inaniskitisha sana.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2009

    DUH HUU UGONJWA WA CCM KAMA SWAIN? hatari jamani mkifatwa hapo mkiulizwa watanzania mnakataa subirini sasa waje wenye mji.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 06, 2009

    si bure, lazima kuna UFISADI fulani hivi. Michuzi tudokezee deal iko vipi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 06, 2009

    Jamani kuna mambo muhimu yanaendelea bongo sasa hivi.. yall need to sit down for a minute. Acheni siasa nchi za nje. for what?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 06, 2009

    Tuna mambo ya ajabu sana, CCM tawi la Urusi! Juzi nilikuwa na jamaa wa Ghana kwenye kijiwe fulani wakatushangaa sana, yaani haijawahi kutokea Baada ya uhuru, bado kuwa na matawi ya vyama vya siasa,badala yake wenzetu wana taasisi za kiuchumi na kusaidia maendeleo ya kwao bila itikadi. inaniskitisha sana.


    Anomy uliyetoa maoni hapo juu unashindwa nini kuanzisha hicho unachokisema?

    ReplyDelete
  6. MI NADHANI TUNGETUMIA MUDA WETU KUANZISHA MAJUMUIYA YA KUSAIDIANA NA KUJIENDELEZA KIUCHUMI, HII MAMBO YA CCM SIJUI WAPI WAPI NI KUPOTEZA MUDA NA MWELEKEO PIA.

    ReplyDelete
  7. PhatlorenzoMay 06, 2009

    Kuna watu wana too much muda on their schedules...eehh Mungu tusaidie haka kaugonjwa ka CCM kasije kuenea na kufika huku Magharibi.

    Phatlorenzo--MN

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 06, 2009

    Hivi wenzetu uko nje hamna chama mnachokipenda, mnachokijua na mnachoshabikia zaidi ya CCM? kila kukicha ni ufunguzi wa tawi la ccm mahari fulani au ndio kujipendekeza? amkeni, tunaitaji kusikia na wengine wakijiunga na vyama vingine. au ukiwa nje ya nje utakiwa kuwa na chama zaidi ya ccm?

    WIVI MTUPU(((((

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 06, 2009

    Haya mambo ya aibu sana ndugu zangu Watanzania. Tunapaswa kuanzisha jumuiya za kusaidia maendeleo ya kiuchumi, siyo upuuzi wa kushabikia vyama vya siasa.

    Lakini pia, hii aibu ya kijana wa chuo kikuu kushindwa kuandika vema, hajui wapi aweke herufi kubwa, hajui wapi aweke object marker, hajui urefu wa sentensi, ni aibu kubwa sana jamani.

    Aibu kwa Tanzania.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 06, 2009

    HAKUNA CHA UPENDO NA CCM AWA JAMAA WANALENGA NAFASI BONGO.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 06, 2009

    Watanzania tupo zaidi ya milioni 40 hatuwezi wote tukawa na mawazo sawa au yanayolingana. Kama mtu anapenda siasa let him/her participate, kuwa nje is not the limit,badilikeni kidogo.

    No wonder mmekazania kanini tusianzishw jumuiya za kusaidiana na za kiuchumi, well it good, je unataka CCM wakuanzishie? grow up kama una mawazo basi yaweke katika mpango wa kutekelezeka na sio kuwa laumu wengine kwa yale ambayo wameamua kuyafanya. Most of the time utakuta haohao ambao wanafanya hizo CCM ndiyo hao pia walioweza kuanzisha mashirikiano mengi, quote me wrong?

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 06, 2009

    Nadhani kutakuwa na wapiga kura wa nje ya nchi 2010. Kumbe kustolowei sio dili tena. Unabaki kuwa mdanganyika kama ukiwa Bongo tu!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 06, 2009

    Inashangaza sana kuona watu wenye akili zao wanakalia kujigawa katika nchi za watu ni dhahiri kwamba kuna watu wanahitaji maslahi fulani kupiti matawi hayo ya CCM nchi za nje, kinacho nisikitisha wengi katika wanachama hawajui hilo, niukweli usiofichika kwamba hakuna mtu yoyote anae anzisha jambo bila kuwa na lengo fulani, kama walivyo sema wasemaji hapo juu ni kheri mkabuni miradi ya kusaidiana inaweza kuwasaidia kiasi fulani sio kuanzisha tawi.

    kwa maoni yangu ni: wizi mtupu!!!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 06, 2009

    DU! WIZI MTUPU.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 06, 2009

    BWANA MICHUZI NIBANDIKIE KATANGAZO HAKA TAFADHALI.



    TANGAZO

    WATANZANIA WOTE MNAOISHI NEW YORK, MAREKANI;
    TUNAWATANGAZIA KUWA MNAMO TAREHE 23 MWEZI JUNE 2009, TUTAFUNGUA RASMI TAWI LA CCM HAPA NEW YORK. WAZALENDO WOTE MNAKARIBISHWA NA ADRESS ITATANGAZWA RASMI KATIKA BLOG HII YA JAMII HAPO FORMALITIES ZOTE ZITAKAPOKAMILISHWA.

    FRANCIC BUTELE

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 06, 2009

    Nasi tulioko China tudumishe chama chetu jamani. Kidumu Chama Cha Mapinduzi...Kidumu! Zidumu fikra za mwenyekiti wa chama...zidumu. Idumu siasa ya ujamaa na kujitegemea ...Idumu!! Wewe kama hutaki chama kimpango wako. Acha wanaokipenda wakienzi na kukiendeleza kuanzia shina hadi matawi(sio miti) matawi ya chama.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 06, 2009

    vijana mmeamua kujiunga kwenye ufisadi na nyie? maana kama nakumbuka vizuri si nyie miezi michache iliyopita mlikua mnapiga mayowe kuwa pesa zenu za mikopo zinaliwa na mafisadi, au sio nyie? mmedanganywa na hivyo vyakula hapo baaasi mnakua wana-CCM. MAKUBWAAAAAAA!!!!!!

    ReplyDelete
  18. KARIBUNI HAPA: www.tanzaniadiaspora.ning.com TUZUNGUMZE MAMBO YA MAANA. AHSANTENI SANA.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 06, 2009

    Ndio tuseme vyama vingine Tz havina wanachama Ughaibuni?

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 06, 2009

    MALAYSIA hatuna mambo hayo ya CCM huku tunasomeshwa kwa hela za wazazi wetu na hatubebi box,vyuo vizuri...

    acheni wajiunge na CCM hao wa RUSSIA huwenda serikali itawatatulia matatizo yao waache kupiga deshi

    si kwamba watu wanapenda kujiunga na CCM njaa kaka wafungue tawi la CHADEMA AU CUF WAKALE WAPI WAKT WANASOMESHWA NA CCM. NJAA ZINATUPELEKA PABAYA JAMANI,UWIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII............!

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 06, 2009

    njaaaaaaaaaaaaaa hizi!

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 06, 2009

    Wabongo tuachane na ushabiki wa siasa. Siasa hazitatufikisha mahala popote. Kazeni buti someni/piga mzigo tafuta hela yako.Jiendelezeni wenyewe na mtajisaidia wenyewe na familia zenu na pia Taifa lenu.

    Wizi mtupu!

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 06, 2009

    HUU UGONJWA UMESHAINGIA HUKU PIA YAKHE?? SASA MIE PIA NTAANZISHA UMOJA WA WAZANZIBARI TULIOKO HUKU! NA NYIE WA BARA PIA ANZISHENI UMOJA WA WABARA!! ndio twagawana taratibu hivi kidogo kidogo.
    badala ya ndugu zanguni tujiungeni na ktk jumuiya zilizopo tayari tuziimarisheni,tumeanza mchezo wa vyama!! kha! haya makubwa sasa ndugu zanguni!twafarakana sasa wewe wa paulo mimi wa apolo n.k

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 06, 2009

    Mnatuchosha, ongeleeni mambo ya maana, matawi ya CCM yatatusaidia nini? Ndio kiliwapeleka huko0 ibu

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 06, 2009

    Hii homa ya wana CCM UGHAIBUNI lazma kuna jambo nyuma yake, SIASA BWANA. ah

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 06, 2009

    hawa akili kuganda ndio manake angalia hilo darasa wanalokula wali wa njano hata bunge she ya msingi pana nafuu. fanyeni mambo ya maana, mnanunuliwa kwa senti tano mtumie nauli zenu wenyewe kuja kuwapigia wezi kura, kalaghabao. stop this nonsense n get busy with your work box, karani whatever so long as u make money for your family, yourself n society. AMKENI

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 06, 2009

    Hivi haitoshi kufanya Association ya WaTanzania ambao wanaishi kwneye nchi hizo za nje ni lazima ifanyikwe kwenye mwamvuli ya CCM? Hakuna wananchi wa nchi yeyote ninayoifahamu ambayo inafanya vituko hivi. Hata waChina wenyewe hawana mikutano ya kujiunga na chama chao na kupewa kadi. Unaweza kuonyesha unaipenda na kuheshimu nchi yako bila ya kubeba vikadi !!
    What a waste of time and resources, nafikiri sisi ambao hatuna kadi - sio raia kamili ? !!!!

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 06, 2009

    Bora mie nilijilipua. Maana TZ haina mweleko kabisaaa. Iwapo nje ya nchi kuna CHADEMA, mara CCM, sasa watanzania watajumuika vipi ugenini?

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 06, 2009

    Mimi nachoka kabisa na haya mambo yetu wabongo huku ughabuni,nilipohamia hapa uk natokea ugiriki,nimekuta mambo ya ajabu sana huku!!?,mara tawi la ccm reading mara manchester jamani jaribuni kuiga mifano ya watanzania waishio ugiriki au italy huko kuna umoja wa watanzania tu!hakuna ccm wala cuf,mnajua huku ugenini mnapoanza sijui mambo ya vyama mnawagawa watanzania kujumuika pamoja,kwani kuna watu hawataki kabisa kusikia mambo ya siasa au vyama ,hivi niulize hapo bongo kuna wazungu kibao wanaishi na familia zao,je ulishasikia tawi la labour party nchini tanzania?au tawi la conservative?! sana, sana utasikia klabu hii ni ya waingereza au hapa ni jumba la utamaduni la watu wa korea au klabu hii ni ya warusi basi ,wanapokuwa nje ya nchi hawahusishi kabisa mambo ya kisiasa wanakuwa wamoja wenye ushirikiano kwa kila jambo,halafu haya mambo sijui tawi la ccm mara cuf yako huku uk, na urusi basi nchi nyingine kuna jumuiya za watanzania tu,mtanzania akifa(mfano mzuri ona italy,greece,ubeligiji,norway)wanahakikisha anasafirishwa au mtanzania akiugua watu wanapokezana zamu kumuuguza,au angalia hata wabongo wanaoishi USA kila ukiwasoma kwenye mtandao wanaelezea mtanzania fulani kafariki au kapata matatizo fulani wanatoa utaratibu wa kumsarisha au kumuhudumia ,mambo ya vyama hayana faida yoyote huku ugenini au matawi hayo ya chama yanafaida gani kwa watanzania wanaoishi ugenini!!?? MAENDELEO SI LAZIMA MTU AJENGE NYUMBA AU ANUNUE GARI "HAPANA".HATA FIKRA MPYA NA MAWAZO MAPYA NI MAENDELEO TOSHA.

    ReplyDelete
  30. Advocate JashaMay 06, 2009

    WANAJAMII NA MBUNGE WA NANIHI NAOMBA UFUNGUE MJADALA KUHUSU HAYA MATAWI YA CCM YANAYOIBUKA KAMA MAFUA YA NGURUWE NINI MCHANGO WA MATAWI HAYA KATIKA KUWAUNGANISHA WATANZANIA UGHAIBUNI NA UMUHIMU WA MATAWI HAYA KWA NCHI YETU KWA UJUMLA?WATANZANIA UGHABUNI TUKO WACHACHE BADALA YA KUHUNGANA KWA MISINGI YA KITAIFA TUNAANZA KUUNGANA KWA MISINGI YA KICHAMA,KIKABILA,KITANGANYIKA NA KIZANZIBAR!INASIKIKITISHA!UBALOZI WA TANZANIA POPOTE ULIPO TUPENDE TUSIPENDE NI TAWIL LA CCM NIMATAWI GANI MENGINE NA KWA AJIRI GANI TUYAANDISHA?AU NDIO MPANGO WA WA WATU KUJIANDIKIA CV MWAKA FULANI NILIKUA MWANZILISHI WA TAWI LA CCM MAHALI FULANI N.K.HIVI KWELI WABONGO UGHAHIBUNI HATUNA LA KUFANYA KUITANGAZA NCHI YETU KATIKA NYANJA ZA UTALII UWEKEZAJI N.K.MFANO HILO TAWI LA MOSCOW KWA KADI ZILIZOTOLEWA 92 INGAWA NATEGEMEA WENGI WALIOHUDHULIA WALIFATA KUNYWAJI!UKIWAGAWA KATIKA NAFASI ZA UONGOZI CCM UMOJA WA VIJANA N.K HAWATOSHI KATIKA NAFASI ZA UONGOZI.HAPA KUNAWATU WANAAJENDA BINAFSI AMBAZO HAZIKISAIDII CHAMA CHENYEWE AU WATANZANIA WENYEWE.AMA KWELI WATANZANIA TUMELOGWA.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 06, 2009

    NAAMINI MTU MWENYE AKILI TIMAMU HAWEZI KUJITENGA NA MWENZAKWE KWASABABU YA CHAMA. VYAMA NI KAMA DINI, KILA MTU ANAWEZA KUJIUNGA AU KUAMINI ANAVYOTAKA. MAANA YANGU NIKWAMBA WANAOSEMA ETI TUTATENGANA KWASABABU YA VYAMA BASI HAO WOTE NI MARAAILA, HAWANA AKILI TIMAMU.

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 06, 2009

    Naunga mkono hapo juu. Kidumu chama cha mapinduzi, kusema ukweli kimetutoa mbali. Hakuna chombo kisicho na kasoro. Mkumbuke CCM ndiyo imetusomesha na kukutibu mpaka tukafika hapa. Wapuuzi wote mnaokashifu CCM mngekuwa walala hoi bila CCM. Mimi personally naishukuru sana CCM na sikatai kuwa dosari zimekuwa nyingi lakini tusisahau wema wake. Mimi nimesoma darasa la kwanza hadi degree ya mlimani kwa pesa ya CCM, labda hawa watoto waliozaliwa juzi hawajui HISTORIA YA CCM. Watu wote, uwe mkulima mfanyabiashara kama bongo yako inafanya kazi utafika unapotaka. Nilivyojua hivyo nilisoma kucha kutwa na kweli wazazi wangu walikuwa wakitaarifiwa kuwa mwanao anakwenda kusoma kilakala au msalato na bila wao kulipa chochote kile, tumealala kwenye mawbweni, tumekula chakula ingawa hakikuwa kizuri na walimu waliotulea kama mama na baba zetu. Baada ya kuja huku ughaibuni na kuona junsi mitoto ya huku inavyolelewa eti mwalimu hathubutu kumrekebisha mwanafunzi, mzazi ukichapa kiboko unaweza lala jela na kama huna pesa basi wewe utaishia high school. I really appreciate nchi yangu kwa kuniwezesha kufika hapa nilipo. Na ingekuwa vizuri zaidi kama tungeshirikiana kuanzisha umoja au vyama vya wasomi na kusaidia kuinua hali ya elimu nchini mwetu. Tunajua bado tuko nyuma ki-technologia! KAMA MNAWEZA KUANZISHA CCM KWANINI TUSIANZISHE UMOJA WA WASOMI WA KITANZANIA WANOISHI NJE NA KUANZISHA PROGRAMM ZITAKAZOWANUFAISHA WATOTO WETU HUKO NYUMBANI. MFANO WATU WANAOJUA COMPUTERS WANAWEZA KUANZISHA LIKE SUMMER PROGRAMM NYUMBANI WAKIWA LIKIZO NA KUWAFUNDISHA WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI AU VYUO AMBAVYO TUNAJUA VINAHITAJI TECHNOLOJIA HIYO. COMPUTERS SASA ZIMEKUWA AFFORDABLE HUKU NJE. HII INAHITAJI MAWAZO NA KUPATA RIGHT PEOPLE. SIASA TUIACHE NYUMBANI, I THINK THIS CAN REALLY MAKE A DIFFERENCE HUKO NYUMBANI. NA HII IDEA CAN BE EXPANDED TO OTHER FIELDS! MY BLOOD IS CCM LAKINI MCHANGO KAMA HUU UNAONYESHA UZALENDO ZAIDI KULIKO KUBAGUANA KUFUATANA NA ITIKADI UNAYOAMINI

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 06, 2009

    Wewe unaesema chama ni kama dini wewe ndio umedata kabisa na watu kama nyie ndio mnachafua sifa ya nchi kwa kuendelea kushikilia mambo ambayo hayakusaidii wewe mwenyewe wala jirani yako. Huku ughaibuni huwezi kunufaika na mambo ya CCM labda kama kuna agenda za siri humo ktka hayo matawi ya CCM. Na inaonekana hivyo, hao wanaonzisha hayo matawi kuna kitu wanalenga. Ukiwa huku huwezi kupiga kura kumchagua kiongozi yeyote Bongo, na hiyo ndio siasa, sasa hizo shughuli zenu zinawanufaisha vipi kama si kuwa kuna mambo ya siri ama ujinga tu unawasumbua? Haya mambo mnatuletea huku sisi wengine ndio yametukimbiza kule, nyie mmeamua kutufuata huku na kuanza kutuletea balaa huku huku. Acheni uzuzu wenu.

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 06, 2009

    WARNING: ATAKAE TOKEA KWENYE HUO MKUTANO WA CCM NEW YORK, AU SEHEMU YOYOTE HAPA MAREKANI LAZIMA AWE NA MAKARATASI.

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 06, 2009

    Watu wanaona haya mambo ya kuanzisha matawi ya CCM ughaibuni sio mazuri kwa sababu zifuatazo:
    - Imani za kisiasa zinaweza kuwagawa watanzania wakati sisi wenyewe tayari tuko wachache sana huku. Pia sisi tunahitaji umoja wa kutuungasha wote ili tuwe na nguvu za pamoja tuweze kusaidiana panapostahili kufanya hivyo.
    - Sidhani kama tawi la CCM la kwa mfano Reading linaweza kujishughulisha na tatizo la mtu ambaye si mwanachama wake, ni sawa kwa kuwa kikundi chochote hujishughulisha na mambo yanayowahusu wana kikundi. Sasa hapo tayari watakuwa wameshafanya kosa, watakuwa wamejitenga kiaina bila kujua madhara yake.
    - Ndio maana wachangiaji wengi hapa wanaona ni bora watu tuliopo huku tuwe na umoja kama watanzania na sio umoja wa vyama. Kwa kuwa umoja wa watanzania utakusanya nguvu za watanzania karibu wote waliopo ktk eneo hilo bila kujali imani zao za kisiasa wala dini.

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 07, 2009

    CCM juu! Juu,juu JUU ZAIDI!
    CCM hoyeeee!!!!!!!!!!!!!
    Ushindi tu 2010.

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 07, 2009

    Kwakweli kunapokuwa na maoni kama haya ndipo unapopata picha halisi ya jinsi tulivyotofautiana kifikra,kimawazo,na hata kiutendaji eti mtu anajisifia kabisa kuwa kasomeshwa na ccm!!!?jamani,karibu wote tunaochangia mawazo yetu humu tumezaliwa mwishoni wa chama cha TANU au mwanzoni wa CCM,kwahiyo hisitoria ya chama tunaijua vizuri sana,mimi binafsi nina elimu ya chuo kikuu mlimani lakini siyo ccm iliyonsomesha ila ni SERIKALI iliyochini ya ccm na SERIKALI ni wajibu wake kunihudumia mimi kama mtanzania,HAKI YANGU kupewa kila HUDUMA ktk nchi yangu,siwezi nikasimama kusifia eti serikali imenisomesha hiyo ni HAKI JAMANI!!!!siyo FADHIRA sasa mtu na akili zake anakaa kuandika oooo sijui mimi nimesomeshwa na ccm,kwahiyo ndiyo unalipa fadhira siyo??jaribu kutembea ili ujue haki yako ktk nchi yako na uone serikali za wenzetu zinavyojali wananchi wao,njoo uk uone lobour party inavyohudumia wananchi wake wa kila umri,wazee kuanzia miaka 60 hawalipi teketi ndani ya basi,hiyo siyo fadhira ni haki yao wazee wa uingereza hata sisi wageni tunanufaika na mambo fulani,na wala huwezi kusikia muingereza anasema asante sana lobour party kwa msaada wako "HAPANA" huo ndiyo wajibu wa viongozi wenye serikali makini na viongozi bora,ELIMU BORA,MATIBABU BORA ,BARABARA NZURI,USAFIRI WA UHAKIKA NI HAKI YA WANANCHI WOTE,SIYO FADHIRA "NARUDIA" ,sasa wewe mtanzania ulitaka usomeshwe na serikali ya NORWAY AU SWEDEN!!? tubadilike jamani!

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 07, 2009

    TANGAZO KWA KABILA LA WAFYOMI WAISHIO LONDON.
    --------------
    Kutakuwa na mkutano wa kuunda umoja wa kabila la wafyomi hapa London, mkutano huu utafuatiwa na wa kabila la Warangi na baadaye Wagogo na wandengereko, kama mjuavyo umoja wa jamii fulani ugenini ni muhimu sana, wachaga na wahaya, wazaramu hawakaribishwi kwenye huu mkutano. msemaji mkuu ni Bwana Mtanzania.
    Karibuni wote.

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 07, 2009

    tunasoma p lumumba kafungue kwenye google upate historia yake chama ndio kinaongoza serikali kwa hiyo tunataka kama vijana kuingia na kutoa mchango wetu katika maeendeleo ya taifa , kuw a vyama tofauti haina maana tu adui apana ila tunatofautian sera bila kugombana kwa hiyo sisi tunatumia haki yetu ya kimsingi kwa maendeleo ya watu ambao ndio sisi

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 08, 2009

    hawa ccm wameshtukia dili, wanajua watu wengi wakitoka nje ya nchi wanazinduka na kujua kama ccm haina maana, so ili kuwawahi wakirudi wasilete zogo wanataka wawaanze ukouko walipo, keep it up ccm, lkn iko cku watu watashtuka na mafisadi wote watajulikana

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 09, 2009

    (Mungu ibariki Tanzania, wabaliki watu wake.....) mbona kila siku zikienda haya maneno ya nakosa meaning... instead of to be united as one national withiout tribalism and politicalism tunaanza kujigawa kwa rangi-njano/kijani , blue/nyekundu, nyeupe/blue na nyingine nyingi zitaibuka 2010.
    Before i though this kasumba is based for old Tanzanian generation which we called watu wa nyerere but sad thing is that this problem as spreaded to our generation which is very bad signal for future of the country.. kama unaona chama kinatumia administration means kupotosha vijana(Tanzanian educated class) ambao ndiyo taifa la kesho mtu mwenye akili timamu inatia hofu na kuondoa matumaini ya future democracy in our country nafikiri muda umefika kwa watanzania kupiga kura kwa chama wakipendacho bila propaganda za kizamani.(convincing power) .....Mambo ya bongo yananikumbusha System ya Kirusi( ruling party -Ednaya rossiya)ambapo mtu kama siyo member wa hicho chama ukiomba kazi upati ,endapo utasema mie ni mwanachama wa chama kingene ata ukiwa waziri kesho kazi imeota mabawa. Ndiyo maana wamarekani wanapinga sana democracy values za kirusi. (Democracy value cant exist in the presence of divide and rule system ).
    Yanayo tokea nchini mwetu wanataaluma wanaita mkumbo au wana sociology wanaita (mobu saikologi)- ninafanya vile kwasababu watu wote wanafanya hivyo, bila kufikiria positive or negative sides. Thus why you see every where new c.c.m branch
    Mie nina uwakika kwamba hao watu tunao waona wamepanga foleni kuchukua kadi wala hawajua whats going on in C.CM.... Wengi wao hata katiba ya chama hawaijuhi even those who called VIONGOZI heri yangu niliisoma kidogo nikiwa primary school...
    The another fun thing about C.C.M -russia ni kwamba hao watu wameitana wanafunzi wanasoma Moscow kula maandazi, sambusa na chai wakakubaliana tunaunda tawi la chama urusi bila consultation and support from other cities and regions in russia walipo watanzania wenzao, and they call c.c.m branch in Russia wakati ni c.c.m branch moscow, halafu kiongozi wa chama ni mwanataaluma ( Doctor ) lakini kashindwa kuwaeleza vijana jamani tufanye hivi na hivi ili hii shughuri iwe na mwelekeo (vision), mie ningefurahi sana kusikia watu wanajioginise na kunda TANZANIA DIASPORE IN RUSSIA ili kusaidia a lot of problems facing Tanzanians and to present our national interest in Russia instead of looking personally green pastures in future by bearing yellow and green tshits…. anyway kuna mwanafalsafa mmoja lisema "kila watu wanastaili uongozi wao" kwavile watanzania tuko hivyo ndiyo maana tunatawaliwa na viongozi kama hao. KIDUMA CHAMA CHA MAPINDUZI (Kimepindua nini for 22 years old myself i don’t know..)

    Mwanafalsafa wa Kibongo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...