Watanzania Waishio Uingereza, Kwa Kushirikiana Na Kwa Kupitia Jumuiya Ya Watanzania Uingereza (TzAUK), Walifanikiwa Kukutana Hapo London - Tanzania House Kwenye Ofisi Ya Ubalozi Siku Ya Jumamosi Tarehe 18 .4. 2009 Kuanzia Saa Nne Na Nusu Asubuhi Hadi Saa Tisa Na Nusu Mchana. 

Mkutano Huo Ulipitia Maswala Mbalimbali Ya Ushirikiano, Na Ulijadili Na Kuunda Kamati Maalumu Ya Muda, Iliopewa Majukumu Ya Kukusanya, Kuangalia, Kupitia Na Kutoa Mapendekezo Ya  Muundo Mpya Wa TzAUK, Ili Kukuza Umoja na Kuboresha Ushirikisho Zaidi Wa Watanzania Wote Waishio Uingereza Na Ireland.
 
Kwa Ufupi, Mchakato Haswa Upo Katika Maeneo Haya:

-Katiba Ya TzAUK

-Mahusiano Kati Ya  Jumuiya Ya Watanzania Uingereza Na Jumuiya Na Taasisi Mbalimbali Za Kitanzania Uingereza Na Jinsi Ya Kufanikisha Na Kujenga

-Muundo Wa Umoja na Uhusiano Wa Kitaifa.

-Kukamilisha Mapendekezo Juu Ya Mabadiliko Ya Muundo Na Katiba Ya TzAUK
 
Tunapenda Kuwakaribisha Wenzetu Wote, Kutoa Mapendekezo Yenu Ili Tuweze Kufanikisha Zoezi Hili. 

Kamati Inatoa Shukrani Kwa Ushirikiano Wako Na Tutapokea Mapendekezo Yenu Na Kuyafanyia Kazi.

Tafadhali Tuma Maoni Yako Kwenye Anuani Pepe Ya Kamati Hii Maalum: Uniting-Communities@Yahoogroups. Com  
 
Wajumbe Wa Kamati Teule Ilioundwa hapo 18/4/2009 Ni: 

1.      Agatha Hamis
2.      Katty Moses Katega
3.      Abdulla Ali
4.      Maira .B Migire 
5.      Davis  Banduka
6.      Rev Tumainin Kallaghe
7.      Wencheslous Ikumla 
8.      Lameck Okello Otieno 
9.      Mariam Mungula
10. Dessa Makoko
11. Apollo Temu
12. Maka Mwamwaja 
 
Kamati Imepewa Muda Wa Miezi Miwili  Kukamilisha Zoezi Hili. 
 
Mapendekezo Ya Kamati Teule Yatawakilishwa Na Kujadiliwa Ili Yafikishwe Rasmi Kwenye Kikao Husika Cha TzAUK Kwa Kufuata Utaratibu Husika.
 
Asanteni

Katibu Kamati Ya Muda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 07, 2009

    HIZI JUMUIYA HAZIFANIKIWI KWA VILE BAADHI YA WATU WAMEZIGEUZA KUWA DILI.HICHO KIKAO KIFANYIKE TH 18/4 TAARIFA ITOLEWE LEO,INA MAANA HAPA KATIKATI WAHUSIKA MLIKUWA MNAJIFUNZA KUANDIKA/KUTUMA TANGAZO KWA MICHUZI?WIZI MTUPU!

    HAKUNA CHA JUMUIYA WALA NINI,ISHI VIZURI NA WENZIO,ACHA MAJUNGU,NK MAMBO YATAKUWA BAB-KUBWA.HIZI JUMUIYA UZUSHI TU.KAMA LONDON WANA JUMUIYA YAO,READING WANA YAO,NK HIYO "UMBRELA JUMUIYA" YA NINI TENA?

    KAMA KARATASI ZIMEGOMA,RUDINI BONGO MKAJARIBU DILI ZA UFISADI.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 07, 2009

    Najua Michuzi uutaibania. Mbona wajumbe wote ni walewale wa umoja wa Watanzania wa nini hii? Ni nani hii amevaa ngozi ya kondoo?
    Asante.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 07, 2009

    ILI KUFANIKISHA UMOJA HUO ITABIDI MUWE MACHO NA WANACCM AMBAO WATAFANYA JUHUDI KUUDHOOFISHA KAMA WALIVYOIDHOOFISHA JUMUIA MPYA YA WANAWAKE TANZANIA KIASI CHA KESI KUISHIA MAHAKAMANI NA WANACCM KUSHINDWA HIVYO MAHAKAMA KUIHALALISHA JUMUIA HIYO. HEKO KWA WATANZANIA WAISHIYO UK KWA KUWA NA MTAZAMO MPANA USIOBAGUA WATU KWA ITIKADI ZA KISIASA.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 07, 2009

    Wandugu wa UK hongereni kwa kuendeleza libeneke la umoja. Ila hicho kichwa cha habari mngebadilisha kidogo, sio kwa walio ughaibuni ni kwa walio Uingereza, maana watu tumetoa macho yote kusoma tukafikiri ni kwa wa ughaibuni wote.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 07, 2009

    khaaaaa
    angalau apa mmefanya akili mana UK kwa mijumuiya isiyo na kichwa wala miguu??mna muda mwingi eee kupiga soga za kibongo??

    lets pray hii sasa ni kwa nia njema kukusanya wabongo wote uko mliko sio u-ccm

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 07, 2009

    yani hawa barozi anawavumilia kweli maana kila kukicha jumuiya ,watu wanataka kufanya mambo kivyaovyao jumuiya itawasaidia nini kama si majungu tu kama mmechoka upweke rudini bongo bar kilakona weunazuka tu barmaid atakupa tafuu sio kuunda vijumuia ushenzi kila kukicha nendeni mkasome mapate kazi za maana.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 07, 2009

    SWALI LAKIZUSHI;
    Hivi mbona balozi wa bongo USA hasikiki kama yupo? halafu hamna ishu kama za jumuia/vitu kama ccm nini sijui kama UK? au ndo box sana hamna kupumua...

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 07, 2009

    Nikadhani I am the only one chukialing this usisiem!
    Je mna jipya? How u gonna take my concerns from coventry?

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 07, 2009

    NI JAMBO JEMA NA ZURI WASHIRIKISHENI WAZANZIBAR PIA NAONA HAWAPO KWENYE KAMATI.

    PIA JIHADHARINI NA WANAOJITIA KUWA WANA CCM HAWANA NIA NJEMA NA WATANZANIA HUKO MBELE WATASABABISHA MGAWANYIKO MKUBWA.

    PIA KUNA KUNDI LA WATU WA MUSOMA NA KILIMANJARO HIVI KARIBUNI WAMEKUWA WAKITAKA KILA KITU WASHIKE WAO KWA MALENGO YA UKABILA WATIZAMENI SANA HAO.
    VINGINEVYO BRAVO ABUU FARAJ NA TIMU YENU YOTE YA TANZANIA ASSOCIATION.

    PIA ANGALIENI UDINI ISIWE KAMA CCM AMBAPO KUNDI LA WAKRISTU PEKEE YAO NDIO WAMEJIWEKA KWENYE HALMASHAURI,KAMATI N.K SI KITU KIZURI NAOMBA MNAZINGATIE HAYA KAMA MNA NIA YA KWELI KUWAENDELEZA WATANZANIA.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 07, 2009

    Keep up! Hizi ndizo habari tunafurahia kusikia kutoka UK. Sio zile za usisiemu. Tutawaunga mkono kwa hali na mali.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 07, 2009

    haya ndio maajabu, mbona mkutano wenyewe haukutangazwa nasi tukaweza kuhudhuria? kama kweli mkutano huu unalengo la kujumuisha wote tuliopo uk kwa nini basi haukutangazwa ejapo hapa ambapo sasa mnaleta yaliokwisha pitishwa?

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 07, 2009

    Afadhali sasa mnaongea sio jumuia kila kona za CCM. Ni vizuri kuwa na Jumuia moja ya watanzania either ni mwana CCM, CUF , NCCR au chama chochote. Sisi ni watanzania kwanza, tukiwa nchi za nje sisi ni watanzania kwanza before anything. Sasa haya mambo ya CCM need to Stop and we come together as Tanzanian.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 07, 2009

    JANJA YA CCM HIYO!90% YA WANAKAMATI HAPO NI VIONGOZI WA MATAWI LUKUKI YA CCM YANAYOCHIPUA KILA UCHAO HAPA UK. HIVI JUMUIA YA WATANZANIA NI KAMA UMOJA WA MATAIFA,YAANI TAIFA LOLOTE LINARUHUSIWA KUJIUNGA!MAANA NAONA WATU WA MATAIFA MBALI MBALI NDANI YA HIYO KAMATI!

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 07, 2009

    Anony wa kwanza kabisa May 07,2009 9:25 kama ulikuwa kweye kichwa changu.Uhasidi,Majungu na Unafiki ndiyo talk of the day.Hakuna kizuri utapata kwenye hizo so called jumuiya.Tuacheni tubebe maboksi yetu kwa amani.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 07, 2009

    mimi niko |UK lakini hata siku moja huu upuuzi akaa!MAJUNGU TU!!kuanzia walio juu mpk chini sory nasema ukweli ila ndo ivo michuzi..wiziii mtupuu!!!

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 07, 2009

    Njaa mbaya, hakuna aliye na moyo wowote wa jumuiya. Hapo mlipo mnajaribu kutafuta kushibisha matumbo yenu, kwa bahati mbaya siku hizi watu wameamka. Hamtapata kitu zaidi ya kugombana wenyewe kwa wenyewe. wazushi wakubwa nyie kafanyeni kazi

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 08, 2009

    UK tumechoka na jumuiya zenu, twataka vitendo. Kuweni wabunifu, Watanzania nyumbani wanahitaji mengi, maana hadi sasa sijaona tuna mwelekeo gani maana tumegeuka kuwa wanasiasa kila kitu!! Hizo jumuiya jamani zituletee vitu vya kimaendeleo na sio kuchaguana maana ni kafashion fulani tumeona, na kumbukeni nyumbani!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 08, 2009

    tangazo maalum kwa walio ughaibuni

    Hivi wa-Tanzania wa ughaibuni wako Uingereza tu?

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 08, 2009

    wenye TA chukueni maoni haya.mimi nimeguswa na mdau hapo juu aliyesema suala la ukabila.kweli kabisa hapa ukerewe kuna makabila mawili yaliyotajwa hapo juu yana agenda ya siri.
    udini umeingia kwa kasi msipokuwa makini mtakuwa mnaunda jumuiya za kabila na dini fulani lengo halitatimia.
    take on board ushauri huu.
    mdau Manchester.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 08, 2009

    watu wameshaanza kulalamika UKABILA na UDINI. wabongo hawana jema kila kitu ni kulalamika tu. bora kila mtu aishe kivyakevyake.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 09, 2009

    May 7th 2009 | DAR ES SALAAM
    From The Economist print edition


    Worries about one of east Africa’s steadier economies

    THE country already gets 40% of its government budget in aid, but now it wants even more foreign cash to help it through the economic downturn. How much is enough? Tanzania’s president, Jakaya Kikwete, smiles grimly. “We’re trying to bring down our dependency, but we’re grateful for what we receive.”
    With 44m people, Tanzania has often been given the benefit of the doubt simply for being the gentler twin of harsher Kenya, which has 40m. What it lacks in dynamism it makes up for in placidity and a common national identity. It is unlikely to fall apart at elections or any other time.
    Its founding party of independence, Chama Cha Mapinduzi (CCM, the Party of the Revolution), formerly the Tanzanian African National Union, known as TANU, still suffocates the country’s ragtag opposition parties with its size and ponderous propaganda. Mr Kikwete is a CCM man; his breakthrough job was as the youthful head of political indoctrination for Tanzania’s armed forces. He will almost certainly be returned to office with a big majority in elections next year. He still charms would-be investors with his sales patter.
    Yet those who set up shop in the country are often disappointed. Tanzania, many complain, is a “slow” or even “terrible” place to do business—and “ungrateful” for foreign aid or investment. Even its boosters admit it is wrapped in red tape and lacks skilled workers. Almost everyone says Mr Kikwete is spending too much time burnishing Tanzania’s image abroad and not enough fixing problems at home. Last year he chaired the African Union.
    In any event, he hopes that aid will keep Tanzania afloat long enough for its economy eventually to make a great leap forward. Shiny new buildings even in provincial towns, along with new roads and water projects, signal optimism. Politics are stable. A rowdy separatist movement in the island of Zanzibar is quiet for now.
    By Tanzanian standards there is a new sense of urgency. The energy ministry says it wants tenders “immediately” for a power station to cover a paralysing shortfall in electricity. Mr Kikwete turns up unannounced at state-owned outfits such as the port and the railways to demand efficiency and rail against corruption. He has also lambasted the country’s “Wabenzi” (those who drive a Mercedes-Benz).
    But Mr Kikwete turns mournful when he spells out the effects of the global recession: missed government revenue targets; a cancelled sovereign-bond issue; projects for a nickel plant and a vast aluminium smelter put on hold; revenue from coffee down; cotton hit even harder; tourism suffering as well. An exception is gold, with new finds still to be exploited and the price holding up fairly well.
    Tanzania may already, in some respects, be falling behind. A recent Chinese state visit failed to bring much investment. The government in Beijing thinks Kenya, not Tanzania, is the gateway to the mineral wealth of Congo. Tanzania’s two main railways are rickety. The port of Dar es Salaam failed to pinch business from Kenya’s port, Mombasa, when Kenya was in turmoil a year ago. No one seems to know how Tanzania’s main port will hit its target of a tenfold increase in goods traffic by 2030. Tanzania is not even spending all the aid it is given. Last year, $2.4 billion of pledged funds were not disbursed.
    Tanzania must also decide whether to integrate more closely into the East African Community (EAC), which includes neighbouring Burundi, Kenya, Rwanda and Uganda. It has dragged its feet over opening its borders and moving towards a common currency, though it recently insisted that a common market would get going next year. It suspects Kenya of using the EAC as a way of grabbing arable Tanzanian land on the cheap. And the country’s tiny middle class fears being swamped in a common market by better-qualified Kenyans and Ugandans. Moreover, the world crisis may bolster old socialists in the CCM who want a return to ujamaa, a failed model of rural collectivisation propounded by Tanzania’s founding president, Julius Nyerere. That would set it back even further.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 09, 2009

    Kweli Watanzania kazi tunayo!!!

    Katika hizi comments za anonymous, nyingi zaidi zimejaa chuki, fitina, frustrations, ujinga (kutokufahamu), uzushi, pengine wivu usio na kiini, backwardness, ulalamishi usio na any action!!

    Kumbuka you will achieve far less ukiwa mwenyewe kwa lolote ufanyalo. Hata MAFISADI wanashirikiano sio mmoja. Sasa wenye nchi mkikaa mnatupiana madongo tuu na matusi mnadhani kuna malaika atashuka kuokoa jahazi?? Huu sio ujinga tuu, pia ni upumbavu ambao watu lazima kizazi chetu kijifunze kuondokana nao. Lazima tujue kufanya kazi na kujituma na kuwajibika sio finger pointing kila kukicha. Tumekuwa Taifa la Walalamishi tuu na Ufisadi Mtupu na Kuota Ndoto kuwa One Day YES - tutauchinja!! Tunaishia kuabudu mambo ya ughaibuni na I dare say ngozi ya Mzungu!! Huu ni upumbavu sio na kikomo na lazima Tuamke sio kushinda kwenye internet bila kujenga bali kulalamika tuu na kufanya majungu matupu!

    Mkiwa wengi na furugu, you will achieve NOTHING, in fact you will achiev grand chaos. Mkiwa wengi and well organized, you will achieve excellent great grand results.

    Nyerere na Kambona na Karume na wenzao in their time did the organizing and leo hii tunajiita Watanzania na wengi ama Baba zenu au Mama zenu wamepata elimu kwa Public funds wameweza kuwasomesha leo mnapata elimu hata can log into a computer, badala kufikiria kujenga nchi, ni majungu tuu.

    Wekeni hizo hasira za maendeleo kujenga nchi na kupiga vita UFISADI sio kutukana watu wenye kujaribu kujenga Kuungana. Watumieni hao watu mawazo yenu on what works and what does not work.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...