si vibaya tukakumbushana viongozi hawa wa bara la afrika. wadau tusaidiane kuwatambua

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Yaani hapo nawajui sesse seko, kenyatta, selassie, KK, mchonga, obote

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 11, 2009

    kwa kweli sina uhakika ila kwa mstari wa nyuma namuona kama yuko Rais Milton Obote,Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere,pembeni yake yuko Rais Kenneth kaunda

    Kwa mstari wa Mbele namuona Kama Hayati Mfalme wa Ethiopia kama sijakosea Emperor Haile sellasie,Rais wa Kenya,Kenyatta na pembeni kabisa mwenye kikofia na miwani ni hayati Rais wa Iliyokuwa zaire Rais Mobutu

    kunradhi kama ntakuwa nimekosea

    mdau

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 11, 2009

    Kama sijakosea, mstari wa nyuma kuanzia kushoto wa pili ni Obote, wa tatu Nyerere, wa nne Kaunda (KK) na mstari wa mbele kuanzia kulia ni Mobutu, wa tatu ni Kenyatta na nne ni Haile Selasie. Wengine naomba nikumbusheni. Kumbe ma-pedeshee wameanza siku nyingi, angalia huyo rais wa pili toka kulia mstari wa mbele!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 11, 2009

    alafu pia kama ntakuwa sijachemsha, huyo hapo nyuma ya mobutu ni Rais wa Zimbabwe, yani Rais.Robert Mugabe

    ReplyDelete
  5. Hatuhitaji msaada kuwatambua Nyerere, Kenyatta, Kaunda, Sellasie, Obote, Mobutu, na Seseseko.

    Tunahitaji kujua hii chap yenye suruali kifuani, no-names mbili za nyuma kulia zenye miwani, na hizi Charlie Champlin mbili za mbele kushoto. Them five negros.

    ReplyDelete
  6. Al MusomaMay 11, 2009

    Huyu aliyeko kati ya Mobutu na Kenyatta ni nani? Mbona anaonekaka kama wale wachezajiwa ndombolo ya solo? Au suruali tu?

    ReplyDelete
  7. Mstari wa nyuma toka kushoto: A, Obote, Nyerere, Kaunda, B, C.
    Mstari wa Mbele toka kushoto: D,E, Haile Sellasie, Kenyatta, F na Mobutu.
    NB: Hao niliweka herufi sina uhakika wa majina yao.

    Mdau
    Faustine
    http://drfaustine.blogspot.com/

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 11, 2009

    jamaa walikuwa na personality za nguvu, baadhi walikuwa masela ile mbaya. umeona suruali imevaliwa kifuani hiyo?

    ReplyDelete
  9. GodfatherMay 11, 2009

    Namwona Emperor Bokassa, Emperor Haile Selassie hapo mbele. Nyuma namwona, Mzee Obote, na Mzee Kaunda.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 11, 2009

    Mie pia naowajuwa mstari wa nyuma Kushoto ya hayati mungu amrehemu JUlius Kambarage Nyerere(mwalimu) ni Obote wa Uganda mungu amrehemu pembeni yake kuna Aliyekuwa Raisi wa zamani Kaunda mbele hapo naowajuwa ni Haile salasie na Kenyata mungu awarehemu. na aliyekuwa Raisi kipindi hicho Zaire Mobutu mungu amrehemu mungu ndio anaye hukumu sio sisi.

    Mie pia kunradhi kama nimekosea

    Mdau

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 11, 2009

    Duh! Inaonekana kama hawa waliokwisha tajwa ndio walikuwa maarufu sana, maana hata mie ni hao tu ndio nilioambulia kuwatambua!

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 11, 2009

    SI UTANI MPAKA SASA WATU WAMEAMBULIA WATU WAO WAKARIBU SANA HATA MIE NIMERUKA ILA KAMA KUOTEA LABDA ALIYEVAA KIKOFIA NA FIMBO NI YULE RAISI WA ZAMANI MUNGU AMREHEMU WA MALAWI Dr. Hastings Kamuzu Banda ILA SINA huwakika wengine Nyerere,Kaunda,mobutu,kenyata,haile salasie,obote jamaa pembeni ya Mobute Bouncer alafu suruali alivyoivaa si mchezo hata mwizi akikutana naye ataomba msamaha. Nimejaribu kuibiam ajina kwenye Net ila nimeenda matupu hawa hapa jamaa nyengine pic. Juma.

    http://www.oopau.org/resources/African+Heads+Of+State+At+OAU++May+1963.jpg

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 11, 2009

    Mstari wa mbele kutoka kulia ni Mobutu wa Ziare, Houphet Bounyie (sina hakila na spelling) wa Senegal au ni Ivory Coast??, Kenyata wa Kenya, Haile Selaasie wa Ethipia, Bokassa wa Kongo Brazaville na wa mwisho kusoto mbele simtambui kabisa. Nyuma kuanzia kulia wawili wa kwanza siwajui lakini nadhani mmoja ni wa Ghana na mwingine wa Nigeria maana walikuwepo. Wanafuatiwa na Keneth Kaunda na Baba yetu Nyerere. Wengine siwajui lakini Mugabe asingekuwepo maana hii inaonekana ni kabla hawajapata uhuru wao. Wengine tusaidiane zaidi kujikumbusha.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 11, 2009

    Nyuma na miwani ni Hubert Maga rais wa Dahomey (Benin)?

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 11, 2009

    Mithupu hii picha iko shady kidogo.

    wadau angalieni hii iko clear zaidi...

    http://www.oopau.org/resources/African+Heads+Of+State+At+OAU++May+1963.jpg

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 11, 2009

    Huyo mwenye kofia na fimbo, ambaye mdau hapo juu amemtaja kwa herufi E ni Emperor Jean-Bedel Bokassa...

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 11, 2009

    Ahmadou Ahidjo Rais wa Cameroon? Pale mbele wa kwanza kushoto.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 11, 2009

    mwenye kikofia mstali wa mbele pembeni ya Aile selassie ni Jean badel Bokassa alikuwa rais wa Afrika kati.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 12, 2009

    enzi zile tai zao zilikuwa ndogondogo!

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 12, 2009

    KENYATA, TANZANIATA, UGANDATA, ZAMBIATA, ZAIRETA, ETHIPIATA, N.K.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 12, 2009

    Picha hii inanikumbusha mashujaa wa afrika kwa wakati ule. hapo palikuwa hapatoshi, hoja zilikuwa makini, wazungu wakisikia mkutano wa OAU walikuwa awapati usingizi, walijua kuwa kutakuwa na hoja nzito na watu wenye vichwa vikali vya kufikili na kutenda.

    Bahati mbaya waliangusha na watu kama Banda wa malawi na mabutu wa zaire,awa waliendelea kuwa vibaraka vya wazungu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...