Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Soni Day iliyopo katika Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga, wakifurahia Msaada wa Kompyuta 8 zenye thamani ya Shilingi Milioni 5.6 baada ya kukabidhiwa radhimi na Mkuu wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba, msaada huo ni mwendelezo wa huduma ya Vodacom Foundition kwa jamii mpaka sasa mikoa 15 ya hapa nchini imekwishanufaika na mradi huo.
Kikundi cha sanaa cha UZAUGALE cha Wilaya Lushoto wakitumbuiza wakati wa hafla ya Vodacom Foundation ilipokuwa inakabidhi msaada wa kompyuta 8 zenye thamani ya shilingi Milioni 5.6 katika shule ya sekondari ya soni day Mkoani Tanga.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 15, 2009

    Ebwana hawa jamaa ndo wanapiga sikinde au bongo flava?.tunaomba utupostie nyimbo yao.Ebwana watu wa lushoto naomba muwasaidie angalau wapate speaker na getear nzuri.wapo serious sana wanaonekana na wanachokifanya

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 15, 2009

    why tanga????????????

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 15, 2009

    Wallah hiyo 'bendi' imenikumbusha mdumange Lushotoooo....in short, huo mdumange, sound inatokea hapo redioni....

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 15, 2009

    ACHA ROH MBAYA WEWE MBONA PROGRAM ILIKUWA ZNZ NA MIKOA MINGINE HUJASEMA!mdau turkey

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 15, 2009

    ACHA ROH MBAYA WEWE MBONA PROGRAM ILIKUWA ZNZ NA MIKOA MINGINE HUJASEMA!mdau turkey

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 15, 2009

    wewe unayeuliza why Tanga, najua jibu unalo na kama huna basi ni kwamba mcheza kwao hutunzwa?? U wish na wewe ungekuwa mtanga si ndio?? mdau USA or Mtanga Halisi. waja leo waondoka leo,

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 15, 2009

    Wee unauliza WHY TANGA, PLZ USIWACHOKOZE WATU WA HUKO, SHAURI YAKO, wee kaa kimya hata wakipewa nini nyamaza ndg yangu yatakukuta MAKUBWA, shauri yako, nakuonea huruma kumbuka unaongea kuhusu TANGA!!!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 15, 2009

    Weee HATER unauliza kwa nini TANGA, njoo TANGA TUTAKUJIBU...

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 15, 2009

    Tanga ndo kwenyewe, peleka Makopyuta tukasome sie, Lushoto Bomba sana, kama hujapata kufika fikiria kufanya hivyo. Tanga Oyeeeeeee, Elimu juu, Kompyuta njooo na vingine zaidi.shukrani kwa kutujali.

    Mgosi mwenyewe.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 16, 2009

    Why Tanga?
    The Answer ni
    Tanga waliandika proposal zikajibiwa na ili kuepuka gharama project zote za Tanga hiki ndio kipindi chake. Na nyie Kigoma, mkiandika matajibiwa.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 16, 2009

    kichwa cha habari hakijatulia

    vodacom...."kuwaga"......???

    kuwaga ndo nini??

    bongo siku izi naona viswahili vimebadilika km vinarudi nyuma vile?

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 16, 2009

    nimeipenda sana iyo redio picha ya mwisho.....

    ukumbusho mzuri,jamen mkiichota msiitupe iweken makumbusho

    tanga bwana???

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 17, 2009

    Te,te,te,te,te,....some things never change at all...Tanga bado kuko nyuma sana...mama yangu alisoma Tanga, dada yangu, kaka yangu alikuwa Soni seminary na mie hivi miaka ya nyuma bado tambarare tu jamani....Makubwaaaaa

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 17, 2009

    mbona huulizi TRA NA KILIMANJARO?ACHA MAJUNGU ULITAKA TANGA ISISAIDIWE? KWANI TRA BADALA YA KUWEKA MZANI WA KIPIMO TANGA KWENYE BANDARI WAKAPELEKA KIPIMO KILE KILIMANJARO ILI MANUFAA YAENDE KILIMANJARO ILIHALI HAWANA BANDARI. MBONA HUKUHOJI? HIZI COMPUTER NANE NDIO ZIMEKUTOA ROHO?

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 19, 2009

    we UNAESEMA TANGA kuko NYUMA halafu ukoo wenu wooote mmeenda huku huko KUPATA ELIMU, AKILI YAKO INA AKILI KWELI?????????????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...