
Marehemu Faraji Badili akipimwa uzito kabla ya pambano lake la mwisho hivi karibuni

Marehemu Faraji (shoto) katika mpambano wake na Rashid Matumla mwaka juzi.

Marehemu Faraji (shoto) akicheza na Chaurembo Palasa mwaka jana
Tasnia ya masumbwi ya kulipwa nchini imepoteza mpiganaji wake hodari, Faraji Badili, aliyefariki leo asubuhi baada ya kuzirai akiwa katika mazoezi jana jioni jijini Dar.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa BigRight Promotions, Ibrahim Kamwe, marehemu Faraji ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 26, alikuwa bondia hodari ambaye katika michezo yake toka akiwa kwenye ndondi za ridhaa alionesha ukomavu wa hali ya juu.
Marehemu Faraji alijiunga na ndondi za kulipwa Oktoba 28, 2000 na miaka mitatu baadaye akajipumzisha ili kuendelea na shule. Akarejea ulingoni mwaka 2007 na kufanya vyema katika mapambano yake ambapo katika gemu 7 alishinda 5, tatu kwa K.O, alitoa droo moja na kushindwa moja.
Kamwe amekishukuru chama cha Pugilistic Syndicate of Tanzania (PST) pamoja na mabondia wote kwa ushirikiano waliouonesha kwa marehemu ikiwa ni pamoja na kutoa michango ya hali na mali kufanikisha mazishi yake.
Marehemu Faraji Badili amezikwa jioni hii katika makaburi ya Kinondoni Muslim, Dar, katika mazishi yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa ndugu, jamaa, marafiki na wadau wa ndondi.
Mola ailaza pema roho ya marehemu Faraji Badili - Amina
duh,so strange ilikuwaje? anyway Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahala pema peponi kwani hiyo ni njia ya kila mmoja wetu.
ReplyDeleteMwenyezi Mungu amwepushe na moto wa jahanam. Kisha Ali Matumla ana umri gani? He was boxing during my early undergraduate years - which is about when the late Faraji (26 years old) was probably born.
ReplyDeleteI am so sorry for that. Lakini kwa ushauri wangu huu mchezo tuwaachie wenyewe ambao wana good medical facitities. Maana kabla na baada ya kila mchezo wanafanyiwa check up ya nguvu ikiwa pamoja na CT scan n.k kitu ambacho ninawasiwasi kama hapo nyumbani bongo kinafanyika.Nakumbuka kunaboddia mwingine alikufa Dar muda mfupi baada ya kuingia uwanjani.
ReplyDeleteSuch a young life lost..may God rest his soul in peace. Poleni wanandugu
ReplyDeleteMungu amlaze mahali pema peponi,kitaaluma amefariki na ugonjwa mmoja wa moyo unaoitwa ''hypertrophic cardiomyopathy'',ni ugonjwa ambao unaua wanamichezo tu,hata marc vivian foe,mungu awarehemu wote
ReplyDelete