wadau wa kila aina wakijumuika katika mazoezi ya pamoja mazizini beach maarufu kama 'kitambi noma'

Brother Michu,
Jana asubuhi (saa 12:00) kulifanyika mazoezi ya viungo ya Pamoja huku Zenj kati ya “Mazizini Beach Exercise Group” linaloongozwa na Kocha mahiri Said Sugu na “Kitambi Noma”.

Mtanange huu ulifanyika katika viwanja vya michezo vya Stone town School iliyopo Migombani. Kwa kawaida makundi yote huwa haya yanafanya mazoezi kila siku isipokuwa Ijumaa katika beach maarufu inayoitwa Ngazi Mia (nyuma ya Ikulu ndogo) na wana utaratibu wa kualikana katika joint perfomance.

Washiriki ni watu wa makundi mbali mbali wakiwemo akina mama, vijana, watoto, wafanyabiashara na “Vibosile” kutoka kila kona ya Mji wa Zanzibar, na wadau wote munakaribishwa. Tafadhali post picha hizi kwenye blog ya jamiiUkija Znz nitafute nikulepele Ngazi mia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2009

    Hahaahahah Kitambi Noma neno zuri hilo, Ila kama watu wanakimbia tu wakazani kitambi kitapunguwa bila mazoezi mengine na kuwacha pombe au vyakula vya ovyo basi mnajidanganya,

    Mwisho kitambi kitapunguwa zitabaki nyama zinaninginia doh.

    Muombeni mungu amkeni mapema Swalini Swala 5.

    Kunyweni maji ya uvuguvugu na vyakula vya majani na Vyakula vya baharini ndio muhimu. Punguzeni Amiraaaaaaaaaa hizo. Mtanga.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 01, 2009

    HIO SAFI SANA WADAU WA ZNZ ,MAZOEZI NI MUHIMU SANA KWA BINADAMU NA HUO NI MFANO WAKUIGWA.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 01, 2009

    Mchangiaji wa kwanza, kwa taarifa yako Watu wengi wakimaliza Swala ya Afajiri ndio wanakwenda ktk mazoezi na baadae kuelekea kutafuta rizki.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 01, 2009

    nyongeza kwa 2:23PM
    ...lakini huwezi kuomba mungu akuondolee kitambi. kama ni kweli hayo mazoezi yasingekuwepo

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 01, 2009

    Jamani mie anon wa kwanza sioni kama kakosea Kumuomba mungu ni muhimu kwa mengi tu ukiamini litakuwekea sawa Unamuombam ungu na mazoezi unafanya na Pombe wacheni kasema kweli lakini. ila si kwamba unaswali na mazoezi hufanyi kama unaamini mwenyezi anauwezo wakukusaidia kwa mengi. kitambi kama unaona kipo kama marazi basi unamuomba akupunguzie kitambi marazi yatoke, Kitambi kama hukioni kama marazi basi huna haja yakufanya hilo zoezi. Jafar. Haya Mazoezi ni mazuri mfano wak uigwa.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 02, 2009

    afadhali wazenji

    mana mmezidi kulegea,mtepweto

    zoezi-zoezi

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 03, 2009

    Hahaha Kijana Kaza Ulimi sio Kulegea ni Kuregea.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...