BABU SIKARE A.K.A ALBINO FULANI

Babu Sikare si jina geni mjini Columbus Oh ni kijana machachari mwenye mbwembwe na ucheshi na kipaji kikubwa cha kughani na kutawala jukwaa ambacho kinajulikana na wachache, yeye ni mzaliwa wa Daressalaam nchini Tanzania.

Amezaliwa na ulemavu wa ngozi (Albino) lakini si wengi wanaotambua hali hiyo kwani wengine wanadhani yeye ni “mzungu” lakini hilo halimzuii kuonyesha cheche zake wala kufurahia maisha yake.

Babu Sikare aka Albino Fulani ameamua kupambana na mauaji ya Albino Tanzania akiwa amekulia Dar na kusoma Oysterbay Primary, anasema anakumbuka wenzake walikuwa wakitemea mate mashati yao ili wasigeuke Albino wakati alipokuwa shule ya msingi na kitu ambacho kamwe hatasahau ni kitendo kama hicho kufanywa na mwalimu wake!

Hivyo akiwa amehamia Marekani kiasi cha takriban miaka sita na nusu iliyopita kwa masomo ameguswa mno na hali ya mauaji nchini Tanzania na Burundi na hivi sasa anafanya juhudi za kupambana kuokoa maisha ya wenzake hao na ameamua kutoa single ya kwanza iitwayo “Barua kwa Mama” hii ni kisa cha kweli baada ya kumpoteza mama yake mzazi hayati Grace Mwasi Sikare.

Albam yake kamili bado iko jikoni inapikwa hapa Marekani na anashirikiana na wanamuziki kama vile Mkali Fulani, Mtaalam Fulani, Chid Benz na Tinted pamoja na mambo mengine ya maisha ya kila siku album hii itaelezea maisha ya Albino kuwa ni sawa na watu wengine wa kawaida.

Single yake hiyo itazinduliwa Columbus Oh 20/06/09 katika ukumbi wa Boomerang. Wadau wa Columbus, Indiana, Michigan na vitongoji vyake mnakaribishwa sana.

Wakazi wa Dar na vitongoji vyake wajiandae kwani Babu Sikare anategemea kutoa albamu yake Tanzania mwezi Julai ambayo itakuwa na nyimbo 9 na itakwenda kwa jina hilo hilo la kwake “Albino Fulani”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Big up Babu Sikare, nimefarijika sana na hatua yako ya kujitolea kuwasaidia watu wenye ulemavu wa ngozi kwa kutumia kipaji chako alichokujalia mwenyezu Mungu. Hakika sisi wote tutakuwa bega kwa bega katika hilo. Nakukumbuka sana tangu ukiwa Tanga, kwani kaka yako alikuwa rafiki mkubwa na kaka yangu. Ndugu zangu watanzania tuungane kwa nguvu zote kuweza kutokomeza haya mauaji. Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 17, 2009

    I like Babu so much.. tangu enzi za Forodhani. im so proud of you... you are talented ... keep it up, all the best. im gonna buy your album.
    forodhani alumni

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 17, 2009

    Du! kumbe mambo ya kuwaona ndugu zetu Albino namna mbalimbali zisizo sahihi, hata katika jamii ya kisomi Dar-es-Salaam Oysterbay haina tofauti na maeneo mengine.

    Kweli wana harakati inabidi wafanye kazi ya ziada kuhakikisha hali hii ya imani potofu kuhusu ndugu zetu Albinos haiachi kuwafunza watu wa tabaka zote iwe wasomi, watu wa kawaida, maeneo ya 'uzunguni' au uswahilini, maana Ndugu yetu Fulani ametufahamisha kazi kubwa inayotukabili.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 17, 2009

    Babu pole sana kwa unyanyasaji uliokupata pale osterbay primary ni mwalimu nani huyo khaa!!aibu,mi nilisoma Dakawa na wewe pia nakumbuka kweli ulikuwa kama mzungu,videmu vilikuwa vinakuzimia bse your so handsome usivunjike moyo kwani your handsome ,intelligent like other man.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 17, 2009

    Nakupa Big Up sana Babu nakumbuka tulikuwa kidato kimoja pale USAGARA SECO pande za Tanga.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 17, 2009

    big babu sikare.....this is Malick from Usagara sec.
    maliqmsk2000@yahoo.com

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 17, 2009

    Babu I love you and you are one big star already. Your new hit "barua kwa mama", just makes me dance with tears on my eyes and a smile on my lips. I am your fan on facebook and for those who are not, check it out here for more of his hits and pictures:
    http://www.facebook.com/pages/Albino-Fulani/206739360602

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 17, 2009

    Yep yep yep!!Kanyaga twende mwanangu.

    Mkulima-Kijijini Gezaulole.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 18, 2009

    hey babu big up,kaza buti mshkaji being albino haimaanishi ukate tamaa.Nakumbuka forodhani watu walivyokuwa wanatema mate vifuani.wakiogopa watazaa ma albino.Good start keep it going!!!

    krissie(ex-classmate, forodhani)

    Pitt,PA

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 18, 2009

    aisee

    kumbe hii ni newz ya kweli??i thought its just a story kule facebook bwana dah

    hongera sana,tunaunga mkono juhudi zite

    ila wee ni kijana au babu ni jina lako??

    shukran

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 18, 2009

    BIASHARA,nani anajua address ya huyu jamaa??Hizo ni hela jamani

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 19, 2009

    Hongera sana babu,keep it up. We are proud of you.

    Your sister Darro aka Mariam.

    ReplyDelete
  13. Babu is a great guy, i had the utmost pleasure to do his portraits for me at my house, can't wait for the album

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...