Wanakijiji wa kijiji cha Singi'si wilayani Arumeru wakibomoa nakuchukua mali za mmiliki wa shamba ambalo wanadai ni mali ya kijiji hicho na kufanya uhalifu mkubwa katika shamba hilo linadaiwa ni la mh. mbunge wa Vunjo mheshimiwa Kimaro.

hapa ni kama wamelifanyia plunning shamba la migomba ambalo liliangamizwa lote na wakaondoka na mikungu ya ndizi.pia katika vulugu hizo askari mmoja alijeruhiwa na kunyang'anywa bunduki ambayo hadi hivi sasa haijapatikana ila wahalifu wapo rumande kuisaidia polisi pia raia mmoja aliuawa katika vurugu hizo.

Mdau wa Vunjo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 11, 2009

    bora tugawane umaskini

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 11, 2009

    Zimbabwe ilianza hivyohivyo

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 11, 2009

    kwa msingi huu hakuna atakefanya ufisadi manake wataogopa hongera sana kwa kazi murua

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 11, 2009

    Pamoja na kwamba ni katika kisingizio cha mali ya kijiji, lakini ni kawaida ya Wameru kutokupenda kuchanganyika na Watanzania wengine. Kila mara wawo wanakuwa na migogoro hata pale ardhi ni mali ya serikali. Nakumbuka kuna wakati serikali ilitaka kujenga Kijiji cha sayansi, International Science Village. Walikogama, kuna wakati kanisa lilitaka kujenga uwanja wa ndege walikataa. Nadhani mtakuwa mnakumbuka Mgogoro wa kanisa la KKKT miaka hiyo. Mji wa Arusha umeshindwa kuwa jiji kwa sababu yao. mashamba mpaka katikati ya mji kisa hawataki maendeleo. Wataki hata uendelevu wa mji kuwa jiji

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 11, 2009

    Nawapongeza wanakijiji kwa msimamo waliouchukua,Ipo siku tutafika tu, Ata wakoloni walitufanya hivyihivyi badae ushindi ukapatikana.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 11, 2009

    Hawa wananchi vipi ni ujinga au wivu?? kama nikunyang'anya mashamba si wangeanza za wahindi, wazungu kuliko mzalendo mwenzetu? au ndio ile kasumba afadahli mzungu tajiri kuliko mwafrika tajiri tutaacha kasumba hii lini?
    pale arusha kuna mashamba mengi tu wa "wazungu, Wahindi, kwanini ya mwenzetu? Jamani I hate this behaviour.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 11, 2009

    Serikali ikijisahau wananchi uikumbusha.Hongera wananchi.

    ReplyDelete
  8. Mdau ArushaJune 11, 2009

    Mbunge Kimaro " Wanavamia shamba langu mimi mzawa la ekari 250 tu wakati kuna Mzungu jirani yangu ana ekari zaidi ya 1000 wanamwacha tu" Sasa huyu ni kiongozi wa wananchi kajaa ubinafsi na ubaguzi namna hii. Wadau mnasemaje ??

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 11, 2009

    Maumivu ya kichwa huanza polepole na taratibu !!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 11, 2009

    Hivi jamani Arumeru ipo Vunjo? Vunjo si ipo Moshi vijijini?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 11, 2009

    Does peace really pay?

    Kila siku tunajifanya nchi yetu twajivunia amani. Kumbe amani hiyo wanaenjoy ni wachache tu na wanaoifilisi nchi.

    Bongo wachache sana ndio wanaishi na wengine wanasindikiza.

    Watu wananjaa hawajui kesho watakula wapi hHebu ona sasa mtu ameuawa kwa ajili ya mambo haya.

    Inabidi viongozi wakomeshe hii tabia ya kuvamia mali za watu lakini pia serikali ionyehse kuwa inawachunguza hawa viongozi wanaotajirika mara tu wanapochaguliwa. Kila kiongozi aonyeshe amepataje hela yake na kuwe na limitation ya kiongozi yeyote kupokea zawadi kutoka kwa raia.

    Really watu wamechoka kuona viongozi wanaishi maisha kama wako nje ya nchi na ni maisha ya nchi zilizoendelea.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 11, 2009

    Ndio jana mnamshauri Lilly arudi nyumbani. Mmmmmhhhhh sirudi ng'o kama mambo yenyewe ndio haya. Mimi sina nguvu. Nguvu zangu zinatosha kunyanyua box tu

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 12, 2009

    Wadau tuwapongeze wenzetu hao.Na tunawaheshimu sana sana kwa kufanya ujasiri huo.kwani tulitaka pia mwekezaji aliyechukua eneo la wahzabe nae akimbie sasa hivi tunakuja.ndugu zetu wanakosa sehemu ya kufanya shughuli zao.Ninawapa heshima vile vile jamaa zetu waliobomoa uzio pale mnazi mmoja ,sehemu ambapo tulisherekea uhuru wetu.Lakini pali uzwa kwa mhindi mmoja. lakini watu wenye uchungu wa nchi hii walibomoa na kuchukua bati.DAWA YA MAFISADI SIO SERIKALI ILA NI WANANCHI WENYEWE.TUMECHOKA SANA SANA.WANA TUCHEZEA AKILI KILA SIKU.KAMA INGEKUWA TUNALIPA PESA ILI BABA WA TAIFA ARUDI DUNIANI NINGEKUWA MTU WA KWANZA KULIPA ILI ARUDI.MZEE ALIONA MBALI SANA.ALISEMA MALI ASILI HIPO ,LAKINI MNATAKIWA MPATE AKILI KWANZA ILI MUWEZE KUITUMIA VIZURI.SASA MNAONA ETI TULIKOSEA KUSAINI KWENYE HUU MRADI WA MGODI MARA ULE MARA KULE.LAKINI HAWA NI WATU WAZIMA NA WENYE AKILI.TUMECHOKA ,BABA WA TAIFA [NYERERE RUDI HARAKA]TUNAKUOMBA.MUNGU MPE NAFASI NYINGINE HATUNA WATU WENYE KUKEMEA HAPA TANZANIA.

    ReplyDelete
  14. Mkuu wa Mkoa adai vurugu za Sing’isi zimetokana na uhaba wa ardhi

    Na Neema Werema Arusha


    MKUU wa Mkoa wa Arusha, Isidori Shirima, amesema vurugu zilizotokea hivi karibuni katika shamba la Madira katika kijiji cha Sing’isi wilayani Arumeru, zimesababishwa na uhaba wa ardhi kwa wananchi.


    Shirima aliyasema hayo jana alipokuwa akitoa taarifa ya awali,kuhusu fujo hizo zilizotokea Juni 7 mwaka huu, na kusababisha watu kujeruhiwa na mali kuharibiwa.


    Katika tukio hilo, wananchi wa Sing’isi, walivamia shamba lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 55, linalomilikiwa na Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro na kuharibu nyumba 15 za mazao.


    Wananchi hao wanadai kuwa hawako tayari kuona eneo kubwa kiasi hicho linamilikiwa na mtu mmoja, wakati wao wakiwa hawana ardhi.


    Akizungumzia vurugu hizo ambazo Kimaro amezihusisha na mambo ya kisiasa, Shirima alikanusha madai hayo na kwamba zimetokana na uhaba wa ardhi,kwa wananchi wa Arumeru.




    Pia alisema uwekezaji wa Kimaro katika eneo hilo ni kujenga hoteli na si kulima mazao, kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti.

Hata hivyo alisema hatua zilizochukuliwa na wananchi kama njia ya kugombea ardhi, ni za ukiukwaji wa sheria za nchi.


    
 Alisema kwa sasa sekretarieti yake kwa kushirikiana na viongozi wa
 wilaya kata na vijiji, inafanya uchunguzi kuhusu vinara wa vurugu hizo, ili sheria ichukue mkondo wake.


    Tayari watu 38
 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani na wengine 36, wanaendelea kuhojiwa.

 Mkuu huyo wa mkoa alisema kwa sasa hali ya usalama katika eneo hilo, imerejea kuwa ya kawaida na kwamba watu wanaendelea na shughuli zao za maendeleo.


    Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Basilio Matei, alisema, uchunguzi wa awali umebaini kuwa kinara wa vurugu hizo ni kiongozi mmoja wa Chama cha TLP, ambaye bado anasakwa.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 12, 2009

    Muosha huoshwa,kwa sisi wachagga huwa tunaneno tunasema "TONDO",huyu Kimaro ni Tondo kabisa ameingia kwenye siasa kichwa kichwa hiyo ndiyo impact yake

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...