Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. James Msekela
(kulia) na Meya wa zamamani wa Dodoma, Peter Mavunde baada ya kwasili kwenye
uwanja wa ndege wa Dodoma kwa ajili ya kikao cha Bunge la Bajeti
kinachoptarajiwa kuanza leo.

MKUTANO wa 16 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano unaotarajiwa kuanza mjini Dodoma leo utachukua mwezi mmoja unusu na si kwa miezi mitatu kama ilivyo kawaida yake.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na kitengo cha habari cha Bunge inaonyesha kuwa mkutano huo unatarajiwa kumalizika Julai 31 wakati mjadala kuhusu hotuba ya bajeti utakuwa wa siku tatu kuanzia Juni 15 hadi 17.

Kwa mujibu wa Afisa Habari Mkuu wa Bunge, Ernest Zullu aliyetoa ratiba hiyo, mjadala wa makadirio ya wizara mbalimbali utafanyika kuanzia Juni 18 hadi Julai 27.

Wakati ratiba hiyo ikionyesha idadi ya siku za vikao hivyo kupungua kesho JK anatarajiwa kuwahutubia wabunge wote na wazee wa mkoa wa Dodoma katika ukumbi wa Kilimani mjini hapa mara tu baada ya kipindi cha maswali na majibu.

Awali ratiba iliyotolewa na kitengo cha habari cha Bunge ilionyesha kuwa JK angelihutubia Bunge (bungeni) lakini ratiba hiyo imebadilishwa na sasa Rais atawahutubia wazee na wabunge wote hiyo kesho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2009

    Hiyo ndege ikawachukue watoto wa JK kwenda shopping angalau Nairobi. Mbona watoto wa Obama wameenda Paris kufanya birthday na UK shopping na watu hawapigi makelele wala nini na bado wanamuona Obama kama mungu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 09, 2009

    WIZI MTUPU.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 09, 2009

    Ukiangalia picha hawa wakuja ndio wanaizamisha Tanzania! Zero Exposure!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 09, 2009

    Hii ni kama Bajeti ya Mwisho ya serikali ya Rais Kikwete katika muhula wake wa kwanza wa miaka mitano.Bajeti ijayo japo ndiyo ya mwisho lakini utekelezaji wake hakika utaanagukia mwaka wa 2011 ambao utakuwa mwaka wa kwanza wa awamu nyingine kabisa ya Utawala mpya baada ya Uchaguzi Mkuu ujao wa 2010.Na hakuna mwenye uhakika iwapo Kikwete atateuliwa tena na chama chake cha CCM kugombea tena Urais wa nchi kwa awamu nyingine ya pili ya utawala.Au hata kama atateuliwa tena na CCM kugombea "iwapo atashinda tena uchaguzi ujao!".Kwa hiyo maana hiyo Bajeti hii ya 2009/10 ni Bajeti ya Kufa Mtu.Watanzania walio wengi hususan vijijini "wamekata tamaa kabisa ya maisha" kutokana na Siasa za muda mrefu za "Mali Kauli bila Vitendo!",licha ya rasilimali lukuki zilizopo katika majimbo yao ya uchaguzi.Bajeti hii haitakiwa kuwa ya KUBAHATISHA.Au ya KUZIDI KUTOA AHADI ZA UTEKELEZAJI.Itatakiwa itoe majibu ya kwanini hili halikutekelezwa na vipi hili bado limepewa kisogo na kusindikizwa na rundo la ahadi hewa.Ni Bajeti Ngumu sana.Watanzania wamechoshwa na Mzigo wa Kodi zisizo na Tija.Kilichobakia kutozwa Kodi hapa nchini "Labda ni Hewa tu tunayopumua-Oxygen!".Lakini fikiria upuuzi mwingine wowote basi ujue utatozwa Kodi.Kodi hiyo inakwenda wapi?Matumboni mwa Viongozi na Watendaji Wakuu Serikalini.Bajeti hii itatakiwa itudhihirishie ni kwa kiasi gani Rasilimali zetu wenyewe hapa nchini "zimetupunguzia Utegemezi kwa wafadhili wa Nje!"Hatutaki Story za Alinacha kujenga ghorofa jangwani!Au za Kuch Kuch HOTAHE!Hapa ndipo mwisho wa Reli!Uongo wa wanasiasa wetu utakapo UMBUKA!Wabunge wengi ndio utakao kuwa muda wao wa mwisho wasikike ili kujipalilia wachaguliwe tena mwakani,na hilo litakuwa gumu sana!Ngome ya Upinzani ikiongozwa na CHADEMA imekuwa ikikubalika zaidi miongoni mwa wapiga kura nchini,hususan Vijana ambao ndio walio wengi hapa nchini,kwa hoja zao na kile walichokisimamia na kukitetea kwa maslahi ya nchi na Taifa kwa ujumla!Wabunge wengi wa CCM watabwagwa chini katika uchaguzi mkuu ujao,na hilo sio la utani!Kwa hiyo CCM bado ina kibarua pevu katika kuwastaafisha wabunge wake wakongwe walioligeuza Bunge kama "MGAHAWA WAO WA KISIASA" badala ya Nyenzo ya Ukombozi na kutokomeza Ufisadi nchini!Hebu tuchangie Hoja hii.Je,Bajeti ijayo itakuwa kama nyinginezo zilizo pita za Kupotezeana Wakati?Au itakuwa ndio Mwanzo Mpya kuelekea kwenye Neema na Mafanikio zaidi?Au Watanzania wataendelea kuwa wasindikizaji tu katika nchi yao wenyewe,miaka 47 baada ya Uhuru?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 09, 2009

    MH pinda haya sasa tunasubiri utekelezaji wa maazimio ya tume ya Mwakyembe,maana umeyapiga danadana ukafikiri siku hazifiki,wapiga kura bado tupo hai piga blabla zingine uone matokeo 2010! tunasubiri RICHMOND,HATMA YA MIKATABA MIBOVU, NA UTENDAJI MBOVU BANDARINI na mwisho utuangalia wafanyakazi kwenye P.A.Y.E mnatuua, tulilipa kodo kubwa kuliko mfanyabiashara mwenye faida kubwa.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 09, 2009

    Ndugu Michuzi plz ndugu yetu acha kutubania comment zetu . sijui hata kwa nini tukituma comment zenye kugusa mahala pake unatubania sio mbaya. lakini hiyo inadhihirisha wazi kuwa wewe ni mmoja wa waleeeee. wewe mtoto wa aggrey unakuwa kama wa kuja ndugu yetu. au mpaka kaka zako kina melabon , chang'walu , chamenya na maina kavu wakiandika ndio utaziweka ? pamoja na kina Mafuru na Lyongo maana hao unawaona wajanja kwako. mdau wa Gerezani.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 10, 2009

    naungana na June 09, 2009 10:45 PM hata mimi najiuliza ni kwanini au kuna watu wanaosponsor hii blog kwa mlango wa nyuma?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...