-----------------------------------------------------------
Mpiganaji mwenzangu Michuzi,
naomba kwa kupitia blog ya jamii, nitume salam zangu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa, jumuiya ya wasomi 'Mlimani' na duniani kote na kwa Watanzania wenzangu kwa kuondokewa na mwanazuoni tunu yetu na niliyemheshimu sana ndugu yetu Profesa Haroub Othman.
Pigo hili limenikumbusha lile la hivi karibuni lililowakuta wasomi wa dunia na sisi 'wapiganaji' pale alipotutoka Dk. Tajudeen kwa ajali ya gari kule Nairobi.
Pia nichukue nafasi hii kutuma rambirambi zangu kwa familia, ndugu, jamaa na Watanzania wote kwa kuondokewa na rafiki yangu na mzee wetu Sheikh Suleiman Gorogosi ambaye kwaye mawaidha yake yaliyojaa hekima yalikuwa hayamithiliki na niliyaheshimu mno.
Wote, naomba Allah azihifadhi roho zao mahali pa amani daima--AMINA.
Mdau Saidi Msonda,
Wote, naomba Allah azihifadhi roho zao mahali pa amani daima--AMINA.
Mdau Saidi Msonda,
Sudan.
Pumzika mahala pema Peponi baba inatia uchungu sana.Tutazidi kukumbuka na kukuombea zaidi maana hiyo ni njia ya kila mmoja wetu.
ReplyDeleteRest in peace.
mdau
mICHUZI HUU NI MFUMO DUME NINI? MBONA WAOMBOLEZAJI WANAWAKE HAWAPO KATIKA PICHA? AU TUELEWEJE?
ReplyDeletetutakukumbuka baba yetu, babu mpendwa, PROF. HAROUB.
ReplyDeleteMungu akulaze pema peponi na kila la heri likutangulie hko uendako.
tutakuwa nawe kiroho kwani kimwili ndio haupo nasi tena.
R.I.P
Walikuwa maelfu kwa hakika, si mamia...
ReplyDeleteAnon wa pili unamaana gani ukisema mfumo dume? wanawake unawataka wa nini? wamekulalamikia kwamba hawakuwepo iliwauma? nadhani ni wakati tuheshimu taratibu za imani za wenzetu sio kila kitu lazima uchangie. Heshima kwa dini ya wenzako plz u r grown up now
ReplyDeleteRest in peace Uncle!
ReplyDeleteThanks for everything!
Mzee kwa kweli amezikwa,yaani umati wote huo.Hiyo inaonyesha ni jinsi gani alivyokuwa mtu wa watu.Mungu akuangazie na akuweke mahala pema peponi.
ReplyDeleteMkulima-Kijijini Gezaulole
sisi ni wa Allah na hakika kwake tutarejea, hakika ya mauti ni mawaidha kwa waumini. hakuna aliyetaraji kua prof angetutoka kwa wakati huu, lakini kazi yake allah haina makosa. mungu akusameh na akupe kauli thabit huko wendako.
ReplyDeletepoleni wafiwa na wazanzibari wote.
mdau coventry university.
M/mungu anlaze mahali pema peponi Amini kwani sisi sote twaenda huko uko ila tu pia tuwape pole wale jamaa wote.
ReplyDeletekwani huyo jamaa hapo juu anataka kujua kuhusu wanawake kwani wewe ujui kuwa pale ni msikitini sio kanisa na pia wacha ujinga kua na heshima ya kueshimu dini za wezako.
Ndambe uk
He was a man of substance. May Almighty God rest his soul in eternal peace.
ReplyDeleteR.I.P - Haroub