Dear Kaka Issa,
Kaka mimi ni mdau mzuri wa blog yetu hii ya jamii na napenda kukupongeza sana kwa kazi nzuri unayoifanya. Nina swali naomba ulikifishe kwa wadau waweze kunisaidia kupata ufumbuzi.
Ningependa wadau mnisaidie kunitajia ni wapi kuna Garage ya kuaminika ya kufanya service ya Subaru hapa Dar na maduka ambayo naweza kupata spare parts za uhakika.
Nimepata Subaru Forester karibuni na ningependa kujua maeneo muhimu ya kuendelea kuliweka katika hali nzuri wakati wa service na matengenezo madogo madogo yatakapohitajika. Natanguliza shukrani.
Mdau Amani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 13, 2009

    Wasiliana na Fund Joseph 0784219599 au 0719110136 ni fundi mzuri sana

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 13, 2009

    Mdau Amani, Naamini kama ulinunua JApan, kampuni waliokuuzia wanaweza kukupa huduma ya spare. Service garage yoyote Dar wanafanya mradi tu uwaamini na ujuzi hao unaowatumia. Kama waliokuuzia hawana uwezo kukupa service ya spares, sema tujaribu kukuangalizia huku huku jikoni/japan.

    Asante
    MdauzJP

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 13, 2009

    Lazima wewe ni muhaya Ok umenunua subaru tumekwisha jua

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 13, 2009

    MIMI NINA GARI KAMA LAKO MWANZO NILISUMBUKA SANA PALE NILIPATAKA KULIFANYIA SERVICE LAKINI RAFIKI YANGU ALINIELEKEZA KWA FUNDI MMOJA ANAITWA SAIDI YUKO MAGOMENI IDRISSA NAMBA YAKE 0784 448 141 NI FUNDI MZURI SANA NA YEYE ATAKWAMBIA WAPI AU DUKA GANI UTAPATA SPEAR NZURI

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 13, 2009

    mdauzJP hapo juu naomba contact zako kama hutamind,mie pia niko ughaibuni na ningehitaji kupata mkoko tokea hapo ina nahitaji mtu wa kuaminika kuniangalizia kwa macho.nilitaka kupitia kule kwa mzee MT.lakini nikaona sio deal sana wao wanamambo yao ya kiofisi.
    naamini hutamind bwnana kaka.
    mdauMP.

    ReplyDelete
  6. Nyerere road ukiwa unatokea TAZARA kabla hujafika vingunguti upande wa kulia kuna kampuni moja ina bang wanatengeneza magari kibao likiwemo hilo la kwako, sijakariri jina lake ila jaribu kuangalia utaona manake bango lao liko clear.

    Goodluck.

    ReplyDelete
  7. Nyerere road ukiwa unatokea TAZARA kabla hujafika vingunguti upande wa kulia kuna kampuni moja ina bang wanatengeneza magari kibao likiwemo hilo la kwako, sijakariri jina lake ila jaribu kuangalia utaona manake bango lao liko clear.

    Goodluck.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 13, 2009

    we nenda zako gerezani k/koo kila kitu chawezekana kwa reasonable price mafisadi watajifanya wao babkubwa lakini wanataka tu wakufilisi achana nao,fundi joseph ni mchaga mmoja mwizi tu yeye mwenye spare anapatia huko gerezani,you don`t need him

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 13, 2009

    Mpelekee Fundi wa Michuzi achukue Viwili vya gari akuwekee kimoja.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 13, 2009

    wa cheki jamaa wanaitwa Berkshire Autoshop wapo shoka 0222667213 DSm jamaa wako njema na vifaa vya kisasa mshikaji kasomea mambo ya kujipaka grease ng'ambo wako poa sana na vifaa vya kisasa

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 13, 2009

    GEREZANI KARIAKOO KILA KITU UTAPATA, FUNDI NA SPARE, UKIKOSA YA SUBARU HATA YA ISUZU UTAUZIWA NA ITAFAA

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 13, 2009

    Wasiliana na Mzee Viriyala, ni fundi wa siku nyingi wa Subaru tangu enzi zile polisi na Railway wanatumia subaru mpaka leo hii. Namba yake 0717 939939

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 13, 2009

    Bwana Amani,

    Siku nyingine ukinunua kitu hasa chenye thamani kama gari, unamuuliza dealer aliye kuuzia. Kawaida dealer au muuzaji anatakiwa ajue uwezekano wa kupata spare parts na mafundi ambao wanaoweza kukusaidia. Pia, wanatakiwa wajue karibia kila kitu kuhusu products zao na kama hawajui unawapiga mkwala wa kuto nunua. Inabidi wajifunze.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 13, 2009

    Fanya hima sana uende kwenye garage yeyote ile ya wachina. Nakuomba usibabaike wala kudanganywa mitaani, la sivyo utashangaa gari inakuwa na msururu wa matengenezo mpaka utashindwa kuiuza

    GJK

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 14, 2009

    Jamani tafadhalini hata mimi naomba msaada na ushauri toka kwenu, natarajia kununu gari aina ya mitsitubishi lakini sinauhakiki na upatikanaji wa spare. Naomba watu mlipo nyumbani (TZ) mnisaidie tafadhali. Natanguliza shukrani zangu kwa yeyeyote atakenipa ushari. Asanteni saana

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 14, 2009

    JAMANI TZ ALMOST KILA KITU KIPO NI PESA YAKO,AUTHORISED DEALER WANASOFTWARE ZA SUBARU,BMW,MINI COOPER NK NI NOBLE MOTORS LTD UKIPITA TAZARA KAMA WAENDA AIRPORT MKONO WA KULIA HATA ANAYEKUJA NA MITSUBISHI NAO WAKO ENEO HILOHILO WANAITWA DIAMONDS MOTORS.WABONGO HATUWAJUI MADEALER SABABU TUNAANGALIA BEI YA CHINA HATUJALI UBORA NA USALAMA WA CHOMBO HATA KAMA PESA UNAYO,NA NDIO MAANA MAGHOROFA YATAENDELEA KUBOMOKA NA MAGARI HAYATADUMU.
    MR LWAGA.E.A

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 15, 2009

    Ni kweli kabisa ninawatu ninaojua wanamagari ya kifahari saana na service zao wanazifanyia garage za wachina tu,niwaaminifu saana waweza kwenda na spare zako wao wanafanya service nakumbuka nikiwa Tanzania walikuwa wanawasifu saana wachina walio pale shekilango kuna garage yao sijui jina ila ulizia pale shekilango njia ya kwenda Sinza baada ya magorofa kama waenda sinza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...