Ras Makunja baada ya kumaliza kazi akiongea na mwanamziki Seif Rengwe mwanamziki bingwa wa kupuliza midomo ya bata ambaye pia ni mwimbaji. Seif Rengwe ni mwanamziki aliyetamba sana na bendi ya The TATU NANE enzi zile.kwa sasa anaiongoza bendi ya Reggae ya SIX NATION, ambayo nayo ilishiriki katika maonyesho ya Masala World Beat Festival huko Hannover, Ujerumani, ambako Ras Makunja na kikosi chake cha The Ngoma Afrika kilifunika bovu na midundo yao moto moto toka Bongo
Ras Makunja akiwajibika jukwaani
Mr.Buti Jiwe aka Galinoma Jr. mwanamziki wa Kizazi kipya cha mziki wa dansi anaefanyia kazi nchini Uholanzi, alialikwa na bendi ya Ngoma Africa akiwa kama Guest Artst. Pichani akiwajibika katika jukwaa la kimataifa la masala Festival,mjini Hannover,Ujerumani
Ebrahim makunja aka Ras Makunja akikiongoza kikosi chake kushambulia jukwaa la Maonyesho ya Kimataifa ya Muziki "Masala World Beat Festival"

The Ngoma Africa Band aka FFU ! aka wazee wa kukaanga mbuyu wakiwasha moto wa kimataifa na mdundo wao toka bongo





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2009

    hi! kaka Misupu,kwanza tunakushuru kwa kutuletea habari njema,kuwa wanamziki wetu walio nje wanajituma kiuhakika katika kulitangaza dansi la TZ,tena ushaidi tunauona wazi kuwa onyesho hilo ni kubwa la kimataifa,sio Kitchen paty,sasa ninachojiuliza kulikoni? watu wanajiita maporomota wa kama vile Miss.Tanzania huko ulaya hawawezi kuwashirikisha wanamziki wetu hawa?
    na badala yake wanawaalika bendi zisizo julikana? hapa ndipo ninapaona kuwa wanamziki wetu watambulika kimataifa lakini sisi wenyewe tunawatupia Kisogo.
    Tubadilike.
    Mdau wa K'ndoni,Biafra

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 17, 2009

    kamanda ras makunja,tunakukubali kuwa wewe ni naodha unaeliongoza jeshi katika mashambulizi ya kimataifa,kaza moyo kaka!endelea kuwa na moyo huo huo wa kuwapa shavu wanamziki wenzio,ukisikiwa ukubwa ndio huo lazima uwe na moyo wa kutoa nafasi kwa kila moja.
    Asante kwa kazi yenu nzuri.
    Mimi Mzee wa minyang'u nyang'u.
    Dubai

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 17, 2009

    te!te!te! mwe!mwe! kaka bro ras makunja,kwanza nakupa Big Up kwa tabia yako ya kukomaa kichwa na ffu wako!nasikia pale Hannover ilikuwa mashambulizi tu hakuna kuremba remba.Pia nasikia umenunuliwa miwani mipya ya zahabu?na baba wa kambo hili mmalize zogo?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 17, 2009

    Kwako Anony wa K'ndoni,Biafra.
    Unajua tatizo kubwa tulilo nalo baadhi yetu watanzania ni KASUMBA ya bora kumkarimu mgeni kuliko watoto wako.Itikadi ya kasumba hii inatumaliza sana na tunabaki kuambulia sifa ya kuwavusha wengine na watoto wetu kuwatupia kisogo kama ulivyosema.
    watanzania wenzetu wanaojiita waandalizi aka maporomota wa shughuli mbali mbali wamekuwa na kasumba ya kuwababaikia wasanii wageni kuliko watoto wao! jambo hili sio geni,Ras makunja mwenyewe analifahamu fika,kwani naye kishapita misuko suko mingi mpaka kufika hapo alipo.
    chukulia mfano mdogo tu maporomota hapa nchini wanaingiza wanamziki na bendi nyingi kutoka nje!? badala kutumia fedha zao na kuzitoa nje ya nchi bendi za hapa nchini.
    Kasumba hii si ya leo wala si kitu kigeni,cha kumshauri Ras Makunja ni kuwa yeye aendeleze libeneke lake la kuwasha moto wa kimataifa,pia ajaribu kuwapa nafasi wanamziki wenzie nao wafikie kiwango cha kupiga mzigo katika majukwaa makubwa kama yeye.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 17, 2009

    kamanda ras makunja,naomba nikuulize kijiswali kiduchu tu,lakini kwanza hongera kwa hiyo suti na kiatu umependeza kweli!
    eti bro kaka ras, nasikia hiyo suti uliyovaa ktk picha na sefu rengwe,suti hiyo umepewa zawadi na MAMA KIMWAGA? yaani ni mapoozeo,wazushi wanadai mpaka kiatu kipya cha bei mbaya vyote kagharamia JIMAMA PESA toka upate zawadi hizo siku hizi umekuwa BUBU!
    Madongo atupiwi tena JIMAMA PESA.
    any way hapa umenishinda

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 17, 2009

    unajua hapa barazani kuna watoa maoni wengine ni wachokozi,wanamchokoza mtu mpole tena mtu wa watu.tena watoa maoni wengine wachimbi.lakini mimi sio
    kaka braza makunja mie tupo pamoja nawe hila naomba niulize mbona rasta wengi wapo mbofu mbofu lakini wewe kila wakati ni mshua tu?soap soap si unaona kiatu?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 17, 2009

    mnyonge mnyongeni lakini haki mpeni! Ngoma Afrika wanajituma vichaa nawakubali wakiamua kuwasha moto ni moto kweli kweli

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 17, 2009

    Hivi ni kwa nini mtu akicheza Bolingo lazma awe na expression flani hivi usoni? Hii kitu ni proven, mwangalieni huyo jamaa kwenye picha ya tatu hapo kutoka juu, pia angalieni videos za wasanii mbali mbali wa muziki wa Dansi.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 17, 2009

    kweli makunja mwanamziki aliyekomaa kichwa tena kazi anaijua,lakini kama ukimsikiliza sana nyimbo zake mara nyingine zinagusa moyoni kiasi unaweza kumpiga mtu,katika mistali yake makunja anagusa mioyo na unaweza kujisikia unaandamana mtaani,kutona na nyimbo zake hii ya sasa "furaha ya maisha iko wapi?" na "baba wa kambo" zimenigusa sana moyoni

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 17, 2009

    hiiii FFU mnapofika nyie mambo yote yanakuwa mswano, chi chi,
    kabwana kichwa ketu kanakamua kama hana akili nzuri.
    chibwana kichwa ngumu kaza buti

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 17, 2009

    Galinoma shikamana nao vichaa hao,shughuli wanaijua.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 17, 2009

    Bro Michu,naomba nikuulize swali.Tena nitafurahi kama wahusika(TATU NANE)wataliona hili swali.
    Hivi kile kikosi kilipotelea wapi,maana mara ya mwisho miaka ya tisini ndo niliona nyimbo zao,nafikiri walirekodi kwenye moja ya concert huko Scandinavia.Ooooooh,that was incredible performance,for real!!

    Kwa nini wele jamaa wasikae chini na kufanya kazi pamoja?tatizo ni nini hasa?

    Naomba kama una-access na hao jamaa basi uwafikishie hili swala.

    ReplyDelete
  13. Nathamini sana mchangowa Ngoma Afrika BAND katika kutitangaza nchi ya tanzania.

    kazi nzuri tupo pamoja

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 19, 2009

    Ras Makunja kiboko kichwa ikunjika kama...uhm..makunja

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...