Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
MKUU WA NANIHII....
NAOMBA NIPE LAU NAFASI NIPATE SEMA KIDOGO JUU YA BABA WA TAIFA AMBAYE TUTAKE TUSITAKE ALIKUWA ANAONA MBALI KULIKO INAVYODHANIWA. NAOMBA UWEKE NUKUU YAKE HII KATIKA WAKATI HUU ILI WADAU WACHANGANUE NA KUCHANGIA BILA KUHARIBU HALI YA HEWA.
"DOLA LAZIMA ISIMAMIE SHERIA ILI KULINDA HAKI NA KUHIFADHI AMANI. WAJIBU HUU USIPOZINGATIWA, WATAIBUKA MANABII WENYE KUIHUBIRI HAKI KWA KUWAHUKUMU WENGINE. HAMTABAKI SALAMA MKIFIKIA HAPO"
-J.K. NYERERE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2009

    Neno "manabii wa uongo" linaonyesha uchanganywaji wa din na siasa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2009

    Kwakweli huyu mzee ni kichwa hasaa! Japo alikuwa na mapungufu yake pia ya kibinadamu. Maana hakuna binadamu mkamilifu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2009

    Ama kweli Nyerere ni kiona mbali, hatutampata Kiongozi mwingine kama yeye.Alichosema miaka kadhaa iliyopita ndiyo yanayotokea leo hii, Serikali imeshindwa kusimamia sheria ipasavyo dhidi ya mafisadi(Rostam & Co.)sasa wametokea Manabii(Mengi & Co.)kuihubiri haki.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2009

    Truly, Nyerere was a great Philosopher of our time.

    ReplyDelete
  5. Mkuu kwa maoni yangu kuona mbali hakumpi mtu utukufu.

    Ukipeleleza mara nyingi wahalifu huwa wanaona mbali sana katika harakati zao za kukwepa vyombo vya dola.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 04, 2009

    Ni kweli alikuwa anaona mbali ukilinganisha na viongozi waliomfuata, ila pia kuna mambo mengi aliyoharibu moja ni kuwa viongozi walioharibu baada yake aliwaweka madarakani yeye. Pia system nzima inayotufanya tuendelee kuwa masikini aliiweka yeye maana wakoloni walimwachia nchi ikiwa na hali nzuri. Ni vyema wakati tunasifia na mapungufu pia yasemwe.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 04, 2009

    Acheni upuuzi wenu kuona mbali..?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 04, 2009

    wewe usiwe kama hujaenda school,kusifia hata madikiteta wewe ungejuwa mwl alivyo tesa watu usingesema,kwanza mwalim yote anayoyasema yoko kwenye bibiria,which hata wewe ukisoma bibilia utaona yamo.eti kicho kichwa what?mtu alifanya watu wakala miti,alifanya watu wakafulia majani,alifanya watu kutemberea matayari ya gari,yani viatu,watu hawakwenda shule,kwa ajili ya mwalim,kwani si tu ni maskini bali nauchoyo wa madaraka ya mwalim,kwani alikuwa anajuwa watu wakisoma watampiku madaraka yake in future,angalia wasomi wenzie alivyokuwa akiwanyanyasa.MWISHO OGOPA MWALIM WEWE.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 04, 2009

    alikua hayumbishwi kama viongozi wetu..viongozi wetu wanaogopa hata kuukemea ufisadi na rushwa.wao wamezungukwa na watu wa milungula.na wafitini...wanachosema sio wanachotekeleza..yaani ccm imejaa mafisadi&company...watu wamenunuliwa kama karanga na korosho..na wahindi koko wa kibongo..mawaziri wanashindwa hata kukemea rushwa..wananunuliwa kwa doti za khanga na crate za mayai..ndio nyerere alikua na mapungufu yake kama binaadamu wengine lakini alikua mtu mwenye msimamo kwa nchi yake.ajawahi kutia saini mikataba mibovu au kuuza ardhi yetu kiholelahola kwa faida yake.na wapambe pembeni kama ilivyo siku hizi..wanajinufaisha wachache wao na watoto wao wanarithishana madaraka.na wadhifa kupandishana kama vile ni ufalme au company zao binafsi....2010 sio mbali kusuka au kunyoa...ya ruanda yana nafuuu...tutakayoyaona hapa hata kenya bora..

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 04, 2009

    Mh.Mkuu wa Wilaya ya Tegeta,
    Kauli hii ya Mwalimu ni muhimu sana katika kipindi hiki cha tafakuri ya wanachotufanya hawa ndugu zetu wachache kwa kivuli cha ubaguzi wa rangi.Ni kweli kuona mbali mkwa Mwalimu hakumpi nafasi ya kutakaswa na kuwa Mtakatifu.
    Jambo ninalotetea hapa ni kauli ya kusema eti Mwalimu alichangia kuzorotesha nchi alipoichukua toka kwa wokoloni.
    Ukweli ni huu:naomba unilinde Mh.
    Nchii hii ilipochukuliwa na wazalendo kipindi kile haikuwa na wasomi wa kutosha. Kwa ukubwa wa nchi ilibidi wazee wengine wapewe nafasi nyeti bila hata chembe ya shule(naomba nisiwataje)kwa utaratibu ule unakuta sekta chache nyeti kama ulinzi na uchumi ndio ziliwekwa kwa wasomi wachache na zile ambazo ndizo muhimu kwa sasa kama Kilimo, Maji, Miundombinu walipewa wale wazee wasio na shule wala ujuzi wa kutosha. Hali ile iliwafanya kutoa maamuzi yaliyotufikisha hapa tulipo sasa. Kwa uchache hiyo ndio sababu kuu ya Tanzania kuwa maskini mpaka leo zaidi ya 40years baada ya uhuru.
    Wote mtaungana nami na kukubali kuwa nyumba nzuri hujengwa juu ya msingi imara, kwa mtaji ule Taifa lilikabidhiwa kwa wasomi wachache na wasiosoma wengi ambao maamuzi yao yametufikisha hapa tulipo
    Mh.naomba kuwasilisha

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 04, 2009

    We anon wa June 04, 2009 3:56 PM, nchi zoote zilivyopata uhuru hazikuwa na wasomi na wala wanachi wake hawakufulia mipapai au kuvaa mawingu au matairi.

    Unaonyesha unatetea udhaifu kwa visingizio. Kuna wasomi walifungiwa wilayani kama Tuntemeke Sanga, kuna waliokimbilia ughaibuni ili wasifungwe baada ya kubanwa na azimio la arusha n,k.

    Tunakubali alikuwa kiongozi bora lakini alishindwa kwa takriban 45% kwa ujumla.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 04, 2009

    Hapa huu ni mstari wa biblia sasa kuona mbali kuko wapi?

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 04, 2009

    Nakumbuka utotoni simulizi za uongo za kuonyesha Mwalimu ni mjanja kwa kutumia udhaifu wa Kawawa. Kama zile hadisi za sungura na fisi. Mfano zile za vijiko vya dhahabu, funika kikombe, kifimbo na glovu ya malkia, n.k. Aliniingia akilini mpaka nikasema nikiwa mkubwa ntakuwa nyerere (raisi).

    Alifanya mengi mazuri, na mabaya pia, Mungu akipenda atamsamehe.

    nahisi hadisi hizo (myths & stereotypes, comedies) ndo zimefanya wengi wakose uwezo wa kuchambua (analyze) mambo na kubaki tunapiga makofi tuu, zidumu.

    Wengine wanasema hatutapata kiongozi kama huyo (kwani yeye ni Yesu au Muhamadi?), tutapata zaidi yake Mungu akipenda. Wengine wanasema ni musa wa tanzania, wengine wanasema Musa alisema na Mungu, mwalimu hajawahi. Uchanganyaji wa dini na siasa.

    Huyu alikuwa raisi wa kwanza wa nchi hii, na amepita kama wengine katika nchi zao.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 04, 2009

    Looo! kwa kupitia haraka haraka tu maoni ya baadhi ya watu pale juu wanaonekana wazi kulevywa sana na Mambo ya magharibi. Nchi mnazoziona vioo kama uingereza na marekani hivi hamwezi jua kuwa pale zilipo sasa zilikuwa nchi zenye vita na misukosuko mingi ya kuonea na kubagua watu wengine????? (USA is 200 years old, UK hata usisema, Tanzania is Just over 40yrs old)
    Ati wakoloni waliacha nchi nzuri- hii ni njozi kabisa. shule zilikuwa ngapi? vituo vya afya??nani alikwenda? wewe baba yako kijijini au babu alikuwa wapi au nani? nchi haikuwa na chochote bwana. watu walikuwa wawindaji na majority of them wakitembia uchi kabisa in the 1950s & 60s. Hata vyeti vya kuzaliwa havikuwepo kama hukupewa cha ubatizo basi umekoma. huwazi dai ati uchumi ulikuwa bora! sasa unataka mwingereza aliye-own shamba la kahawa Arusha asipewe bei nzuri na wazungu wenzake anapoiuza uingereza? No thoughts kabisa.
    Marekani walipigana sana huku wakiwanyanyasa watu weusi na wahindi wekundu- lakini hata siku moja most of them hutawasikia wakiwasema vibaya viongozi wao waanzilishi wa taifa.
    Nyerere hakuianzisha Tanzania kwa Mtutu, alibuni mbinu ya kila mtanzania kusoma, na utaifa. Kwa hilo mimi mtu haniambii kitu, maana nimesaidika sana hadi nikafika huku niliko. UPE umenilinda, Kurudishiwa nauli secondari etc hadi kusoma chuo kikuu ni kuku. Hivi sasa ninavyosumbiliwa nyumbani kwa ada, hela ya afya, n.k. inaniudhi sana na nadhani nchi maskini kama TZ watu walio masikini kama nilivyokuwa mie wameshakiona cha mtemakuni-they will get no where-has ukiangalia over 95% ni wakulima wanaoishi ktk mbavu za mbwa.
    Be a countryman and be Loyal to you country

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 05, 2009

    Haoni mbali hata kidogo, niwakati wake wananchi walichukua sheria mikononi na kuwachoma moto wezi baada wananchi kukata tamaa na Judicial system yake

    Viongozi wakubwa hawakuwai kulaumiwa wala kuface justice

    Katuletea wakina mkapa wakatengeneze Network ya kifisadi

    Nchi ilikua njaa kila kona nk Hanampango aende na akirudi kipindi hiki wa TZ watampiga mawe.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 05, 2009

    Mtake msitake nyerere alikuwa kichwa! Na kabla hajafa alikiri kama binadamu alikosea! Ni vingozi gani baada ya yeye wamewahi kukiri makosa yao? Na kikubwa ambacho ametuachia ni kwamba watanzania hatutambuani kwa makabila! Ingawa sasa watu wameanzA CHOCHO CHOCHO ZA UKABILA NA UDINI! KIONGOZI HAKIFANYA HOVYO WATU WAKISEMA WENGINE WANAKIMBILIA ATI NI UDINI!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 05, 2009

    Nina wasi wasi kidogo na upeo wa uelewa wa wachangiaji wenzangu,samahani kama nitaeleweka vibaya.Mimi bado naamini kuwa Nyerere ana upeo mkubwa sana hata kama yeye si Yesu au Muhamad,lakini ktk kizazi hiki simuoni anayemkaribia kwa upeo hata kama ni aya ya biblia lakini biblia na vitabu vingine bado vipo mbona viongozi wa sasa hawachambui kama yeye na kuyatumia kwa faida ya jamii, waliopo ni kupiga vijembe na mipasho kama wasanii au waimbaji wa taarabu. Nasema tusitarajie kupata viongozi wanaoona mbali ktk kizazi hiki, labda wanaona mbali kwa kuwadanganya huku wanawaibia wananchi, viongozi kama hawa wenye tamaa ya utajiri Nyerere aliwaweka ndani na wengine wakakimbia,watu wakamwita dikteta, lakini alikuwa serious halei ujinga.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 05, 2009

    I'm telling you! Ndiyo maana hotuba zake zimefichwa. Maana zikiwekwa wazi zitawaumbua watu wengi walioko kwenye madaraka. Hakuna alichokiacha na yote aliyoyasema ndiyo yanafanyika hapa duniani na si Tanzania tuu, IMF, world bank, united nations.I'm sure umoja wa mataifa wanamiss speech zake maana alikuwa haendi kujikomba kwa wakubwa bali alikuwa anawaambia ukweli. I was privilleged kuwa na mzazi aliyefanya kazi naye karibu na ninakumbukumbu ya matukio mengi ambayo nilibahatika kusikiliza hotuba zake na kumsikiliza live. Kusema kweli huyu mtu ni wa kipekee! Alikuwa ni mkweli na bila kujali nani yupo karibu yake awe mchina mkorea mmarekani anamwaga cheche zake. Kumbukeni madeni nchi nyingi za afrika zilisamehewa na wakubwa miaka ya nyuma, haijawahi kutokea na sababu kubwa ni yeye kupambana nao. Mwenyezi mungu akulaze peponi baba yetu, you are really missed ungekuwepo huu utapeli wote wa bongo usingetokea, maana tunajua ungewaumbua watu redioni au kwenye TV!

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 05, 2009

    Tatizo hapa Mwalimu analinganishwa na viongozi waliomfuata ambao kimsingi aliwaweka au kuwatengeneza yeye kama angeona mbali angetakiwa ajue kuwa hawa si viongozi bora bali walivaa ngozi ya kondoo kwa ajili yake!!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 05, 2009

    WE ANON WA KWANZA KABISA KUCHANGIA INABIDI UPANUE MAWAZO KIDOGO. SIO KUCHANGANYA DINI NA SIASA, AMETUMIA LUGHA YA PICHA TU...

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 05, 2009

    We anan wa June 05, 2009 3:26 PM, kutumia mistari ya biblia badala ya mistari ya katiba katika kuongoza jamii ndo kuchanganya dini na siasa au UDINI.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 05, 2009

    wadau, jamani someni kwa makini hiyo hiyo nukuu ili kupata falsafa iliyojikita humo. hii ni zaidi ya mipaka ya tanzania. fikiria mtikisiko wa uchumi wa 'global' na sikiliza wataalamu wanasema nini kuhusu chanzo chake!!!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 05, 2009

    Right person at the the right time. Sijui sasa kama angeiweza dunia ya leo.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 06, 2009

    The best of the worst bunch! The guy was the most educated when the country was uneducated! No TV, no imports....he kept Tanzania in the dark, no one knew anytthing about the outside world so whatever he said was magical! Clever he was, but to the expense of the ordinary Tanzanians!
    Micuzi tafadhali!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...