Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Uswisi Dk B. S. Nyenzi (kushoto) na Mgeni wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya watanzania wanaoishi Japani Dk A. Y. Simba walipokutana katika Mgahawa wa La Lomana mjini Geneva kwa mazungumzo juu ya Jumuiya zao.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Uswisi (TAS), Dr B. S. Nyenzi, juzi jioni (12/6/2009) alikutana na Mwenyekiti wa Jumuiya Watanzania wa Japani (Tanzanite Society), Dr A. Y. Simba, katika mgahawa wa La Lomana mjini Geneva. Katika mkutano huo viongozi hao walijadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupeana historia na mchakato mzima wa uanzishwaji wa Jumuiya hizo, malengo ya jumuiya hizo, mafanikio waliyopata na matatizo wanayokabiliana nayo.

Kimsingi malengo ya Jumuiya hizi ni kuwakutanisha watanzania wanaoishi katika nchi hizo ili kuweza kusaidiana wakati wa shida na raha. Jumuiya hizi mbili zimefanikiwa kupata wanachama wengi kwa kipindi kifupi kutokana na viongozi wa Jumuiya hizo kufanya shughuli zao kwa uwazi zaidi.
Kwa mfano, Dr Simba alisema yeye na viongozi wenzake walipoingia madarakani, waliamua kuwa suala la mapato na matumizi ya fedha za Jumuiya kuwa ni ajenda katika kila mkutano wa wanachama wote, na kuruhusu wanachama kupata mahesabu ya fedha za Jumuiya muda wowote watakapotaka taarifa hizo.
Ikumbukwe kuwa ubadhirifu wa fedha za Jumuiya limekuwa ndio tatizo kubwa linalosababisha migogoro ya Jumuiya nyingi za watanzania waishio ughaibuni.

Viongozi hao pia walikubaliana kuwa wakati umefika kwa Jumuiya hizi kuangalia uwezekano wa kuwa na malengo ya kutoa misaada nyumbani Tanzania kadiri uwezo wao utakavyoruhusu. Kwa mfano Jumuiya hizi zinaweza kuamua kusomesha wanafunzi wasio kuwa na uwezo au kutoa misaada ya madawati kwa shule nyumbani Tanzania. Jumuiya hizi na watanzania wa ughaibuni kwa ujumla hawawezi kukwepa Jukumu la kutoa misaada ya maendeleo ya jamii.

Pia kwa kuwa kumekuwa na mwamko wa uanzishaji wa Jumuiya za watanzania, Wenyeviti hao pia walijadili kuhusu umuhimu wa kuanzisha Jumuiya mama ya Jumuiya zote za ughaibuni ili kuweza urahisi wa kubadilishana mawazo na kusaidiana kwa urahisi zaidi.

Mwisho viongozi hao wanapenda kutoa wito kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi kuanzisha Jumuiya katika nchi ambazo hazijafanya hivyo, na katika nchi zile ambazo kuna Jumuiya basi watanzania wajiunge kwa wingi kwenye jumuiya hizo. Pia walilisitiza suala la kuepusha migogoro isiyokuwa ya msingi na kuongeza upendo miongoni mwetu.

Mwenyekiti wa Tanzanite Society aliwashukuru wenyeji wake kwa kufanikisha mkutano huo, na hasa katibu mkuu wa TAS Bw. S. M. Sillayo, ambaye hata hivyo hakufanikiwa kuhudhuria kutokana na kuwa Tanzania kikazi. Dr Simba alindoka Geneva Jumamosi kuelekea Davos kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa madhara ya mawimbi ya mawasiliano kwa afya za binadamu.

Umoja ni nguvu na utengano ni udhahifu


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 15, 2009

    haaha hahahahah! Ya Leo Kali! Hizi Jumuiya hazisaidii lolote na ndo chanzo cha migogoro kwa wabeba box.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 15, 2009

    wabongo kwa kutafuta ulaji utawaweza, wakiwa bongo utasikia oooh mimi nina NGO yangu, wakiwa nje za nchi OOOH jumuiya ya tanzania, afu kila mtu anataka madaraka, waangalie hao walivyo na mikwara utafikili mawazili duh bongo noma ile kinomanoma!!!!

    Mshauri Mkuu!
    university of Cuba.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 15, 2009

    Hongereni Dr. Nyenzi na Dr. Simba, huyo anayejiita Mshauri Mkuu (University of Cuba) ni mmoja wa wanafiki hapa katika mitandao ya jamii, Bongo wameshaanza kuwaogopa na hizo jumuiya zenu za ughaibuni, what are they trying to do is to crash you guys before you landed in Tanzania, msife moyo, siku moja watajua umuhimu wenu katika jamii ni suala la kuwaelimisha tu

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 15, 2009

    Wazee naona baada yakukamua "book" mpaka mkawa madaktari...sielewi "in which capacity" lakini in any capacity...nawafagilia kwa hizo tittle zenu Dr. we need u in Tanzania, things are the way they are because you are hiding in places that doesn't even aknowledge your contribution.

    Mumeniacha hoi mnavyofonza hizo zabibu za dodoma kwa kusonga mbele...kateni mayi wana maisha yenyewe ndiyo hayo hayo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 16, 2009

    huyu babu anaye tabasamu anaonekana is nice lakini huyo aliye uchuna mmmmmm! anaonekana ni munoko kama alivyo.

    mwinyi mpekuzi!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 16, 2009

    Naunga mkono kabisa wadau wa juu hapo. Mimi nipo Japan na mtu yoyote atakwambia hapa kuwa hatuna muda wowote wa kupiga story. Nchi hii ni ghali kuishi na muda wako ni pesa. Usafiri wa kukutana peke yake ni chakula cha siku mbili kwangu. Pili sioni faida yoyote na kukaa katika hii mikutano. Mara nyingi wanataka ulipe ada ya uanachama au kuchanga pesa ili ziliwe. Nikiwa na shida yoyote naenda ubalozini, at least najua kuwa uhakika nitasaidiwa. Muda wa kupiga story hapa hamna.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...