WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA BANDARI WAKIZIBA TUNDU KATIKA MGONGO WA MELI YA MV FATIH ILIYOZAMA IKIWA NI JITIHADA ZA KUOKOA ABIRIA WA MELI HIYO NA KUIONDOA
MWILI WA ASHURA SULEIMAN NA MTOTO WAKE MCHANGA ALI HARUOB MOHD UKITEREMSHWA KATIKA BOTI YA RUBANI

BOTI YA RUBANI YA SHIRIKA LA BANDARI IKIWA NA MAITI YA MAMA NA MTOTO

ZOEZI LA UOKOAJI LIKIENDELA SIKU YA TATU LEO 31-5-2009 KAMA WAOKOAJI WAKIWA JUU YA MGOGO WA MELI WAKIZAMUA MAITI TATU JANA ZA MAMA NA WATOTO WAKE WAWILI BI. ASHURA SULEIMAN MTEGE, MTOTO ALI HARUB MOHAMED WA MIAKA 3 NA KAKA YAKE MUKRIM MOHAMMED MIAKA 6 WAKAZI WA KILIMAHEWA ZANZIBAR

MGONGO WA MELI YA MV FATIH UNAVYOONEKAN UKIWA UMEZAMA MAJINI
TIMU YA WAOKOAJI WAKIPANGA MKAKATI WAKIWA JUU YA MGONGO WA MELI HIYO. PICHA ZOTE NA MDAU OTHMAN MAULIDI MAPARA


HABARI KAMILI

IDADI ya watu waliokufa maji katika ajali ya meli ya abiria na Mizigo ya MV Fatih Zanzibar iliyopinduka na kuzama baharini, muda mfupi baada ya kuwasili katika Bandari ya Malindi ikitokea jijini Dar es Salaam imefikia sita .

Taarifa toka Zenji zinasema kwamba maiti watatu zaidi hizo wameopolewa leo.

Jana Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Mgharibi Unguja Bakar Khatib Shaaban, alisema kwamba ajali hiyo ilitokea saa 3:00 usiku na kuwa maiti watatu walikuwa wamepatikana. Inaaminika maiti zaidi zipo zikiwa zimebanwa na mizigo.

Watu 27 walitoka salama katika kadhia hiyo na kwamba idadi kamili ya abiria waliokuwapo katika meli hiyo ambayo ni ya mizigo ni utata mtupu.

Awali Nahodha wa meli hiyo alisema kuwa alikuwa na abiria 25 wakati wao wakiwa mabaharia 13 lakini ukichanganya hesabu za waliokoka inaonekana meli ilikuwa na abiria wengi. Chanzo cha ajali hiyo bado kujulikana.

Alieleza kuwa chanzo cha tukio hilo bado kinaendelea kufanyiwa uchunguzi lakini wanawasiwasi kwamba meli hiyo ilipinduka, baada ya kuzidiwa na mzigo upande mmoja, kwa vile ilikuwa imebeba shehena za mbao, gari moja trekta na vyakula.

Mkurugenzi wa Shirika la Bandari Mustafa Aboud Jume alisema kwamba waokoaji 30 wakiwemo wazamiaji kutoka Kikosi cha KMKM wanaendelea na kazi ya kusaka maiti zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2009

    Mbona ukoaji wa hii meli inaonesha kama vile haijulikani nini cha kufanyika?

    Kana kwamba haitoshi, watu wamesimama juu ya huo mgongo wa meli wengine wakiwa hawana hata Life Jackets, hivi kweli mamlaka za usalama zipo kazini au likizo?

    ReplyDelete
  2. Phatlorenzo--MNJune 01, 2009

    Nakuunga mkono kabisa mdau wa mwanzo kabisa. Wapi vitendea kazi? Wapi Safety Measures kwenye huu uokoaji? Yaani inaonekana bado tunafanya kazi kienyeji. Vitu kama Life jackets ni lazima kwa wote walioko kwenye eneo la maji regardless skills za uogoleaji. Hopefully tunajifunza as we go along. Poleni kwa wafiwa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 01, 2009

    Jamani jamani, siku tatu na hakijulikani cha kujulikana! Uzembe umetokea na hata huruma haionekani

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 01, 2009

    yaani huu ni uzembe wa hali ya juuu sijapata ona na cha kushangaza siku 3 still meli ipo chini hivi nchi yetu tutafika kweli? halafu sasa ajali imetokea walefika kabisa inamaana hakukuwa na meli za usalama kama kitu kikitokea? huyu rais wa zanzibar anakalia kitu bure na iwe wazi meli ya mizigo ni mizigo sio watu kubebwa jamani kaaaaaaaaaaaa inatia huruma na ukiangalia ni uzembe tu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 01, 2009

    Mkurugenzi anaitwa Mussa Aboud Jumbe na sio Mustafa....

    Poleni wafiwa na mungu awape uwepesi pia.

    Je wakati inaondoka bandarini haikukaguliwa? Jamani ebu tufanye jitihada kuokoa maisha ya waTZ katika kuepuka kukutwa na majanga.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 01, 2009

    inauma na pia ni aibu kuwa nchini kwetu hadi sasa miaka ya 2009 tunatumia style zile zile za miaka ya 70 za kutafuta maiti baharini, ni kuzisubiri maiti zenyewe zishibe maji na kuanza kuelea. ushahidi ni huo katika picha watu wamejikalia tu hawana hata vyombo vya utendaji kazi, hawana mavazi ya kuzamia baharini, na ona jamaa anaziba tundu ya meli kwa welder! tena hata hana hata vifaa vya kumuokoa yeye endapo hiyo meli ikipinduka tena wakati yuko juu ya mgongo wa meli. Halafu wanatokea watu hapa kukasirika tukisemwa kuwa watanzania hatuna maendeleo.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 01, 2009

    Serikali ime invest zaidi kwenye rasilimali watu (KMKM, Kikosi cha Ukoaji, KVZ nk) ambao ni strategic kwa kupiga kura zaidi ya mara moja na kuwatesa wananchi inapokaribia siku za uchaguzi, lakini hakuna plan maalum ya kupambana na majanga kama haya. Imagine meli hii ingezama nje ya bandari ya Zanzibar, maiti wangeweza kupatikana kweli? its hight time kwa SMZ kuanza na kupanga vyema rasili mali zake.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 01, 2009

    Yaani??Aagh eti zanzibar ni nchi. Kwa kuwa inayo serikali ya mapinduzi...Nakubaliana na wote mliochangia. Yaani the body language inayoonyeshwa na viongozi wa serikali kama ile picha ya juzi wamekaa pale utafikiri wako picnic. Na hao mwaliko juu ya mgongo wa meli. Hoovyo. No seriousness at all. Zoezi hilo linaweza likachukua hata juma zima. Hiyo ndiyo zbar. uswahili mtupu. Yaakhe maana suala hili la meli kuza ma wallahi kuna nkono wa ntu hapa si bure//

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 01, 2009

    Jamani hakuna umaskini mbaya kama wa kukosa maarifa, watanzania ninyi mnapiga kelele na ufisadi kila kukicha, mafisadi yenyewe yanatumia ubabe na dhamana yaliyopewa. Tazama sasa mali inateketea na maisha ya maskini hawa yanapotea hivi hivi kwa kukosa maarifa. Maana hata hakieleweki kama ilikuwa ni meli ya mizigo au abiria. OK, maskini hana choice yote kwake ni sawa bora liende.
    Inakera sana kuona viongozi wetu kutolea macho na nguvu nyingi kwa mambo ya ushabiki wa kisiasa, hususani kwenye chaguzi ndogo kama Tarime, Mbeya, Busanda na sasa nguvu zitaelekezwa huko Kagera.
    Hivi mtabadilika lini? Au ndio kafara mnazozifanya kwa kuwatoa wenzenu uhai, Mbona hatuoni juhudi zozote, mmepooa kama mmenyeshewa mvua ya mavi!!
    Tunahitaji mabadiliko 2010. Hatutaki!!!! kuendelea kuona nchi yenye utajiri wa maliasili kama Tz watu wake wanaangamia kwa kukosa maarifa. hata ukifisadi huzifanyii mambo ya maana badala yake ulimbukeni wa kuwanunulia vi-used car vyekundu. Hii ni moja ya dalili za ule ugonjwa wa kukosa maarifa, sijui ni laana! Tunahitaji tufanye utafiti.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 01, 2009

    HEBU NIPE BOFLO NA SUPU YA PWEZA MIE NILE YAKHEEE...HIZI PICHA NA HII HABARI NI YA WEYE MICHUZI MBONA HIVYO ATIII.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 01, 2009

    hiyo meli ikifika wiki itaenda chini na maiti mpaka zishibe maji ndio zitapatikani,

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 01, 2009

    Wadau hii meli ni meli kweli au zile zinazoitwa beach crafts.Meli hii ni zile za aina ya kutua kwenye beach na haziruhusiwi kuchukua abiria.Kwa vile sasa iko juu chini ni dhahiri meli hii haina ile kitu initwa "keel" upanga wa kuistabilise meli yenyewe baharini.
    Meli za aina hii ni rahisi sana kuroll over na kwa kawaida ni kama ungo unaoelea.Sasa iliruhusiwaje kuchukua abiria?

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 02, 2009

    anonymous wa June 01, 2009 5:23 PM are you trying to be funny? ok hakuna jamaa yako alokufa but hebu onyesha heshima na utu kwa waliopeteza ndugu zao!!!! au kwa vile ulihisi ni wazanzibari tu ndio waliopoteza maisha na hivyo ni sawa kubeza? basi kwa taarifa yako mmoja wa waliopoteza maisha ni ndugu kutoka bara.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...