baada ya kutoa watu machozi kwa video ya awali ya hawa vijana wa shule ya msingi kule same, mdau baraka wa chibiriti aliyeko Cesena, Italy, anasema kafurahishwa sana na jinis wadau mlivyofurahishwa na video hiyo. na leo kaamua kutupa ingine

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 11, 2009

    mdau Chibiriti inaonyesha wewe una fan ya ualimu, na unanitia machungungu ya kutamani niende nika-visit shule moja nikasikilize nyimbo hizo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 11, 2009

    laiti huo wimbo ndo ungekuwa wimbo wa taifa kaka ulivyo tarajiwa, labda watu wangepnguza ufisadi. wadau mnsemaje, sasa ndo tukachukua wimbo wa afrika kusini. kina mzee sykes wakadharauliwa.ASANTE KAKA IMETULIA.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 11, 2009

    Duh safi sana. Yani hiyo school band inanikumbusha mbali sana wakati na mimi napiga drums kwenye school band ya kisutu primary school in 1986 and 1987

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 11, 2009

    Enzi Hizo Unakaa nyuma kabisa Sema Wengi humu wamesoma Enzi za Unaimba Chama Chetu Chamapinduzi cha jenga nchi Nyerere eeeeeeeeeeeeh na Mwinyi wajinga nchi hahaha kudadeki tulikuwa tunalazimishwa yasiokuwa na msingi. Bora nyimbo ya Taifa. walionyuma hawajui kuimba kimya. James

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 11, 2009

    kudadadeki Chibiriti, narudi songea

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 11, 2009

    they are more patriotic than our leaders.
    CHIBIRIT NI SHULE GANI HIO KAMA VIPI UNAONAJE TUWAFANYIE HARAMBEE HUMU?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 11, 2009

    Nilikuwa nacheck nione kama kuna mtoto asiye na viatu kama sisi enzi zetu za sabini lakini naona afadhari. Ila naona kuna baridi lakini wenye sweta ni watatu tu. mdau wa Italia basi fanya mchango wa kutuma angalao mitumba. Thanks for the pics.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 11, 2009

    Uongo mbaya watoto wanakumbuka wimbo vyema kuliko nilivyofikiria. Siwezi kuimba kama walivyoimba wao!

    Good job!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 11, 2009

    Barack Chibiriti, naona unafuata nyayo za rais mmoja hivi mwenye jina kama lako."kuipenda nchi yako"

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 11, 2009

    Nyerere was so successfull kwa kuwa brain wash watu kuhusu patriotism.
    I surggest kila siku kabla ya bunge kuanza wabunge wajipange waimbe kama hawa watoto.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 11, 2009

    ahavache avae!ndi ndi mdevedhi))
    swafi sanaa kiberiti aka chibiriti.
    watu tumetoka mbali sana sijui nami nilikuwa dogo kama waonekanavyo hao lakini fujo tupu za LY! wato wa O-BAY Primary mpo?1987

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 11, 2009

    namwunga mkono mdau aliyesema "laiti huo wimbo ndo ungekuwa wimbo wa taifa kaka ulivyo tarajiwa, labda watu wangepunguza ufisadi". Ni kweli au yule mdau aliyesema hii mibunge iwe inaimbishwa na Mh. Spika wimbo huu kabla ya kuanza kikao.
    Wamenipeleka mbali sana enzi za 1970s wakati huo mwalimu wetu katoka JKT tunaimbishwa nyimbo za uzalendo. Hapo inanifanya nimkumbuke mzee wetu Nyerere. Mjitu siku hizi imekengeuka na kupoteza uzalendo utafikiri haikuzaliwa wakati huo. Hongera ndugu yetui Chibiriti kwa kutukumbusha. jamani inauma kuona mifisadi hii. natamani mnipe urais niitie "chibiriti" niwashe moto

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 11, 2009

    Ndugu zangu kuna mtu ana lyrics kamili za huo wimbo? Naupenda sana ila huwa sijui maandishi yake kamili.
    Tafadhali tusaidiane

    ReplyDelete
  14. HII inanikumbusha mbali sana,wakati huo mimi sina hili wala lile,wakati unaimbwa huo mwimbo nilikuwa nimejibanza sehemu fulani nikila chabo mwalimu akae vibaya na mimi nijiunge kwenye mstari hapo nimeshachelewa shule na ukijipeleka ovyo mwalimu akikuotea unakula bakora kuliko anazokupiga baba yako na hata akiambiwa na yeye kama mzazi anakuongezea,ila kusema ukweli tulikuwa na adabu sana ingawa tulikuwa na tabu kuandika tunakaa chini wenye viatu ni wachache na wote viatu vinacheka chini,du pindi ile.ukiangalia hao watoto utadhani na wewe hukupitia huko ila miaka ndio inakata uwanja tena.big up chibiriti

    ReplyDelete
  15. hapo mtu mzima ukiwa mpiga ngoma basi hupigwi ukichelewa na shule nzima inakutambua ila kasheshe ipo kwa hao wengine usiponyoosha mstari unakula za uso na kunyoosha mstari inabidi umshike mwenzako begani.nakumbuka pinde hiyo hananasif primary school kinondoni nakumbuka niliwahi kurekodi kipindi mama na mwana sijui aliyekuwa host wakipindi hicho alikuwa ni mama deborah mwenda sina unakika vizuri hapo.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 11, 2009

    Ni kweli kabisa inafaa kabla ya Bunge kuanza wanatakiwa waimbe hawahawa watoto labda hao viongozi watakumbuka wametoka wapi.

    ReplyDelete
  17. TVZ KicartoonJune 12, 2009

    Tanzania Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote,
    Nchi yangu Tanzania, jina lako ni tamu sana,
    Nilalapo nakuota wewe, niamkapo ni heri mama wee!
    Tanzania Tanzania, Nakupenda kwa moyo wotee!.

    Tanzania Tanzania, Ninapokwenda safarini,
    Kutazama maajabu, biashara nayo makazi,
    Sitaweza kusahau mimi, mambo mema ya kwetu kabisaa!
    Tanzania Tanzania, Nakupenda kwa moyo wotee!.

    Tanzania Tanzania, Karibu wasio kwao,
    Wenye shida na taabu, kukimbizwa na walowezi,
    Tanzania yawakaribisha, mpigane kiume chema wee!
    Tanzania Tanzania, heri yako kwa mataifa!.

    Tanzania Tanzania, Watu wako niwema sana,
    Nchi nyingi zakuota, nuru yako hakuna tena,
    Na wageni wakukimbilia, ngome yako imara kweli wee!.
    Tanzania Tanzania, Mola awe nawe daima!.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 12, 2009

    Kaka chibiriti umenikumbusha mbali sana wakati niko TABATA SHULE YA MSINGI 1979 wakati huo shule ilikuwa ya udongo na makuti. Sasa niko nabeba box kwa wazungu kuna siku nakumbuka nyumbani basi kitu cha kwanza kuniingia kichwani ni huo wimbo nawexza kuuimba hata siku nzima mpaka nitoke job.
    Kuna mdau ameeleza jinsi ya kuwasaidia watoto kama kuna mtu ataanzisha njia yoyote mimi niko tayari na kuchangia nilicho nacho.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 12, 2009

    mdau TVZ kicartoon...

    oyaaa kuna ubeti mmoja,km sio wa mwisho uo unaanza na "Nchi nzuri Tanzania" au "Nchi yangu Tanzania,"

    ila umepatia uko juu dah!!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 12, 2009

    michu unabana nini??

    unajua kama mtu unataka kusaidia sasa ivi watu/kundi la wasiojiweza BORA tena BORA uende phisically toa msaada sehemu husika ishia zako,usilogwe upitishe eti sijui sirikali au whatsoever,hauwafikii walengwa,longolongo kibao...

    itabidi tujitoe sana wadau,umepewa bure toeni bure

    me naanzia MAKETE-IRINGA,

    nashuka na misaada wa milele mayb nife ndo iwe mwisho mf kujenga ku-adopt families pale nk nk

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 12, 2009

    TVZ Kicartoon, ahsante sana wengine tulikuwa hatujui maneno kamili ya wimbo.

    Be good,

    ReplyDelete
  22. TVZ KicartoonJune 12, 2009

    thanx!
    ni huo wa mwisho nafikiri, ni zamani sana,


    Nchi nzuri Tanzania, Watu wako ni wema sana,
    Nchi nyingi zakuota, nuru yako hakuna tena,
    Na wageni wakukimbilia, ngome yako imara kweli eeh,
    Tanzania Tanzania, Mola awe nawe daima!.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 13, 2009

    WAMEKOSEA CAMON THIS IS WESTERN CRAP HUU WIMBO HAUIMBWI NAMNA ILE. KUNA MAKOSA YA KIMSINGI SANA CHIPUKIZI HUWEZI SIMAMA UKIWA MKONO UKO LEGE NAMNA ILE. INABIDI UWE MGUU PANDE NA MKAKAMAVU MWILI MZIMA. KAMA HUJAKIMBIA MCHAKAMCHAKA BASI JASHO LINAKUTOKA WIMBO UKIISHA!! NAOMBA MWALIMU WA pE AKAPEWA ADHABU KWA KUSIMAMISHA WATOTO LEGE LEGE WAKATI WIMBO WA BENDERA UNAIMBWA.
    MVUTA UGORO KILEMA

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 16, 2009

    Ahsante, kuna watu wanapenda kujenga mazingira ya kuudhi wengine, basi leo tangu asubuhi kuna watu wanajitahidi kuniudhi. lakini nilivyosikiliza haka ka wimbo kakanfariji, ubarikiwe sana kwani wewe si mchoyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...