Mh. Mohamed Dewji akiwa na kocha wa African Lyon Eduardo Almeida toka Ureno
Mkuu wa wilaya ya nanihii, naomba nirushie hii. Jumapili jioni nilienda kuangalia mechi ya African Lyon FC timu iliyopanda daraja msimu huu ikicheza dhidi ya vijana wa Jangwani Yanga.
Mpira uliisha huku Yanga wakilambwa mabao matatu. Kilichonifurahisha ni kuwa timu hiyo haijasajili majina makubwa na wamejikita zaidi kukuza vipaji kwani line up yao ilijaa chipukizi wadogo ambao walionyesha kiwango cha hali ya juu.
Kwa nyepesi nyepesi nilizokuwa nazo ni kuwa timu hiyo ambayo inafadhiliwa na Mbunge wa Singida mjini Mohammed Dewji “ MO” amejenga hosteli bab kubwa kule Mbagala kwa ajili ya vijana hao, na on top of that nasikia anataka kujenga uwanja in coming years.
Na kwa wale tulioangalia mpira jumapili kama vijana hao wakitunzwa vizuri basi watafika mbali. Binafsi siwafagilii Simba na Yanga kwa sababu wanakuwa wanaharibu vipaji vya watoto wengi na hakuna maendeleo tunayoona zaidi ya sasa kuwanyenyekea wachezaji wa kigeni badili ya kuendeleza vipaji vya ndani. Hata Uingereza wanalalamika hilo, taifa lenye ligi inayopendwa kuwa wageni wanaifanya timu yao ya Taifa iwe inalega lega.
Ili mpira wetu ukue timu inabidi zianze kuwekeza kwenye timu za vijana. Wenzetu Uingereza wachezaji lazima wapitie Academy za vijana ukienda Manchester, Liverpool, Arsenal hizo zote zinakuwa na njia za kupata wachezaji wapya.Akina Gerrard, Rooney, Messi wote wamepitia kwenye Academy za vijana ambao wanalelewa vizuri na kuandaliwa mazingira ya kuwa professional footballers.
Hivyo naunga mkono hostel ya African Lyon ambayo imejengwa kwa ajili ya wachezaji ni hatua nzuri kwa ajili ya kuendeleza soka la bongo.

Nikikumbuka enzi za Simba kuitoa Zamalek chini ya uongozi wa Mo, I believe hii African Lyon itafika mbali, na watanzania tuamke na tujaribu kuendeleza soka nchini kwetu kwa kuziunga mkono timu zenye mipango na muongozo. Its time to think beyond Simba and Yanga.
Baada ya kutoka uwanjani nikaenda kwenye tovuti yao na nikacheki habari za kipigo cha Yanga zishawekwa kwenye website yao.

MDAU NV

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2009

    Great great!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 20, 2009

    ahsante mdau kwa hiyo insight. labda kwa kuongeza tu ni kwamba hawa jamaa African Lyon wana-establish uhusiano na timu mbali mbali za ulaya, na tayari they have a professional relationship with Kongsvinger (sp?) ya Norway, ile timu ambayo imemsajili Henry Joseph...

    Nadhani wakizingatia policy yao watafika mbali sana!...

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 20, 2009

    Pengine mambo yaweza kuwa sasa, ingawaje kajina akajakaa uzuri. Kila la HERI "simba wa afrika"

    ReplyDelete
  4. Kaka TrioJuly 20, 2009

    Mdau NV unajichanganya kwa kusema UK wanalalmika kuwa timu yao ya taifa inalegalega kutokana na ligi yao kuwa na wageni wengi wakati huo huo unatola mifano ya nchi hiyo hiyo kuwa ina vipaji na inajua kuchimbua vipaji na kwamba vipaji vingi vimepitia academy zao, kwa ivo wapemepitia academy lakini hawasaidii nchi yao, UK.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 20, 2009

    ...Mdau NV, ni kweli kabisa Simba na yanga ndiyo wanaoua mpira TZ. Ebu tizama mpira unaochezwa na Yanga ama Simba, ule ni mpira kweli? Si afadhali hata mtu uende kuangalia mpira wa mchangani.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 20, 2009

    Mdau NV mimi pia sizipendi Simba na Yanga kwa ajili ya sababu ulizotaja hapo juu, lakini natumaini MO asije akaichoka timu hii ikafa kama zingine, lakini kwa mapenzi yake kwa ajili ya soka hata mimi naamini itafika mbali, Kaka Trio mdau anaamanisha Academy zinasaidia kutoa wachezaji lakini wageni wanapewa kipaumbele sana siku hizi kwani wanakuwa tayari wana uzoefu na hivyo hawapewi nafasi kuchezea timu kubwa mfano Mathew Upson ex Arsenal, Danny Guthrie ex Liverpool,hivyo timu yao ya taifa inakua haina options nyingi from big teams na sasa hivi wageni pia wanafanya watoto wetu wasipate nafasi hapo nchini badili ya kuwapa nafasi vijana......

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 20, 2009

    Nilikuwepo uwanjani na kipindi cha pili niliona African Lion walicheza vizuri, lakini kikubwa sasa wacheze hivyo kwenye ligi na wakiwa na Dewji na uhakika timu haitaganga njaa na watafanya vizuri. Naona Academy za UK zilikuwa zinafanya vizuri zaidi zamani zilizotoa Butt, Giggs, Beckham,Gerrard,Terry, Owen... lakini sasa wanalalamika kwa sababu academy kids hawapati chance ya kuonyesha uwezo kwenye vilabu hivyo kama zamani kwa sababu wachezaji wengi wa kigeni wanapatakina ambao wanaihakikishia klabu mafanikio ya haraka kuliko kutegemea vipaji hali inayoua timu yao ya taifa.......na sisi tukitaka tufanikiwe lazima tuwekeze kwenye timu za Yosso

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 20, 2009

    Hawa watu kweli wanataka kuendesha soka kisasa. Nimecheki website yao, ikikamilika itakuwa bomba sana.
    Wachezaji wao hata ukiangalia picha zao wanaonekana kufanana na umri tunaoambiwa, sio sawa na tunavyosikia kwamba eti Oba ana miaka 19.
    Tengenezeni mfano labda na klabu nyingine zitaiga.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 21, 2009

    Asante Mdau NV kwa habari hii njema ktk soka la Tanzania. Hatahiyo natofautina kidogo na wewe ktk yafuatayo:

    1. Simba na Yanga sio cause ya kuharibika soka soka la Tanzania. Tena mimi nadhani Yanga na Simba ndio roho iliyoshikiria soka la bongo hadi leo. Anayedhani Yanga na Simba zikifa soka la Tanzania litakua, aangalie michezo mingine ambayo timu hizi mbili hazishiriki (riadha, kikapu, ngumi, netiboli n.k) ni upi ambao Tanzania ni kinara duniani? Simba na Yanga ndio timu ambazo hata kama hazichezi soka kubwa kama timu za Ulaya, lakini mamilioni ya wabongo wana feelings kwamba ni timu zao.

    2. It is unfair kusema Simba na Yanga hazifanyi chochote kukuza soka la Tanzania. Yanga kwa mfano imetumia mamilioni ya fedha kubadili benchi la ufundi na kuendesha timu kisasa (at least). Na anayedhani kusajili wachezaji wa nje kunaua vipaji vya ndani hajui anachoongea. Wachezaji wa nje wanaongeza ushindani kwa wachzeaji wa ndani na hivyo kuwaimarisha. Mfano, Jerry Tegete mekuwa mchezaji mzuri kwa muda mfupi sababu alikuwa anagombea namba na kina Mwalala na Ambani. Angekuwa na Mwaikimba pekee unadhani angekuwa kama alivyo sasa?

    3. Siwatetei Simba na Yanga, wana sehemu yao ya lawama, lakini wa kulaumiwa wa kwanza ni serikali ambayo kwa miaka zaidi ya 15 haina sera ya michezo.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 21, 2009

    Hello mjomba michu mimi naomba kama inawezekana tuwekee hiyo picha ya hostel ya African lyon nasi tujione kwani kasi zao sio mchezo.vile vile kuna mdau huku majuu anatuambia kuwa park wa manchester united ana night club yake hapo dar tunaomba utuwekee picha ya hiyo club.
    mdau
    kisiju pwani

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 21, 2009

    Wewe anoni 06:52 am ndio wale wale maneno mingi vitendo bla blah. Eti serikali? Serikali hata kama itakuja na sera ya namna gani ikiwa mimi na wewe tunaleta mambo ya usimba na uyanga kusonga mbele tusahau. Acha kelele tuwaunge jamaa mkono tufanye mambo kwenye soka.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 21, 2009

    MO NI MMILIKI WA HII TIMU NA SI MFADHILI KAMA WADAU WENZANGU WALIVODAI!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 22, 2009

    Anony wa 02:22:00 PM, sikubaliani kuwa tatizo ni Usimba na Uyanga. Tatizo la msingi ni sera. Mfano serikal hii ya JK ilipoamuakuwa soka ni mojawapo ya vipaumbele vyake, tunaona improvement ndani ya miaka 5. Sasa unadhani kama kungekuwa na msukumo wa namna hii kipindi cha Mzee Mwinyi na kuendelea na Mkapa sasa hivi si tungekuwa mbali?

    Kutarajia maendelea bila sera ni sawa na kutarajia mavuno bila kupanda mbegu na kupalilia. Sera inatakiwa iseme mf. kila timu inayoshiriki ligi kuu ile na timu za U15,U-20, n.k. TFF na timu kama Simba, Yanga, A. Layon, mimi, wewe n.k kazi yetu ni kutekeleza.

    Naunga mkono changamoto ya A. Layon na timu zingine zinazojitahidi kuleta ushindani kwenye soka, lakini sikubaliani na majibu mepesi ya kulaumu timu 2 kwamba ndio zimeharibu soka la Tanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...