HABARI ZIMEINGIA PUNDE TOKA TEMEKE ZINASEMA KWAMBA MAJAMBAZI KADHAA YAMEVAMIA TAWI LA BENKI YA NMB WILAYANI HUMO LILILO KARIBU NA HOSPITALI YA TEMEKE MIDA HII HII......
MAOFISA WA BENKI YA NMB WAMETHIBITISHA UVAMIZI HUO, ILA HAWAKUWA NA DATA ZA KUTOSHA KUFAFANUA KIASI GANI KIMEPORWA NA KAMA KUNA MADHARA KWA MAISHA YA WADAU. MAANA MAOFISA WANASEMA 'KILA MTU AMEPANIKI ILE MBAYA' KIASI TAARIFA ZINAPATIKANA KWA SHIDA BADO.
INASEMEKANA MAJAMAA HAYO BAADA YA KUVAMIA NA PORA YAMETOKOMEA. HABARI ZINGINE ZINASEMA KIKOSI MAALUMU CHA KUPAMBANA NA MAJAMBAZI KIKO MBIONI KUYASAKA..
GLOBU YA JAMII INAFUATILIA NA ITALETA NYUZZI ZAIDI KWA KADRI ZITAVYOPATIKANA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 31, 2009

    Braza Michu, Mimi nina swali naomba kuuliza, Vipi serikali ipo active kweli, Maana Jana Kamanda Kova amesema kuna kundi wa Majambazi wameingia Dar es salaam na wanampango wa kuvamia taasisi za kifedha, hivyo tuwe makini, na leo tu wameshavamia huko NMB, Je hii kweli si ni uzembe tu, Kama RPC ameshatoa Warning kama hii, Polisi walitakiwa kuwa macho na kila Mwenendo hasa kwenye Taasisi za Kifedha. Hii ni Aibu

    ReplyDelete
  2. Mdau, GenevaJuly 31, 2009

    Anko nanihii, si ni siku mbili tuu tangu Kamanda Kova atoe tahadhari ifuatayo!:
    Tahadhari kutoka kwa afande Kova

    Tafadhali wajulishe wote wanaohusika kwamba kuna kundi kubwa la majambazi wenye silaha kali, ambao wameingia Jijini Dar es salaam hivi karibuni. Wahalifu hao ni pamoja na Wakenya ambao wana tabia ya kupora fedha katika taasisi kubwa kama,mabenk,kampuni za mafuta na sehemu zenye biashara kubwa n.k .


    Aidha watu hawa wana mbinu ya kula njama na watumishi wasiokuwa waaminifu.Ni muhimu mkafuatilia mienendo mbalimbali katika benk zenu na sehemu zilizotajwa hapo juu pamoja na kuimarisha usalama julisheni kwa message kupitia namba hii

    0783034224 .
    au kwa simu ya mdomo

    0754-034224 .
    0787034224 .

    zote ni namba za Kamanda wa Polisi Kanda
    Maalum ya
    Polisi Dar es salaam.
    Namba zingine za simu ni

    0754- 276217
    0776880000

    namba hizi ni za mkuu wa Upelelezi Kanda maalum.
    Lengo la maelezo si vitisho kwenu bali ni tahadhari muhimu ,
    inayofaa kuzingatiwa,
    S. H. Kova - SACP
    KAMANDA WA KANDA MAALUM
    DAR ES SALAAM

    Bongo kweli tambarare!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 31, 2009

    Kama Hio Mijambawazi Ni Mikenya Hapo Soooo Ila Kama Ni Wa Kwetu Acha Tugawane Tu Umasikini

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 31, 2009

    Mimi sio polisi lakini na swali kwanini ujambazi kwenye mabenki ni kila mwaka mmoja kabla ya uchaguzi??

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 31, 2009

    Wizi huu hauna tofauti na ule wa EPA, Rada, mikataba mibovu n.k. wote hawa ni majambazi kwa style tofauti.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 31, 2009

    Angakaa kimya mngesema hafanyi kazi, amesema mumepuuzia habari ndio hiyo

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 31, 2009

    Watanzania tuwe wakweli hata kama siyo majambazi kutoka Kenya!! Hata sisi ujambazi ndo umetujaa tu.mimi nashangaa watu kuona kama tukio,kwani hao wameiba kutumia bunduki lakini wanaoiba bila bunduki ndowanaoiba fedha nyiiingi sana.yani wanaitwa mafisadi.Hao walivamia benki wenyewe lazima mtawasaka tuu,lakini mafisadi walio ndani ya maofisi hamtagusa.Ama kweli nchi ya wizi!!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 31, 2009

    LAKINI UNAJUWA NINI KIBAYA KAKA MICHUZI KUUWA MTU TU..KAMA UNACHUKUWA KWA MBWEMBWE TU AAH MICHUZI TUNAGAWANA UMASIKINI WETU.SI KAMA EPA AU RICHMOND AU UMESHASAHAUUUUU!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 31, 2009

    DAH! TANZANIA WIZI MTUPU,,,,,,,

    ReplyDelete
  10. Hali sasa inarudia kulekule ambako tulidhania tumeshatoka. Hivi vitendo visipo dhibitiwa nchi haita fika popote. Watu wote sasahivi wamejijengea mawazo kuwa bila ya kuiba huwezi kupata maendeleo na watu wengi katika jamii yetu wanaonekana kubebwa na fikra hizo potofu. Wezi wanaiba kila mwaka lakini hawakamatwi, wakikamatwa kesi zao zinaishia juu juu tu wanaachiwa. Wananchi naomba tubadilike tusishabikie aina yoyote ya uhalifu, uwe ujambazi, ufisadi nk. Hawa viongozi tuwabadilisheni mwakani katika uchaguzi ili tujenge jamii mpya Tanzania.

    ReplyDelete
  11. Hapo ndio kujua jinsi gani mabomu ya mbagala yatakavyofaidisha majambazi. Polisi ndio wapate kujifunza kupitia makosa sababu kipindi cha nyuma hakukuwa na uwizi wa mabomu ila sasa ndio unaanza.

    Napeleka pole zangu na salamu kwa wale waliojeruhiwa na walio fiwa. Nawaasa pia Polisi vunjike moyo kupandana ha watu hawa.

    ReplyDelete
  12. Yaani ni aibu hata kusema eti majambawazi haya ni kutoka Kenya,hii inaonyesha udhaifu mipakani,hakuna SCRUTINY,kwahiyo baada ya hapa nini?hizi nchi za jirani kutuambukiza ukabila au? Maaaaaaaaan,somebody somewhere needs to step up their game,ushenzi kama huu ndo unafanya nchi zingine kuwa na military rule,maana yake kila mtu antaka kujifanyia Commandoo au Mafia.wanaoteseka sasa ni akina sisi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...