HABARI TOKA ZENJI ZINASEMA AJALI YA GARI IMETOKEA LEO MAJIRA YA SAA 11 JIONI HII MAENEO YA BUNGI, MIEMBE MINGI, WILAYA YA KATI MKOA WA KASKAZI UNGUJA AMBAPO WATU WAWILI WAMEPOTEZA MAISHA.
KWA MUJIBU WA KAMANDA WA POLISI MKOA WA KASKAZINI UNGUJA, AFANDE RASHID SEIF, GARI HILO LA ABIRIA LILIACHA NJIA BAADA YA TAIRI MOJA LA MBELE KUPASUKA NA GARI KUGONGA MWEMBE
KAMANDA RASHID SEIF AMESEMA MMOJA WA MAREHEMU AMETAMBULIWA KWA JINA LA MUSTAPHA MTAMBO (50) NA MWINGINE AMBAYE NI MWANAMKE BADO HAJATAMBULIWA.
AMESEMA JUMLA YA MAJERUHI 13 WAMELAZWA KWENYE HOSPITALI YA MNAZI MMOJA WAKIPATIWA MATIBABU, NA KWAMBA GARI HILO ILIKUWA NA ABIRIA WENGI WAKITOKEA HARUSINI
mwenyezi mungu awalaze mahala pema waliopoteza maisha na walioko hospital mwenyezimungu awape uhauweni.
ReplyDeletemdau coventry
Huyu Kamanda Rashid Seif ni yule ajulikanaye kama "Saddam" ambaye aliwahi kuwa pale polisi Chang'mbe na baadae akahamishiwa Iringa kama OCD. Ni mchapa kazi hodari na hana chembechembe za ufisadi.
ReplyDeleteInna lillaahi wainna ilayhi raajiun, mungu awalaze pema peponi marehemu na awape subira wafiwa.
ReplyDeleteJengine anko nanihii kwa marekebisho ya taarifa zijazo wilaya ya kati iko mkoa wa kusini na sio kaskazini unguja