HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. JAKAYA KIKWETE, WAKATI WA KUFUNGUA MTAMBO MPYA WA KUZALISHA SARUJI KWENYE KIWANDA CHA SARUJI CHA WAZO TAREHE 8 JULAI, 2009
Mhe. Dr. Mary M. Nagu (Mb), Waziri wa
Viwanda, Biashara na Masoko;
Mhe. William Lukuvi - Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam;
Waheshimiwa Mawaziri;
Viongozi wa Chama na Serikali;
Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana.
Awali ya yote, naomba nianze kwa kukushukuru wewe Ndugu Waziri, Wawekezaji na Uongozi mzima wa Kiwanda cha Saruji cha Wazo kwa kunialika kushiriki katika ufunguzi wa mtambo mpya wa kuongeza uzalishaji wa saruji katika kiwanda hiki. Hii ni siku muhimu katika historia ya Tanzania hususan kwa wakazi wa Dar es Salaam na Watanzania wote wanaotumia saruji inayozalishwa hapa.
Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Kwa mfanyabiashara au mzalishaji yoyote, kufanikiwa kupanua biashara yake au kuongeza uzalishaji ni jambo kubwa na la kujivunia. Kwahiyo basi, nawapongeza sana Manejimenti na Wanahisa wa kiwanda hiki kwa uamuzi wao wa kuongeza uzalishaji na kufanikiwa kupanua kiwanda hiki. Matokeo ya uamuzi huo wa kuongeza uzalishaji wa saruji kiwandani ni kuongezeka kwa mahitaji ya saruji nchini jambo ambalo lina manufaa kwa kiwanda na watumiaji wa saruji nchini na hata nchi jirani.
Pengo kubwa la mahitaji ya sementi kulingana na mahitaji nchini litapungua. Ni matumaini yangu na ya wengi, pia, kwamba bei ya saruji nayo itapungua.
Kama mnavyofahamu, katika miaka ya hivi karibuni, nchi yetu ilikumbwa na uhaba mkubwa wa saruji. Kwa ajili hiyo saruji ikawa bidhaa adimu na bei yake ikawa kubwa kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya nchi yetu. Bei ilipanda sana na kufikia shilingi 17,000/= kwa mfuko wa kilo 50 hapa Dar es Salaam na shilingi 25,000/= kwa maeneo ya pembeni mwa nchi hasa yale yaliyoko mbali na viwanda vya saruji.
Kimsingi uhaba wa saruji na kupanda kwa bei yake kumesababishwa na mahitaji kuwa makubwa mno kuliko uwezo wa uzalishaji wa viwanda vyetu. Mahitaji hayo makubwa ni yahapa ndani ya nchi na ya majirani zetu na hata nchi nyingine katika kanda yetu ya Mashariki na Kusini mwa Afrika. Kwa kweli, haya ni matatizo yaliyotokana na kukua kwa kasi ya maendeleo na mahitaji ya saruji nchini na katika nchi jirani na za kanda. Ni matatizo yenye sababu nzuri, yaani maendeleo. Ni viashiria muhimu kuwa uchumi unakua na hivyo nchi yetu inapiga hatua mbele.
Mtakumbuka hapa nchini kumekuwepo na ongezeko kubwa sana la shughuli za ujenzi wa barabara, shule za sekondari, zahanati na nyumba za watumishi wa umma. Shughuli za ujenzi zimekuwa kubwa hata kwa majirani zetu na kwa Afrika Kusini ambapo miundombinu inaboreshwa kwa sababu ya Kombe la Dunia mwaka 2010.
Tatizo la uhaba na bei kubwa za saruji lilitokea kuwa changamoto kubwa kwa Serikali. Katika kukabiliana na upungufu huu, ilibidi Serikali ichukue hatua za haraka za muda mfupi za kuwezesha uingizaji saruji kutoka nje ili kufidia pengo. Hii ilikuwa ni pamoja na kuondoa suspended duty kwa saruji inayoingizwa nchini. Juhudi hizo hazikufanikiwa sana katika kumaliza au kupunguza tatizo kwa ukamilifu. Bado tatizo liliendelea kuwepo ingawaje makali yake yalipungua kiasi. Jawabu la kudumu lipo katika kuongeza uzalishaji wa saruji nchini. Bahati nzuri rasilimali za kufanya hivyo zipo kwa wingi katika maeneo mengi hapa nchini. Tumechukua hatua za makusudi kuhimiza uzalishaji wa saruji nchini kwa kushirikisha wawekezaji.
Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Upanuzi wa uzalishaji katika kiwanda cha saruji cha TPCC Wazo tunaouzindua leo ni hatua muafaka kwa ajili hiyo. Aidha, ni kielelezo na matokeo ya uhusiano mzuri ambao umeendelea kujengeka kati ya wawekezaji na Serikali. Ni dhamira yetu kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji katika kuongeza uzalishaji wa saruji nchini. Lengo la Serikali ni kuvutia wawekezaji wapya na kuhamasisha waliopo kuwekeza zaidi. Nawashukuru tena wamiliki wa kiwanda cha TPCC Wazo Hill kwa kuitikia wito wa Serikali na kuchukua hatua thabiti kuongeza uzalishaji wa saruji nchini ili kukidhi mahitaji makubwa yaliyopo.
Nimeelezwa kuwa kabla ya Kampuni ya TPCC Wazo kuwekeza katika mtambo huu mpya kwa lengo la kuongeza uzalishaji, uwezo wa kiwanda ulikuwa ni kuzalisha tani 650,000 tu za saruji kwa mwaka. Aidha, baada ya uwekezaji wa takriban Dola za Kimarekani milioni 108 (USD 108 million), uwezo wa uzalishaji umeongezeka zaidi ya mara mbili na kufikia tani 1,400,000 za saruji kwa mwaka. Mafanikio haya ni makubwa na kwamba yanastahili pongezi.
Ndugu Wananchi, Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana;
Kwa jumla hivi sasa, uwezo wa kuzalisha saruji hapa nchini kwa viwanda vyote vitatu vya Dar es Salaam, Tanga na Mbeya umeongezeka kutoka tani 1,770,000 mwaka 2007 hadi kufikia tani 2,470,000 kwa sasa. Uwezo huo unatarajiwa kufikia tani 2,970,000 mwishoni mwa mwaka huu hapo Kiwanda cha Saruji Tanga kitakapokamilisha upanuzi. Hii itatoa nafasi ya viwanda hivi kutosheleza mahitaji ya saruji nchini ambayo kwa sasa yanakadiriwa kuwa tani 1,900,000 kwa mwaka na kuwepo ziada ya kuuza nje ya nchi.
Ni matumaini yangu kuwa saruji inayozalishwa nchini itaweza kuhimili ushindani unaotokana na saruji inayoagizwa kutoka nje kwa bei na ubora. Hili linawezekana endapo TPCC na viwanda vingine vya saruji vitatumia “comparative advantages” tulizonazo hapa nchini zikiwemo za upatikanaji wa malighafi ya madini ya chokaa na gesi asilia.
Napenda kuwahakikishia kwamba Serikali inatambua wajibu wake wa kuwalinda wawekezaji na vitega uchumi vya nchi dhidi ya ushindani usiokuwa halali na kusababisha hasara kwao. Napenda kutumia nafasi hii kuwakumbusha viongozi na maofisa wa vyombo husika vya Serikali kutimiza ipasavyo wajibu wao katika jambo hili. Hap nazungumzia Tume ya Ushindani (Fair Competition Commission [FCC]) yenye jukumu la kuhakikisha kwamba kuna mazingira mazuri ya ushindani na TRA yenye wajibu wa kuhakikisha kila mtu analipa kodi za Serikali ipasavyo. Kimsingi TRA inao wajibu wa kuhakikisha kuwa hakuna mtu anakwepa kodi ya kuingiza saruji kutoka nje. Hayo yakifanyika siyo rahisi kwa saruji itokayo nje kuuzwa kwa bei ndogo kuliko inayozalishwa hapa nchini. Kwa kufanya hivyo, tutaungana na wawekezaji hawa katika kujenga uchumi imara wa viwanda.
Lakini pamoja na kusema hivyo, napenda kuitumia nafasi hii kuwakumbusha wenzetu wa Wazo Hill na wengineo wenye viwanda nchini kufanya kila muwezalo kuhakikisha kuwa bei za bidhaa mnazozalisha zinakuwa nafuu kuliko bidhaa zitokazo nje. Kaeni chini mjiulize mtafanyaje au nini kifanyike ili iwe hivyo. Kama ni gharama kubwa za uzalishaji nini kifanyike gharama zipungue. Yako mambo mengi yaliyoko kwenye uwezo wa kiwanda chenyewe kufanya. Tafadhali fanyeni. Kiwanda hiki ni mfano wa kwamba ukitumia teknolojia ya kisasa unaweza kupunguza gharama za uzalishaji hivyo kumudu ushindani.
Natambua kuwa yapo mambo ambayo yako nje ya uwezo wa kiwanda ambapo menejimenti haina budi kuzungumza na wahusika kuchukua hatua zipasazo. Wizara ya Viwanda na Biashara isaidie kuvisemea viwanda kwa mamlaka husika katika kutafuta majawabu ya matatizo ya namna hiyo. Lile litakalowashinda tuhusisheni na sisi. Yuko Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na mimi. Naamini mkishirikiana vyema na wenzenu wala hamtalazimika kukata rufaa. Hayo yakifanyika mtapata ufumbuzi wa takriban kila changamoto labda liwe ni jambo lililo nje ya uwezo wetu sote.
Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana;
Serikali itaendelea kuchukua hatua za makusudi kupatia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazokabili wawekezaji na uwekezaji nchini ili kuhakikisha kuwa mazingira ya uwekezaji yanaboreshwa. Miongoni mwa mambo ambayo tunayapa kipaumbele ni pamoja na kuendelea kuboresha na kuimarisha miundombinu muhimua ya umeme, gesi asilia, barabara, reli na bandari. Kuboreka kwa miundombinu hiyo kutaongeza ubora na kupunguza gharama za uzalishaji na huduma za usambazaji wa saruji na bidhaa nyingine za viwandani. Pia kutapunguza bei ya saruji kwa mikoa iliyo mbali na kiwanda hiki na vingine vya saruji nchini.
Kwa upande wa umeme, tunaendelea na mipango mbalimbali ya kuongeza uzalishaji wa umeme na kuimarisha miundombinu ya usambazaji wa umeme nchini. Kwa mfano, hapa Tegeta tunajenga mtambo mpya wa kuzalisha megawati 45 za umeme ambao utasaidia kuhakikisha upatikanaji wa umeme kwenye kiwanda hiki. Wakazi wa maeneo haya nao watanufaika.
Ndugu Wananchi,
Kuongeza uzalishaji wa saruji nchini ni jambo moja, lakini lingine lililo muhimu sana nalo ni kuhakikisha kwamba saruji inawafikia wananchi kwa urahisi kwa bei nafuu. Kwahiyo basi, mfumo mzuri wa biashara ya usambazaji wa saruji ni jambo linalostahili kupewa kipaumbele. Sio jambo jema na ni kinyume na kanuni za soko huria kupunguza kwa makusudi upatikanaji wa saruji makusudi ili kuongeza bei kwenye soko. Nawaomba wenye viwanda na wauzaji wa saruji wajiepushe na vitendo hivi viovu.
Vilevile, ni mategemeo yangu kuwa wenye viwanda vya saruji nchini watajitahidi kufungua maghala makubwa (depots) za kuuzia saruji katika mikoa hasa ya mbali na viwanda ili kuungana na Serikali katika kuhakikisha kuwa mlaji anapata saruji kwa bei nafuu.
Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Baada ya maneno haya, sasa nizindue rasmi mtambo mpya wa kuzalisha saruji.
Asanteni sana kwa kunisikiliza

tunahitaji kiwanda Mwanza
ReplyDeleteNILISIKIA TETESI KWAMBA NASISI MTWARA TUTAJENGEWA KIWANDA SIJUI HUU NI UKWELI AU? NISAIDIENI WADAU KAMA MNA HABARI YEYOTE
ReplyDeleteAnd what about our dear environment? I mean pollution to the environment? I hope it is also taken into consideration. Yeah, expansion of industries is marvelous but environmental issues need to be accounted as well.
ReplyDelete--Proud Tanzanian.
priud tanzanian...nenda kacheki North Mara
ReplyDeleteafu me uwa simuelewi uyu baba,eti "ANASHANGAA" kwanini wananunua malighafi nje badala ya Tz
khaaaaaaaa