Salaam kwa wadau wote wa blogu hii ya jamii.
Kina Klothing ina furaha kuwafahamisha kuwa tumefungua duka letu mtandaoni na unaweza sasa kununua Tshirt moja kwa moja kupitia www.kinaklothing.com
Kina ni kampuni mpya ya nguo ambayo inawakilisha Bongo na Afrika kwa ujumla. Kwa utambulisho tumetoka na collection inayoitwa Uhuru St. kwa sababu neno uhuru linabeba sababu nzima ya sisi kuanzisha Kina.Vilevile hii ni lebo ya mavazi ya kitaa na Uhuru ni mtaa wa kwanza katika mfululizo wa kollektion zitakazobeba majina ya mitaa mbalimbali ya Bongo na Afrika kwa ujumla.

Kama kauli mbiu yetu inavyosema “Vitu vyetu. Kivyetu” basi ndio tunavyotarajia kuendesha lebo yetu, yaani full uhuru wa kutengeneza kazi zinazotuwakilisha, kwa namna tunayoamua wenyewe.

Fulanazz hizi zimesanifiwa mahsusi kwa ajili ya wabongo na marafiki zao ili kuonyesha kuwa wabongo nao tumo katika medani hii ya design; lakini si hivyo tu, ujumbe unaobebwa na nguo kina ni mchango wetu katika harakati za kujenga madaraja kati ya waafrika barani na diaspora kwa kusambaza na kusheherekea yale yanayotuunga pamoja kama waafrika.

Hata hivyo, katika collection hii ya kwanza
tumeamua “kucheza kwetu” zaidi, tunatumai utatutunza.

Tutembelee
na tuambie mawazo yako.
Pia usisahau kujiunga nasi katika ukurasa wetu ya facebook http://www.facebook.com/pages
/Kina-Klothing/101720604819
na kutufuatia katika
http://www.twitter.com/kinaklothing

Kaa mkao wa kula kwa collection inayofuatia,
Samora avenue. Iko jikoni.
Amani.
Mkuki na Susan (Kina Klothing)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 21, 2009

    This is very nice, Hongera sana na tutanunua tu :)

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2009

    Mbona hiyolink ya facebook haifanyi kazi ndugu zetu?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2009

    http://www.facebook.com/pages/Kina-Klothing/101720604819?ref=ps try this.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 21, 2009

    asante kwa maelezo mazuri juu ya mradi wenu mzima, nimefurahi na kuelewa vizuri, hata hivyo ningelipenda kujuwa zaidi juu ya nembo yenu, inaashiria nini? ina ujumbe gani na hiyo kama misumeno hapo ni nini? nimeona kk mbili ambazo mara moja kuziona na nimefahamu maana yake ila vyenginevyo nimeshindwa. asante.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 21, 2009

    Hi1
    Hii imetulia sanaaaa! hongereni sana kama niko nje ya TZ nazipateje na gharama zinakuwajeeee??

    ReplyDelete
  6. Bwana anon, mimi naitwa Mkuki ni creative director wa Kina Klothing na msanifu wa hiyo nembo pamoja na collection nzima ya nguo za kina.

    Nembo yetu ni kweli kama ulivyoilezea kuwa ni K mbili ambazo ninaunda kiumbe fulani ambaye ndio "personification" ya kampuni yetu yaani hizo KK zinaungana kuzaa huyo kiumbe!

    Vilevile utaona kuna idea ya "ferocity" ndio maana huyo kiumbe anatema moto.
    Hiyo misumeno ni abstraction ya manyoya ya huyo kiumbe lakini hapo chini hizo K zinapoungana utaona mshale unaoashiria kuchimba chini yaani kuongeza Kina (depth/deep)

    Mwisho utaona hii nembo ina mahadhi ya kifalme/au uongozi fulani hiyo ni makusudi pia kwa hiyo utaona kuna layers nyingi za fikra ambazo zilikwenda katika ubunifu wa nembo hii.

    Nisingependa kuichambua sana maana nataka pia na wewe utengeneze maana yako kutokana na experience zako vilevile.

    Kama jina letu linavyosema huwa tunapendelea usanifu wenye kina basi hiyo ndio falsafa yetu tunayoifuata katika kazi zetu.

    Anon uliyeuliza kuhusu kuzipata nje ya nchi tafadhali nenda katika site yetu www.kinaklothing.com ukishamaliza kuorder utachagua nchi uliyopo na tutakutumia moja kwa moja. Kwani uko wapi?

    Asanteni sana wote kwa maswali na mawazo yenu, karibuni sana mtutembelee mtandaoni www.kinaklothing.com au facebook http://www.facebook.com/pages/Kina-Klothing/101720604819

    Tupo pamoja, Mkuki

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 22, 2009

    Mbona mwaonea lakini nilikua nataka niode mbili moja yangu na moja ya mama yangu ambaye yupo bongo...kuiship Tanzania naambiwa $5.99 kuiship US ni $3.99....sasa kama ziko hapo bongo si mngeship kwa bei rahisi bongo then huku ni mtucharge that much jamani mbona bongo hakuna pa kupumulia

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 22, 2009

    nimeimaind sana hiyo t shirt nyeusi tz 1961,ningpenda kuhagiza hiyo t shirt,big up watanzania wenzangu mnajitahidi sana dont give up,mambo pole pole sio tutafika where we are supposed to be,

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 22, 2009

    Tafadhari naomba mnijulishe mpo wapi kwa hapa TZ,
    Nimesoma samora Ave sasa sijajua kipande kipi/karibu na wapi?
    Nataka sana product zenu
    please

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 22, 2009

    Maswali yoyote juu ya kuorder, tafadhali wasiliana nasi kwa kupitia info@kinaklothing.com
    Tunatanguliza shukurani zetu.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 22, 2009

    Tuelekezeni kwa Hapa Bongo mnapatikana wapi? Tumependa T shirts zenu

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 22, 2009

    Ndugu yetu sio uonevu ila Kwa sasa hatujaweka duka Bongo, tunalifanyia kazi hilo swala maana kama unavyoelewa hivi vitu vyote vyataka pesa. Tunashughulikia kuleta mzigo Bongo (Kwa sababu kwa sasa shughuli zetu tunafanyia USA) na kama ukiwasiliana nasi kwa email tutakujulisha mzigo utakapofika Bongo.
    Njia rahisi ya kupata updates kwa haraka ni kwa kutumia facebook page yetu ukijiunga kama fan wetu basi utapata habari zote kuhusu Kina mara moja tunapozitoa. Link ni hii hapa copy and paste kwenye browser yako uelekee huko.
    http://www.facebook.com/pages/Kina-Klothing/101720604819
    Asante sana kwa maswali yenu wote ndugu zetu.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 23, 2009

    ooh kumbe hamjafungua duka bongo

    asante

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...