kamanda suleiman kova akiongea na wanahabari mchana huu kuhusu matukio kadhaa ikiwa ni pamoja na la mazoezi dhidi ya ugaidi bandarini, na pia ametangaza kwamba kambi mbili maalumu kwa kuhifadhia maiti walioopolewa katika mabaki ya ajali ya ndege ya Yemen huko Comoro na kupwelea kisiwani Mafia zimeandaliwa Dar na huko Mafia na maiti wataletwa Muhimbili kwa uhifadhi na utambuzi.
'boti la magaidi wa kisomali' likiwa limezingirwa na wanausalama baada ya 'maharamia' wawili kutiwa mbaroni. walikutwa na matango na matikiti maji yenye nyaya kama za mabomu.

askari na boti zao wakiwa wamelizingira la 'boti la maadui'

shed namna 3 na 4 haina mtu
wafanyakazi bandarini wakihadithiana muvi lilivyokuwa. wengine waliifananisha boti ya polisi kama mbeki aliyepigwa chenga na 'boti la maadu' kuwa mfungaji ambaye aliachiwa hadi nyavuni


HABARI NI KWAMBA BREKING NYUUUZZZZ YA HAPO CHINI IMEDHIHIRIKA KWAMBA ILIKUWA SI KWELI BALI NI TIZI LA ASKARI WA USALAMA BANDARINI WA NAMNA YA KUANDAA WAFANYAKAZI NA WADU WENGINE WA MAMBO YA DHARURA ENDAPO LITATOKEA TUKIO LA UGAIDI BANDARINI HUMO.

AKITHIBTITISHA HAYO MCHANA HUU KAMANDA WA MKOA MAALUMU WA KIPOLISI WA DAR AFANDE SULEIMAN KOVA AMESEMA KWAMBA BOTI LIENDALO KASI LILOKUWA LIKIANDAMWA NA MELI YA DORIA YA JESHI POLISI LA MAJINI HADI BANDARINI ILIKUWA NI MOJAWAPO YA TIZI HILO

MESEMA KATIKA 'DHARURA' HIYO ILITANGAZWA KWAMBA KUNA BOTI INA MAHARAMIA WA KISOMALI WAKIWA NA MABOMU, NA WAMEINGIA BANDARINI BILA IDHINI NIA YAO IKIWA NI KUVAMIA GHALA YA MAFUTA.

KAMANDA KOVA AMESEMA TENA NA TENA KWAMBA HAKUNA MABOMU WALA MAGAIDI AMA MAHARAMIA WAKISOMALI, BALI DHARURA HIYO ILIKUWA NI MAZOEZI TU NA WANA USALAMA WA MAJINI PAMOJA NA VIKOSI VINGINE VYA ULINZI NA USALAMA.

HATA HIVYO SHED (GHALA) NAMBA 3 NA 4 BANDARINI HAPO BADO YAMEFUNGWA KWA DHARURA HIYO, HUKU WAFANYAKAZI KADHAA WAKIWA WANATIBIWA MAJERAHA NA BP.
MAJIRA YA SAA NNE HIVI, WAFANYAKAZI WOTE WALITOKA MKUKU WALIPOAMRIWA KUFANYA HIVYO KUELEKEA NA GETI NAMBA 3 NA 4 AMBAKO KUNA KAMUINUKO KIDOOOOOGO - HIVYO REJETA KIBAO ZA WADAU ZILICHEMSHA.

ZOEZI KAMA HILI HUTOKEA MARA KWA MARA UWANJA WA NDEGE, NA KWA BANDARINI HII NI MARA YA KWANZA NAIONA. WENYE UHAKIKA ZAIDI TUNAOMBA MWANGA ZAIDI ENDAPO KAMA TIZI KAMA HILI LIMEPATA KUFANYIKA HAPO.













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2009

    ahaaa ....thanks kwa habari
    keep it up!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 08, 2009

    ...ila mna wazimu nyie....

    iyo newzz apo awali kidogo niseme acheni masihala ayo,kumbe ni kweli?

    ivi ina mana ayo ma-tizzi yakifanyika ndo msumbue raia na wengine watakufa apo izo pressure,ivi mnaelewa lakini?na NO taarifa JAMANI KWELI?mnafanya tizzi sijui sehemu ya kadamnasi?

    wengine tuko mbali na uko kwetu,mnafikili kazi zimefanyika uku,na tuko salama??

    HII MPYA KALI YA MWAKA,APA NSHAPIGIA MY NDUGUz dar nijue chochote

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 08, 2009

    INAMANA MAZOEZI KAMA HAYO NDIO WAMESHINDWA KUWATAARIFU WA KAZI WA MAENEO HAYO KABLA HILI KUEPUKANA NA USUMBUFU WOWOTE? MBONA NCHI ZINGINE HUWA WANATANGAZA AU NDIO KILA KITU SIE HATUPO MAKINI?
    SASA SIKU NYINGINE TUKIO LIKIWA LA KWELI NA WATU WAKIPUUZA ITAKUWAJE?
    KWELI AKILI NI NYWELE KILA MTU ANA ZAKE.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 08, 2009

    mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Mimi binafsi nimeipenda hii ya mazoezi.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 08, 2009

    Zoezi la namna hii haliwezi kufanyika kwa kutangazwa kwenye vyombo vya habari, kwani kufanya hivyo kutapotosha lengo la zoezi la kupima utayari wa wadao wote.

    Iwapo zoezi kama hilo lingekuwa linafanyika mara kwa mara, hata hali ya panic isingekuwa kubwa hadi rejeta kibao kuchemsha. Nawapa pole sana wote waliohitaji matibabu kutokana mshtuko wa zoezi kufanyika, hasa ikizingatiwa kwamba kuna miezi miwili na kitu tu tangu yatokee maafa kutokana na yale mabomu ya Mbagala...

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 08, 2009

    Zoezi kama hili ni lazima lifanyike bila kutangaza kwa kuwa majambazi na maharamia hawatangazi. Kilichofanyika ni sihihi kabisa, inabidi vikosi vya usalama wapime ni haraka kiasi gani watu wanaweza kupokea amri ya kustukiza vinginevyo ikitangazwa watu wanajitayarisha na kuharibu maana nzima ya lengo la zoezi lenyewe.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 08, 2009

    Tunapoteza muda na fedha kupigana vita visivyo vyetu. Makazi yanaungua moto kila kukicha, wataalamu na vifaa hamna. Ajali zinatokea, watu wanatumia nyundo na Tindo kuokoa raia. Hata ambulance kwa mjamzito kukimbizwa hospitali Hatuna!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 08, 2009

    INA MAANA WAFANYAKAZI WA BANDARI HAWAKUPEWA TAARIFA AU MAELEKEZO MAPEMA KUHUSU KUWEPO KWA ZOEZI HILO? KAMA NDIYO HIVYO BASI VYOMBO VYA USALAMA NA UONGOZI WA BANDARI WAMECHEMSHA!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 08, 2009

    ...weweeee acha zenu

    ivi mtawafidia ao wataopata tatizo la kiafya na ayo magari mkweche yetu tulojipinda wee kupata?au mtu afe apo mtakuwepo kuwafariji wahusika??

    nchi isiyo na fidia hii!!! kaaazi kweli

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 08, 2009

    (!) Kumjibu mdau wa hapo juu (anon July 08 02:51:00 alasiri (pm), si lazima wafanyakazi wapewe taarifa kwani wanapoajiriawa wanakuwa au wanatakiwa wawe wameambiwa maelekezo yote haya (jinsi ya kuepukana na matatizo yote haya endapo patatokea mitafaruku kama "ilivyotokea jana")

    (!!)Je mazoezi kama haya yanafanyika mara ngapi kwa mwaka/mwezi?

    (!!!) Nafikiri ni vema mazoezi haya yawe yanarudiwa mara kwa mara nna yasiwe kwa ajili ya maadui tu bali pia kwa kuokoa maisha ya watu kutokana na moto (fire drills) au hata majanga mengine yanayoletwa na technologia zetu za sasa.

    (!!!!) Mwisho hongera sana kwani naona zoezi zima lilifanikiwa

    Nawasilisha

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 08, 2009

    Kwa kawaida mazoezi kama haya ufanyika bila kutangaza kwa watu japo wapo wachache walio ngazi ya juu katika taasisi husika zoezi linapofanyika wanaweza kupewa taarifa lakini kwa ujumla wake bado uwa ni siri ya hao wachache.

    Lengo siyo baya kwani wanataka kuangalia response ya watu walio sehemu ile iko vipi kama kutatokea janga la kweli mahali hapo.

    Nakumbuka mazoezi kama haya yamepata kufanyika JNIA (Dsm Airport), Pia Bandarini dar mwaka jana, na pia Pale PPF Tower.

    Tatizo langu ni kwamba pamoja na mazoezi hayo ambayo washiriki wake nao hawaishi kuweka mikogo yao lakini pale inapotokea majanga ya kweli huwa hakuna response ya haraka kutoka kwa vyombo husika. Mfano majanga kibao kama moto, uhalifu wa kutumia silaha, kuzama kwa vyombo vya usafiri kwenye maziwa au baharini, ajali barabarani na hata kuanguka ndege lakini mara nyingi uwa hakuka prompt response kwa upande wa vyombo vya serikali na vyombo vingine kwa ujumla.

    Simaanishi kwamba hakuna uwajibikaji kabisa. wanajaribu jaribu lakini mambo bado.

    Kwa maana hiyo basi mbwembwe hizi zisiishie tu kwenye mazoezi haya gheresha lakini ziwepo pia wakati majanga halisi yanapotokea.

    Mie Scallywag.

    T

    ReplyDelete
  12. Pongezi kwa jeshi la polisi kuweka hizi drill.Mambo haya yanatakiwa yazingatiwe na kila mtu anayejishughulisha na kitu chochote hapo bandarini.Isiwe mara ya mwisho kwa jeshi la polisi kufanya haya mazoezi.

    By the way.
    Anon #2 kama huwezi au hujui kuandika kiswahili fasaha acha kubonyeza keyboard.Rudi darasa la 3 ukajifunze kuandika kiswahili fasaha.Unaharibu Lugha yangu.Siwezi kuelewa unachosema au unachomaanisha.Dah inatia kinyaa kusoma unachosema.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 08, 2009

    wewe mtoa maoni wa pili unaishi wapi? kwani haya mambo yaktokea kweli kweli yatatokea wapi? kambini pasipo na raia? mbona nchi zote hivi ndivyo wanavyofanya? wanajifunza kwengine na from time to time wanafanya zoezi zima kwenye mazingira ya kawaida ili kuona kama kweli walichojifunza kinaweza kutendeka in real life.

    ReplyDelete
  14. MTz mpenda usalamaJuly 08, 2009

    We anonymous wa 02:49:00 PM, wewe utaendelea kuwa kama mbuni ambae akiona hatari anajificha kichwa mchangani mpaka lini? Unasemaje tusipigane vita ambavyo sio vyetu? Na hali ya sasa ya ulimwengu ilivyo kiamani, maharamia hawachagui nani wa kumfanya nini. Je umesahau kwamba miaka 11 tu iliyopita kuna bomu lilipigwa Ubalozini na kuua watanzania 10 na kujeruhi kadhaa? Msijidanganye kuwa hamna atakaewagusa, una uhakika gani kwamba siku moja haitatia nanga meli ya kimarekani hapo maharamia wakaamua kuifanyizia. Achilia mbali matukio yanayoweza kuwa ajali, kama ile ya mbagala. Unadhani ile mifuko ya mbolea kule kwenye maghala ikiwaka moto utakuwaje, kama sio vurugu mechi? Ndio maana shughuli kama hizi huandaliwa na vyombo vya usalama, JNIA huwa wanafanya mara kwa mara.

    Kwa nini watanzania tunataka kujiaminisha kuwa na amani yetu hamna atakaetugusa? Ulimwengu umekuwa mdogo, humu humu ndani unaweza kuta kuna vijana wanaandaliwa kwa ajili ya kufanyiziana. Mi nalipongeza jeshi kama limefanya "drill" kama hii, na kulishauri inabidi ziwe zinafanywa mara kwa mara hasa kwa maeneo nyeti kama hayo ili watu wanafanya kazi huko au kuyatembelea mara kwa mara wasijisahau sana kama ilivyokuwa leo.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 08, 2009

    KWA MTAZAMO WANGU MDOGO
    ZOEZI KAMA HILO NI MUHIMU SI KWA RAIA TU BALI HATA KWA VYOMBO VYA USALAMA PIA KUWA TAYARI ENDAPO KUNAWEZA TOKEA JAMBO KAMA HILO WAWE NA UTAYARI NA KUJUA NAMNA YA KUEPUKA

    KWA UPANDE WA TAARIFA HAKUNA SABABU YA KUTOA TAARIFA KWANI UKITOA TAARIFA RAIA HATAKUWA NA WASIWASI NA HATAWEZA KUMBIA KWANI ATAKUWA ANAFAHAMU KUWA NI ZOEZI

    SWALI KWANI JAMBAZI ANAPOKUJA KUKUIBIA ANATOA TAARIFA,

    HIYO NDIYO SABABU YA KUTOTOA TAARIFA.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 08, 2009

    Hili swala haliitaji raia kujulishwa na sasa ndio twakumbuka JKT muda wote Raia watakiwauwe mkakamavu kama sote tunge pitia JKT walatusinge pata shida ya kukimbia.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 08, 2009

    serikali nafikili imefikia wakati iendeshwa kisomi au kitaram inakuwaje zoezi la kijeshi lifanyike bila kutoa riport this crazy really how come.hiyo nikuonyesha watu wanaburuzwa,kungekuwa na respect kwa raiya na mari zao,hili lazima wangewatambulifu watu.sasa inakuwa hao watu walioumia watashuglikiwa matibabu bure? na hizo gharama itakuwa ya nani?? si pesa ya mulipa kode,yani inachekesha lalikini pia inasikitisha,hawa viongozi wamekwenda shule kweli? wangekuwa wamekwenda mambo ya safety wangekuwa wameyasomea.hiyo ndo bongo bwana.marlesa mussa wa 22.hapa.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 08, 2009

    Hahahah This is So so funny!

    ReplyDelete
  19. Michuzi !!zoezi kama hilo linaitwa DRILL.. ni vitu vya kawaida kwa nchi za dunia ya kwanza .. Hivyo Watanzania wanatakiwa waelewe jinsi ya kutumia vifaa vya kujiokelea na jinsi ya kujiokoa endapo itatokea dharura .. na sio Bandarini tu au airports, hata maofisini ,majengo makubwa yote shuleni ,hospital na kadhalika wanatakiwa wajue jinsi ya kujiokoa na moto .. sio ughaidi tu

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 08, 2009

    Get ready to have your mind blown. Ready? Here we go ...

    -- Michael Jackson signed his will on 7/7/02.
    -- Michael Jackson's memorial was on 7/7/09 ... exactly 7 years after the will was signed.
    -- Michael Jackson's two biggest hits -- "Black & White" and "Billie Jean" -- were each #1 for 7 weeks.
    -- Michael Jackson's three biggest albums -- "Thriller," "Bad" and "Dangerous" -- each produced 7 top 40 hits.
    -- Michael Jackson was the 7th of 9 children.
    -- Michael Jackson was born in 1958 ... 19 + 58 = 77
    -- Michael Jackson died on the 25th ... 2 + 5 = 7
    -- Michael Jackson has 7 letters in his first and last name.


    If you're looking for lottery numbers tonight, we recommend something with the number 7 in it.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 08, 2009

    HUU NI MCHEZO WA MTOTO KUMDANGANYA MAMA YAKE KUA AMEONA NYOKA NA SIKU NYOKA AKITOKEA KWELI NA KUMGONGA MTOTO SIJUI ITAKUAJE

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 09, 2009

    Watanzania tumezidi slow life. Changamkeni. Huku drills zipo kila siku na hamna anayepanda BP. Na ikiisha ndio mnaambiwa ilikua ya kitu fulani lakini before that ni mchakamchaka tu. Na hamna anayelalamika kwa Govt.

    Ebo hebu changamkeni na hayo mavitambi ndio maana kitu kidogo BP. Kesho kitu kikitokea kweli hata pa kujificha hamna, meeting place hamjui au emergency plans yeyote hamjui ni maafa tu.

    Huku kuna drills za kila aina matornado, fire,biochemical, floods, emergency evacuations you name it. Na emergency kits tunazo na kila miezi sita tunachange maji. Thanks God sijapata dharura ya kutumia hii kit na naomba mungu nisiitumiage but lazima niwe nayo. You never know...hivyo Big up kwa watu waliypoandaa hiyo drill....manatakiwa muwe sharp sharp

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 09, 2009

    wewe dogo wa Wed Jul 08, 08:51:00 PM mambo ya MJ hapa yamehusu nini? tena unaleta mambo ya kitoto kabisa. MJ is dead end of story, move on.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 09, 2009

    Good Job! Tanzania tunaendelea sasa.

    Mimi binafsi nafanya kazi one of interational organisation, Once a while tunaletewa fire grill.

    Fire grill means moto fake, kwahiyo wanatangaza kuna moto ndani ya jengo ili wafanyakazi wajue la kufanya,Kuna mtu special anakuwa anacheki zoezi linavyoendelea tunavyojiokoa. Hii inasaidia siku moto wa kweli umetokea kila mtu anajua anachofanya...

    Congrats Kova.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 09, 2009

    Mimi nafanyakazi kwenye hospitali binafsi hapa Dar nimeshashuhudia mara nyingi mazoezi haya yanafanyika kule airport Dar na kukimbiza majeruhi hospitalini kwetu, lakini Mkurugenzi na Matron huwa wametaarifiwa, lakini sisi wafanyakazi hatuambiwi, lengo lao ni kujua kama kweli mnaweza kukabili hali hiyo ya kupokea majeruhi walioanguka na ndege. Kweli jasho huwa linatutoka tunadhani ni kweli kumbe ni zoezi tu.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 09, 2009

    Kama huu si uzembe basi nini?
    kwa wakati wote wa zoezi hili hili kazi bandari zisimame wakati tunajua wazi hile ni sehemu muhimu kwa uchumi.ina maana wafanyakazi walisimama kufanya kazi na wakaandikiwa masaa yao na kulipwa!
    Pili:ni juzi juzi raia hapa Dar.walishtushwa na mahafa ya mabomu ya mbagala,leo hii bado hatujapumzika tuna stushwa na zoezi la mchana mchana na kutuweka raia Roho Juu za mashaka.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 10, 2009

    HAO WAFANYAKAZI MBONA KAMA VILE WAPO BREAK...SASA MBONA KAZI IMESIMAMA AU BADO WANAVUTA MUDA.SASA SHUGHULI ZIMESIMAMA NA WANALIPWA BURE AU BADO WANAHADITHIANA NINI KIMETOKEA?

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 10, 2009

    JAMANI EEH!welcome back to reality,ndugu waheshimiwa wabongo.hakuna kitu kama mtu kutaarifiwa kwenye emergency response,sasa wakikutaarifu si hata wewe ukiwaona uta CHILL TU ukifikiria ah si walisema kutakuwa na zoezi.lazima mtu uwe ALERT saa zote kwenye hii Dunia ya sasa ya mguu nje mguu ndani.mi nishafanya kazi bongo miaka 8 na yote hayo mnaelezewa na mnapewa DEMONSTRATION siku ya kwanza kwenye ORIENTATION,kuna fire drill,bomb threat,CPR na kadhalika,halafu at least kila mwezi mnapitia hiyo drill.kwa hiyo hizo sio weather forecast eti mtaarifiwe ala.Usalama wako unaanzia kwako mwenyewe,ujuwe tunaishi dunia ya aina gani sasa.na wewe mdau wa thur july '09 09:00am the word is DRILL NOT GRILL hatuko kwenye BBQ hapa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...