mazagazaga ya wadau wa toronto baada ya mgomo wa wazoa taka
ha ha habari ndiyo hiyo....
kama mwananyamala kwa kopa vile....
dah!
daraja mdebwedozzzzz...

Mh. Anko Nanihii,
Naomba uwatundikie wadau video na taswira hizi waone kuwa hata Majuu mambo ni tambarare kama Bongo. Hahahhaa!

Hivi karibuni shimo kubwa lilitokea katika barabara ya Finch mjini Toronto, Canada. Pia kulikuwa na mafuriko katika mitaa mbalimbali ya jiji la Toronto baada ya mvua kunyesha.

http://www.youtube.com/watch?v=occ0vFcevas
http://www.youtube.com/watch?v=kM_FgtGKLv0

Pia mgomo wa wafanyakazi wa halmashauri ya jiji la Toronto uliodumu kwa takriban siku 39 ulioisha jana ulipelekea jiji kujaa takataka na uchafu kila mahala.

http://www.youtube.com/watch?v=8KWkgOqJ9RA
--------------------------------------------------------
Hello Anko Nanihii,
Nashukuru kwa kutundika taswira za Toronto. Nimesoma maoni ya wadau waliotoa maoni hadi dakika hii na ni kama nilivyotegemea. Watu wengi wanaponda Bongo, na kulinganisha Bongo na Toronto; na hii sio mara ya kwanza, kila ikiwekwa picha ya "majuu" kuonyesha mambo yalivyo "tambarare" watu waakimbilia kusifia "majuu" na kuponda kwetu.
Nia yangu ya kuweka taswira hizo ni

1. Vyombo vya habari vya nje vimekalia kuonyesha mabaya yaliyo kwetu kila siku - vita, njaa, uchafu, n.k. Sikatai matatizo yapo, lakini mazuri pia yapo na ningependa angalau siku moja wayaonyeshe. Inafikia hatua watu wa huku nje ambao hawajawahi kusafiri kweli wanaamini kuwa Afrika yote ni vumbi, porini kwa wanyama, n.k. Kwa mantiki hiyo, nimeona si vibaya na sisi tukaonyeshana kuwa hata kwao mambo sio mswano dakika zote.
2. Watu wa nyumbani wengi wanadhania kuwa majuu ni kama mbinguni na kila kitu ni swafi kila sehemu, kila dakika. Sikatai kuwa wenzetu wameendelea na kwao ni kuzuri. Lakini kwa kuwaonyesha watu kuwa hata kwao kuna mambo mawili matatu ambayo hayajakaa sawa, itapelekea kupnguza kuwaabudu sana hawa jamaa na kuwachukulia kuwa nao ni watu kama sisi tu.
3. Mwisho, taswira kama hizi huwa zina nia ya kufurahisha umati na kuleta majadiliano motomoto, ni sehemu ya burudani na stori za jamvi la jamii.
Kinachonisikitisha sasa ni kuwa wengi wetu hatujipendi, hatupendani na hatupendi kwetu.
Kwa kuweka taswira hii watu wanafikiri kuwa tunajiliwaza, au kujilinganisha na nje. Sio hivyo, tunayajua mabaya yaliyo kwetu - ufisadi, njaa, n.k. si vibaya mara moja moja tukabadili stori. Kila kitu watu wanataka walinganishe Bongo na mtoni, sijui kwanini. Hatujivunii ya kwetu jamani; watu wanasahau nyumbani ni nyumbani hata kama porini.
Ndimi
mdau wa Toronto

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 31, 2009

    kamwe msijifananishe na dunia ya kwanza wadanganyika!!!!!!!!hayo ni matatizo ambayo ukirudi baada ya wiki hutayakuta,jaribuni kuwaamsha viongozi wenu walio lala usingizi tororo ili wawajibike KAMWE MSIJIFANANISHE NA DUNIA YA KWANZA NO MATTER WHAT!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 31, 2009

    Sisi kweli machizi hivi nchi kama canada tunaifananisha na tanzania duuu bro daraja lilijengwa haikupita muda, kuhusu mafuriko wanayasolve mara moja, khs mgomo hapa ndio penyewe sio kama tanzania ukigoma utakiona na kufukuzwa kazi moja kwa moja hakuna haki za binadamu balaa tu.

    Mjomba tanzania tunatakiwa tuwe na maendeleo sio tusubiri america au nchi za magharibi kitokee kitu halaf useme aaaa hata ulaya si hivohivo tu hio ni nomaz tuangalie nchi yetu na tuangalie mazuri sio mabaya.

    ReplyDelete
  3. Kazi kwelikweli wakati hata Rwanda inatushinda kwa usafi leo tunajifananisha na nchi zilizoendelea.Sishangai ndio maneno yetu Kikwete alisema hivihivi hata Japan kuna ujambazi..viongozi wetu ni kanyaga twende usafi ni majumbani kwao tu.

    ReplyDelete
  4. WANYARWANDA NA WAKENYA WANATUSHINDA. MIPANGO YETU OVYO.
    KILICHOBAKI NI KUJILIWAZA KII HIVYO?
    ....Tanzania Tanzania,
    Nakupenda kwa moyo wote,
    ....sitaweza kusahau mimi , mambo mema ya kwetu Africa....

    ReplyDelete
  5. Tunajipa auheni kwa kutazama uchafu wa wengine. Kweli sisi wapumbavu.

    ReplyDelete
  6. wewe uliyetuma hizi picha ni mbumbu kweli mafuriko ni mambo ya mother nature yanaweza kutokea popote pale kama vile tetemeko la ardhi na akina wenzie sunami sioni cha ajabu hapo grow up!
    mdau VANCOUVER

    ReplyDelete
  7. Sawa mafuriko ni nature na mgomo je? kwii kwiii kwiii asante sana uliyetuma hizi taswira hatimaye umetupa break ya wale "huku majuu" si unaona walivyokuja juuu eti waambieni viongozi wenu(anon wa kwanza) wakati na wao ni waTZ sijui kwanini wasiwaambie wao kisa wamejilipua na kuukana utaifa. Anon wa kwanza ni jukumu letu wote kupinga mfumo mbaya wa uongozi usijitoe kwenye hii kazi

    ReplyDelete
  8. kaka alituma picha hizi nashukuru sana kwa picha kwanza ni lazima tulingishe majiji kwa majiji ndio tupate sisi tuko wapi unaposema usilinganishe toronto na dar sikuelewi kabisa wakati wakiita ma meya wa majiji Mh.Kimbisa hakosi lazima tufike mahala tukubali changes kutokana na wenzetu walipo, hata wao hawakuanza kama walivyo wameanzia mbali sisi miaka 40 ya uhuru Mfano Usa wanamiaka zaidi ya 200 watch out watz safari bado ni ndefu hata

    ReplyDelete
  9. Mdau, TorontoAugust 02, 2009

    Ginfizz, nakubaliana na wewe kuwa ni lazima kuinganisha kwa nia ya kujifunza mbinu za maendeleo. Ni vyema kujilinganisha iwapo unafanya hivyo kwa nia ya kuona wapi walipotushinda, na pia kutathmini ni wapi tunapaswa kuwa kwa kiwango cha maendeleo yetu ya kiuchumi, n.k.


    Lakini kulinganishwa kunapozungumziwa hapo juu ambao hakufai ni kulinganisha wanakofanya Anony wa 1, 2, 5 na 6. Wao wanalinganisha kwa dharau, sio kwa nia ya kujenga. Ni sawa na we uende kijijini kwenu Katelelo leo na uanze kumuambia babu yako aahhh... huku kijijini hakufai, Dar bwana kuna mataa na majumba, huku "kwenu" kumechoka. Kweli nduguzo watakuelewa?

    Tunashukuru sana lakini kwa maoni, mjadalauendelee

    ReplyDelete
  10. Duh!kuna watu kweli Ulaya wamefika!ongea yao tu utajua,upeo mdogo wa kufikiri,kuridhika na vya watu,mpaka kukana kwao....mwe,eti viongozi wenu,utafikiri yuko kwenye MOON,mnajiona untouchables...eeh? mie hata cha kusema sasa sina,mwingine anisaidie.

    ReplyDelete
  11. nyie wenye kujikomba na nchi za watu muache hiyo tabia. mzungu hata siku moja hajikombi na nchi zenu. mnakasirika kuona hizo picha kwani ni uongo. huo mgomo umekuwa toronto kwa zaidi ya mwezi mmoja. huko dumping sites kumejaa panya na racoons. kumekuwa na wadudu wengi wakiwemo mende. mbona wazungu wanafurahi kuonyesha jinsi kuliko kubaya africa. kwanini musionyeshe pia ubaya huo unatokea kwao.

    ReplyDelete
  12. HIVI MKO SERIOUS AU NI MASHINDANO YA KIPUMBAVU AMBAYO NDIO YANAYOIRUDISHA NYUMA TANZANIA. ETI SASA HIZI PICHA NDIO KIGEZO NA PROOF KWAMBA WALIO UGHAIBUNI WANAIKANA NCHI YAO. HII NI OUTCOME YA MANISPAA YA JIJI KUGOMA NDIO HALI IMEKUWA HIVYO, MIJI MINGI MIKUBWA YA NJE ISIPOSAFISHWA HATA SIKU MOJA MATOKEO NDIO KAMA HAYO, HII INAONYESHA UWAJIBIKAJI WA WATU NA WATU WANAOJALI KAZI ZAO, MJI WOWOTE MKUBWA LAZIMA UNA UCHAFU NA MAENEO MABOVU SASA CHA AJABU NI KITU GANI, NA NYIE MLIOKUWA MNAFIKIRI KUWA MAJUU HAKUNA UCHAFU BASI NI WAJINGA PIA. PILI TANZANIA TUNAJIPA FARAJA ETI KWA KUWA TORONTO KUNA UCHAFU BARABARANI BASI TUKO SAWA NAO, HIVI MKO SERIOUS AU MNATAKA KULETA MCHEZO WA KUIGIZA HAPA, TZ WIZI KUANZIA VIONGOZI MPAKA UCHAFU WA MJI NI KITU CHA KILA SIKU NA MLICHOKIZOEA LEO MNACOMPARE EFFECTS ZA MAFURIKO NA KUGOMA KWA WATU WA JIJI NA KUJIPA MOYO ETI KUMBE MAJUU NAO NI TAMBARARE WHAT A BUNCH OF CRAP, HATA LEO HII TORONTO WAMWAGE MAVI MJI MZIMA BADO TZ ITABAKI HIVYO HIVYO ILIVYO MILELE NA KESHO YAKE TORONTO ITASAFISHWA NA WATU WANAOJUA WAJIBU WAO KULIKO HAO VIONGOZI WENU WEZI WA BONGO, NDIO NIMESEMA WENU MAANA NIMEUKANA UBONGO WANGU KWASABABU YA WIZI WA VIONGOZI NA TABU WANAZOZIPATA WANANCHI WA KAWAIDA KWA SABABU YA TAMAA ZAO. IT'S SAD KWAMBA HATA HUYO MTOA MADA ANA AKILI KAMA ZA WACHACHE KWAMBA ETI UCHAFU WA BARABARA UMEKUWA NI KITHIBITISHO KUWA MAJUU NI KAMA TZ TU, BADALA YA KUANGALIA MAMBO MBALIMBALI YA MUHIMU YANAYOIRUDISHA TZ NYUMA KAMA UZEMBE WA VIONGOZI NA KUTEGEMEA MIKOPO KUIENDESHA NCHI YETU TUNACOMPARE BONGO NA VITU VYA KIPUUZI KAMA HIVI. KWA VIJANA WOTE WANAOONDOKA KWENDA MAJUU WALA SIWALAUMU, YOUR LEADERS HAVE LET YOU DOWN, KWA HIYO BADALA YA KUKAA NA KUSUBIRI MIRACLES FUNGASHENI MKATAFUTE MAISHA KWINGINE MSAIDIE FAMILIA ZENU, EVERY MAN FOR HIMSELF SASA HIVI ACHENI KUJIDANGANYA. TANZANIA NILIYOKUWA NATAMANI KURUDI IMEONDOKA NA NYERERE NA MWINYI, SASA HIVI NI WIZI MTUPU NA KUPOTEZEANA MUDA TU.
    -Mdau Toronto_

    ReplyDelete
  13. ASNTE SANA MDAU WA TORONTO KUNA WATU WANAJIFANYA MUCH KNOW SANA KAMWE NA HAITAKAA ITOKEE BONGO KUWA KAMA CANADA ACHILIA MBALI SOUTH A.MIE TANGU NIJE HAPA NIMESHAISAIDIA SANA FAMILIA YANGU NA BADO NAENDELEA KUENDELEZA KWETU TOFAUTI NA NILIPOKWA HUKO HM HATA MR PRESIDENT ALIPOTEMBELEA UGHAIBUNI ALISEMA MSIBWETEKE NA MAJUU JENGENI KWENU SASA WE UNAYEKAZANA KUTUMA PICHA ZA UCHAFU BADALA YA KUTUMA MADOLA KWENU KUPENDEZE VILE MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA IMEKUWA NDOTO WE UNAONA HUU UPUZI NDO WAKUTOLEWA HOJA JENGA KWENU UPIGE PICHA UWEKE HUMU NDANI
    mdaus vancouver

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...