
Wanakijiji Wapokea Wito wa
Kilimo kwanza kwa Vitendo
Wanakijiji cha Masaera , Katika Kata ya Kilema Kusini, Tarafa ya Vunjo Magharibi Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro, wamepokea wito wa Rais Jakaya Kikwete wa Kilimo Kwanza kwa kuanza na juhudi ya kukarabati Mfereji wao wa Umwagiliaji.
Mfereji huo wa asili ambao ulijengwa takriban miaka 75 iliyopita umechakaa na kuanza kuvuja na kumomonyoka ,jambo ambalo limepunguza kasi na wingi wa maji ya kumwagilia mashamba ya kijijini hapo.Wanakijiji wameanza mradi wa kuukarabati Mfereji huo kwa kushirikiana na shirika la Canada la Veahavta, ambao walituma mtaalamu Christine Sinclair kukaa kjijini Masaera kwa miezi mitatu akichambua hali halisi ya eneo na kuwasaidia wanakijiji kuandika andiko la mradi.
Andiko hilo limepokelelwa na Wahandisi wasio na Mipaka wa Marekani. Wahandisi na wasidizi wapatoao kumi, wanaotoka Chuo Kikuu cha Valparaiso , katika Jimbo la Indiana Marekani walifika nchini mwezi Mei na kushirikiana na wanakijiji na kupanga mikakati ya kuukarabati Mfereji huo katika mradi utakaodumu kwa miaka mitatu hadi minne.
Baada ya uchambuzi wa mwanzo wa Kihandisi, wataalamu wa Marekani walitoa mapendekezo ya mwanzo ambayo yanahusu usafishaji wa Mfereji, jambo ambalo kwa sasa wananchi wanalitekeleza.Wanakijiji wameamua kuchangisha fedha za kununua zana za kupasua mawe makubwa mferejini na kutumia nguvu kazi ili kazi hiyo iwe imekamilika mwishoni mwa mwezi chini ya kauli mbiu, KILIMO CHA UMWAGILIAJI KWANZA.
Picha na Taarifa kwa hisani ya
Canute Temu.
Development Consultant, Translator, Editor, Documentalist;
Residence: Vanilla Farm , Masaera Village,
P O Box 270
HIMO,
KILIMANJARO,
Tanzania.
+255787258877 and +255754282101
Do good and do it well.
Fanya mema na yafanye vizuri.
TUKO PAMOJA HAMNA KIJIJI KITAKACHO ACHWA NYUMA CHARITY WILL START TO THE FAR NEIGHBOUR NEXT TIME.
ReplyDeleteMichuzi, asante sana kwa huduma nzuri ya kutuhabarisha na pia kutuunganisha na ndugu na marafiki tunaoishi katika pembe tofauti za dunia hii mtandawazi. sina budi nikiri hapa kuwa nimehemkwa kupita kiasi kuona kwamba taarifa hii imetolewa na rafiki yangu, ndugu (enzi hizo tukiitana ndugu) Canute Temu, ambaye hatujuliana hali siku nyingi. Bw. Temu nimefurahi kuona jitihada zako. Hongera sana na endeleza jitihada hizo. Tukipata wasaaa siku nyingine tutajadili kwa kirefu hizi kaulimbiu za siasa za JK 'kilimo kwanza' ambazo kwa hakika kinakinzana na ukweli wa mambo ambao ni 'biashara kwanza' hata kama hatutengenezi hata fulana wala soksi!!
ReplyDeletebwenge
cbwenge@africa.ufl.edu
aisee WACHAGGA kwa kujituma nawaaminia!!
ReplyDeleteDo, Historia yaonyesha kuwa mfereji huo ulijengwa na wamisionary
ReplyDeleteVipi kuhusu mti wa kwanza wa kahawa kuoteshwa Tanzania? Mzee michuzi zile picha za hicho kitalu ambacho kimesahaulika ambacho kingekuwa kivutio cha utalii vipi?
Mr Temu ana vyeo kibao consultant,Translator,Editor,Documentalist and the resident du,kweli huyu jamaa ni mkubwa
ReplyDeleteHongera kwa wanakijiji wa Masaera lakini mlihitaji wahandisi kutoka Marekani kuja kuwaelekeza jinsi ya kuukarabati mfereji huo? Wahandisi wa umwagiliaji SUA walishindwa hiyo kazi? Je wahandisi wa Mlimani, "Dar Tech", "Arusha Tech" nk nao walishindwa shughuli?
ReplyDeleteWahandisi wenye fani hii kama mmeona hii habari mjue ni changamoto kwenu. Mna nafasi kubwa kuwezesha mambo haya kufanyika nchi nzima.
hapo nina wasiwasi kuwa ni msukumo binafsi, kungekuwa hakuna hizo ngozi nyeupe ningefarijika sana. nafikiri tulisharogwa, kaulize tu ,utaambia hao jamaa wameweka ushawishi. kwani hadi jk aongee ndo watu wajue mfereji huo ulikuwa dili.
ReplyDeletekilimo kwanza, serikali haitaki kusema kuhusu soko.
mfereji wa kwanza ulichimbwa chini ya miinuko ya kilimanjaro miaka takriban 700 iliyopita. haukuchimbwa na wamarekani wala wayugoslavia, ulichimbwa na wachagga wenyewe. hii ni historia na nikweli , kizazi cha sasa si kwmba kimekataa kuchimba mifereji tuu ila hata kuitizama japo kwa macho tuu hawataki. sasa tujiulize? ni mzungu kaja kutuloga au tumejiloga wenyewe?
ReplyDeleteHaya ndio maendeleo...hata kama tumechelewa kidogo,muhimu ni kwamba nia tunayo.
ReplyDeleteKwa kweli tupo pamoja.Nami nimeanzisha blogu la uchumi,soma zaidi hapa:
http://wachumi.blogspot.com/
unaitaji uwe na mawasiliano ya barua pepep mzee.
ReplyDelete