Wadau wapendwa,
Hivi karibuni log ya jamii ilipata fursa ya kuongea na mwanamuziki wa kimataifa Lister Elia anayeishi na kuendeleza libeneke katika jiji la Tokyo nchini Japani.Fuatilia mahojiano yetu yaliyofanyika kwa njia ya mtandao.
Swali: Ilikuwaje ukaamua kupiga kambi katika moja nchi zilizo mashariki ya mbali ambazo kwa kawaida kiingereza hakitumiki?.
Jibu: Kwanza nikushukuru kwa kunikaribisha kwenye blog ya jamii na asante kwa kazi nzuri ya kutuhabarisha hasa sisi tunaoishi ughaibuni kwa njia ya mtandao. Muziki naweza kusema ni "universal language" na hauna mipaka wala ubaguzi wa rangi,lugha au jinsia. Muziki unapomuingia na kumliwaza yeyote awe mzungu,mweusi kama mimi au mjapani, humfanya mlengwa aingiwe na mzuka wa namna fulani ambao utamfanya aidha atingishe kichwa au kuchezesha miguu yake kinamna ili mradi kuonyesha kuridhishwa.
Uamuzi wangu kujitosa katika nchi ya wasiozungumza kiingereza ulikuwa katika msingi wa kutafuta maisha kwa kutumia talanta Mungu aliyonijalia kama msanii,na nilichukua advantage ya lile dokezo la muziki kuwa "universal language" na kwa hakika likawa limenifaa.
Swali: Tunatambua kwamba ki-taaluma umesomea muziki tofauti na ilivyo hapa nyumbani kwamba wanamuziki wengi hujifunzia mtaani. Hebu tueleze umejikita zaidi kwenye chombo gani cha muziki na si vibaya pia ukawaelezea wananchi mgawanyo wa kikazi wa makundi ya vyombo vya muziki.
Jibu: Maswali mazuri na ya kitaalamu. Nipe nafasi nikujibu pia kitaalamu.
Mimi ni "PIANIST" na pia ni "Keyboardist". Piano ni kinanda kikubwa ambacho kina "tone/sound" moja tu iitwayo piano. Chombo hiki asili yake ni katika nchi za magharibi.
Keyboard ni kinanda kidogo kwa umbo chenye vibonyezo vyeusi na vyeupe kama ilivyo piano(Grand piano).Keyboard inaweza kuchukuliwa huku na kule na imejazwa sound za vyombo vingi ndani yake. Mfano sound kama za saxophone,gitaa,brass,na milio mingi ya sythesizer hupatikana.Keyboards za kisasa hujengewa ndani kitu kinachoitwa "sequencer" au mashine inayomsaidia mpigaji kujitengenezea nyimbo zake mwenyewe katika mtindo wa "track recording".Keyboardist anayeijua kazi yake vizuri anaweza kuchukua ajira ya watu wawili/watatu katika bendi kutokana ufanisi wa chombo chenyewe.
Sehemu ya pili ya swali lako kuhusu mgawanyo wa makundi ya vyombo vya muziki na kazi zake ni kama ifuatavyo.
Vyombo vya muziki vimegawanyika katika mafungu makubwa manne ambayo ni

1.Strings instruments-vyombo vinavyotoa mlio wake kwa kutegemea nyuzi kama vile,gitaa,kinubi (harp) nk.
2.Membranophones-vyombo vinavyotegemea mtetemo wa ngozi ili vitoe sauti yake kama ngoma nk.
3 Aerophones-vyombo vinavyotegemea hewa ili vitoe sauti kama tarumbeta,ftute nk.
4.Idiophones-vyombo ambavyo ni mpaka vigongwe ndio vinatoa mlio kama xylophone marimba,kengele nk.
Pia Kuna vyombo vinavyowekwa kwenye kundi la "chordophones" yaani vyombo vinavyoweza kutoa mlio wake kwa kubonyeza "CHORD"(sauti tatu au hata nne kwa mara moja) kama kinanda,gitaa nk,vyombo hivi pia vinaweza kupiga "ghani" au melody,rythym ya wimbo na hata solo,na kwasababu hio vinaitwa "perfect instruments".

Mpiga piano mzuri peke yake anaweza kuuridhisha umati wa wapenzi wanaomsikiliza kwani kwa kutumia vidole vya mikono yake miwili anaweza kupiga melody ya wimbo,rythm na bass kwa wakati mmoja.
Vyombo vingine kama tarumbeta,saxophone,flute vimetengenezwa maalum kama leading instruments.Wapigaji wa vyombo hivi wanaweza kufanya "harmony" endapo idadi ya wapigaji itaongezeka wakawa wawili, watatu au hata wanne na hivyo kugawana sauti mojamoja katika kufanya harmony.
Swali: Wasifu au profile yako inaonyesha kwamba wewe pia ni mwandishi wa vitabu mbalimbali. Hebu waeleze wadu wa Globu ya Jamii vitabu vyako vinahusu nini hasa?
Jibu: Vitabu vyangu viwili vya "PIANO" na "JIFUNZE GITAA" vinahusu elimu ya muziki. Walengwa ni wanamuziki wanaochipukia na watu wa kawaida wanaopenda kujifunza piano na gitaa lakini wameshindwa kutokana na uhaba wa waalimu pamoja na vitabu.
Kitabu changu cha tatu "The mystery of Tamko's death" ni cha riwaya nikiwa na lengo la kutoa mafundisho na maadili mema kwa njia ya hadithi ya kubuni ambayo nimeitunga mwenyewe. Vitabu vyangu ni mchango wangu kwa ndugu zangu ili kuwamegea kijielimu kidogo nilichopata na wengine wafaidike.
Nimekuwa nikisisitiza kila ninapohojiwa kwamba umefika wakati Serikali yetu iweze kutambua umuhimu wa wanamuziki na kazi yenyewe ya muziki kwamba ni kazi kama kazi nyingine zote.
Katika nchi za wenzetu mfano Marekani wanamuziki,wanamichezo na wasanii mbalimbali wengi wao ni matajiri na wanatoa mchango mkubwa katika kuijenga nchi yao kutokana na kulipa kodi na mambo mengine. Serikali zao zimewawekea mikakati mizuri katika ufanisi wa shughuli zao kama kuwa na shule,vyuo na taasisi mbalimbali ambazo mwanamuziki anaweza kujielimisha na na kufanya muziki kama taaluma yake.Hapa Japan somo la muziki liko kwenye silabi kuanzia kwenye shule za msingi na kuendelea.
Tanzania,vyuo vya muziki ni vya kuhesabu..,shukrani ziwaendee taasisi mbalimbali za baadhi ya madhehebu kwa kuuona umuhimu wa kutoa elimu ya muziki.Mfano mzuri ni chuo kiitwacho Ruhija Musical Academy ambako nilipata mafunzo yangu ya awali ya miaka mitatu.
Natoa wito kwa Serikali yetu ianzishe na kuingiza somo la muziki katika shule za msingi,ili tuanze kupata vipaji vya wanamuziki tangu utotoni,tuwajengee msingi bora unaoendana na viwango vya kimataifa,kuliko kuwaacha wanamuziki wajifunzie mitaani,kuwatumia tu katika kampeni mbalimbali za wanasiasa na kutegemea wanamuziki hao hao waliojifunzia mtaani wapasue hadi kufikia level ya kimataifa.
Swali: Ili Mwanamuziki aweze kupiga muziki ki-mataifa anatakiwa awe na sifa zipi?
Jibu: Kuwa na elimu ya muziki ni advantage hasa kwa sisi wapiga vyombo,ni muhimu sana mwanamuziki ajue kusoma na kuandika muziki yaani "staff-notation,itamsaidia kujichanganya na wanamuziki wa nchi za nje.
Kujua lugha ya kiingereza japo kidogo kutasaidia kwani kiingereza ni moja ya lugha ambazo zinatumiwa na wengi duniani,itasaidia kujenga mawasiliano na wanamuziki wengine duniani. Inatakiwa wanamuziki wa Tanzania waondoe uoga wa kusafiri na kwenda mbali ili kujaribu bahati.
Swali: Je, una maoni gani kuhusu muziki wa kizazi kipya au kama unavyojulikana "bongo flava" pamoja na ule wa dansi?
Jibu: Napenda neno hili bongo flava ambalo linaashiria miziki yenye vionjo vya bongo,pia nazifurahia kazi za baadhi ya wana bongo-flava...,ila tatizo ninaloliona hapa ni kwamba miziki ninayoisikia haina vionjo vya bongo kama bongo-flava inavyojieleza.
Nikisikiliza miziki hii nagundua kwamba kuna vionjo vya "hiphop" ya wa-Marekani zaidi ,sema tu tofauti ni vile wanatumia lugha ya kiswahili.Nagundua kitu kingine kwamba vijana hawa wana vipaji vya kuwa na tenzi na kuzi-ghani vizuri,lakini wengi wao deep down si wanamuziki na miziki yenyewe hawaijui kabisa.Ku-ghani peke yake si kigezo cha kumfanya anaye-ghani aitwe mwanamuziki.Ni kama kuimba,kila mtu anaweza kuimba lakini kuimba huko hakumfanyi mtu aitwe muimbaji kwani kazi ya kuimba ina wenyewe waliobarikiwa kipaji hicho. Mimi mwenyewe naimba lakini si-muimbaji.
Nionavyo mimi bongo flava wanaonekana kuwa na success kwani baadhi yao wanafanyiwa promotion sana na vyombo kama redio,TV na magazeti na hivyo ni rahisi kupata umaarufu hata kama level ya miziki na nyimbo ni ya chini.
Hapa baadhi ya vyombo vya habari vinashiriki katika kuangusha level ya miziki. Haya ni maoni yangu binafsi and i stand to be corrected. Kwa wenzangu wa muziki wa dansi naona kama wamesahauliwa na vyombo vya habari hawapewi matangazo yanayowastahili. Pia naona kama wamekata tamaa na kukosa creation ambayo miaka ya nyuma muziki wa dansi ulikuwa juu.
Kuna bendi nyingi za muziki wa dansi Tanzania na kwingineko Afrika,wamekuwa wakijipachika neno jazz kwenye majina ya bendi zao,mfano OK JAZZ,BEMBEA JAZZ,TABORA JAZZ nk. Kwa mtazamo wangu naona ni kosa kubwa kwa bendi zisizopiga muziki wa Jazz kujipachika majina hayo yenye nyongeza ya neno jazz ,jazz ni aina ya muziki iliyoanzishwa na wa-Marekani wenye asili ya kiafrika. Muziki huu una taratibu na sheria zake kama ilivyo katika miziki ya rock,reggae,rumba nk.
Wageni wanapokuja Tanzania na kuingia kwenye ukumbi ambao Tabora jazz wanapiga,watategemea kusikia jazz music,badala yake wanasikia miziki yenye ladha nyingine,wanakwenda na habari kama hizo ambazo hazisaidii maendeleo ya fani hii.
Swali: Kama mwanamuziki wa kimataifa...unawasaidiaje wanamuziki wa hapa nyumbani ili wajiendeleze kimuziki,umma wa wa-Tanzania unafaidika vipi na elimu na uwepo wako huko ng'ambo? na pia nini matarajio yako kwa siku za usoni?.
Jibu: Ni vigumu kumsaidia mwanamuziki mmoja mmoja na ndio sababu iliyonifanya kuandika vitabu ili niweze kuwasiliana na kutoa msaada kimuziki kwa wote wanaouhitaji kitaifa. Pamoja na vitabu vyangu kuwa na manufaa kwa umma wa wa-Tanzania,nyimbo zangu,video zangu pamoja na hiki kitabu kipya cha riwaya vinalenga kuupa burudani umma wa wa-Tanzania.

Nilipotembelea Tanzania mara ya mwisho,nilijihusisha katika kutoa msaada katika kituo cha watoto yatima cha "New life Orphans Centre",kama mchango wangu japo kidogo kwa jamii.Siku za usoni nategemea kuanzisha "Foundation" maalum ya kutoa elimu ya muziki/upigaji ala za muziki na studio za kurekodi muziki wa wasanii mbalimbali.
Swali: Unapiga na kuimba muziki wa aina gani huko Japani?.
Jibu: Kama mwanamuziki wa kimataifa,nimejiandaa na niko tayari kupiga muziki wa namna yoyote kama nitakavyoombwa na mteja.Naweza kupiga muziki wetu wa dansi(African pops),reggae,classic piano,jazz piano,hata nikiombwa kupiga marimba ya kitamaduni toka kwetu Dodoma nilikozaliwa niko tayari.
Swali la mwisho: Wa-Tanzania wangependa kuona kwa vitendo ukiwa kwenye jazz piano ili wasikie vionjo vya jazz.
Jibu: Ningependa wasikilize nyimbo "Misty",hii ni moja ya nyimbo za jazz zinazojulikana duniani,niliipiga live katika moja ya maonyesho yangu jijini Tokyo.Tembelea
http://www.listerelia.com
hicho nacho kichwa! Nimekubali.. Big up!
ReplyDeleteYaani huyu Lister angekuwa anajua ninachowaza muda wote tungekuwa marafiki daima. yeye ktk interview yake hii ameweza kuwakilisha mawazo yangu yote kuhusu mtazamo wangu ki-muziki na ushauri wangu kwa wanafani wa muziki especially Bongo flava. msiridhike na misifa tu ya hapa na pale, angalieni na jifunzeni ala na notations za muziki. hawa producers wanawafanya mlale na waendelee kuwafyonza kwa kuwafanya tegemezi. naweza kukubet pesa kuwa wanafani kama akina professor J hawajui hata key za music wanazoimbia.
ReplyDeleteLister baada ya kufuatilia interview yako jinsi ulivyokuwa unajibu niliona ni bora nifungue web yako nijionee mwenyewe na kuisikiliza miziki yako nimekubali uliyoyasema muziki wako uko juu ni kweli umeenda shule wewe ni mwanamuziki wa kimataifa . pia hongera kwa kutunga kitabu cha hadithi unastahili sifa kwani utunzi wa kitabu unahitaji muda na ni mgumu lakini wewe umeweza kufanya kazi 2 tofauti hapo Bro nazidi kukumwagia sifa , ingawa ulishatunga vitabu vingine viwili lakini hivyo vilikuwa ni ara za muziki niliona kwako ilikuwa rahisi kwa vile unavitumia kwenye muziki , ingawa nimejaribu kufuatilia vitabu vyako vya jifunze gitaa na piano nasikitika baada ya kwenda kwenye maduka ulioorodhesha kupata jibu la kutokuwepo hivyo vitabu kwani wamesema vimekwisha sijui una mpango gani wa kutoa vingine kwani nina kijana wangu anapenda kujifunza muziki na hicho cha hadithi tutegemee lini kukipata ?. Lister kwa kumalizia, Mungu azidi kukukujaalia kwa kuwakumbuka watoto yatima , unapomsaidia yatima unapata baraka tele. HONGERA LISTER. Be.
ReplyDeleteHuwa unapiga wapi lesta, sisi huku Osaka hatujakusikia bado. Jitangaze katika magazeti kidogo.
ReplyDelete