Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) Mama Salma Kikwete akikata utepe kuzindua SACCOS ya Wanawake ya Umoja ni Nguvu SACCOS ya mjini Kaliua,Urambo Magharibi, Mkoani Tabora, jana mchana.Mama Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya wiki moja mikoa ya kanda ya ziwa chini ya uratibu wa Taasisi ya WAMA anayoingoza.

Mke wa Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, maybe pia ni mbunge wa jimbo la Urambo Magharibi, Mama Kapuya akikabidhi mchango wake wa shilingi laki moja kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) Mama Salma Kikwete katika harambee ya papo kwa papo aliyoianzisha Mama Kikwete wakati wa hafla ya uzinduzi wa SACCOS ya Umoja ni Nguvu ya Kaliua,Urambo Magharibi jana mchana.Katika harambee hiyo ya papo kwa papo zaidi ya shilingi 3.3m/- zilipatikana ikiwa ni fedha taslimu na ahadi.


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete(wapili kushoto) akikabidhi hundi ya mfano yenye thamani ya Shilingi Milioni Mbili 2m/-, kwa viongozi wa SACCOS ya Wanawake ya Umoja ni Nguvu ya mjini Kaliua,Urambo Magharibi jana mchana.Mama Kikwete alitoa fedha hizo kupitia taasisi ya WAMA anayoingoza wakati alipofanya ziara mjini Kaliua,Mkoani Tabora, kukagua shughuli za maendeleo ya wanawake.



Mweyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) Mama Salma Kikwete akisalimiana na baadhi ya wauguzi wa Kituo cha Afya Kaliua,mkoani Tabora muda mfupi baada ya kukabidhi vitanda viwili maalumu kwaajili ya wanawake wajawazito kujifungulia na seti moja ya vifaa maalumu kwaajili ya kumwezesha mama mjazito kujifungua salama.




Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akimkabidhi Kaimu mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Urambo Dr.Francis Nyemba mashine ya hewa ya Oksijeni kwaajili ya kuwasaidia wanawake wajawazito wanaojifungua kwa upasuaji katika hospitali hiyo.Mashine hiyo imatolewa kwa hisani ya WAMA jana wakati wa ziara ya Mama Kikwete wilkayani humo kukagua shughuli za maendeleo. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2009

    mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. huyu mama ni mchapakazi. She's probably the most effective and hardworking first lady our country has ever had.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2009

    First Lady funika bovu. Kiboko cha vyote. Wizara za Elimu, Kazi na Mendeleo ya Vijana, Wanawake, Jinsia na Maendeleo ya Watoto, UWT, BAWATA, TAMWA kafunika First Lady. WAMA Oyeeeee!!!!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2009

    Mama anajituma kuhamasisha maendeleo kuliko mawaziri kibao. Kama wewe ni mmoja wa mawaziri hili ni jambo la aibu.

    ReplyDelete
  4. mzee wa bunjuJuly 22, 2009

    OOps!!!! nilitaka kusema mama anamfunika baba, maana mama amejipanga kikweli kweli, hana mbwembwe ila action ndo zinaonekana

    Mungu akubariki mama yetu

    Mzee wa Bunju

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 23, 2009

    keep it up mama salma!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...