JK akimkaribisha Ikulu Mkuu wa Majeshi ya Afrika ya kusini Jenerali Godfrey Ngwenya wakati yeye na ujumbe wake walipomtembelea ikulu jijini Dar leo
JK akipokea zawadi kutoka kwa mkuu wa Majeshi ya Afrika ya Kusini jenerali Godfrey Ngwenya wakati alipomtembelea ikulu jijini Dar leo.Klia ni mkuu wa Majeshi ya Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange.

JK akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa majeshi ya Afrika ya kusini Jenerali Godfrey Ngwenya(kushoto), Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange(kulia) pamoja na maafisa waandamizi wa majeshi ya Afrika ya kusini na Tanzania ikulu jijini Dar


JENERALI NGWENYA AISHUKURU TZ
Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Afrika Kusini (SANDF), Jenerali Godfrey Ngwenya ameishukuru Tanzania kwa mchango wake mkubwa katika ukombozi wa Bara la Afrika.

“Tanzania ilitoa mchango mkubwa siyo tu katika ukombozi wa Afrika Kusini, bali katika kulikomboa Bara la Afrika,” Jenerali Ngwenya amemwambia Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Jenerali Ngwenya ametoa shukurani hizo kwa Tanzania wakati yeye na ujumbe wake ulipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Kikwete, leo, Jumanne, Julai 14, 2009, Ikulu, Dar es Salaam.

Jenerali Ngwenya amemwambia Rais Kikwete jinsi Afrika Kusini inavyothamini mchango wa Tanzania katika ukombozi wa Afrika Kusini na nchi nyingine hasa zile za Kusini mwa Afrika.

“Tunapokuja Tanzania, kwa kweli tunarudi nyumbani. Tumeishi hapa, mlituhifadhi sote hapa iwe ni ANC, PAC, Frelimo, ZAPU, ZANU…kila mtu alikuwa hapa,” amesema Jenerali Ngwenya na kuongeza:

“Tunashukuru na kutathmini mchango wa Tanzania katika kutuwezesha kufikia malengo yetu,” amesema Jenerali Ngwenya katika mazungumzo hayo yaliyohudhuriwa pia na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange.

Naye Rais Kikwete amemweleza Jenerali Ngwenya kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali kuhifadhi historia ya ukombozi na vyama vya ukombozi kama ilivyotokea katika Tanzania.

“Shughuli zote za vyama vya ukombozi Kusini mwa Afrika zilianzia pale Kongwa, kabla ya kusambaa katika maeneo mengine ya nchi yetu…hii ni historia ya heshima sana katika nchi na bara letu…hivyo tutahakikisha kuwa tunaihifadhi historia hiyo,” amesema Rais Kikwete.

Ameongeza kuwa kama inawezekana vyama vilivyopigania uhuru kutokea Tanzania na Serikali ya Tanzania vinaweza kwa pamoja kuanzisha aina ya taasisi ya elimu ambayo itaendeleza historia hiyo yenye heshima kubwa.

Jenerali Ngwenya na ujumbe wake aliwasili nchini jana, Jumatatu, Julai 13, 2009, kwa mwaliko wa Jenerali Mwamunyange kwa ziara ambako atatembelea maeneo mbalimbali yanayohusiana na historia ya ukombozi na yanayohusu uhusiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini katika nyanja ya ulinzi na usalama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 14, 2009

    Afande wetu anaonekana yuko fiti fizikale. Huyo wa bondeni mmh... Mambo ya vita za tekenolojia yamebadili kabisa mahitaji ya kuwa na msuli

    ReplyDelete
  2. Duu!! angslia jamaa walivyoshiba.. wanajeshi wa sauzi .. hii nni kuonyesha kwamba hawana uzoefu wowote wa kijeshi zaidi ya kukaa pale Dakawa Moro kama freedom fighters kisha waliporudi nyumbani wakapachikwa hizo nafasi ..ndio maana nchi inakwenda mrama sasa . wangiwaachia wazungu nao waendelee kushika nafasi nyeti..

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 14, 2009

    Michu!Yule jamaa mwene nguo za kijeshi anaekuwaga mgongoni kwa JK kila anakoenda vipi?leo hayupo hapo?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 14, 2009

    Duu! Taabu hii huyu mkuu wa majezshi sauzi hata koti halimtoshi,tunasema bongo epa wameshimiri kumbe huko sauzi ndo kibao mpaka kwenye nyazifa za serkali.Nimefurahia kumuona huyo mkuu wa majeshi yetu akiwa fiti na anaokana hajaanza kuzulumu walipa kodi na walala hoi.
    Wasukuma mpo jamani! Sisi ndiyo waamuzi kwenye nchi yetu na ninajiandaa kuja kugombea ubunge hapo jimbo la Nyamagana au Ilemela hivyo Masha na Diallo wajiandae na wakae chonjo gambishi siogopi kwani mie ni mzaliwa wa hapo hapo. Usukumani tunasema tukwibona bageshi tondo!!!!.
    Wabeja bageshi Michuzi!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 14, 2009

    JAMANI ACHENI MANENO..UNENE MWINGINE WA KUZALIWA BWANA..KWAI MBONA HAO WENGINE SIO WANENE..ACHENI HIZO BWANA

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 15, 2009

    Namuunga mkono mmoja wa watoa maoni hapo juu kuwa si kila mtu mnene basi ndio lelemama,hapana, kuna unene mwingine ni asili ya kifamilia hata ukijifua vipi, ndio kwanza unazidi kunenepa.
    Inawezakana kabisa huyo ndugu yupo fiti kuliko hata hao wembamba.
    Tuache mawazo kuwa unene ni ufisadi hayo ni mawazo mgando kabisa.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 15, 2009

    Inashangaza mkuu huyu wa majeshi kuisifia Tanzania bila kumtaja Marehemu Baba wa taifa Mwl J K Nyerere kwani ndie alikuwa kinara wa ukombozi kusini mwa Africa na sio mtu mwingine yeyote.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 15, 2009

    Mataifa yaliyoanzisha vyuo vya kijeshi miaka mingi iliyopita kama Marekani, United kingdom, France, Russia,Germany,Japan n.k pamoja na taifa changa kama Tanzania, huwezi kumkuta jenerali wa ngazi ya juu akiwa na kitambi cha kupitiliza, sana sana anakuwa pandikizi la mtu.

    Kuna haja SANDF kuleta vijana wapitie Monduli.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 15, 2009

    Aro hapo juu kumbe hamjuagi ga mutu ka sauzi wana gamwili kakubwa kweli mij dada tako tako mi baba miili hio na kuwaga na limwili sio kutokuaga fisikali hey weye usipimage yako fisikali fiti hayo noma poleni kajamaa

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 15, 2009

    jicho la mwamunyange tu basi...

    baba anatishaaa uyu!ilo jicho balaa

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 15, 2009

    hao wanaowachake wanajeshi wa sauzi wanaishi dunia gani? mumewaona wanjeshi na polisi wetu mitaani? tele wana vitambi maji, isitoshe wengine wana buti mbovu kiasi unajiuliza hawa kweli pakitokea tifu hapa wanafukuza mtu namna gani? polisi wetu tele hawana stamina kabisa!!!! wacheni tabia za nyani!!!!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 15, 2009

    Jicho la kamanda wetu, weeee!!! la asili mwanangu is so hot. kamanda kama ana mabinti na wakalipata hilo. watakua warembo wa asilia.wangu.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 15, 2009

    annonymous Wed Jul 15, 04:56:00 PM with tha kind of comment i hope you are a woman!!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 16, 2009

    ANATUSHUKURU NINI WAKATI SASA HAWATUTAKI HUKO WANATUCHOMA MOTO NA KUTUFUKUZWA WAKATI WA SHIDA ZAO WALIKUWA HAPA KWETU KIBAO WAKITUOLEA DADA ZETU HAPO MOROGORO NA IRINGA, WANA ROHO MBAYA SANA.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 16, 2009

    Yule askari wa kikwete kila siku leo yuko kwa ndani ya ikulu maana hao waliopiga picha wamemtuma maji ya kunywa

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 16, 2009

    Cheo cha askari wa kikwete kwa leo ni sawa na askri wa jiji ndo maana haumuoni kwenye picha ya majenerali. anaogopa kutwanga Gwalide na saluti kwa hao wote

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 16, 2009

    Nyie wadau mnauliza askari anae kaaga nyuma ya kikwete yuko wapi? Jibu Yuko na Membe EGPTY wanamwakilisha JK, Michuzi embu watumie Picha ya Membe akiwa Egpty na yule askari yuko nyuma yake.
    Mzee wa kibondo

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 16, 2009

    Ndugu Anonymous wa 03:23 kwani wao kutuolea dada zetu kuna ubaya gani? Umenyimwa nawe kuwaoa dada zao? Suala la wasauzi kuwapiga na kuwachoma waafrika wenzao halihusiani na huyu Generali kuishukuru Tanzania kwa msaada iliyoutoa kufanikisha ukombozi kusini mwa Afrika. Cha msingi alitakiwa kukumbushwa kuwa wawafundishe kizazi cha sasa (wale wanaowachoma moto wengine-kwani hawajui) kuwa nchi yao ilisaidiwa na nchi nyingine za Afrika (hasa Tanzania) ili kuondokana na ubaguzi wa rangi. Kuhifadhi historia ya ukombozi kusini mwa Afrika ni hatua mojawapo, nyingine na bora zaidi ni kukubaliana kuwa nchi hizo ziwafundishe vizazi vya sasa na vijavyo historia za ukombozi na misaada waliyoipata kutoka nchi jirani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...