afande wa FFU akiwa na guruneti moja ambalo halikulipuka katika uporaji wa benki ya NMB tawi la Chang'ombe huko Temeke leo.
damu ya wafanyakazi wa katika kaunta ya benki ya NMB tawi la Temeke ambapo majambazi yapatayo saba hivi yalivamia kwa mabomu ya mkono ambapo baada ya kurusha mawili nje na kuua mlinzi wa kampuni binafsi aliyekuwa getini, yakarusha risasi ndani na kujeruhi watu 13, ikiwa ni pamoja na askari polisi wawili na kukomba takriban shilingi milioni 150 kabla ya kutoroka. Walitoroka na Escudo na Prado zilizokuwa na namba za 'SU' na 'STJ'

Hii si mara ya kwanza kutokea uporaji wa aina hii na umekuja siku moja tu baada ya Kamanda wa kanda maalumu ya Dar Afande Selemani Kova kutoa tahadhari kwamba taarifa za kiintelegensia zao zinaonesha kuna kundi la majambazi yenye silaha kali linataka kufanya uhalifu jijini.Tukio kama hilo lilipata kuonekana benki ya za Ubungo, Mwanga na Mbeya.


Mkurugenzi wa Upeleleza wa Makosa ya Jinai afande Robert Manumba akiongea na wanahabari sehemu ya tukio. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Lawrence Masha, Mkuu wa Polisi IGP Saidi Mwema na Mkuu wa mkoa wa Dar Mh. William Lukuvi pia walikuja eneo la tukio baadaye na kutembelea majeruhi waliolazwa hospitali ya Temeke iliyo jirani na Benki hiyo.



Msako kabambe unaohusisha hedikopta, magari, farasi, mbwa na askari wa miguu umeanza toka asubuhi na mapema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 47 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 31, 2009

    POLENI NA MSUKOSUKO HUO.. DUH KWELI BONGO TAMBARARE.. LAKINI HAO HAWAFIKI MBALI WATATIWA MIKONONI.. UJAMBAZI HADI KWA MABOMU NI HATARI KWA KWELI, ISIJE IKAWA MABOMU WALIYAIBA MBAGALA..

    MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 31, 2009

    inatisha, keleuuwiiii

    ReplyDelete
  3. hivi wtz tuko vipi mpaka hao watu wanafikia atua hiyo kwa vyovyote vile kuna mabosi ambao ni wtz wa hapa ila inauma sana kuwaona watu hawana huuna na binadamu wenzao wapi tunaenda.kwanini watani wafanye haya mambo nchini mwetu inatia hasira mimi nimwona mkenya lazima nimpe bisibisi kwanini wasianzie kcb ya kwao.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 31, 2009

    Pole mtanzania,poleni wafiwa.

    ...Hii ni 'wake up call'.Kama ni mtu wa kufuatilia matukio ya uhalifu vizuri na kufahamu pattern ya uhalifu ulivyokuwa unaripotiwa huwezi kushangaa kwa tukio kama hili kutokea.

    Natarajia mengi zaidi ya hilo kwasababu vyombo vyetu vya usalama vimo katika karne ya mazoea.Wahalifu wamebadilisha mbinu,lakini watu wetu wa ulinzi bado wanatumia mbinu zisizoweza kupambana au kushindana na majambazi.Uwezo wa kufikiri wa watu wa ulinzi ni mdogo sana sana sana kuliko wakati wote.

    Wake up call ilikuja kuanzia tukio la mabomu la Dar (ubalozi marekani),tukio la kupigwa raisi mwinyi tukio la kuawawa askari na majambazi kitu ambacho kilikuwa si cha kawaida katika nchi na jingine ni tukio la Arusha ambako yalipatikana mabomu kama hayo yaliyotumika hapo Dar.Kwahiyo unaweza kuona kwa mbali mabadiliko ya zana za ujambaziyalianza kitambo yakionyesha ishara kamili lakini watu wa ulinzi wapo tu. .

    Katika ulinzi tunahiji 'to think out side the box'.Polisi wafikiri zaidi kuliko ya ulinzi mazoea.Siku zote watu pia hawako `alert` na mambo ya usalama au nini kinatokea katika mazingira yao.

    Moja ya mazingira yanatia shaka katika ulinzi hebu angalia hata katika picha hii huwezi kuanza kushika vielezlezo vya mabomu kwa mkono kuna mengi yanaweza kufanyika hapo.hii tu ni ishara ya kuonyesha hatuji tunachokifanya katika shughuli za ulinzi.

    Majambazi wamekuwa na inteeligence kuliko police maana wanajua ni wakati wapige,wanajua kabisa polisi hawako alert au namna gani.Jamani!

    Tunahitaji asakari wetu wafahamu mambo mengi kuhusu ulinzi,wananchi nao watoe taarifa maana watakuwa walikuwa wanajua mambo kama hayo.

    Nitakuwa nikifutilia tukio hili kwa karibu zaidi ili kufahamu namna amabvyo benki ilivamiwa

    ReplyDelete
  5. hivi wtz tuko vipi mpaka hao watu wanafikia atua hiyo kwa vyovyote vile kuna mabosi ambao ni wtz wa hapa ila inauma sana kuwaona watu hawana huuna na binadamu wenzao wapi tunaenda.kwanini watani wafanye haya mambo nchini mwetu inatia hasira mimi nimwona mkenya lazima nimpe bisibisi kwanini wasianzie kcb ya kwao.

    ReplyDelete
  6. Pole wafiwa, ugua pole majeruhi, naungana na wote walioathirika kwa namna mmoja au nyingine.
    Hii Ni vita kama vita zingine, serikali na vyombo ya dola vijipange sawa, kuanzia tule tuvibaka tunatonyakua simu za watu ndio tunabadirika kuwa majambazi sugu ya siraha kali. Hii Ni vita tumia chochote kinachoweza wawekeni watu wenu salama.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 31, 2009

    "Kushikilia bomu la mkono sio ushujaa,bali ni udhaifu nani kuharibu uhalisia wa tukio"

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 31, 2009

    makubwa!!!!!!!!iyo ni bongo!!!mbona mambo

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 31, 2009

    Hebu polisi linganisheni modus operand ya tukio la Arusha na hili ili kuweza kubaini kama kuna signature" au " calling card" ya watuhimiwa.

    Kuyalinganisha hayo matukio mawili kutatoa mwanya wa kusogeza upelelezi mbele na pia kutasidia kujua ni watu gani wamehusika katika tukio hili na hayo mabomu yametoka wapi.

    Nitachangia maoni ya kitaaluma kadri mambo yanavyokuwa yanakwenda

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 31, 2009

    naelewa kwanini mlinzi kafa. manake angepona, basi polisi wangembinya sehemu zote ili kuficha wahalifu. michuzi baba, nitawasiliana nawe ili nitoe ubani wangu kwa familia yake.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 31, 2009

    UUWIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII....?????????????????????????????

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 31, 2009

    Poleni sana wafiwa, matokeo ya mwenzio kufariki au kujeruhiwa kazini yanauma sana kweli tunakosa ubinadamu. Fikiria mtu umeachana nae asubuhi anaenda kutafuta riziki alafu mchana unapata habari hii, jamani poleni wafiwa na majeruhi inshaallah mtapona

    ReplyDelete
  13. Hali inatisha. Nawaombea ugua pole waliojeruhiwa na uvumilivu wafiwa. Tunataraji wahusika watakamatwa muda si mrefu. Hii mbaya sana hii.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 31, 2009

    Allah wahkbal......

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 31, 2009

    Hi Poleni na msiba na wizi
    mawswali:
    Was there any CCTV camera? If yes was it on?

    Has the area been condoned for forensic examination?
    Has the area and evidence not contaminated?

    What type of evidence have been collected for investigation?

    Hapa UK millions of money are used to tip up police such crime. do we have similar systemm in Tanzania?

    Kwa nini Mh. Masha usijiuzulu?
    Something is wrong somewhere!

    Hii ni dalili ya kuchoka na kukua kwa gap ya umaskini Tanzania.
    JK kaa macho!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 31, 2009

    Hawa majambazi inawezekana wamefanya ukusanayji wa habari za kupiga eneo hilo kwa muda mrefu sio kazi ya siku moja tu.Vilevile lazima kutakuwa na wafanyakazi au watu wanaofahamu ndani ya benki nini kilikukinaendelea kuhusu pesa.

    Majambazi hawawezi kupiga mahala bila kuwa kujua behaviour ya walinzi (askari/private security) na eneo zima kwa ujumla,vilevile lazima wajue watatokea wapi mambo yakisharibika na wataingilia wapi.watatumia usafiri gani.Na siku zote hawawezi kwenda kwenye tukio wote wengine watabaki maeneo mengine wakiwa wanaangalia nini kianendelea.

    Aidha naweza kusema pia wanaweza vilevile wako kundi kubwa na pia mabekni mengine nchini yawe alert maana watu awanweza kuwa na "tunnel vision" ya tukio la dar wakapiga mbeya ,Mwanza,Moshi au Arusha.Walinzi watumie tukio hili katika njia pana zaidi.au wanaweza kupiga maduka ya fedha au shopping malls.Kuweni alert.

    Naamini kwa wapelelezi wazuri na wafuatiliaji makini hawa watu hawaendi mbali,lakini kama ni upelelezi mlipuko basi itakuwa story.

    Je CCTV cameras zilikuwa katika benki hiyo ya temeke? tunaweza kuretrieve images za tukio na kusoma?

    Watu wa makampuni ya simu wanaweza kuhusishwa katika upelelezi ili kufahamu ni mawasiliano gani yalifanyika kabla ya tukio.Hawa watawasaidia katika upelelezi pia.

    Je hayo ni mabomu ya mbagala ?swali la kujiuliza katika kupeleleza.

    Na kwakuwa kulikuwa na taarifa za kiitellejensia basi naamni zitakuwa "developed" zaidi maana mtoto amekata mbeleko sasa.Waliotoa hizo habari sasa watatoa picha kamili.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 31, 2009

    INSHA ALLAH kamera zıtawafıchua 2.bası mambo yahuko kwetu unaweza kuona bank haına recorded kamera

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 31, 2009

    Fikiria hii ikitokea kwenye vituo vya uchanguzi mwaka kesho itakuwaje?

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 31, 2009

    Fikiria hii ikitokea kwenye vituo vya uchanguzi itakuwaje ?

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 31, 2009

    Poleni sana wafiwa na ugua pole waliojeruiwa. Watanzania; sasa hivi sio wakati wa kumnyooshea kidole yeyote. Niwakati sasa wa watu wenyewe kuamka na kujijua wako wapi. Ninaimani hawa wanyama sio watanzania. Sisi hatujafikia hali hii kwa sababu amani yetu tumeifanyia kazi muda mrefu.
    Tunajua wote kwamba policing system has to be updated. Immigration system has to be awake kwa sababu hawa wanyama wamefikaje hapa na kujua kutumia plate number za SU na STJ ili wasitiliwe shaka.
    Bajeti lazima iwepo kwa ajiri ya ku tip watu au polisi wanaoweza kupambana na matukio ya namna hii.
    Kikubwa watu kuweni macho. Dont wait for the police to alert u, be alert (period).
    Tukifanya hivyo, huu unyama utapungua.
    Poleni sana watanzania, tulinde amani yetu. Pamoja na hayo bado tuko-better ukilinganisha na Kenya au Nigeria kwa sababu kwao haya mambo ni vitu vya kawaida sana.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 31, 2009

    I can not insists the importance of securing our areas. Here comes one of many solutions. Some Laws should be passed and enforced that all financial institutions must have CCTV Systems installed for the sake of detering crimes as well as a way of documenting on how crimes started and a way to recognize and put to book all those envolved. Lets be real Tanzania. By the way these guys here under could be part of solutions.

    Manyase Investment Company
    I
    s the supplier of high-quality surveillance cameras, digital video recording systems (DVRs) and supplies for remote monitoring and safety. Our surveillance solutions provide complete security to both commercial and residential sectors by protecting them against theft, vandalism, and crime. Our surveillance and digital recording systems help to monitor your business and home 24X7. Our CCTV cameras are suitable for offices, schools, retail stores, hotels, restaurants, parking spaces, government buildings, banks, hospitals and more.
    Our Service, Products & Associated Costs/Price

    F
    or as little as $1500, you can buy a professional CCTV surveillance system from Manyase Investment Company, including 4 dome security cameras, a 4-channel surveillance DVR including DVR viewer software and all of the cables and connectors needed for a simple plug and play installation. These systems will record video of what is happening at your facility digitally onto the hard drive of the DVR. The DVR of this particular system comes with a 250 GB hard disk drive that is capable of storing about a week worth of video. Upgrades are available if more video storage is needed, and the surveillance video can be backed up using the built in CD burner or USB drive. This system is also networkable which means that you can access your cameras remotely over the Internet using the DVR viewer software that comes with the system.

    Manyase Investment Company is also deals with:
    Beauty supplies
    Building Hardware Supplies
    Construction design, development and management.
    Electronics office equipments and supplies (Computers, Faxes, Projectors etc).
    General Supplies
    Our Contacts
    For help with your surveillance system needs and other services please call us @ +255754433389 or +255715433389 or write to Kasulwa@live.c

    ReplyDelete
  22. AS IF KAMA SIKIAMI NINACHOKIUMA NA KUKISOMA!!! MWEEEEE,KWELI KWA HALI HII SAFARI BADO NI NDEFU MNO!!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 31, 2009

    Watu wengine bwana, wanaangalia CSI basi wanaona wanajua kilakitu. Sasa unamuuliza nani hayo maswali, hii ni bongo bwana, hawa wayu watapatikana bila forensic examination wala nini. Usijaribu kufananisha nchi ya dunia ya tatu na huko UK.

    Na kwanini Mh. Masha ajiuzulu? Nani alijiuzulu UK mlivyopigwa mabomu kwenye mabasi na underground zenu? Halafu kiingereza chako kibovu.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 31, 2009

    POLE NYINGI ZIENDE KWA WAFIWA,WAFANYAKAZI WA BENKI PAMOJA NA WATANZANIA KWA UJUMLA.

    Hoja yangu ni kama ifuatavyo:

    1.Ninaamini kuwa kukitokea any crime incident,the whole area inakuwa ni crime scene na hivyo basi chochote kinachokutwa hapo kina-qualify kuwa evidence.Sasa swali linakuja,huyo FFU pamoja na kuwa anaonekana ni mwenye ka-cheo,hajui kuwa anaharibu hiyo evidence aliyoishika?Au anadhani yeye no shujaa kwa kuwa ameshika bomu kinamna hiyo?Vitu vingi vinaweza kupatikana kwenye hilo bomu aliloshika - Fingerprints,material for DNA na kadhalika.Forensic experts wa Polisi wapo wapi?Ni kosa sana ku-temper na vitu kama hivi.Hata kama hatuna database ya kuhifadhi kumbukumbu kama hizi,leo tunaweza takaweka kumbukumbu hizi kwa rekodi za wakati ujao.Tuangalie mbeleni jamani.Tungeweza kufananisha alama za vidole kwa matukio yaliyokwishatokea hapo awali na hili.Tungeweza kujua pia makadirio ya umri wa watu waliohusika.

    2.Kinachosikitisha ni utayari wa askari polisi.Kwa nchi za wenzetu,tahadhari ikishatolewa na Mkuu wa Kipolisi iwe ni wa Kanda au wa Nchi,Mkuu anayesimamia operesheni za ulinzi kwenye taasisi za fedha angetakiwa aimarishe doria kwenye sehemu zote hizi ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya polisi au makachero ambao sio lazima wawe wamevaa magwanda.Tumeshuhudia kuwa baada ya kuona kuwa taarifa za kipelelezi zimewashtukia,majambazi hayo yakaamua kuwa hatua nyingi mbele ya Polisi na kuvamia kabla hata Polisi hawajajipanga.

    3.Utayari wa Wafanyakazi pamoja na uadilifu:
    Ni kweli kuwa katika benki zetu nyingi tu hapo Tanzania,kama sio zote,wafanyakazi hawajapewa mafunzo yoyote ya utayari na hakuna semina zenye kuwafundisha wafanyakazi utayari wakati wa matukio kama haya.Mimi nilifanya kazi kwenye mojawapo ya benki hapo nchini kwa muda takribani miaka minne na hakuna hata siku moja kulikuwa na mafunzo ya aina yeyote kuhusu haya mambo zaidi ya wakati wa mafunzo ya ndani kuelezwa ukiona tatizo bonyeza kitufe cha alarm.Hii haisaidii bado.Benki nyingi zinaogopa kutumia fedha kuwafundisha wafanyakazi wake mbinu za kujihami yakitokea mambo kama haya.Pengine maisha ya wafanyakazi yangeweza kuokolewa,nani ambaye anajua?PIA suala lingine ni wafanyakazi kutokuwa waaminifu.Wengi tumeshuhudia wafanyakazi wengi wa taasisi za fedha wakijihusisha na mitandao ya ujambazi na hatimaye mambo yakitokea wanakuwa hatiani.Mojawapo ya kigezo cha kuwa mfanyakazi wa benki ni uaminifu wa hali ya juu.Kwa maisha ya Kitanzania kufanya kazi na pesa kama milioni 300 zipo pembeni,shetani anaweza kukuingilia wakati wowote,hivyo uaminifu wa hali ya juu unatakiwa.Kitu kingine huwezi kutegemea pia huyo mfanyakazi awe ana-handle milioni 300 wakati mwisho wa mwezi analipwa laki 2-Unakaribisha wizi.Benki ziangalie.

    4.Wito kwa serikali:Kuna tabaka kubwa sana kati ya masikini na matajiri.Kupunguza tabaka hili kutasaidia sana kupunguza malalamiko mengi ambayo yanasababisha mambo mengi mabaya kutokea.Sidhani kama serikali inaliangalia hili kwa mtazamo wa hali ya juu.Kusema kuwa Watanzania ni wavivu(kama Waziri Kapuya alivyosema Bungeni wakati fulani)hakutasaidia kupunguza matatizo haya.Cha zaidi serikali inatakiwa kufanya ni kutimiza ahadi inazoweka na sio kuwadanganya wananchi ili wachache watimize ndoto zao na kuwa matajiri tena sana na wengine kuzidi kudidimia kwenye umasikini.Damu za Watanzania zinamwagika sana wakijaribu kutetea kitu ambacho hawakijui au wanakijua lakini hawakifaidi.
    Udhibiti wa mipaka yetu.Ni vizuri sasa kukawa na strict rules za kuwabana watu wanoingia nchini.Lazima Serikali ijue ni nani ameingia nchini na anafanya shughuli gani.
    Ombi langu ni kwa serikali kuwa makini na utendaji wake.Kuwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki sio sababu ya kutoilinda nchi yetu.Tumezungukwa na watu wengi wenye tamaa na utulivu pamoja na mali za nchi yetu.Ni ukweli kuwa watu hawa hawaji nchini kutuchekea au kuindeleza nchi BALI kuiharibu halafu watuachie Somalia nyingine ambayo haina sheria wala serikali inayoeleweka.Sasa serikali inataka watu wajilinde wenyewe?Kutakuwa na maana gani ya kuwa na dola?

    Asanteni sana.

    Mdau,Oxford.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 31, 2009

    m nimesikitika tu kuuwa watu na kujeruhi watu wasio na hatia,lkn kiukweli maisha ni magumu sana na serikali haifanyi jitihada zozote.ndomana watu wanakuwa na roho ngumu kiasi hicho.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 31, 2009

    poleni wafiwa na majeruhi mola awajalie mpate nafuu mapema,inasikitisha sana sana binadamu tumekuwa wanyama mno,kweli inasikitisha,jamani watanzania huwa tunalinda nini mpaka watu wanapiga mabomu,wanaiba wanaondoka na magari,sie vikosi vyetu bado havijafika??????? jamani hii sasa inatisha,tusipobadili system nzima ya ulinzi tutegemee haya kila kukicha maana hayajaanza leo,kweli inatia uchungu.mungu tuongoze.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 31, 2009

    Michuzi usiibane. Mimi naona haya mambo yanatokea na yatazidi kutokea sana kwani hapa tz mambo yametaiti. Kama huna mtu unayemjua hata kama umesoma utabaki unasaga viatu na watoto wa wakubwa wanakutimulia vumbi. Naona ni wake up call kweli wakishindwa kwenye taasisi za fedha wataanza kuwafuata wanaoita billion senti.
    Pole Wafiwa.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 31, 2009

    Kwa Kweli inashangaza saana jinsi polisi inavyofanya kazi, wanakua mbele na defender zao kufuatilia na kupeleleza wapi mzigo wa mfanyabiashara utashuka ili wakachukua pesa badala ya kupeleleza na kuwa karibu na wananchi ambao wameshakata tamaa na polisi kwa sasa ili waweze kupata taarifa za ujambazi na wanaohusika na ujambazi kataika jiji la Dar es Salaam na kwengine TZ kwa sasa.Itabidi jeshi la polisi lifanye kazi kwa manufaa ya umma na siyo yao binafsi. Tigo na madefender yasiyo kama njia ya kujipatia mapato badala ya kufanya kazi walizoajiriwa kufanya.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 31, 2009

    je ni bank ngapi hapo dar na tanzania kwa ujumla zina madirisha na milango ambayo ni bullet proof kuzuia access ya wateja kwenda counters kirahisi kama ilivyo kwenye banks nyingi za europe...mfano halisi ni balozi za UK na USA Tanzania!

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 31, 2009

    BRO MICHUZI HII YA MAJAMBAZI KUTINGA NA MAGARI YENYE NAMBA ZA ''SU '' NA ''STJ'', IMEKAAKAAJE HII?? YANI WAMEAMUA KUWAONYESHA SERIKALI KUWA WAO NI KIBOKO NAMNA HIYO HADI KUTUMIA MAGARI YENYE NAMBA ZA UMMA NA JESHI?? DUH HII KALI

    ReplyDelete
  31. Hali inatisha. Nawaombea ugua pole waliojeruhiwa na uvumilivu wafiwa. Tunataraji wahusika watakamatwa muda si mrefu. Hii mbaya sana hii.

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 31, 2009

    AAH ACHENI TUU NISEME UKWELI WA MOYONI MWANGU. KAMA KWELI WAMEONDOKA NA NA MILIONI 150. BASI HAPO SI DHANI KAMA ATAKAMATWA MTU. POLENI SANA NDUGU WAFIWA NA MLIOJERUHIWA UGUENI POLE.

    ReplyDelete
  33. AnonymousJuly 31, 2009

    Poleni wote yaliyowakuta,mi pia nimeiona kwenye Local TV News,inasikitisha kwa viongozi wetu wa kisiasa na usalama maana hawajui kuongea na vyombo vya habari,yaani wanahitaji semina endelevu ya nini cha kuongea..Achilia mbali uharibifu wa ushahidi wa wazi wa askali polisi ulionekana,mimi na_deal na hawa icons wa taifa letu,mfano pale mkuu wa mkoa anatoa kadilio la fedha zilizoibiwa,wapi na wapi maana inatakiwa kutolewa na bank yenyewe si inawasemaji wake!?

    Tujifunze jinsi ya kuzungumza na media wakuu wetu,hii ni mfano tu ila mengi yanaonekana,wewe angalia tu local tv,aibu!!

    -Mdau (The Dreamer)

    ReplyDelete
  34. MDAU READINGJuly 31, 2009

    WENGINE TUNASHAMBULIWA NA WAVUTA BANGE TURUDI MAKWETU KUNA KAZI KEM KEM MABENKI? WACHA TUZITAFUTE HIZI KAZI HUKU HUKU UK, NYUMBANI KWELI TAMBARARE AIBU AIBU TUPU. MILIONI 150 MPAKA MTUMIE MABOMU KUZIPATA NAONA AIBU SANA KWA NINI WASITAPERI KAMA WENGINE KULIKO KULIPUA WATU NA MABOMU?

    ReplyDelete
  35. So RPC knew this halafu akaacha watu wanaumia na hata kufa,kweli bongo tambarare

    ReplyDelete
  36. Kwa mtazamo wangu RPC must be taken into account. Huyu mtu alijua kuhusu hili tukio, na alitoa taarifa za kuingia watu wanaopanga kufanya uhalifu, je alichukua hatua gani? kutoa taarifa tu kwenye vyombo vya habari inasaidia kuzuia uhalifu? Ni muhimu kwanza kupitia hatua za kiusalama alizochukua, mana mpaka anasema kuna kundi limeingia nchini (Dar) ni lazima atakuwa anawajua kwa majina, sura, mahali walipo, na wenyeji wao pia....hawezi kutoa taarifa bila kuwa na vizibitisho.....ndio maana naona kwanza afanyiwe uchunguzi mana ataweza kusaidia sana kwenye hili.....

    Hii inaonyesha ni jinsi gani vyombo vyetu vya usalama haviko makini....kwa kweli tunahitaji kujenga upya jeshi letu la police....na ipite sheria kila jengo kubwa, petro stations, mipakani na kwenye junctions kuwa na CCTV, hii itaweza kusaidia identification za wahalifu...

    ReplyDelete
  37. HII NI AIBU YA MWAKA KWA NCHI KAMA TANZANIA,KITUO CHA POLISI CHANG'OMBE KIPO KAMA MITA 500-600 HIVI TOKA TUKIO LILIPOTOKEA LAKINI KWA KWELI HAKUNA TAHADHALI YA HARAKA ILIYOCHUKULIWA,HATA KAMA NI DAKIKA KUMI WANGEWEZA HATA KUZUIA AU KUFUNGA BARABARA ZOTE WACHA TANZANIA IENDELEE KUIBIWA WANANCHI WATAENDELEA KUKOSA IMANI NA VYOMBO VYAO VYA ULINZI,HAKUNA JIPYA HAPA SUBIRINI WALIPOANZA CRDB ILIKUWA HIVIHIVI MWISHO IKAENEA KWENYE MABENKI MENGINE,HIZO YAELEKEA NI SALAMU TU

    ReplyDelete
  38. Napenda kuchukua nafasi hii kuawaonya watanzania wenzangu kuwa popote pale tukio la namna hiyo linapotokea ni vyema kutokusogea katika eneo hilo maana majambazi hutega vitu vingi mabomu mengine yamekusudiwa kuwaua wanaokimbia kwenda katika tukio.wapeni vyombo vya usalama nafasi kufika pale kwanza maana wao pengine wanajua nini cha kufanya.

    Mtanzania Afghastan/Pakstan Border.

    ReplyDelete
  39. inasisimua sana majambazi mnaingia na style ya holywood ni balaa enyi majambazi na hakika mnasoma blogu ya nanihii ebu kuweni na huruma mna watungua wenzenu na mabomu mmekuwa magaidi nyinyi kama mlitaka kuiba si mngeenda kimyakimya kama pale crdb? sasa mmeshafanya watu wajane au hata mayatima halafu hizo hela mnaenda kutumbua na familia zenu wallah mungu awapige radi damu ya mtu haimwajiki bure mtapatikana tu tuone kama mtajenga kempiski lol!!!
    mdau CANADA

    ReplyDelete
  40. kosa kubwa kama hilo ambalo limewakost raia maisha na imani na jeshi la polisi huwa halina msamaha.
    maafande wote wenye busara HUJIUZURU.

    ReplyDelete
  41. HALAFU NINYI MAJAMBAZI MNAONEKANA SIYO PROFESHENO KWANI HAMKUITAJI KUTUMIA MABOMU HASA SEHEMU AMBAYO KUNA RAIA. ONA SASA MMEUA MMEJERUHI JUST BECAUSE HAMTUMII AKILI MNAPOKWENDA KUIBA.
    PROFESHENO BANK ROBBERS DONT KILL PEOPLE. SO PLEASE NEXT TIME TRY TO BE MORE PRO.
    BANK ROBBER PRO

    ReplyDelete
  42. KWA KIFUPI POLISI SS HIVI LAZIMA WAKUBALI KAZI IMEANZA KUWALEMEA,WAJIPANGE UPYA/KIJICHI WANAISHI MAPOLISI WENGI,LKN WAYA ZA TANESCO MPK NGUZO NA MAJUMBANI WATU KILA SIKU WATU VANAMIWA OVYO,SS HUYU KOVA NAYE AANGALIE...!HII SIYO SAWA,INA MAADORIA NI FEKI

    ReplyDelete
  43. RUSHWA
    Nchi iliyooza kwa rushwa unaweza kwenda jeshini ukaazime kifaru ukafanyie ujambazi na ukapewa.
    Mabomu, uniforms, SMGZ, grunediz zote zinatolewa kwa pesa ndogo sana.
    Na maafisa wakubwa sana serikalini na kwenye majeshi wanajua na ndio wanaotoa taarifa kuna shs ngapi leo ili zipolwe
    List ya majambazi wote iko hapa kwa IGP na hata waliofanya tukio wanajulikana kwa majina-Rushwa inatufunga midomo na hakuna wa kuchukua hatua kuanzia raisi hadi mgambo.
    Tunakaribia utawala wa kijeshi ili nasisi tutanue nje kama warundi na wanyarwanda na wasomali
    Cant wait for hiyo siku ili tuondokane na ujinga

    ReplyDelete
  44. inasikitisha kuona polisi mwenye cheo kikubwa anadiriki kuharibu kielelezo muhimu katika kesi hii.ni kweli amepita chuoni nakufuzu kuwa askari au ni kujuana na hivyo kupewa madaraka ya kuongoza bila kuwa na sifa?endapo watuhumiwa watapatikana,kuunganisha kesi ili kupata ushahidi wakuwatia hatiani utakuwa na mapungufu.
    polisi sasa waache kufanyakazi kwa mazoea,utalaamu zaidi utumike kukabiliana na changamoto kama hizi.
    matukio ya arusha,mwanga kilimanjaro,misungwi mwanza namengine ambayo polisi wanakumbukumbu na yanafanana na hili la temeke,ni wazi kuwa watuhumiwa watakuwa walewale kwa sababu ya namna kosa walivyotenda.karibu matukio yote silaha zinafanana yaani mabomu na silaha kubwa.
    kitengo cha upelelezi kinatakiwa kipewe elimu zaidi na wakumbuke kushirikiana na idara nyingine mfano walaamu kwa kuchora ramani,mkemia wa serikali,mtalaamu wa fingerprints,barristres,walaamu wa mabomu.kitendo cha polisi kushika bomu na kulionyesha wakiwa bado kwenye tukio ni uzembe,kwani mlipuaji angeweza kutumia remote control au kulipiga kwa bunduki toka mbali madhara makubwa zaidi yangetokea kwa kutpoteza nguvu kazi kubwa iliyokuwepo hapo.any way nitachangi zaidi baadaye.

    ReplyDelete
  45. 1-MOJA.
    Mhaishimiwa Masha na mwenzio Kova mjiuzulu.
    2-Mbili.
    Wewe uliyeshika hilo bomu ambalo halikulipuka [aren't you contaminating evidence,au ndo ushachukua finger prints?]
    3-Tatu.
    Benki inayoweza kushikilia pesa za watu saba kuja na Grenades,haiwezi kuafford CCTV?au ndo mnataka kucollect INSURANCE serikalini?maana yake i am sure hizo pesa ziko INSURED.
    4-Nne.
    It's easy to tell,that was a SETUP,hiyo ni inside job.
    5-Tano.
    Nimenotice majambawazi bongo wameanza kuwa very BOLD,wameanza kugain confidence kwamba bado kuna LOOPHOLES in our security system.
    ......unaona watu walivyo business minded,hapo juu mdau wa Manyase,amechukua fursa hii kuadvertise biashara yao...hiyo kali!

    ReplyDelete
  46. Hawa polisi wetu tatizo hamna shule

    ReplyDelete
  47. Kwa wanasheria wajanja tayari wameshaona udhaifu wa ushahidi tokana na tukio lilivyoshughulikiwa.
    Polisi wakumbuke yote ambayo wamaeyafanya hapo huenda yakawaathiri katika ushahidi mahakamni.Mahakama haitasikia kelele za huruma isipokuwa ushahidi ulio makini na uliokusanywa kwa taratibu zilizopo.

    Mhakamani hakuna ushujaa nilishika bomu namna hii au vile bali ulikuta nini na kinamuunganishaje mtuhumiwa na kosa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...