HONGERA SANA MKUU WA NANILIIIIIII KWA KULIENDELEZA LIBENEKE LA KIKWELIKWELI.
NADHANI HII MADA YANGU IMEKUJA MUDA MUAFAKA KWANI NAONA KAMA NAHITAJI MSAADA WA WADAUZZZ.
NI KWAMBA KWA SASA NAMILIKI VEHICLE (PIKIPIKI-AVENGER CRUZ). HII PIKIPIKI NIMEINUNUA MPYA KAMA MIEZI 8 ILIYOPITA HAPA INDIA. NI PIKIPIKI NZURI, POWERFULL NA KIKUBWA ZAIDI INA MILLAGE KUBWA(LITA MOJA NI KAMA INAENDA KILOMETA 60 HIVI-NI NZURI KWA MAZINGIRA YA TZ).
KWAHIYO NILIKUWA NAFIKIRIA KUIVUKISHA MAJI MPAKA BONGO MWEZI DECEMBA.SASA KUTOKANA NA KUSOMA THREADS NYINGI HAPA KUSUHU UFIRAUNI NA UFISADI UNAOFANYIKA KWENYE BANDARI YA SALAMA NA KWINGINEKO,NIMESHIKWA NA WOGA,(HADI NAFIKIRIA NIIUZE TU).
SASA MASWALI YANGU NI HAYA...
1. KWA VEHICLE KAMA VILE PIKIPIKI, VIPI WALE JAMAA WA PALE BANDARINI DAR WANAWEZA WAKANIZINGUA,AU KWA VILE NI PIKIPIKI WANAWEZA WAKAWA FAIR? (KWA VILE WENGI NAONA WAKIZUNGUMIZIA MAGARI)
2.WENGI WALIKUWA WANAPENDEKEZA KUTUMIA BANDARI YA MOMBASA,SASA KWA KUFIKIRIA HILO,UTARATIBU WA PALE MOMBASA UPO VIPI,KWA MANTIKI KWAMBA KUTOKA PALE MOMBASA MPAKA IFIKE NINAPOISHI(MTWARA-SOUTHERN TZ) ITAKUAJE? INABIDI NIKIFIKA PALE DAR,NIANZE TENA PROCESS ZA KUTAFUTA VISA NA KWENDA KENYA,HALAFU NIANZE MISHEMISHE TENA ZA JINSI GANI NIIINGIZE BONGO(HII NAONA KAMA NI COMPLICATION ZAIDI KWANI MIZUNGUKO YOTE NA KUISAFIRISHA TENA TOKA MOMBASA HADI MTWARA NAYO NI HEAD-ACHE-KWANI ITACHUKUA MUDA NA ITAKUWA GRARAMA SAWA TU NA ILE YA KUWAHONGA WALE MAFISADI PALE BANDARI YA DAR),AU NICHUKUE NDEGE ITAYOFIKA KENYA,THEN NISHUKE KWA LABDA SIKU 2 HIVI NIKIFUATILIA MZIGO(MAY B THIS IS MORE CONVINIENT-KUMBUKA NINA MIZIGO MINGI,KWAHIYO SIKUPENDA SANA NISHUKIE KENYA)
3. KWA PALE MTWARA KUNA BANDARI,TENA KUBWA TU...SASA SINA UHAKIKA SANA KAMA NITAWEZA KUTUMIA BANDARI YA MTWARA DIRECTLY,PIKIPIKI ISISHUSHWE PALE DAR-ES-SALAAM,JE HII NAYO INAWEZEKANA??JE VIPI KUHUSU UFISADI'ZZ KULE KUSINI, SIPO AWARE SANA ,LABDA KAMA KUNA MDAU ANAWEZA KULIFAFANUA KWA HILI WADAU NAOMBA MSAADA KWA HILO..
MKUU WA NANILIIIIII
NAOMBA JINA NA MAIL ID ZITUPIE KAPUNI NITAFURAHI ZAIDI
MDAU FROM INDIA
Siri ni kupata clearing agent shapu. Ukiweza kumtumia makaratasi ya mzigo kutumwa mapema halafu akayaprosesi mzigo wako ukishuka tu melini utautia mikononi. Ili kuwa na uhakika, tenga miezi miwili kwa ajili ya makaratasi kupita kwenye mfumo. Kuna hadithi nyingi sana zinatokeaga...umeme ulikatika, jamaa alikuwa likizo nk. Mzigo wako ukizubaazubaa bandarini lazima wazee wa kazi waufanyizie!!!
ReplyDeleteMdau una siku ngapi tangu upate breakfast kwa mara ya mwisho???
ReplyDeleteHatutaki Vibajaj Bongo, hiko ki-pikipiki chako kiache huko huko kwa wahindi.
ReplyDeleteI can`t wait siku ya siku nikikutana na mzee wa PCB uso kwa uso ana maswali milioni ya kujibu ila hua hao jamaa wanakujibu kwa jazba ila nitamuuliza anyways.
ReplyDeleteKWANINI KUNA CORRUPTION?
Jamani elimu yetu Tanzania ina tatizo kubwa. Huyu bwana anaandikwa kwa lugha zote na zote anazikosea. Halafu sijui huko India anafanya nini, labda biashara, lakini ni masomo, basi kuna hatari. Inakuwaje mtu hufahamu mambo mengi kiasi hiki na wakati ni msomi? Yaani hata kufahamu kwamba Mtwara si bandari ya meli zote za mizigo za kimataifa? Jamani Wakenya wakichukua ajira zetu tusilie.
ReplyDeleteHINT: kwenda kenya huitaji viza. Utagongewa mpakani wakati unaingia.
ReplyDeletehuyu mdau naye hajatulia. sifagilii bandari yetu wala ufisadi wao, lakini huyu mdau mdau anahitaji kupepelewa. yaani anaongea kama vile.. duh anyway ndo wabongo.
ReplyDeleteacha kubwabwaja
Kama una gari au pikipiki,shushia mzigo wako Zanzibar,una uhakika angalau utaupata kwa wakati,nivutie kwa +255713238684 naweza kukusaidia mzee,Hizo gharama za Mombasa mpaka NTWARA ni bora ununue pikipiki hapahapa Bongo mzee.
ReplyDeletekama ni pikipiki unapanda nayo ndege ikizidi uzito itabebwa kama kago
ReplyDeletemdau unavituko sana maana kila lugha unaikosea kama umefanikiwa kuvuta nondo india basi elimu ya india idumu kama chama.....!
ReplyDeletewe mdau hapo juu unayedai kwamba mtwara si bandari kubwa kwa meli za mizigo nadhani upo wrong sana,huwa hapa india kuna meli nyingi zinazobeba korosho na mbao zinafika direct mtwara,kwahiyo hiyo huna jipya na haujui chochote kuhusu hilo,anyway ni mawazo ndiyo yanahitajika zaidi na sio kukandia tu...oh mara hujui lugha mara nini....nonsense,sio kila mtu ni mwandishi,ilimradi kinaeleweka,iz better..umesikia we mbeba box!!
ReplyDeleteMadau kama umetoka siku nyingi Tanzania, ulizia kwanza bei za pipiki Tz, maana wachina wamemwaga pikipiki kama baiskeli za phoenix Bongo. Kwa Tsh 1.2M unapata CC125 mpya, na imekamilishwa kodi, plate number na mafuta lita kadhaa. Kama ni Bajaji sawa, maana tokea zimekuwa taxi bila usajili zimepanda bei haswa! Tafiti, ili uone kama italipa manunuzi, usafiri, usumbufu na rushwa! Vinginevyo, piga bei uje ununue tu Bongo.
ReplyDeleteandika kihindi nitakujibu
ReplyDelete