Naomba radhi kwanza kuzungumzia jambo
lifuatalo maana hapa siyo mahala pake.

Leo 15/07/09 kati ya saa 9:30AM-11AM asubuhi niliegesha gari langu nje ya ubalozi wa marekani ambako nilikwenda kwa ajili ya Visa. Baada kutoka huko nikawasha gari langu na nikapiga U-turn kurudi mjini.

Baada ya hatua chache tu, nikasimamishwa na askari mmoja wa JWTZ ambaye alikuwa analinda Ubalozi huo. Huyo askari akaniuliza kwanini nimepiga U-turn pale karibu na ubalozi? mie nikamwambia kwasababu ninakwenda mjini. Yeye kaniambia ni kosa kupiga U-turn pale. Mie sikutaka kubishana sana hivyo tukapelekana hadi kituo cha karibu cha polisi cha Oysterbay.
Huko nilikutana na polisi mwenye Kwanja 3, yeye nikamuelezea hayo na nikamwambia kule hakuna kibao cha kusema ni marufuku kupiga U-turn? Huyo askari kaniuliza ati wewe uliona kibao kilichokuruhusu kupiga U-turn pale? Nilishangazwa sana na swali la mkuu huyo na sikuwa na jibu lolote, Hivyo nikakubali kosa langu na niliandikiwa notification namba 1/82810 ambayo nililipa faini ya Shs 20,000 na kupewa risiti namba 35331902.
Swala ninalojiuliza mpaka sasa, Je hilo Kosa na faini niliyolipa lilikuwa la haki?

Maana ya kuandika barua hii ni kuwatahadharisha wengine ili wawe makini wanapoenda Ubalozini.
Ahsante,

Alihusein Mohamedali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 54 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 16, 2009

    kwenye barabara huruhusiwa kupiga U-turn unless ni kwenye intersection yenye traffic light na U-turn sign upo. Next time try a 3 point turn instead

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 16, 2009

    Sikubaliani na mdau wa kwanza, 3 point turn ni kwa barabara ndogo, lakini kwa barabara ambayo ni kubwa na gari inaruhusu ninapiga u-turn kama kawaida.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 16, 2009

    Hamkuelewana Lugha na afande!!!!
    Kaacha Lindo kukupeleka kituoni!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 16, 2009

    acha kulalamika yakhe...kwenu rushwa ndipo kilizaliwa!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 16, 2009

    Kwa suala la faini buku 20 ndio yenyewe kwa makosa ya trafiki.
    Japo sio mwanasheria lakini kitu ambacho hakijakatazwa kimeruhusiwa. Ndi omaana mtu akifanya jambo ambalo linaonekana kama ni kosa lakini hakuna sheria ya kumshitaki basi hahesabiki kama ametenda kosa. Jamii inaweza kutunga sheria mpya kwa ajili ya kuiongoza kwa siku zijazo. Kwa hiyo swali la sajini kwamba umeona alama ya kukuruhusu kupiga U-turn lilikuwa la kipumbavu. Hata swali la kwa nini umepiga u-turn karibu na ubalozi nalo ni la kipumbavu. Ile barabara inamilikiwa na Tanzania na hivyo kuongozwa na sheria za Jamhuri ya Muungano Tanzania.
    Asante kwa kutuhabarisha yaliyokusibu. Nami nitaenda hapo na kupiga u-turn halafu nimuone huyo askari atakayeniuliza maswali utafikiri nipo ughaibuni. Patakuwa hapatoshi. Hii nchi si ni yetu bado, au?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 16, 2009

    huyo askari aliwezaje kuondoka lindoni na wewe?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 16, 2009

    Agreed but how come JWTZ akawa trafic??

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 16, 2009

    Nijuwavyo mimi U-turn mahala popote duniani kama inakatazwa mahala fulani kutakuwa na alama inayoonyesha kuwa U-turn inakatazwa, kama hamna alama inayokataza unaweza kufanya U-turn ilimradi uliridhishwa na usalama, kilichofanyika hapo ni uonezi na kutaka kuonyesha how much the guy was important, na kwanza si kazi yake, pamoja na kusema kuna msemo huko Tanzania kwamba KILA MTU NI ASKARI, hata kama ni kosa onyo la verbal lingitosha. KIFUPI HUKUFANYA KOSA LOLOTE HAPO.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 16, 2009

    Asante kwa kutuhabarisha. Ulikuwa sahihi kabisa, unless kuna alama inayozuia kupiga U turn, ulikuwa na uhalali wa kufanya hivyo. Ni watu wengi hunyanyasika mikononi mwa watu wanaopaswa kujua sheria lakini nao hawajui. Mwanajesi kutojua hiyo hakuna anayeshangaa, ila Polisi kutojua... Walitaka hongo anyway

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 16, 2009

    umepata viza??

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 16, 2009

    A friend of mine was stopped by the traffic police at the same place, just outside the embassy. He had to pay the fine. I don't know the rules but definitely don't do a U-turn at that area.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 16, 2009

    thanks mimi huwa nina matatizo ya kupiga u-turn mara kwa mara nashukuru kwa kunihabarisha.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 16, 2009

    kama hukupata visa basi hiyo fine si halali. kama ulipata visa fine ni halali, ukija huku America shoplift hata shati la wal-mart utakuwa umerudisha hiyo 20 yako kiulaini.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 16, 2009

    Ninakazia maelezo ya mdau wa kwanza hapo juu. Barabara zote zinazopita hapo pembeni mwa ubalozi na nyinginezo kama hizo haziruhusu kufanya U-turn. Ulichotakiwa kufanya ni kwenda kugeuza mahali ambapo gari lako lingetoka kabisa barabarani na kuingia upya kwenye upande ambao unataka kwenda. Kwa mfano kuna common mistake ambayo hufanyika hasa kwa watumiaji wa Nyerere Road (a.k.a. Pugu Road) ambapo watumiaji wa barabara hiyo hufanya U-turn bila ya kwenda kwenye service road, hili ni kosa na wakikukamata unastahili adhabu kali.
    Faini ulipigwa ni sawasawa tu na ninakusifu kwamba hujashawishi mambo ya kumalizana.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 16, 2009

    hivi huko bongo, police, mgambo, sungusungu wote wanajihusisha na mambo ya traffic kivipi? au wanajichukulia sheria mkononi tu kwa vile wamevaa uniform. if ulimake u-turn kwenye intersection ambayo haina sign inayokataza u-turn rudi ukachukue 20 yako. na ulivyokwenda kituoni i am sure ulimpandisha kwenye gari yako mwambie akulipe nauli, na lindo sijui alimwachia nani?

    ReplyDelete
  16. kalume kengeJuly 16, 2009

    wewe, wewe, wewe acha uongo sheria za wapi hizo, iko hivi kama uko kwenye barabara yenye broken middle line haani hivi - - - - unaweza kufanya U tani bila kosa lolote labda tu iwe kuna kibao cha NO U Turn. kama middle line ni 'solid line' na ni mweupe(angalia hii point) unaweza fanya kama ni mmoja na uko upande wa mwenzako huku ukichukua tahadhari. Na kama mstari wa kati ni wa njano na ni miwili na haiku katika katika huruhusiwe kabisa No overtaking at all no U_turn.ndiyo maana utakuta kuna sehemu mstari wa njano umetenganishwa ili kuwaruhusu watu wanao ishi upende mmwingine kukata kona kwenda makwao tu na kwa tahadhari,vinginevyo utafanya hivyo tu kama kuna gari mbele yako imekufa unaruhusiwa kuipita kwa tahadhari.( sheria hizi zina tofauti kidogo sana inategemea uko wapi) Na nyogeza, kama mstari wa njano uko pembeni mwa barabara huruhusiwi kusimama labda kwa hali ya dharula tu. Three point turn haisaidii chochote kama ni No U turn ni No U turn full stop. hata kwenye intersection zingine utakuta NO U TURN. jambo lingine muhimu sana hapa ni kwamba three point turn huwa hasa kukufundisha kugeuza gari lako ukiwa katika njia nyembaba, si lazima unapo kuwa na nafasi ya kutosha ufanye three point turni, ila kwenye driving test atakuambia anataka three point turn na atakupeleka kwenye barabara ndogo.
    Mwingine anisaidie. Na siyo hivyo tu ,iwapo kama ndugu yetu aliye pata mkasa angekuwa na muda na kupelekeshana nao mahakamani angeshinda lakini hajachelewa sababu anayo risti na kosa limeandikwa ni nini na ni wapi limetokea anaweza akafungua kesi ya madai na ikasaidia watu wengi kujua sheria na haki zao na vilevile ikasaidia polisi kuwa makini. kesi kama hizi ndiyo watu huwa wanalipwa dolla million moja na watu wanashangaa.( nenda kapige picha hilo eneo na kamera yako iwe na kalenda kuna pesa hapa-fungua madai ya kwamba umepata mstuko wa moyo na hupati usingizi na umeathrika ki saikilogia unahitaji couselling. hahahahaaa dolla millioni moja chwaaaaaa. fidia)

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 16, 2009

    Pole sana mdau hata mimi nilishawahi kukumbwa na masahibu hayo ya hao askari wa ubalozi wa Marekani.Anony wa kwanza kakurupuka na haelewi anachoongea.Suala lililopo hapo ni kuwa mdau kapaki gari kwa muda na anataka kuondoka kuelekea uelekeo alikotokea na hakuna maelekezo yoyote wala kibao kinachozuia.Nilipopatwa na hali hiyo mimi niliburuzana nao hao askari na mwishowe tukafikishana kituoni Oysterbay.Niliomba kuonana na OCS nikamweleza mistreatment niliyopata na akaniruhusu kwa kuwaambia askari wapo hapo kulinda amani na si kutafuta mchawi.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 16, 2009

    Hivi askari wa JWTZ ndio walinzi wa kwenye balozi? Wanalinda balozi zote au hapo tu? Y?

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 16, 2009

    JE VISA ulipata au walikutosa?
    Ulifanya makosa kupiga U-turn actually hiyo fine ni halali kwani next time unatakiwa kujiunza kuendesha kwa usalama. Hiyo ni kwa faida ya maisha yako binafsi na wengine. Kwani madereva wengi bongo husababisha hajali za kizembe na kukatisha maisha ya wengi. Asante kwa kujianika mwenyewe kwa makosa yako. Next time fine itakuwa mara tatu ya hiyo uliyolipa! umesababisha watot wasinywe chai na mkate kwa kulipa hiyo elfu ishirini. Blogu ya jamii tunakusamehe ila usirudie tena kosa kama hilo uwe mwangalifu na maisha yako na wengine.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 16, 2009

    sina uhakika nyumbani wanasheria gani kuhusu hili lakini kama kuna uwezekana unge "plea not guilty" halafu kama kuna uwezo wa kupata lawyer wa mambo usalama wa baraba/(sijui kama kuna course hii au inayofanana na hiiipo), ungemuelezea case yako naye angekupa maadili'professional'. Natambua wakili atahitaji kulipwa ila ukienda mahakamani na ukashinda case unaweza(sina uhakika sheria za TZ) kurudishiwa gharama hizo na 'compansation'.Jaribu uchunguzi zaidi au we mwenyewe waweza kuangalia sheria ya kosa hilo kutoka library au web.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 16, 2009

    hahaha umeniacha hoi sana eti afande anakuulize je wewe uliona kibao kibao kilichokuruhusu kupiga U-turn pale? hahaha

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 16, 2009

    Swali hilo ungewapelekea trafic, na kwa vile ulileta ubishi ndio maana wakakupa haki yako, na kwa vile pia jina lako linauadui na hao watu ikawa ndio kisingizio. Wanachukua tahadhari hawo, maanake leo umepiga `U-TURN' kesho utapiga X-turn, booom

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 16, 2009

    Sheria hairuhusu kabisa kupiga U-turn kwenye barabara na sii lazima iambatane na vibao kila mahali. Naomba urudie notes zako za driving school kama bado unazo au nenda kwenye driving schoool yoyote hapa mjini au ofisi za trafiki watakuelewesha vema. Hili ni suala la SHERIA na wala siyo ALAMA ZA BARABARANI

    Halafu kaka inaelekea ulikuwa na jazba pale alipokusimamisha yule askari wa JWTZ ulitakiwa umalizane naye kiutu uzima. Nafikiri unanipata

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 16, 2009

    Kaka umefulia,

    iweje upige U-Turn, au ndio maharaka.Pole sana ila next time usirejee.

    Walivokukongoli hao wazee wa noma ni sawa kabisa, hakuna tatizo.

    Mwanazanzibaar.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 16, 2009

    Kwanini ulisimama na wewe ulikuwa tayari umo ndani ya gari? Ungeendesha zako tu ukaona kama huyo polisi angekufukuza. Ushauri wangu ni kuwa usingesimama.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 16, 2009

    Ndugu kwa kweli unamakosa! naungana na mjumbe hapo juu kwamba next time jaribu 3 points turn.
    Pia zingatia Tz sheria nyingi za barabarani haziko wazi, unaweza kukuta alama ilikuwepo na labda ikawa imetolewa na wahuni tuu , sasa siku ukifanya kosa mkubwa wanakunasa na wanakushtaki, mfano mkubwa ni taa za kuongazea magari ,hasa pale palmbeach unaweza pita moja kwa moja wakati alama inaonyesha green kwenda seaview, unaweza kamatwa pale kuwa umepita taa RED na ukibisha askari anaweza kukwambia twende na kweli unakuta kweli umepita RED

    ReplyDelete
  27. Pole ndugu, ni kweli ulikosea kupiga u - turn japo na serikari kwa upande wao wana kosa kwa kuto kuweka kibao. sheria za nchi yetu nyingi hazieleweki, Mimi nilinyang'anywa leseni na askari wa usalama barabarani na akanipa namba yake ya simu. sasa nimekwenda ostabay police kuchukua lecen yangu yule afande kaniambia kaiacha nyumbani, sasa kasema kesho atakuwa ubungo hivyo niende na 20,000 nitapata lessen yangu. hiyo ndiyo bongo yetu.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 16, 2009

    NI sawa tu kwa adhabu uliyopewa, ulifanya kosa la uzembe na kuhatarisha usalama wako na watumiaji wenzeo wa barabara. na wala hapa suala sio ubalozi wa Amerika, bali ni kosa la barabarani ambalo ungeweza kukamatwa sehemu yoyote kwa kulivunja.
    Asante kwa kuwashtua wadau wengine kuwa waangalifu, lakini na wewe unapaswa kujifunz vizuri alama na sheria za usalama barabarani na sio kujifanyia tu unavyotaka wewe.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 16, 2009

    Sidhani kama unakosa ingekuwa vizuri kama ugeenda mahakamani na ujitete baada ya kupitia sheria za barabarani za TZ na kupata ushahuri wa kisheria, lakini 20,000 sio nyigi sana kuanza kuagaika kwenda mahakamani na kupata ushauri wa kisheria

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 16, 2009

    Kwanza naomba kukusahihisha mdau .. askari walindao hapo ni FFU sio JWTZ kama ulivyoandika .. mimi walishawahi kunikamata.. ilikuwa saa za jioni unajua foleni kuelekea mikocheni . basi nilifanya faulo.. nikaovatake pembeni .. basi jamaa akanitolea mtutu akanisamisha .. akadai hongo .. hakuna wanachotaka zaidi ya rushwa .. nikamwambia sawa .. akaniomba driving lincese yangu nikamtolea ya America .. kwani sina ya bongo .. kisha nikamtolea kitambulisho changu cha kazi .. ilibidi aniombe msamaha .. baada ya kuona mimi nina mamlaka zaidi ya kulinda ubalozi huo zaidi ya yeye..

    ReplyDelete
  31. Pole sana swahiba...Nahisi Jina lako """Alihusein Mohamedali"" limekuponza, askari alihisi wewe ni gaidi umetumwa na osama ..... next time wadanganye jina lako..

    ReplyDelete
  32. kigozi kigumuJuly 16, 2009

    Wewe Kalume kenge unamdanganya mwenzako eti kwa kuwa ana risiti anaweza kwenda mahakamani. Na aende aone na hiyo risiti yake atajikuta risiti ikisomwa mahakamani malipo aliyolipa sio ya gari atageuziwa kibao anaweza kuambiwa malipo aliyolipa ni rushwa akapata kosa jingine. Mdau ushauri wangu wewe umetoa sadaka basi lakini kwa afande ukirudi hushindi maana huo ndio mtaji wao hao. Na kitabu cha risiti hakitapatikana utakoma. Eeehe Eeehe Bongo tambarare!!!!!!!

    ReplyDelete
  33. Ndugu,Kwa hali ya kawaida na ya kufikirika kwa njia hiyo ya Namanga hadi Msasani Hakuna naona ya wewe kuweza kufanya U-turn,Hivyo ni kosa haijalishi amekukamata nani.Kwa nini U-turn kwa narrow road na nyingine zinafananazo na hiyo Hairuhusiwi kwa Sababu sio Umefanya u-turn Ubalozini la ila utaweza weza sababisha ajali,Ni ustaarabu kwa tu Ukutoa rushwa umechangia Serikali hiyo ndio POLISI JAMII<,Pole

    ReplyDelete
  34. AnonymousJuly 16, 2009

    kalume kenge bwanaa....hahahaaaaa

    inabidi tujue sheria za roads Tz.

    JWTZ???

    eti umepiga U-turn ubalozini!kwani ubalozi uko nchi gani??USA ni ndani ya jengo tu..nyambaf ulimbukeni

    eti kwani wee umeona kibao kinachokuruhusu??yan kuna aya mamtu yakivaa magwanda yanajiona babkuuubwa!!kutaka tu mtu upandishe hasira

    ila rushwa geshini/polisi HAITAISHA HUU NI UKWELI wala usibane hii email...

    nachukia sana

    ReplyDelete
  35. Horty (London)July 16, 2009

    Wasomaji,
    Msimlaumu huyu jamaa aliyepatwa na tatizo hilo.

    Tatizo hapa tanzania ufundishwaji wa kuendesha magari na matumizi ya alama za barabarani bado haujatiliwa mkazo

    ukiwa ulifundishwa na kuelewa bila ya kuletewa leseni nyumbani, then vitu kama hivi haviwezi kutokea.

    Tanzania tunahitaji utaratibu mpya wa namna ya kufundisha madereva wetu katika ngazi zote.

    Wafundishaji wawe independent

    Wanaotoa certificate ya kuwa umeelewa vyema alama za barabarani wawe independent na ukipewa cheti chako kumbukumbu zipelekwe ka watoa leceni

    Wanaotahini kuwa umefaulu kuenesha barabarani na unauwezo wa kuzielewa alama za barabarani wawe independent chini ya jicho la serikali

    Watoa leseni wawe independent china ya jicho la Serikali.
    Ninapendekeza kuanzishwe kitu kinaitwa Tanzania Drivers Licence Authority (TDLA)

    Hawa ndiyo pekee watakao kuwa wanatoa leseni na waliofaulu wawe wanatuma certicate zao kwa njia ya posta, DHL, au kwa namna nyingine zilizopo kama EMS

    Faida:
    Itapunguza ajali barabarani
    Kuwapa madereva wapya nafasi ya kujua wajibu wao
    Kuondoa rushwa
    Kuthibiti fake leseni
    Nk.nk

    Tatizo
    Tanzania trafiki ndiyo wanaotahini kutoa leseni.... uwezekano wa rushwa

    TRA ndiyo watoa leseni kuna matatizo ya uthibiti.. kwa mfano mtu wa TRA anakuuliza "cheti cha macho" kitu ambacho si kazi yake unapokwenda kuapply leseni

    Nk nk
    Kwa ujumla utoaji na ufundishwaji wa kuendesha magari tanzania ndiyo tatizo kubwa.

    ReplyDelete
  36. AnonymousJuly 16, 2009

    Ku U turn mahali patakapo zuia mpitaji mwingine si sawa, hiyo ni kwa kutumia akili za kuzaliwa tu. Sasa eneo lile ni nyeti magari kusimama ovyo si salama pia. Pole lakini huo ndo ukweli.
    GJK

    ReplyDelete
  37. AnonymousJuly 16, 2009

    Pole ndugu yangu kwa yaliyokukuta na pia mchakato huu wa majibu utatusaidia wengi, ila trafiki wetu wa Tanzania ni hatari tupu wanaweza kukubandikia kosa ambalo hujafanya, mie kuna siku moja usiku trafiki mataa ya pale kamata trafiki karuhusu magari ile napita kuelekea kilwa road akanisimamisha akasema sijakuruhusu - akatoka matusi makubwa ya nguoni - nikamwuliaza ndugu mbona matusi makubwa hivyo - alichofanya yule trafiki alikimbilia mbele ya gari yangu na kuita wenzake kwenye radio kwamba nataka kumgonga!!Bahati nzuri kulikuwa na police wa kike pembeni akaja mbio akamwambia yule trafiki achana na redio mbona unaeneza habari za uongo kuhusu uyu mama?kilichofuata alimwamrisha yule dada anipeleke kituoni pale central, yaliyoendelea pale ni machungu kusimulia ila niliamriwa niache gari pale mpaka kesho yake hapo ni usiku na mie ni mwanamke sina hata pesa ya akiba nitafikaje ninakoenda! badae wakanipa gari the next day nikalipa notification yao 20,000/=! Trafiki Police wana lugha chafu za matusi, hii yote ni wengi wao wanaingia police sio kwa kupenda ila sababu hana pa kwenda kufanyia kazi sababu vyeti haviruhusu.Wanatakiwa wawe wanapewa short courses za mara kwa mara kuwakumbusha njia sahihi za jinsi ya kutumikia nchi na raia wake -

    ReplyDelete
  38. AnonymousJuly 16, 2009

    KOSA LA KWANZA NDEVU ZAKO KOSA LAPILI JINA LAKO ALIHUSEIN-BIN-MOHAMEDALI KOSA LATATU UNATAKA NINI UNYAMWEZINI SHEIKH,NA KILA KITU SAUDIA KIPO.FULLSTOP.

    ReplyDelete
  39. AnonymousJuly 16, 2009

    nakubaliana na maelezo ya Kalume Kenge. Uwezi kufanya U turn kama hakuna kibao cha kukuruhusu kufanya u turn mpaka uone hizo mishale ya kukuonyesha ufanye u turn. Kwenye barabara nyingine kuna intersection lakini bado unakuta kuna kibao cha kukuonyesha husifanye u turn au unafanya hivyo at your own risk kama alivyosema huyu mdau kama hakuna vile vile alama za --- huwezi kufanya u-turn. Unajua watu kimazoea wakiona hakuna gari na barabara ni pana wanajifanyia u turn bila kujua ni makosa. Ingawa sijui ubalozi unaingiaje lakini kama unaruhusiwa kuingia na gari kutakuwa kuna jinsi ya kutoka na si kujipigia u turn upendavyo. Askari wa JWTZ kumpeleka kituo cha polisi mhusika ni sawa kabisa maana yeye kama hasikari na kisheria ni mlinzi wa amani, pale atakapoona kuna kosa la jina linafanyika au linataka kufanyika yuko halali kukupeleka kituoni mradi hajachukua sheria mkononi na amefuata sheria zote za kukukamata ambavyo kulingana na maelezo ya mdahu naona alifuata hatua zote za kukukamata na faini uliyotozwa ni halali. Kuhusu kituo kukiacha peke yake hatujaambiwa kama kwenye lindo alikuwa peke yake kiasi cha kuacha lindo na kumpeleka polisi, kwa hiyo ilo tuliache kwa sababu hatujambiawa ilikuwaje. Ila mradi mdahu ujue kuna utaratibu wa kufanya u-turn barabarani na sio lazima awe traffic ndiye atakukamata. hata mimi kama nitakuona naweza kuwaarifu polisi kuwa umetenda kosa kiasi kwamba ungesababisha ajari wataniita nitatoa ushaidi. Kila mtu anatakiwa kuangalia sheria zisivunjwe. Siwezi kukuona unaiba eti mimi sio askari nikakuacha

    ReplyDelete
  40. AnonymousJuly 16, 2009

    Guyz I think your missing the point:
    Maaskali wabongo wote ni MADIKTETA Mafunzo wanayopewa ni ya kuwatesa na kuwanyanyasa raia.
    Wengi wao hawajui sheria na katiba ya nchi sasa watatekeleza vipi sheria ya nchi?
    kazi yao ni kulinda usalama wa raia, wanachofanya wao ni kinyume na sheria inavyowataka hii inaonyesha jinsi gani mafunzo yao yalivyo duni yasiyojali haki za binaadamu.
    Maaskari wengi wa bongo wanatumia mawazo yao kuwahukumu watu, vichwa vyao vimetawaliwa na Udicteta.
    Sasa huyo askari hapo US embassy kichwa chake kinamwambia kwamba U turn hairuhusiwi na vilevile anajua kwamba hakuna alama yoyote inayo onyesha hivyo ktk barabara hiyo kiasi kwamba kama mtu ni mgeni maeneo hayo itamwia vigumu kujua kama kuna sign ya NO U TURN
    badala ya kuongea na uongozi husika ili waweke alama hizo HASA UKIZINGATIA KWAMBA HAPO NI EMBASSY, US EMBASSY, anaamua kutumia mawazo yake kwamba kila mtu anajua,UNLESS TANZANIA IS NO U-TURN COUNTRY!!!!?????
    INAWEZEKANA KWAMBA NCHI YETU HAINA UWEZO WA KUWEKA ALAMA ZA BARABARANI KWA KILA BARABARA LAKINI KWANINI WATU WAADHIBIWE KWA KUTOKUWEPO ALAMA ZA BARABARA???????!!!!
    I have a message for u Mr policeman YOUR JOB IS TO ENFORCE THE LAW NOT TO MAKE THE LAW.
    POLICE ACADEMY SHOULD TEACH OUR BOYZ ALOT OF LESSONS ABOUT HUMAN RIGHTS NOT HOW TO BE A DICTATOR
    Kitu alichofanya jamaa pale US embassy kilihitaji onyo la mdomo bila ya kutoa hongo till when u put the signs
    Michuzi can u plz double check at the Road if there is no signs and if u can have a chart with any police at the embassy.Take a video plz!!!!!!
    Ukifanya hivyo utaonyesha jinsi gani unakea kuhusu WADAU wako na yanayo wasibu.
    Mungu ibariki globu ya jamii
    Mungu mbariki mdau no.1
    thnx

    ReplyDelete
  41. AnonymousJuly 16, 2009

    Nenda mahakamani kama unafikiri umeonewa. Nyie ndio mnaotuletea shida hapa mjin mradi mnajua kuweka gea na kushika usukan basi. Barabara ni sheria sio upeleke gari kama upo nyumbani kwenu, hilo ni fundisho kwako na wenzako wenye tabia kam yako. Sawaaa??

    ReplyDelete
  42. AnonymousJuly 16, 2009

    Mdau Tarehe Thu Jul 16, 04:54:00 AM, Umenivunja mbavu mpaka machozi yametoka... hahahaha Asant, niliamka na hasira sasa niko safi, japo ushauri wako ni pumba, acha kushauri watu uhalifu. eti kashoplift marekani wallmart shati moja tu. hela yako isharudi...

    Pole mdau kwa yaliyokukuta...Lakini swali la askari>.. ! mwe.. mi hoi.

    ReplyDelete
  43. AnonymousJuly 16, 2009

    Baada ya kusoma yaliyokukuta niligundua kuwa umevunja sheria kwa kucross solid line kama wadau walivyoandika hapo mwanzoni.Nipo likizo nyumbani kwa muda mfupi.Namekwenda palepale ulipopiga u-turn.Baada ya kuhakikisha kuwa nina eye contact na askari wa JWTZ nikapiga U-turn mbele yake ili anikamate nikalipe faini.Alikuja kama simba aliyejeruhiwa na kuniashiria nisimame.Nikajua mambo yatakuwa yaleyale ya kwenda polisi kulipa faini badalayake akaanza kupandisha na kuniamuru nitoke nje ya gari.Alipoanza kuniuliza kwanini nimepiga U-turn nikamjibu
    "I'm sorry officer,I cant speak swahili at all,would yu p'se put your questions in english?Akanijibu kwa upole"U-Tuns are not allowed here,show me your passport and lisence please".Nikatoa my US passport na international DL nikampa.Akazisoma kwa muda kidogo,akamwita mwezie na kumuonesha,baadae wakanirudishia na kuniamuru kwa kiswahili "potea" mwenzie akarudia "GO".Nikaingia kwenye gari nikaondoka.Tanzanians are fined while Americans are ordered-"POTEA".It was was a childish thing thing to do but it was good experience.I dont advice anybody to do it 'cause it may end in a bad way.
    Jumapili naondoka kurudi TX.
    Thanks

    ReplyDelete
  44. AnonymousJuly 16, 2009

    Hivi huzijui sheria za bongo? Ni porishi tuu ndo ana mamraka ya kisheria ya kumtia raia chini ya urinzi siyo mangereza wara ri-jkt wala ri-jw.

    Hata mganmbo wanaruhusiwa na sheria kwa sababu ni vibarua wa porishi.

    Siku nyingine ijue hiyo.

    ReplyDelete
  45. AnonymousJuly 16, 2009

    Kabla ya kujibu/kukuelewesha swali lako, je leseni unayo na umeipata baada ya kufaulu katika chuo kinachotambulika? Yaani sio ya wapiga debe?

    ReplyDelete
  46. AnonymousJuly 16, 2009

    MDAU HORTY(LONDON) NDIO ULIYETOA POINT NA UNAELEWA TATIZO LIPO WAPI.TUNAHITAJI WATU KAMA WEWE MRUDI NYUMBANI.

    ReplyDelete
  47. AnonymousJuly 16, 2009

    Hayo nimatatizo ya nchi nzima ya Tanzania,,kwa nchi zote ambazo wananchi wanatembea na shelia mkononi Tanzania ni ya kwanza,,wallah mimi siwezi kutoa hela kama sijaona bango la kunikataza,,,tunaweza kuingizana nahuyo aliye niomba hiyo hela mpaka mahakamani nanikatoa hiyo hela baada yakuona shelia hiyo iko wapi,,tatizo watanzania weengi akipigwa buti la hela anatoa tuu bila kukagua kama anaitoa ki ukweli au la,,,nyie watu mnaoishi TZ inatakaiwa mjifunze kuwa wagumu,sio mnatoa tuuu hata kama sio kosa,,ila samahani najua mlisha zoea kutoa hongo kwa kila kitu.ila nakushauliwewe jamaa uliye tafuta visa ya kuja Marekani hakuna vyakutoatoa hela hovyo,,selikali zahuku sio zamafisadi kama huko kwenu,,,sitamani kurudi huko naweza kukumbwa namatatizo mengi,,puuu..najua utanibania misupu!!!

    ReplyDelete
  48. AnonymousJuly 16, 2009

    Mdau, ulikosea kumpandisha askari kwenye gari lako eti mpelekane polisi. Mimi ningemwambia atangulie kituoni. Gari ni langu na nna haki ya kumpandisha mtu nnayetaka.

    ReplyDelete
  49. AnonymousJuly 16, 2009

    Wewe ulishakubaliana makosa sasa iweje uanze kuhoji kama faini ilikuwa inaenda sawa na kosa. Ulishajikaanga mwenyewe

    Nashangaa kwanini hawakukuchukulia kabisa leseni maana kama ulikuwa unajua umeonewa kwann hukujitetea kulingana na sheria za barabarani zinavyosema

    ReplyDelete
  50. AnonymousJuly 17, 2009

    Bongo hakuna sheria! Uhuni mtupu!

    ReplyDelete
  51. AnonymousJuly 17, 2009

    Hii ni tofauti kati ya nchi yenye demokrasia na nchi inayofikiri na kujigamba kuwa ina demokrasia.

    Katika sheria ya nchi kila mtu ana haki lakini haki haifuatwi na maofisa wetu kuanzia polisi mpaka mahakamani. Kama mdau anapinga kosa, ingetakiwa aende katika korti inayosikiliza kesi kama hizi. Wenzetu wana korti maalumu zinazohusu faini zote kama za barabara na kadhalika. Nilipopinga faini yangu marekani, polisi aliyenikamata alitakiwa aje mahakamani. Hajaja na nikafutiwa faini hio. (faini pia inasababisha insurance ya gari kupandishwa kwa sababu unaonekana hujui kuendesha gari kwa usalama). Na kama angekuja ningepunguziwa faini vile vile kwa kuwa ni neno lake dhidi ya neno langu. Jaji anaona wote tuna haki na anapunguza faini kuwanufaisha wote na kutopoteza muda wa korti.

    Tanzania polisi ni Mungu na hapingwi. Pili, huyo polisi hausiki na kazi za usalama barabarani kwa kuwa lazima ajifunze kwanza kabla ya kufanya hio kazi. Kithibitisho hiki peke yake kinatosha kutompa faini Mdau kama kweli nchi inazingatia haki za binadamu.

    Nilishawahi kupelekana na askari wanaolinda benki waliponisimamisha kwa kuendesha ONE WAY mjini. Nilikataa kuwapa chochote na tukaenda polisi. Walikataa kutoka katika gari langu tulipofika kituoni. Nilipotoka kumwita afisa mhusika, wakakimbia zao. Nikaondoka zangu pole pole.

    ReplyDelete
  52. AnonymousJuly 17, 2009

    16th July 2009B-pepeChapaMaoni
    Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Jamal Rwambow.
    Zaidi ya Shilingi Milioni 12 zimekusanywa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kama faini zilizotozwa kutokana na makosa mbalimbali ya barabarani.

    Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Jamal Rwambow amesema fedha hizo zilikusanywa katika operesheni maalum iliyoendeshwa kati ya Julai 6 na Julai 12 mwaka huu.

    “Wapo waliotozwa faini za papo hapo na wale waliopewa maonyo makali wasirudie tena makosa ya aina hiyo ”akasema.

    Amesema jumla ya kiasi cha pesa kilichopatikana ni shilingi 12,650,000.

    ReplyDelete
  53. AnonymousJuly 17, 2009

    Mi nadhani watanzania wengi tuna dharau kwenye kufuat sheria za barabarani, wapo wanaojua sheria kisha wakizuvunja kwa haraka zao, na wapo ambao hawajui sheria na wanajifanya wanajua, swala liko wazi sehemu ya U-TURN,bila kujali wingi wa magari barabarani,kwa haraka zako unaamua kula short kati,mi naona faina iliyotolewa ni sawa,Dokezo uan habrai hata gari yako ikiwa chafu ni kosa la kulipa faini ? ,

    ReplyDelete
  54. AnonymousJuly 17, 2009

    sheria ni kama kwa kama kawaida siyo wala si hongo hongo itatupeleka kaburini yesu tuchukue utubebe utufikishe salamah saliminih huko kwenye njia nyembamba.
    K'zoo MI Concorde

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...