

Ile timu ya vijana wenye vipaji na uwezo wa kutandanza soka lenye kiwango cha TBS,Stars United inayoundwa na vijana kutoka DC, Atlanta, North Carolina,New Jersey na New York, siku ya Jumamosi August 8 watatinga uwanjani mjini Boston tayari kwa mpambano wa kufa mtu na wenyeji wao wa huko.
Hii ni katika kusherehekea Nane nane sherehe ambazo hufanyika kila mwaka. Kwa sasa timu zote zipo mafichoni na zinaendelea na matayarisho ya mpambano huo wa jumamosi unaosubiliwa kwa hamu na mashabiki wa soka Boston na miji ya jirani.
wachezaji wa stars united watakao kuwemo kwenye msafara ni Makipa-Dedi Luba, Chochala Manka na Luke Kinyang'anyiro-mabeki-Henry Kente, Adam Tenga,Libe Mwang'ombe, Kheri Yahaya, Steve Boaz, Simon Marco, Adam Jongo,Lemy Mhando na Aris Maruma-viungo-Ebra Nyagaly,Denis Geoffrey, Hadji Helper, Hussein Ebrahim na Owen Hampley-washambuliaji-Junior Ceaser,Mody Majaliwa,Shawn Shaban,Innocent Geoffrey na Vicent Ndusilo.
kutokana na Ushauri wa daktari wa timu Didi Vava,kiungo Seif Ndosa na beki Evans Shangalai hawatacheza kwenye hii mechi ya Boston kutokana kuwa na maumivu ya misuli.
Kiungo Elvis Mnyamuru Dotto pia hatakuweno kwenye msafara kutokana kutopata ruhusa ya mwajili wake.Timu zote zimeahidi kutoa burudani tosha kwa washabiki wao, Stars United(Kandanda safi kiwango cha TBS) wamewaomba wenyeji kutafuta kiwanja kizuri kusudi watoe burudani kwa washabiki wa Boston.
mahundi aka paroko mbona siwaoni na ngonyani aka gupta? mkowapi wazee wa kinyanyiko?au nyie kabumbu halipandi?
ReplyDeleteHao DC CJUI all starz wazushi sana kama vp Boston wapelekeni kiwanja cha football kama walivyotufanyia Houston memorial weekend..na bahati yao sare kwao ilikua kama ushindi uwanja bovu kama nn!!!!!!!
ReplyDeletehuyo wa Boston aliyepiga goti kulia sio mdogo wake Hasheem Thabeet?
ReplyDelete